Thursday, 10 March 2016

MWANAMKE KUKOSA HAMU.

Linapokuja suala la mapenzi, upendo na ndoa asilimia kubwa ya kila binadamu huwa na ndoto kubwa.
Hata hivyo hizi ndoto wakati mwingine huyeyuka pale mtu anapokutana na mambo ambayo ni kinyume chake mojawapo ni mwanamke au mwanaume uliyenaye kuwa baridi kabisa linapokuja suala la tendo la ndoa ukiongelea sex tu ni wa baridi na pia hafurahii kabisa tendo la ndoa.
Mwanamke kuwa wa baridi na kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa na kushindwa kabisa kufika kileleni au mwanamke kuwa baridi kuhitaji mapenzi, kukosa moto wa kutaka mapenzi.
Mambo mengi sana husababisha mwanamke kuwa na frigidity mojawapo ni:-
HATIA-Wapo ambao kutokana na malezi ya dini na jadi zao wamedumazwa na mafundisho kwamba sex ni uchafu na dhambi hivyo wakiingia kwenye ndoa bado hujisikia ni dhambi na uchafu pia mwanamke huwa na wakati mgumu sana kubadilisha gear na kujisikia sex ni haki yake na ni baraka ambazo Mungu amewapa wanandoa.

Pia huyu mwanamke anaweza kuwa na mzigo wa hisia na kuumizwa kama vile kubakwa au kunajisiwa wakati mtoto au kabla ya kuolewa hivyo akikmbuka tu mwili unakuwa barafu kuhusu sex.
Pia inawezeana mwanaume aliyenae anamuudhi sana na kumtesa na mwanamke hujisikia hatia kwamba amedanganywa kuingia kwenye hiyo ndoa na matokea ana freeze kabisa kuhusu sex.
Au inawezekana wameoana baada ya kudanganya wakat bado hawajaoana na kwa kuwa walidaganya na mimba ikapatikana na wakaozeshwa kwa nguvu sasa mwanamke haridhiki na mwanaume so anajisikia ama kauziwa mbuzi kwenye gunia hivyo hisia za mapenzi kwa mwanaume zimekufa.

HOFU, MASHAKA NA WASIWASIInawezakana mwanamke anapata hofu na mashaka au wasiwasi na kuumizwa (uke) na mwanamke hasa kama mwanaume yupo rough katika technic zake za mahaba.

Pia inawezekana uke ni mkavu kiasi cha kumuumizwa.
Pia kama mwanaume ana maneno ya kutisha na kukatisha tamaa wakati wa mapenzi au badala ya kuwa tender yeye anakuwa na hard.

Wanawake huwa na hofu hasa kutokana na mwanaume kuwa ignorant kwenye suala zia la tendo a ndoa kiasi kwamba wanamke hujikuta amejawa na hofu na mashaka kwani mwanaume hana uhakika na kile anafanya.

Wanaume wengi hujifanya wanajua kila kitu kumbe si hivyo na ukweli wanawake hujua zaidi na kwa kuwa wakionesha wanajua wataulizwa nani kakufundisha na matokeo yake ni balaa.
Pia wapo wanawake ambao hujiweka kwenye kundi la zero linapokuja suala la mahaba pia inawezekana ni kutokana na jinsi mwanaume anavyomkandia kwamba hajui.

Pia inawezekana mwanamke anatumia Tv, films, movies na media zingine kupima uwezo wake kitandani sasa akishindwa hujiona failure na matokea hukosa libido.
Dunia ina vipimo vyake ya kuonesha unajua sex hata hivyo hujaitwa kuja kwenye ndoa kujilinganisha na vipimo vya dunia (world sex performance standars) bali kumridhisha mumeo. Muhimu ni ku-focus kwa mumeo au mkeo na si kujilinganisha na masuperstar wa sex duniani.

Pia mwanamke anaweza kuwa frigidy pale anapokuwa na hofu hasa akiwa anahisi kuna watu wanawaona au wanachungulia au watoto wanawaona au watu wanasikiliza wakati wa sex hasa kutokana na mazingira ya chumba cha mahaba kilivyo, wanaume wengi huwa hawajali ila kwa mwanamke ni issue nzit sana ambayo huwezakufanya awe wa baridi.
Kumbuka privacy is a basic need to sex
Pia mwanamke anaweza kuwa frigidy hasa kama anakuwa na hofu ya kupata mimba hasa kama mimba yake huishia kwenye miscarriage, hivyo emotions zake huwa zimeumizwa kiasi kwamba zina overrule hamu ya sex na mwili kuwa baridi kabisa kuhusu sex.Pia inaweza kuwa ni stress, anxiety, depression.
Pia inaweza kuwa hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaaa.

Nini tiba yake? Tiba halisi kama una tatizo la kuwa baridi kuhusu tendo la ndoa ni kuwaona washauri wa saikolojia au madaktari wa taaluma za wanawake na sex.

No comments:

Post a Comment