Tuesday, 1 March 2016

MUNGU AMEKUWA KIMYA KWAKO?

Kila mmoja wetu, mimi, wewe na yule tunakutana na milima na mabonde, nuru na giza katika maisha yetu ya kila siku.
Hata hivyo jambo moja kubwa ambalo linatoa tofauti kati ya mtu na mtu ni namna tunavyochukulia namna Mungu anahusika na maisha yetu.
Hata baada ya juhudi ya kuomba na kufunga, kujitoa na kujitakasa mbele za Mungu na kuishi maisha ya uaminifu na utakatifu bado Mungu amekuwa kimya katika kujibu maombi yetu au kukutana na mahitaji yetu ambayo ni kilio chetu kwake kila iitwapo leo.
Katika Biblia kuna maelezo yanayohusu Lazaro na dada zake Maria na Martha, rafiki wa karibu wa Bwana Yesu katika kijiji cha Bethania.
Lazaro aliugua na akawa serious (naamini alipelekwa hadi ICU) na wakatuma habari kwa Bwana Yesu ili aje amfanyie maombi na ndugu yao apone; hata hivyo Bwana Yesu ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa hii familia hata baada ya kupata habari aliendelea na ratiba yake kwa siku mbili zaidi.
Lazaro akafa!
Naamini tafsiri ambayo Maria na Martha walikuwa nayo ni kwamba Yesu alikuwa Hawajali na kuwaona hawana maana.
(Yohana 11:1-10)
Fikiria walivyojisikia Maria na Martha kwa kitendo au kwa ukimya ambao Bwana Yesu aliuonesha kwao?
Fikiria huzuni waliyokutana nayo familia hii huko Bethania kwa Bwana Yesu kukaa kimya kwa siku mbili zaidi hadi mpendwa wao akafa?

Je, Mungu amekuwa kimya kwako?

Pamoja na kuomba bado Mungu amekuwa kimya na umefika Mahali unakata tamaa na kumuwazia Mungu vibaya?
Mungu yupo kimya kwa sababu anataka kutenda muujiza katika maisha yako, anataka kukuonesha ishara ambazo zitakufanya umtukuze yeye maisha yako yote.
Inawezekana Mungu amekuwa kimya kujibu maombi yako ya kutaka kuwa na ndoa yenye amani,maombi yako ya kutaka kuolewa, kazi, ndoa, shule, fedha, watoto, familia, elimu nk hata hivyo jambo la msingi unatakiwa kuwa makini sana namna una behave katika kipindi kama hiki kwani ni wakati wako wa kumjua Mungu ili kupokea baraka.
Mungu anataka kukuonesha Mpango kamili wa maisha yake kwako.
Tunatakiwa kumuamini, kumpenda, kumtegemea, kumsadiki na kumngoja Bwana hata akiwa silent.
Fikiria namna walivyofurahi baada ya Yesu kumfufua Lazaro siku nne baada ya kufa? Matumaini na kukua kwa imani na kutukuza matendo makuu ya Mungu?
“Trust in God stays strong even when He is silent”

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment