Tuesday, 18 August 2015

NI PENZI AU PESA?

Huwezi kuongelea mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia penzi kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.

No comments:

Post a Comment