Friday, 7 August 2015

UMUHIMU WA MAWASILIANO KTK NDOA.

Mawasiliano katika Ndoa ni kama barabara ya njia mbili inayoruhusu magari kuingia na kutoka; yaani wanandoa wawili ambao mmoja akiongea mwingine anasikiliza na mwisho wanapata jibu la kudumu la tatizo lililokuwepo.
Mawasiliano mabovu husababisha kutokuelewana ktk ndoa na mahusiano ya aina yoyote.

Ni kitu cha kawaida kwa sasa kuona mabishano ambayo yanaanza asubuhi jua linaochomoza na kuendelea hadi jua linapozama jioni bila ufumbuzi.


Mabishano kama hayo yasiyo na ufumbuzi ni kama Bomu linalosubiri muda ili lilipuke.


Baadhi ya wanandoa hudhani kwamba kuacha tatizo bila kulizungumzia ni kutatua, hiyo si kweli na hali kama hiyo haileti afya ya ndoa bali ugonjwa na matokeo yake ndoto ambazo mtu alikuwa nayo kuhusu ndoa huyeyuka kama barafu lililokutana na jua la mchana.

Kanuni muhimu katika kuhakikisha ndoa inakuwa imara ni pamoja na kila muhusika kujitoa na kuelekeza jitihada za kuhakikisha kila siku anawekeza ili ndoa kustawi.

jambo la msingi ni kuwekeza katika mawasiliano bora

Mawasilinao katika ndoa au mahusiano yoyote ni kama gundi inayounganisha ndoa.


Na ikitokea hiyo gundi ikaacha kufanya kazi basi mahusiano au ndoa huanza kukatika vipande vipande, na ndoa bila kuwasiliano lazima itakufa.

Katika jamii nyingi za kiafrika watu hawapo wazi sana kujieleza kile anahitaji kutoka kwa mwenzake

Sema kile unataka bila kuzunguka.

Kama hujaridhika na style za sex za mpenzi wako sema ili ajue unataka kitu kipya, kama hujaridhika na chakula anachopika sema ili msaidiane na kuona inakuwaje, watoto, huduma kanisani maana wengine ni kanisani tu na mambo ya nyumba hana mpango, ndugu, kama hujaridhika na jinsi anavyotumia pesa sema ili ajue.

Kubaki kimya na kudhani atajua mwenyewe hata kama utahuzunika hatakuelewa eleza wazi ili kujenga ndoa yako.

hakuna njia nyingine zaidi ya ninyi wawili kuelewana na kukaa pamoja kupata jibu.

Kama unahitaji kitu Fulani kutoka kwa mwenzi wako sema nahitaji kitu Fulani, na kama kuna kitu Fulani anafanya wewe unaona kinakuletea shida mwambie kwa upole na moyo wa upendo na pia mwambie kwa nini unaona kinakuumiza kubaki kimya ni kama bomu ambalo linasubili muda na muda ukifika litalipuka.


Kama unahitaji muda wa kujibakia mwenyewe tu kufikiria mambo fulani fulani sema ili mwenzako ajue ila si kuwa mkali na kufukuza watu bila kusema kulikoni;

kuna wakati binadamu huhitaji awe yeye mwenyewe na Mungu wake, muhimu mawasiliano.


Huishi na malaika kwamba atajua kila kitu ambacho wewe unapenda au hupendi

Ndoa ni kujengana kila iitwapo leo


Na kama mwenzi wako anakasirika kwa kile umemwambia inawezekana hajakulewa so unahitaji kurudia kumwelekeza vizuri hadi aelewe kwa upendo na hekima.

Jinsi tunavyowasiliana tunatiofautiana kijinsia na kimalezi na ni muhimu sana kuwa makini kusoma lugha ya mawasiliano ya mpenzi wako.


Wanaume mawasiliano yetu ni ya moja kwa moja na wanawake mawasilino yao yanabebwa na hisia na wao ndo wanaoumizwa sana

Pia si busara kuongea na mpenzi wako kwa hasira kwani hasira wakati mwingine husababisha

Kulia machozi,

Kupiga au kupigana,

Kutupa vitu hata kama ni vya thamani kama simu za mikononi, vyombo nk,

na wengine hubaki mabubu na kushindwa kuongea.


Ndoa zote imara zina kitu kimoja kinachofanana nacho ni

Mawasiliano mazuri.

Na bila kupinga ndoa zenye matatizo nyingi matatizo huanzia kwenye

Mawasiliano mabaya.

Mawasiliano ni pamoja na

Kuwepo wakati wa maongezi,

Kumsikiliza mwenzi wako anapoongea,

na kusema kila unachohitaji kwa mwenzako.


Msingi Hasa wa Mawasiliano Katika Mahusiano Yoyote ni Katika Mambo Makuu Matatu

(a) Uwepo katika maongezi kwa mpenzi wako, upatikanaji wako pale mwenzi wako anataka kuongea kitu.

Wote mnahitajika kuwepo katika maongezi tena kwa kuhusika vizuri kwa lile linalozungumzwa.

Pia wewe unayetaka kuongea hakikisha mwenzi wako yupo tayari kukusikiliza siyo kulazimisha akusikilize wakati unajua anafanya kitu kingine muhimu tafuta muda muafaka.


(b) Msikilize kwa makini mwenzi wako na kama huna muda wa kusikiliza mwambie ni wakati gani utakuwa tayari na utasikiliza kwa makini kuliko kusikiliza huku unafanya kitu kingine.


(c) Husika katika mazungumzo au maongezi, hakikisha mwenzi wako anapata hisia kwamba unasikiliza na unajali pia unachangia kile anaongea na ongea kwa upendo, ukaribu kwani anayeongea ni mtu muhimu sana kwako hapa duniani.

Pia uwe wazi kueleza hisia zako na mawazo yako halisi kuhusiana na lile mnaongea


Mambo ya kufanya na kutokufanya wakati mnawasiliana
Lenga katika kutatua tatizo siyo kushinda mjadala au mabishano

Hakikisha unamsikiliza mwenzi wako vizuri na unaelewa ana maanisha kitu gani

kwani wanaume wengi hata kabla mke hajamaliza kuongea tayari tunadakia “nilikuwa najua unataka kusema hivyo”

Jieleze vizuri kama hujaelewa kuliko kujidai umeelewa then ukafanye sivyo

Heshimu mawazo ya mwenzako hata kama huwezi kupata jibu sasa kwa tatizo alilokwambia; kuliko kutoa majibu ambayo huishia kumkatisha tamaa mwenzako

Tumia muda mwingi kufanya maongezi kujadilia mambo unayodhani ni ya msingi kuliko kutumia muda mwingi kuongea kile ambacho si muhimu na kuacha kile ambacho ni muhimu

Kuwa mwepesi kusamehe na mwepesi kusahau pia, hakuna nafasi ya kitu kinaitwa "Nimekusamehe ila sitasahau."

Uwe mwangalifu lugha yako au maneno yako na body language kwani unaweza kuwa unaongea kitu kingine na mwonekano wako ni kitu kingine;

Ongea kile unamaanisha; wengi hupenda kulalamika badala ya kuongea kile anataka.

Usiende kulala kabla ya kutatua tatizo, Usilale na gubu au donge moyoni hakikisha umeliyeyusha kabla hujalala.

Usiongee na mpenzi wako kijeuri au kihuni au bila heshimu au kibabe hasa wanaume.

Usimlaumu mwenzi wako mbele za watu.

Unapotoa maamuzi yoyote usitoe kwa hasira

Usianze mjadala kwa kukumbushia mambo yaliyopita zamani hasa wanawake


Usidhani mwenzi wako anakuumiza kwa sababu hakubaliani na wewe inawezekana yupo sahihi hivyo mpe muda.

1 comment: