Tuesday, 18 August 2015

NI HATARI KUWA NA NDOA ISIYO NA MAONO.

Wapo wanandoa ambao ndoa yao ipo kwenye hatari kwa kuwa hawana vision au dreams za ndoa yao au mahusiano yao yaweje au iwe na pattern ya aina gani.
Wanaingia katika ndoa au mahusiano huku wakiwa hawana picha kamili ya ndoa yao itakuwa vipi na wengine hali ni mbaya kwa kuwa mume anatofautiana na mke kwa kila wanalofanya au tenda na kuwaza.
Hii haijalishi wamesoma kiasi gani au hawajasoma kiasi gani, haijalishi wana uwezo kifedha kiasi gani au ni masikini kiasi gani bila maono ya ndoa waliyonayo ni kuangamia.
Bila maono au ndoto ndoa huwa mfano wa wajenzi wawili wa nyumba moja huku kila mmoja akiwa na ramani yake.

Mwingine ana ndoto au maono ya kuhakikisha anakuwa karibu na mwenzake (closeness/intimacy/romance) na akipata hivyo kwake ndo maana ya kuridhika na ndoa, mwingine ndoto zake au maono yake ni kila kitu kifanywa kwa wakati wake bila kukosea na maono au ndoto za kuwa na watoto 12 na akipata hivyo basi kwake ndo kuridhika na ndoa.
Kwa kuwa kila mmoja ana maono ambayo ni yake peke yake basi kutotimizwa kwa hayo humfanya kujiona yupo frustrated na ndoa.

Bila kuwa na maono au ndoto ya ndoa yako, maono ambayo yanakuwa shared na mwenzi wako huweza kupelekea kuanza kuwekeza energy kidogo sana kwenye ndoa yako.

Hapa tunazungumzia maono ambayo ni correct kwani kuwa na maono ambayo si correct ni sawa na kutokuwa na maono kwani ni sawa na kuwa vipofu na kipofu akimuongoza kipofu mwenzake wote huishia kwenye shimo na kupotea.


Mahali pasipo na maono, watu huangamia, bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

No comments:

Post a Comment