Thursday, 3 March 2016

UPENDO HUU KATIKA NDOA..

Tumeona kwamba mwanamke anatakiwa (lazima) amheshimu mume ili mume naye ampende na matokeo yake kila mmoja aridhike na mwenzake na hatimaye kuwa na uhusiano mzuri idara zote.

Mke anahitaji mume anayempenda na kumuonesha upendo kuanzia asubuhi, mchana na jioni wakikutana mume anahitaji kuwa karibu na mke wake ili mke ajisikie anapendwa na hatimaye ajisikie relaxed na kuwa tayari hata kwa activities zingine usiku.

Je, mume kuwa karibu na mke wake ina maana gani?

Maana ya kuwa karibu kwa mke na mume ni kuambatana, shikamana, kushikana, ng’ang’aniana, fungamana, kaa jirani jirani, songamana, karibiana, kuwa pamoja (cleaving, cling or intimate)
Kuwa karibu ni kuungana uso kwa uso na kuwa mwili mmoja.
“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”.
(Mwanzo 2:24)

Katika uimbaji wa Mungu ni Binadamu peke yao ambao huweza kuwa karibu kimapenzi (sexual intimate) uso kwa uso.
Kuambatana kati ya mke na mume ni zaidi ya kuwa mwili mmoja.
Kuambatana kwa mke na mume ni kuwa karibu au mwili mmoja kiroho na kimwili.
Kama wewe ni mwanaume inakupasa ufahamu kwamba mke wako hufurahia na kujiona anapendwa na wewe pale unapomkaribia na kufanya ajione unataka kuwa karibu kwa namna unavyomtazama, unavyomgusa, unavyomkumbatia, unavyotabasamu na kumbusu na kumwambia NAKUPENDA.

Katika ulimwengu wa sasa ni rahisi sana kwa mke na mume kuchukuliwa na kuwa busy na kujisahau kujenga ukaribu ambao ndiyo msingi wa mwanamke kujisikia anapendwa na mume wake.
Wanandoa wenye busara huchukua dakika si chini ya 15 kila siku wakikutana jioni baada ya kazi; huhakikisha kila mmoja anajihusisha na mwenzake kwa ukaribu wa kimaongezi na sharing ya information za namna siku ilikuwa kwao wote na matokeo yao jioni na usiku vinakuwa exciting.
Mke akirudi anataka connections, anataka involvement na mume, anataka face to face talks na Mume akirudi kazini anataka kupumzika hata hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuhakikisha anapata muda wa kutosha ili kufanya connection na mke na hasa kama unataka mambo yawe safi kuanzia jikoni, sebuleni hadi chumbani huo usiku pia usigande kwenye TV au Gazeti bila kuongea na mke wako na kusaidia kazi ndogondogo hapo nyumbani.
Kuna ubaya gani kama utakuwa unapiga story na yeye anaandaa dinner au na wewe unasaidia kupika (kama hamna wafanyakazi wa ndani)

KUMBUKA KUWA KARIBU NA MKE SI GHARAMA BALI MUDA:

Mke atafurahi kama mara kwa mara:
Utamshika tu mikono,
Utamkumbatia na kumbusu wakati wowote,
Unapokuwa affectionate bila wazo la sex,
Kufanya kitu kinachosaidia kuwa na “togetherness”
Pale unapomwambia unampenda, yeye ni mwanamke mzuri (mrembo).
Kumbusu mke kwa sababu unataka sex tu ni turn off.
Pale mnapoangaliana na kupeana story zinazowafanya kuwa na kicheko.
Unapotumia muda wa kutosha kuwa na yeye katika kazi ndogondogo kama kupika, kufua nguo, kuogesha watoto, kusafisha nyumba nk.
Pale unapomfanya ajisikie unafurahia kujadili vitu mbalimbali na yeye.
Pale unapoendelea kuongea naye, au mkumbatia na mbusu baada ya tendo la ndoa.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment