Sunday, 13 March 2016

MISINGI YA NDOA.

Wataalamu wa masuala ya ndoa (marriage experts) walikaa pamoja kujadili misingi muhimu ya ndoa ambayo wanandoa wakiifuata ndoa zao zitakuwa imara na zenye afya hadi kifo kitakapowatenganisha.
Misingi hiyo imeinamia zaidi kwenye imani ya Kikristo, ingawa mtu yeyote bila kufuata dini yake anaweza kuifuata na bila shaka ndoa yake itakuwa ya tofauti.

Kuna mambo mengi sana muhimu ya kufanya katika ndoa ili ndoa iwe imara na yenye mafanikio, hawa wataalamu walichambua yale ya msingi tu ambayo yakifuatwa basi vitu vingine muhimu katika ndoa inakuwa ndani yake.
Tumeshayaongea sana haya mambo hapa hii inaweza kuonekana kama kurudia, hata hivyo kuna kitu muhimu na kipya unaweza kukipata hapa.

Je, ni Misingi ipi hiyo?

1. MUNGU KUWA KIONGOZI WA NDOA.
Ndoa ambayo inaendeleza, ongeza, imarisha na kufurahia mahusiano na Mungu itakuwa na picha kamili ya Mungu.
Kila mwanandoa atakuwa na uhusiano mzuri na Mungu na atajitahidi kuishi katika maadili ya dini na matokeo yake dhambi itakaa mbali na dhambi kukaa mbali basi upendo wa kweli wa kimungu huongoza ndoa.

Ndoa yenye msingi wa Dini huwa na maombi na maombi ni mawasiliano ya wanandoa na Mungu, hivyo kwa kuwa na connection kati ya Mungu na wanandoa, Mungu atakuwa anaipa stabilization ndoa yao kila wanapokutana na tatizo, shida au jaribu.

Unajua kuna siku shetani huwa anaamua kumpaka matope mmoja ya wanandoa ili asipendwe (unajisikia kutovutiwa na mwenzako), ni kwa maombi tu unaweza kuharibu kazi za aina hii za shetani si pesa, wala elimu wala ujanja.

Kwenye ndoa kuna good times na bad times na Mungu huweza kuwapitisha wanandoa vizuri kama wanamtegemea yeye, hilo halina ubishi ni amini na kweli.

2.UPENDO WA KUJITOA.
Maisha ya binadamu ni safari ndefu, si sahihi kwamba siku zote ndoa itakuwa na mapenzi yaleyale ya motomoto, au kupendana kule kule kama mwanzo, kiwango cha mahaba kupanda tu graph kila iitwapo leo; si kweli, kutokana na kuwa na malezi tofauti na mambo mengine inawezekana ndoa kupita kwenye wakati mugumu sana, kuna stress, kuna kukata tamaa, kuna business kufilisika, na kuna wakati tu inatokea mume na mke kila mmoja hampendi mwenzake bila sababu, hivi vyote vinahitaji watu wenye Upendo wa kujitoa ili kurudi kwenye mstari.
Katika ndoa conflict na disagreement hutokea bila upendo wa kujitoa basi ndoa haiwezi kufika popote.
Kwenye ndoa hakuna mtu perfect wote bado tuna tumia Learner driving license kwa maana kwamba tunaendelea kujifunza na kutoa efforts za kuhakikisha ndoa inakuwa na afya na inaendelea kudumu na kudumu na kudumu.

Kuna utafiti ulifanywa kwa wanandoa waliopata talaka, asilimia 40 walisema wanatamani kurudi kwenye uhusiano wao wa kwanza, hii ni kuthibitisha kwamba wangekuwa na upendo wa kujitoa basi wasingeamua kuomba talaka zao kwani kuna watu ambao conflict kidogo tu, tuachane!

Hawana dogo na wengine sasa kuoa na kuolewa ni kama shopping!

3. MAWASILIANO.
Utafiti unaonesha kwamba watoto wadogo wa kike wamebarikiwa sana (talented) na uwezo wa kuongea na lugha kwa ujumla , huweza kuongea haraka na mapema kuliko watoto wadogo wa kiume.
Hiyo tabia huendelea hadi wanapokuwa watu wazima na kwa maana hiyo wanawake na wanaume lipokuja suala la kuongea na mawasiliano kwa ujumla kuna tofauti kubwa.
Inajulikana kwamba wanawake huongea maneno kati 40,000 hadi 50,000 kwa siku wakati wenzao wanaume huongea maneno 15,000 hadi 25,000 kwa siku.
Hivyo basi wanawake ni viumbe wanaohitaji mwanaume kuuongea ili na yeye aongee hayo maneno yake, ndiyo maana kwa mfano kama umetoka kazini basi mwanamke anapenda sana umwambie mambo mbalimbali kama vile unafikiri kitu gani, nini kilitokea kazini, watoto wameshindaje, unajisikiaje kuhusu yeye mwanamke nk.
Wakati huohuo wanaume hujisikia sawa tu hata asipoongea chochote akifika nyumbani kutoka kazini matokeo yake mke anakuwa bored na hayo ni mawasiliano mabovu.
Wanaume kushindwa kuelezea hisia zao kwa wake zao ni kitu kinachowaumiza sana.

Panga muda maalumu kwa ajili ya maongezi ya maana na mke wako hata kwa kuwa na matembezi au outing.
Hata hivyo wanawake wanapaswa kufahamu kwamba kuna wanaume ambao hawawezi kuwa kama wanavyotaka wao kwani ndivyo walivyo.
Mume wako hataweza kukutimizia mahitaji yako yote kwani hakuna mwanaume duniani ambaye anaweza kumpa mwanamke vyote anavyohitaji, ndiyo maana hata wewe mwanamke mwenyewe hupo perfect mia kwa mia.

Kumbuka

Unapowasiliana na mume au mke;
Badilisha kile ambacho kinaweza kubadilishwa
Elezea kile ambacho anaweza kukielewa
Fundisha kila ambacho anaweza kujifunza
Patanisha kile ambacho anaweza kukubaliana
Rudia kile ambacho anaweza kukiimarisha.

No comments:

Post a Comment