Wednesday, 5 August 2015

EPUKE HAWA,UNAPOTAFUTA MWENZI WA MAISHA YAKO.

Nyumba ikijengwa kwa msingi imara huweza kusisimama kila aina ya dhoruba, hata suala la mahusiano ni kitu kilekile ukijichanganya wakati wa kutafuta mchumba utaishia kwenye ndoa inayochanganya.
Hata hivyo ni muhimu sana kuwa makini na ishara ambazo unaziona kwa yule unaamini anaweza kuwa mke au mume baadae.

Je, yafuatayo ni sehemu ya maisha yake?

Msumbufu:
Anasumbua ingawa ana kazi nzuri.
Jinsi mtu anavyokufanya ujisikie ukiwa naye ni muhimu mara mia kuliko vile asivyokuonyesha ukiwa naye.
Hii ina maana kama ni msumbufu itafika mahali utamchoka hata kama ana kazi nzuri.

Mficha vitu:
Ingawa umekuwa naye kwa muda mrefu lakini unajiona humfahamu yeye halisi.
Anakuficha mambo mengi kuhusu yeye na kila kitu kuhusu yeye.
Anayefaa anakuwa wazi, anakushirikisha mambo mazuri na mambo mabaya yanayotokea katika maisha yake.
Anakwambia vitu vinavyomhusu yeye mwenyewe bila wewe kuchunguza.

Ahadi tupu:
Anaendelea kukuahidi na kukuahidi kwamba atafanya hivi na vile, ila ukimuuliza ni kwanini hatimizi anatoa sababu zaidi ya mia moja na moja.
Anakuahidi kukununulia gari wakati yeye mwenyewe anatunzwa.
Anakuahidi kukutafutia kazi wakati yeye mwenyewe hana kazi.
Ipo siku hasira na kukatishwa tamaa kutakufanya ujute.
Kumbuka anayefaa anatimiza ahadi zake na anayetimiza kile anasema na kuahidi anafaa zaidi kuliko yule wa maneno matupu na asiye timiza ahadi zake.

Mtu wa kupenda sifa:
Kawaida mtu mwenye hekima na busara husifiwa na wenzake na asiye na busara (mjinga) hujisifu mwenyewe.
Matokeo ya kujipa sifa mwenyewe inafika mahali anadharauliwa na kuonekana mtu mdogo sana asiye na maana.

Mtu wa kulaumu:
Kila kitu kibaya kikitokea anakulaumu wewe; mtu wa aina hii hajui responsibility ni kitu gani.
Hata kama ni yeye amefanya makosa atapindisha ili uonekane wewe ndiye uliyekosa.
Hupenda kulaumu kila kitu kama vile chakula, ndugu, marafiki, hali ya hewa, Rais, Boss wake, jua, baridi, mvua nk.

Mwongo:
Kama ameweza kukudanganya jambo kubwa, basi ujue upo na mtu ambaye hushughulikia mambo makubwa kwa kudanganya.

No comments:

Post a Comment