Tuesday, 14 July 2015

UKIWA "SINGLE" JIAMINI..

Ukijiamini una kuwa huru kimawazo na kutokuwa tegemezi kusubiri wengine wakupe furaha.
Ukiwa single unahitaji kujiamini kwani wewe mwenyewe ni chanzo cha furaha, upendo amani na maamuzi mbali mbali ya kila siku katika maisha yako.
Lakini linapokuja suala la sex wapo wanaothani kwamba kuwa na mtu ambaye una share naye mapenzi au sex unaweza kupata furaha ya kweli na na wewe kujiona mtu unayejua kutoa upendo kwa wengine.
Hii hupelekea kuwa tegemezi kimwili, hasa linapokuja suala la hisia zako na matokeo yake unakuwa target rahisi kwa partner asiye sahihi anayeweza kukuumiza moyo wako.

Kwa hiyo ufahamu na elimu ya kujiamini ni vitu muhimu sana vinavyoweza kukusaidia usiweze kupata maafa yanayoweza kukuangamiza na kuuumiza moyo wako kuuvunja vipande vipande hasa wakati huu ambapo unatafuta mwenzi wa maisha.

Kujiamini hujengwa kwa msingi wa mafanikio ya kitu kimoja kwanza.
Mafanikio huzaa mafanikio na kushindwa kuzaa kushindwa.
Tunapojifunza kitu kipya kama vile kuendesha gari mara ya kwanza huwa tunakuwa na hofu ya kushindwa na tukishaweza tunaendelea kujiamini na kuweza zaidi na zaidi..
Mafanikio madogo madogo ni ngazi za kupanda kupelekea mafanikio makubwa.
Kwa hiyo Kukosa kujiamini (self confidence) kunaweza kukufanya kuwa dhaifu katika hisia zako na maisha yako kwa ujumla.
Unahitaji kufahamu kwamba hata kama huna mwanaume au mwanamke bado maisha yanaweza kuwa ya furaha na yenye kukupa amani.

Kutojiamini kunaweza kukufanya upoteze nafasi nyingi katika maisha yako na pia Kukosa uwezo ulionao kujiendeleza na kufanya mambo makubwa katika maisha.

No comments:

Post a Comment