Thursday, 10 March 2016

NI VIZURI KUKAGUA MSINGI.

Katika kujenga au kusimamisha jengo lolote duniani kawaida kuna taratibu ambazo ni sharti zifuatwe ili jengo lisimame, liwe imara na lidumu.

Tumekuwa tukishuhudia majengo mengi yakiporomoka hii ni kutokana na kutofikia viwango hasa uzembe wakati wa kufanya ukaguzi wa ujenzi tangu msingi.
Pia hata kama jengo likiimarishwa juu wakati msingi ni ovyo au haujafikia viwango bado jengo zima lipo hatarini na haliwezi kufika mbali kwa sababu msingi hautaweza kuhimili kila aina ya dharuba, mitikisiko, upepo na wakati mwingine hata mvua.

Tunaporudi kwenye suala la mahusiano wakati wa uchumba ndiyo wakati wa kuchunguza msingi, ni wakati wa kufanyia inspection msingi kuhakikisha ni kweli una standards zinazotakiwa kuhakikisha jengo linadumu karne hadi karne.

Mtu unayechagua kuoana naye na kujenga maisha yako yaliyobaki hapa duniani ni vizuri akawa na imani, values, interest, standards, mitazamo unayoridhika nayo na kufikia uamuzi wa kukubali kupitisha hati ya kusaini kwamba msingi umefikia viwango vinavyotakiwa (engagement ring) ingawa bado unaweza kuahirisha ujenzi ukigundua kwamba bado jengo linaweza lisisimame kwani kuachana katika uchumba ni kiroho na pia afadhari kuvunja uchumba kuliko Ndoa.
Ni busara kuvunja msingi kuliko kumaliza jengo la ghorofa 25 then linavunjwa.

Wakati unaendelea na inspection ya msingi kama unaona kuna dalili na umethibitisha kwamba nyufa zilizopo zinaweza kusababisha jengo lisisimame, deal with it!,
Usifanye terrible mistake kwani kufikiria kwamba nitaishi naye hata kama ana matatizo hayo au hata kama hili ni tatizo ambalo nitasaidiana naye hadi nambadilisha; thubutu! kawaida hatuwezi na hatutaweza kumbadilisha mtu hata kama upo smart namna gani au una skills za ajabu za kushawishi, suala la ndoa na mapenzi ni gumu utajuta!

Binadamu ni wazuri sana kwa kutoa ahadi hasa katika mapenzi,ingawa ahadi nyingi ni kwa ajili ya kukupata wewe hivyo ni juu yako wewe kuamini kama kweli atakununulia gari wakati kazi hafanyi na mvivu, hana tatizo na dini yako wakati haitambui dini yako, atakupenda milele wakati juzi ulikutana naye ana kwa ana amekaa na rafiki yako katika mkao wa hasara uliotikisa moyo wako kiasi kwamba ile picha ikikurudia unajisikia he is the wrong person.
Anakwambia anakumiss wakati huohuo kuwasiliana na wewe hadi umkumbushe maana hakuna cha simu wala sms wala email wakati simu anayo.
Hapa unafanya uamuzi wa aina yake katika maisha yako na watu wanaweza kukushauri ila mwamuzi ni wewe.
Pia hata kama umeachwa na mchumba inawezekana huo ni muujiza wa kumpata aliyesahihi kwako hivyo usiumize kichwa.

“Don't cry for a man who's left you, the next one may fall for your smile.”

No comments:

Post a Comment