1. Kutokuheshimiana
Si vizuri kumtamkia maneno mabaya mwenzi wako mbele za watu.
Mke au mume anahitaji kuheshimiwa, kupewa asante kuwa appreciated na zaidi kumsifia mbele za watu na sivinginevyo.
Kuongea mambo mazuri kwa mke au mume wako mbele za watu ni muhimu sana.
Wapo wanaume hutukana wake zao mbele za watu na wapo wanawake hujibu mbovu waume zao hata mbele za watu au wageni. Kama kuna kitu amekuudhi kwa nini usisubiri mkaongee chumbani mkiwa wawili?
2. Kutosikiliza mmoja akiongea
Hii inajumuisha kuwa na mawazo ya mbali wakati mume au mke anaongea, yeye anaongea wewe unaendelea kuangalia TV, Unaendelea kusoma gazeti, unaendelea kusoma kitabu, Unaisikiliza laptop kuliko mume wako au mke wako.
Pia hii inajumuisha kuwa mbali kimwili (body language) wakati mwenzako anaongea, wapo wanandoa ambao hata mwenzake hajamaliza kuongea tayari anadakiwa kwamba najua ulichokuwa unataka kusema, pia wapo ambao hata ukiuliza swali yupo kimywa, mbaya zaidi ni pale unapoona na kuhisi mwenzako ana tatizo lakini ukimuuliza anabaki kimya au anakwambia hakuna tatizo, Inaumiza sana hasa kwa wenzetu wanawake ambao asilimia kubwa ya wanaishi kwa hisia, na kuumiza hisia zao ni kitendo kibaya sana, ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuliko unavyodhani.
3. Kukosa mahaba (sexual intimacy)
Ukiacha mke wako au mume wako anahangaika na kutoridhishwa kimapenzi maana yake unachimba shimo ambalo ukijifukia utatokea jehanam, na kama unaona umepoteza interest na sex fanya kila njia kupata ushauri na msaada ili urudi kwenye mstari.
Matatizo mengi ya ndoa zinazokufa huanza kwa ugonjwa wa kutoridhishwa kimahaba na mume au mke.
Kumbuka ndoto za watu wengi kuoana ni kupata mtu atakayemtosheleza kimapenzi.
4. Kujiona sahihi mara zote
Hii inajumuisha wewe kuwa ndo msemaji na muelimishaji wa mke wako au mume wako, yaani wewe ndo unajua kila kitu, upo sahihi siku zote, au bila neno lako la mwisho basi information haijakamilika.
Siku zingine kubali kwamba umekosea au huna jibu, hakuna mtu anaweza kufurahia kuwa na mtu ambaye siku zote yeye ndo yupo sahihi labda kama unaishi na mtu mwenye mtindio wa akili.
5. Kutokufanya kile unasema
Siku zote Imani bila matendo imekufa na Imani ni matendo, “Actions do speak louder than words”. Ukisema utafanya kitu Fulani, fanya.
Wanawake ni viumbe ambao hutunza sana ahadi tunazowapa, hivyo usiahidi kitu ambacho huwezi kufanya, kwani mwenzio anaandika kwenye ubongo wake siku akija kukutolea mahesabu ya ahadi hewa umefanya utaipata fresh, pia na wanaume (si wote) kwa ahadi hewa hatujambo, tujifunze kufanya kila tunachosema.
Tusitoe ahadi tamu kumbe hewa, unaumiza sana.
6. Utani unaoumiza
Kama mwenzio anakwambia utani wako unamuumiza achana nao, kuna utani mzuri lakini kuna wakati mnaweza kufikishana pabaya na lazima uwe makini kusoma saikolojia za mwenzi wako, kuna wengine anaweza kukutania wewe usikwazike, na utani huohuo ukimrudishia yeye anakwazika so be very careful usimuumize mwenzako.
7. Kutokuwa mwaminifu
Kudanganya na kuwa na siri zako binafsi katika mahusiano huweza kujenga wawili kuwa mbali na kutokuaminiana.
8. Kuwa mtu unayeudhi kila wakati
Inaweza kuwa ni mzembe, mchafu, mtu wa kuchelewa kila mahali, mtu wa kusahihisha kila kitu mwenzio anafanya, mtu wa kulalamika tu kila wakati kila kitu, kuwa kimya tu mwenzio akitaka muongee masuala ya ndoa au familia. Unajua unaushi lakini unaendelea kuudhi.
9. Kuwa mchoyo
Yaani unatumia pesa nyingi sana kwa mambo yako na mume wako au mke wako akitumia pesa kidogo tu kelele na zogo hadi nyumba inakuwa moto.
Hadi nyumba yako haipo friendly maana hata kuburudika kwa soda tu kwako ni issue wakati ukiwa mwenyewe unajichana ile mbaya na kuku kwa chips na kitimoto na watu ambao ni nje na familia yako, hiyo ni aibu!
10. Ukali kama pilipili kichaa
Kila mwanandoa anahitaji kuwa mstaarabu linapokuja suala la kutatua mgogoro wowote, wapo ambao tatizo likitokea mke au mume na watoto wanatamani kuhama nyumba maana hapakaliki, Ni kweli kwa kelele zako na mihasira yako unaweza kuwin huo mgogoro lakini mbele ya safari bado utajikuta ni wewe ndo umeharibu zaidi.
Sidhani kama kuna mtu anapenda kukaripiwa kama mbwa ndani ya ndoa

No comments:
Post a Comment