Wednesday, 12 August 2015

UUME KUSHINDWA KUSIMAMA.

Ni matatizo ya uume kushindwa kusimama (kudinda) kiasi kinachotakiwa ili kufanikisha kuingia ndani ya uke wakati wa tendo la ndoa, au ni kitendo cha uume kusimama kwa muda unaotosha kuhakikisha mwanamke ameridhika na tendo la ndoa.

Matatizo ya uume kushindwa kusimama wakati wa tendo la ndoa ni tatizo la kawaida kwa wanaume wambao umri umeenda sana, kiukweli wanaume wengi hii hali imewahi kuwatokea na hii haina maana kwamba wanamatatizo ni mpaka hii hali iwe ni ya muda mrefu na kinatokea mara kwa mara hapo ndipo litakuwa tatizo.

Kama tatizo linazidi kujirudia linaweza kuharibu kujiamini kwa mwanaume na matokeo yake linaweza kuanza kuwa tatizo la kudumu na pia kuharibu uhusiano wako na yule umpendaye hasa kwa yeye kutoridhika na huduma yako.

Tangu kale tatizo la uume kushindwa kusimama lilikuwepo na mara nyingi lilikuwa linahusisha akili au mawazo kichwani mwa mwanaume na wengi walikuwa wanashauri kwamba
ni mwanaume kuondoa hofu,
kutulia na baadae hali itarudi yenyewe.
Kwa sasa tuna madaktari ambao wanashauri kwamba tatizo si kichwani peke yake bali linaweza kuwa ni la kimwili zaidi.

Njia ya kawaida ya kujua kama una tatizo la kimwili kwa uume wako kushindwa kusimama ni kwa mwanaume kutafiti je, wakati wa usiku ukilala unasimamisha mara ngapi kwani ni kawaida mwanaume hata mtoto wa kiume kusimamisha uume mara 3 hadi 5 kwa usiku mmoja.
Au wakati wa kuamka asubuhi ukiona uume umesimama basi wewe kimwili upo fiti kabisa na inawezekana tatizo la kushindwa kusimamisha ni la kisaikolojia zaidi.

Kukojoa mapema au ugumba hauna uhusiano na kushindwa kusimamisha uume kwani mwanaume anayeshindwa kusimamisha uume anaweza kutoa mbegu ambazo zinaweza kurutubisha yai na mtoto akazaliwa.
Vilevile mwanaume anayekojoa mapema akipewa msaada wakisaikolojia anaweza kutumia muda mrefu ndipo aweze kukojoa.

Nini husababisha jogoo kushindwa kuwika:?

Ili uume usimame na kuwa imara kwa tendo la ndoa huhusisha
Ubongo,
Mishipa ya fahamu,
Homoni,
Mishipa ya damu na
kitu chochote kitakachoingilia huu mfumo, basi kitendo kizima kinapatwa na tatizo.
Kawaida husababishwa na:
Magonjwa kama vile Kisukari, pressure (mgandamizo wa damu), moyo.
Matatizo ya damu kushindwa kuzunguka vizuri kwenye mwili.
Kiwango kidogo cha homoni za testosterone.
Matatizo ya uti wa mgongo
Kuharibika kwa nerves kutokana na upasuaji.
Tiba za madawa kama vile BP (Blood Pressure), matibabu ya moyo, ulcer.
Dawa za usingizi, na dawa za kutibu stress.
Kuvuta sigara, pombe, na madawa ya kulevya aina zote.
Mawasiliano ovyo na mwenzi wako
Stress, hofu, mashaka, na hasira
Matazamio au mtazamo tofauti kuhusu tendo la ndoa, badala ya kupata raha (plessure) mwanaume anakuwa anahisi kama ni kibarua au kazi (task)

Je, kama jogoo anapenda kuwika mara kwa mara bila utaratibu?

Hii huwapata sana ma-teenager wenye miaka kuanzia 15 - 20 na hili ni suala la kisaikolojia tu na huwa inawatokea sana wakiwaza kuhusu mapenzi au kumuona msichana anayevutia inaweza kuwa njiani, darasani au mahali popote na huo ni utoto tu ukikua hiyo hali utaacha.

Je, ni jinsi gani mtu anaweza kuondokana na hili tatizo?

Kwa wanaume wengi mfumo wa maisha ndio unatakiwa kubadilika.
Achana na sigara, pombe na madawa ya kulevya
Pumzika muda wa kutosha na kurelax
Fanya mazoezi na pia chakula bora ili damu iwe inazunguka vizuri mwili mzima hadi huko kwenye uume.
Pia uwe na mke mmoja au mpenzi mmoja kwani hofu ya kupata UKIMWI na magonjwa ya zinaa wengi husababisha hata jogoo ashindwe kuwika.
Uwe wazi kuongea na mpenzi wako linapokuja suala la mapenzi kama huwezi nenda kwa washauri wako, hata hivyo kwa nini ushindwa kuongea na mpenzi wako sasa wewe mwanaume gani unashindwa kuongea na mpenzi wako.
Pia wanaume ambao wana matatizo kuongea na wapenzi wao feelings zao kuhusu mapenzi huwa mbali na wanapata shida sana kuelekeza matatizo yao kuhusu kiwango cha ufanyaji wa tendo la ndoa hivyo hubaki amekumbatia tatizo lake na matokeo yake ndo jogoo analala tu wakati anatakiwa kuwika.
Pia kuna dawa ambazo unaweza kutumia ingawa unahitaji msaada wa dakatari kama vile viagra,
cialis,
levitra
Uwe mwangalifu usibugie hizo dawa bila ushauri wa Daktari kwani kama una matatizo ya BP unaweza kufia kufuani mwa mtu.

Kama tatizo la uume kushindwa kusimama umegundua linatokana na dawa unazotumia ni vizuri kumuona daktari akakushauri kitu cha kufanya kuliko kukatisha (kuacha) kutumia dawa kwa ajili ya tendo la ndoa wakati dose hujamaliza.

Ni hadi iweje ili kumuona Dakatari au mshauri?

Pale unapoona juhudi zako hazizai matunda na jogoo anazidi kugoma kuwika.
Pale unapoona dawa unazotumia ndiyo sababu ya jogoo kushindwa kuwika.
Ukiona tatizo linajitokeza hasa baada ya kufanyiwa surgery kwenye viungo vyako vya uzazi.
Pale unapoona uume unashindwa kusimama na wakati huohuo unapata maumivu ya mgongo (back pain), maumivu ya tumbo au mabadiliko katika mkojo (haja ndogo).

No comments:

Post a Comment