Friday, 7 August 2015

NI MAMBO MADOGO LAKINI NI MUHIMU SANA.

Weekend ni wakati mzuri kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa na muda mzuri na mpenzi wako, mke wako, mume wako, mchumba wako, soul mate wako, partner wako, honey au sweetie wako nk.
Naaamini utasema kwamba dunia ya leo mambo muhimu ni uchumi, kazi zetu nk, kitu cha msingi bila amani, upendo na furaha ktk nyumba zetu bado hata kama tutakuwa na pesa nyingi.

Kama wewe ni mwana ndoa jitahidi hii weekend kufanya mambo tofauti kabisa na jinsi unavyofanya kila siku hasa weekdays.

Kitu cha msingi ni wewe kuwa mbunifu kufanya vitu vidogo vidogo (kama unaweza kufanya makubwa fanya) ambavyo vitasababisha mwenzi wako akuone unamjali na unawajibika katika mahusiano.
Kama ni mwanaume unaonaje hii weekend angalau unasaidia kazi ndogondogo pale home kama vile
kutandika kitanda,
kupika kama unaweza,
kuwaandaa watoto,
kufanya usafi, kusaidia kufua nguo nk
Fanya hivyo kwa upendo..

Na ukitoka leo kazini unaonaje pia kama utaenda kununua zawadi yoyote kwa ajili yake, ingawa hii weekend zawadi muhimu ni wewe mwenyewe kuwa na muda na yeye.

Na kama ni mwanamke naamini utakuwa mbunifu zaidi kufanya vitu vipya kwani wanaume siku zote wanataka kitu kipya katika mahusiano.
Unaonaje ukihakikisha chumbani kunakuwa tofauti kabisa kuanzia
Kitanda na mashuka yake nk
marashi mbalimbali chumbani
na pia wewe mwenye kuhakikisha una nukia vizuri kwani smell of your body affects emotions, jipambe sawaswa tofauti na siku za kawaida kwa ajili yake,
Tafuta time kuwa naye yeye tu na kama hukupika wewe mwenyewe wiki nzima jaribu weekend hii kumpikia mwenyewe kwa mikono yako chakula cha uhakika.
Pia usisahau kumuombea mkeo au mumeo maana (maombi) ndiyo yatawahakikishia kwamba kitanda chenu shetani hapati nafasi kulala maana akilala, kuangalia TV kunakuwa raha kuliko faragha ya chumbani kwenu.

Kama wewe ni single na ndo upo kwenye process za Uchumba najua hii weekend umepanga mkutane mkaongee mipango yenu, nahisi tangu mmekutana wiki iliyopita umeona kama siku haziende, Mungu ni mwema weekend ndo hiyo.
Jitahidi unapokuwa na mke/mume wako mtarajiwa unatumia jina lake vizuri kwani kuna raha yake mtu ukimtaja kwa jina lake mwenyewe kama vile Mungu anavyojitambulisha kwetu kwa jina lake na kututaja majina yetu.
vijana wa siku hizi Badala ya jina mnatumia maneno kama ‘
"Oya twende zetu!"
"Hey nikununulie nini!"
Tumia jina lake hiyo inakupa point kwamba ni presentable
Pia tumia huo muda kumfurahisha kwa maneno matamu, yanayotia moyo ili kumsahaulisha na yale amepitia wiki zima, kwani hapo ndo mnaanza kutoa picha ya nyumba yenu jinsi itakavyokuwa.
Pia ni muhimu unapokutana naye Ongea mambo muhimu; siyo mambo ya watu wengine au ku-discuss michezo ya kwenye TV, muda mnaotumia kukaa pamoja na kuongea ni muhimu sana mtakuja kuukumbuka mbele ya safari


Nawatakia weekend njema na Mungu awabariki sana

No comments:

Post a Comment