Wednesday, 5 August 2015

MIGOGORO BAADA YA NDOA.

Dafrao!Baada ya kufunga ndoa au baada ya honeymoon baadhi ya wanandoa hujikuta katika mgogoro inaweza kuwa si kupigiana kelele kama walevi bali ile kujisikia umeumizwa baada ya mambo ambayo ulikuwa unategemea kuwa yangekuwa safi yanakuwa tofauti kabisa na matarajio yako.

Hata hivyo migogoro kama hiyo au mshtuko kama huo husababisha kuleta mabadiliko au kubadilika na kukua na kujuana zaidi ninyi wawili ambao sasa mnaenda kuishi pamoja na kuwa kitu kimoja kimwili, kiakili, kimawazo, kihisia na kiroho kama inawezekana.

Kuna huu msema ambao kwa asilimia 100 nauamini ni kweli

Hata hivyo mgogoro wowote ukitokea jambo la msingi ni busara na namna au njia inayotumika kutatua

Mara nyingi wanandoa wanashidnwa handling ya migogoro katika ndoa kwa sababu wengi hukwepa badala ya kukubali na kukaa pamoja na kupambana nayo na hii inatokana na mitazamo kwamba mgogoro wowote ni kitu kibaya sana katika ndoa hasa kama wewe ni mkristo safi.

Wapo wanandoa wanaumia mioyoni mwao hawataki kusema na kuongea na waume zao au wake zao kwa kuogopa kwamba akiweka jambo lake mezani basi wataanza kupigishana kelele hivyo dawa ni kubaki kimya hata hivyo kubaki kimya ni kujimaliza mwenyewe.

Binadamu ni tofauti na aina yoyote ya mashine hivyo kutofautiana katika mawazo ni jambo la kawaida.

“Migogoro hujitokeza kwa sababu wanandoa huanza kufanana kwani kazi ya ndoa ni kuwafanya wawili wanaopendana kufanana”

Ni kama kuunganisha mito miwili yenye kelele chini ya mlima; kutakuwa na kelele, hekaheka, kububujika, chemka na kufanya povu na kila aina ya msuguano kwani mito miwili inaunganika kufanya mto mmoja strong.

Kutokukubali mgogoro katika ndoa huweza kusababisha mambo mawili:-
Kwanza mgogoro ukijitokeza tu utaamini kwamba na utaanza kumlaumu mwenzako.

Pili utapata mshtuko wa kukatishwa tama kwa kuwa ulitegemea kwa njinsi unavyompenda na mnavyopendana basi hamuwezi kutofautiana kama wakati mlipokuwa wachumba.

Unajua mgogoro wa kwanza kwenye ndoa unakuwa na disappointment zaidi ya ile ya kuona mende au nywele kwenye chakula nyumbani kwa mama mkwe.
Vinginevyo wanandoa wanaweza kuanza kutoa reaction bila kutumia busara

No comments:

Post a Comment