Wednesday, 5 August 2015

JINSI YA KUISHI NA MAMA MKWE..

Kuna mabinti wengine wanapoolewa wanakuwa na busara na hekima jinsi ya kuishi na mama mkwe.

JINSI YA KUWEKA MIPAKA NA MAMA MKWE

Kila binti ambaye anatarajia kuolewa au ambaye ameolewa mara nyingi likitajwa neno “Mama Mkwe” hupata mshituko kidogo hasa jamii zetu za kiafrika ambazo bado mtoto wa kiume mara nyingi humsikiliza sana mama yake katika maamuzi mengi ya kwenye ndoa yake kuliko mke wake anayeishi naye.
Wanawake wengi walio katika ndoa mpya hupata wakati mgumu sana pale wanapoona mama mkwe anakuwa na uwezo wa kum-control mume wake na matokeo yake utani wa jadi unaanza (vita) kati ya mama mkwe na binti na wakati mwingine huleta mvurugano mkubwa kabisa wa ndoa.
Wakati mwngine matatizo ya mama mkwe huanzia tangu kijana wa kiume anapotoa taarifa kwamba amepata mchumba kwani wazazi nao wakati mwingine huwa wanataka uoe mke wanaotaka wao na kitendo cha wewe kuoa mke wa aina nyingine tayari vita huanza.

Pia wakati mwingine matatizo kuanza wakati wa maandalizi ya harusi kwa mama mkwe kutaka wanandoa wafanye anavyotaka yeye.

Kitu cha msingi ni kwamba wewe binti siku ya harusi ni siku yako na siku maalumu kwako si siku yake hivyo akuache wewe na mume mpange jinsi mnavyotaka siku yenu iwe.


Kwa kila mahusiano iwe urafiki, iwe ndugu, iwe mashemeji ni muhimu kuwekwa mipaka ambayo haipaswi kuingiliwa ili mahusiano yawe mazuri na yenye mafanikio.

Kila mafanikio huwa na siri basi hata kuishi vizuri na mama mkwe kuna siri zake muhimu ambazo ni kama ifuatavyo.

UPENDO NA KUCHUKULIANA
Mama mkwe ni mama ambaye bila yeye huyo mume uliyenaye usingempata, hata kama ungeolewa na mwanamke mwingine bado hata huko ungepata mama mkwe ingawa asingekuwa yeye.

Na pia kama unahitaji mahusiano bora na familia imara basi mahusino mazuri na mama mkwe ni muhimu sana.
Hata kama hapa mwanzoni mama mkwe unaona anasumbua au haeleweki, jitahidi kuwa naye karibu kwa upendo na upole na kuchukuliana wakati unamsoma tabia zake.

ONGEA NA MUMEO
Wapo wanawake ambao baada ya kuolewa tu kasheshe zinaanza na mama mkwe, Kitu cha msingi ongea na mumeo kama unahisi mama mkwe anaingilia ndoa yako, maana umeolewa na mwanae siyo ukoo, hata kama mumeo alichangisha michango kwa ukoo mzima ili kulipa mahari kwani hiyo wewe haikuhusu, muhimu yeye ni mumoe na ni wako peke yako.
Kuwa na mawasiliano na mumeo ni jambo la kwanza au hatua ya kwanza kabisa kupambana na matatizo ya mama mkwe.

Likitokea tatizo usibaki nalo moyoni eti kuogopa mumeo asijue, ndoa nzuri ni ile ambayo mwanamke unakuwa huru kueleza hisia zako kwa mumeo bila woga wala kuogopa hata kama zitaleta maumivi muhimu usitunze siri moyoni.

MUME MWENYEWE
Kama limejitokeza tatizo kati ya mke na mama mkwe basi mume anatakiwa kuchukua hatua kama kweli anajali mke au anajali ndoa yake.
Kuna wanaume ambao husikiliza zaidi mama zao hata kama waongo na hawasikilizi chochote kutoka kwa mke wake.
Kuna wanaume ambayo mama zao huongoza ndoa zao kwa remote.
Katika maamuzi mengi mke akitaka kujua utasikia mume anasema
"Mama amesema"
Hiyo ni mbaya sana na huwaumiza sana wanawake wengi kwenye ndoa. Yaani mwanaume unashindwa kuwa na maamuzi hadi mama aseme kwani wewe bado mtoto mdogo wa shule?
Mwanaume ndiye unatakiwa kumtetea mke wako na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoa inakuwa na amani na mwanaume ndo mtu wa kuchukua hatua kuongea na mama yako kuweka mambo sawa.

UMOJA
Wakati mumeo anaongea na mama mkwe ahakikishe ana present issue kwa umoja yaani aongee kwa maana kwamba ni wewe na yeye na kwamba kama kuna tatizo mama mkwe analeta, basi mnaumizwa wote wewe na mume na si wewe peke yako.
Kwa mfano badala ya kusema
‘Mke wangu anatatizo”
anatakiwa kusema
“sisi tunatatizo”
au
"mimi na mke wangu tunatatizo”

UWE WAZI NA MKWELI
Uwe muwazi na mkweli jinsi unavyojisikia kwa mama mkwe wako kwani kama unajisikia unahitaji kuwa na muda zaidi na mume wako, basi mwambia mama mkwe kwamba unahitaji muda na mumeo. Pia unapoongea na mama mkwa unahitaji kuongea kwa hekima na busara ili usimkwaze. Unaweza kumwambia jinsi unavyofurahi kuwa katika familia yake na jinsi unavyofurahia kuwa naye ingawa pia unahitaji muda na mumeo peke yenu.

WEKA MUDA
Kama unaishi na mama mkwe nyumba moja unaweza kupanga muda maalumu kila siku hasa kama unafanya kazi na hushindi hapo nyumbani. Weka muda ili wewe na yeye muongee pamoja ili msiingiliane muda wa wewe na mumeo na yeye na mtoto wake (mumeo)

MFANO
Kabla ya kuoa kaa na wazazi wako kuwaeleza kwamba wasitegemee kwamba utaoa mke wanayetaka wao badala yake utaoa mke unayemtaka wewe mahali popote duniani.
Pia mke awe wa kwanza kwako, kisha wazazi, ndugu zako mliozaliwa tumbo moja, ndugu na rafiki zako.
Wasipomheshimu mke wako maana yake hawajakuheshimu wewe. Wakimuheshimu mke wako maana yake wamekuheshimu wewe

No comments:

Post a Comment