Saturday, 5 March 2016

UPENDO WA NDANI..

Mapenzi katika ndoa huweza kugawanywa katika sehemu mbili yaani upendo wa ndani na upendo wa nje.

Tunapozungumzia upendo wa ndani tuna maana jinsi tunavyoonesha katika emotions kama vile tendo la ndoa, kuwa pamoja karibu (intimacy), pamoja kimawazo, kujieleza katika feelings, maneno matamu yanayoonesha kujali na kupenda, kupeana busu, kukumbatiana, kupeana zawadi nk.

Tunapozungumzia upendo wa nje huu hujikita zaidi katika huduma kama vile kupika chakula, kuzaa watoto, kujenga au kukarabati nyumba, kufua nguo, kupiga pasi nguo, kuogesha watoto na kazi (ajira) ambazo zinatupa vipato.

Hapo zamani (mababu na mabibi) wao upendo external ulikuwa na maana zaidi kuliko internal na kizazi cha leo ni kinyume chake.

Ndiyo maana ni rahisi sana leo kuishi kama mke na mume zaidi ya miaka miwili na ikafika siku mke au mume akamuuliza mwenzake
“je, unanipenda?”

Hata kama wamefanikiwa kujenga nyumba au kuwa na gari au familia na maisha mazuri kwa ujumla.

Kuuliza je, unanipenda ina maana something is wrong kwenye upendo wa ndani (internal) inawezekana ni tendo la ndoa (love making) au ukaribu kimapenzi (intimacy) au maneno ya kutia moyo na sifa kimoja au vyote havipo sawa.

Leo wanawake wanategemea sana mume alete zawadi kuliko kuleta mkate.
Mke anataka mwanaume ambaye anaongea maneno matamu na si anayefanya kazi nzuri tu.

Mwanaume kiasili ni bread winner na anapenda mke atambue kwamba kwa kazi anayefanya maana yake anampenda mke na familia sasa baada ya kazi kutwa nzima na kurudi nyumbani na mkate na mke akamuuliza
“Je, Unanipenda?"
Eti kwa sababu asubuhi wakati anaondoka hakuaga kwa busu na hug kwa mwanaume bado ni kitu kinachoshangaza.

Hata hivyo industrial revolution imeleta mabadiliko ambayo wanaume na wanawake wote sasa wanafanya kazi (mchanganyo wa duties na responsibilities za mke na mume) na leo tupo kwenye information society kwa maana kwamba information zina flow ajabu na kila mwanandoa anataka Mapenzi (romance/intimacy) bila kujali sana kazi anayefanya mwenzake.

Je, siri ya ndoa imara ni ipi?

Siri ya ndoa iliyobarikiwa na imara ni ile inayohakikisha upendo wa ndani unaenda sawa na ule wa nje, ni ile ndoa ambayo inachanganya tendo la ndoa na majukumu kuwa kitu kimoja na kukipa nafasi sawa.

Mwanandoa halisi ni yule ambaye leo anaweza kumsaidia mwenzake anayeumwa kwa kufuta matapishi yake na baadae akaendelea kumpa kisses za kutosha.

Mke halisi ni yule anayeweza kuwa mama mchana na kuwa mpenzi usiku chumbani na kumfurahia mume wake kimapenzi kwa kwenda mbele.
Ndoa iliyo imara ni ile ambaye wanandoa ni waaminifu katika kutekeleza uhitaji wa ndani na nje katika ndoa.


posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment