Thursday, 6 August 2015

KUFICHA SIRI..!

"Ndoa ni institution ambayo ni takatifu na hujengwa kwa msingi wa kuaminiana.
Huu msingi wakati mwingine hujikuta una hofu ya kubomoka na kusambaratika kwa vitu vidogo vidogo kama suala la siri katika ndoa.

Siri katika ndoa huweza kuharibu msingi wa ndoa ambayo imejengwa vizuri na kuonekana mbele za watu ipo imara.
Ni kweli inawezekana mke wako au mume wako hatakiwi kujua kila kitu kuhusu wewe vile umefanya ana unajua kila siku inayopita duniani hata hivyo ukiangalia kwa undani zaidi siri unazoficha kwa mume wako au mke wako zinaweza kukupeleka pabaya.
Iwe siri nzuri au siri mbaya kumbuka kwamba inaweza kuweka madoa mabaya sana kwenye ndoa yako.

Jambo la kujiuliza ni je, kwa nini unaficha hizo siri?
Kumbuka kiapo (vow) namna ulivyoahidiana wakati mnaoana kwamba ninyi ni kitu kimoja na kama unajikuta unajitahidi kuficha siri basi unaelekea kwenye big trouble.

Je, unaficha matumizi ya pesa?
Kumbuka siri katika ndoa mara nyingi ni hatari kwani itafika siku utaangukia pua, kwa mfano kama unaficha namna unatumia pesa na madeni yanazidi kuingiliana ipo siku wanaokudai watakuja kuuza nyumba ndipo mke au mume atajua kulikuwa na tatizo na utakuwa umeshachelewa!
Inawezekana unamficha mchumba wako kwamba huna mtoto wakati mtoto unaye, siku akigundua hata kama mmeoana miaka 5 au 10 gharama ya kurudisha trust itakuwa kazi ya ziada, Utajuta!

Inawezekana unaficha siri kwamba mtoto uliyenaye si wa huyo mume wako na umeamua kula jiwe, hata hivyo siku akigundua hapata tosha!

Je, ni siri kiasi gani unamficha mke wako au mume wako au mpenzi wako?
Kumbuka mahusiano ya kweli hujengwa kwa trust, kuficha siri ni moja ya bleach ya trust na zaidi kuliko yote hakuna siri duniani.

No comments:

Post a Comment