Tuesday, 8 March 2016

SEX KABLA YA NDOA..!

Sex kabla ya ndoa si sahihi na msimamo wangu ni kwamba kabla ya ndoa sex ni dhambi na kuna athari kubwa sana zinazopelekea kutokuaminiana na zaidi kusababisha ndoa kuanza kufa mapema.
Sipendi kuhukumu na kuwa mzungumzaji sana kwenye issue muhimu na personal kama hiyo, hata hivyo naweza kukushauri uende kwa kiongozi wako wa dini na muulize kama atakukubalia sex kabla ya ndoa na akikubali urudi uniambie ili nami niongee naye.

Nikupe mfano wa kweli
Neema ni dada ninayemfahamu anaishi Kinondoni Dar es salaam na alimpata mchumba Jimmy mwanaume wa miaka 40 naye anaishi Msasani jijini Dar es salaam, wamekuwa wanaenda wote sehemu tofauti na kujiona ni kweli kuna kila dalili ya kuwa mke na mume.
Kwa kuwa Neema ana miaka 36 kumpata Jimmy kwake ni kitu adimu na alijipanga tayari kuolewa kwani muda unaenda na nguvu ya uvutano ilishaanza kuvuta kwenda chini.
Jimmy alikuwa akimshawishi Neema walale wote kitanda kimoja mara kwa mara na Neema alikuwa anagoma na kumuahidi wasubiri hadi siku ya harusi.
Hata hivyo miezi miwili baadae, Jimmy alimualika Neema kwenye sherehe ya rafiki zake huko Msasani (jumapili) na sherehe zilichelewa kumalizika kitendo kilichopelekea Jimmy kuondoka na mchumba wake (Neema) na kwenda naye kwake.
Walipofika kwake (Jimmy) walikaa kwenye sofa wakaweka movie wakaanza kuitazama na hatimaye Neema akajikuta yupo kifuani kwa Jimmy.
Movie ikanoga, mara wakaanza kuwekeana miguu kila mmoja juu ya mwenzake, mara kushikana mikono, mara kukumbatiana, hatimaye kisses zikaanza, miguno ya raha ya mahaba ikaendelea kujikoleza, joto la mahaba likapanda na romance ikanoga na hatimaye wakajikuta wameingia ulimwengu mwingine wa kurusha kila nguo waliyovaa kusikojulikana, kilichoendelea Naamini unajua……
Asubuhi Neema akajikuta kile amefanya si kile alipanga na akarudi kwao huku amejawa machozi na mawazo maana hata kupima walikuwa hawajaenda.
Siku iliyofuata ilikuwa Jumatatu Neema akaamua kumpigia simu Jimmy na hakupokea na akaanza visababu.
Jimmy aliacha kumpigia simu Neema na hata baada ya Neema kulalamika na kuuliza kwa nini hapigi simu tofauti na nyuma kabla ya kupewa zabibu, Jimmy aliendelea kujibu utumbo kama si pumba.
Baada ya hapo Jimmy alipotea kabisa kwenye uso wa dunia na mbele ya macho ya Neema kwa namna yoyote.
Kuona hivyo Neema akaamua kupiga kiguu na njia hadi kwa Jimmy na kwa kuwa hakutoa taarifa alichokikuta ni Jimmy yupo kifuani kwa mrembo mwingine.

Kwa asili wanaume huwa na respect ndogo sana kwa wanawake ambao wameshalala nao, so kama unataka ndoa kaa mbali na sex kabla ya ndoa.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment