Wednesday 27 July 2016

KUWA NA UMRI MKUBWA.


Huwezi kugoma kutozeeka, ni muhimu sana kutarajia mabadiliko jifunze kukabiliana na hiyo hali au tarajia mabadiliko kwani mwanamke mwenye umri wa miaka 29 hawezi kuwa sana na mwanamke mwenye miaka 40 na mwanaume mwenye miaka 28 si sawa na mwanaume mwenye miaka 45.
Inawezekana wewe ni mwanaume na umeanza kupoteza nywele kichwani na inawezekana umeanza kujazia uzito wa ziada kwenye tumbo na una kakitambi ka kiana.
Ulizoea kuruka kirahisi sasa ni mzito huwezi kuruka tena, hapo sijakuuliza masuala chumbani na huo uume wako una behave vipi.
Inawezekana wewe ni mwanamke na umri ni kweli unaenda na huamini namna gravitational force inavyokuvuta kila kitu kushuka chini ya sakafu.
Unashangaa matiti yanashuka chini na kulala tofauti na zamani, uso nao unainama na kuweka wrinkles, unashangaa nywele zinakuwa ngumu na kuanza kupotea zenyewe bila taarifa, chini kunagoma kuwa wet hata baada ya kusisimuliwa kama ilivyokuwa kawaida yako kwani kwa maongezi tu kila kitu chini kulijibu.


MABADILIKO YA KIMAPENZI HUWA NI KAWAIDA KWA MWANAUME ANAPOONGEZEKA UMRI.

Kumbuka ulipokuwa teenager (siyo wote) ile kusoma gazeti ambalo ni romantic ulikuwa unasisimka, ile kumpita mwanamke mrembo mwili ulikuwa unasisimka.
Mwanzo wa ndoa yako, ukiona mke wako kapanda kitandani tu ulikuwa unasisimka na kuwa tayari kwa uume wako ulikuwa tayari ushajinyosha na unakugusa ceilings.
Inawezekana kutokana na mwili wako kusisimka kimapenzi haraka kumejenga tabia fulani kwako na kwa mke wako na siku mambo yakiwa tofauti mnaanza kuhaha kudhani kuna tatizo limejitokeza kumbe ni kawaida kwani ni kuongezeka kwa umri.
Inawezekana hata namna ya kuandaana ilikuwa ni one sided kwa maana kwamba mwanaume ndiye alikuwa anasisimuliwa kwa muda mrefu zaidi na mwanamke kwa muda mfupi.
Sasa umri umeongezeka na usipoandaliwa vizuri unaweza kujikuta uume unabaki soft muda wote bila kuleta mabadiliko yoyote kama kawaida yake.
Maana yake mwanaume anapoongezeka umri anahitaji direct penile stimulation kuliko zamani.
Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa kijana hadi kuwa mzee ni mfano wa godoro jipya, ukilinunua huwa gumu na baada ya miaka kadhaa utaona kasheshe yake.
Pia mwanaume anapoongezeka umri anaweza kushangaa anamaliza sex bila kukojoa (ejaculate) kitu ambacho haikuwa kawaida yake, kwani older men kawaida hawahitaji kufika kileleni kama young men.
Hata hivyo hiyo ina faida kwa mwanamke kwani sasa mwanaume anaweza kufika mbali katika kumridhisha mke wake ndiyo maana umri unavyoongezeka mwanaume huwa mzuri zaidi kimapenzi.
Kama ni mwanamke Kumbuka kwamba si kushindwa kwako kama ukiona mume wako wa 40+ amemaliza nusu saa bila kufika kileleni, wala haina maana kwamba humvutii au hupendeza bali ni kuonesha kwamba mwili wake unazeeka.
Inawezekana ilikuwa kawaida yake akimaliza mara ya kwanza baada ya dakika 2 au 3 anaweza kurudi na kuanza upya kukupa mahaba wewe mke wake na sasa hawezi tena.

No comments:

Post a Comment