Wednesday, 15 July 2015

DALILI ZA NDOA INAYOELEKEA KUFA.

Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza.

Wanandoa wengi hujikuta wamefika mahali ambapo ndoa haiwezi kuwepo tena (talaka) na tatizo kubwa ni kwamba wengi hukaa bila kuchukua hatua zinazostahili (serious) wakati tatizo au mgogoro unapojitokeza ili kumaliza tatizo
Kutoshughulikia vizuri tatizo lolote kwenye ndoa hupelekea
Chuki,
Uchungu,
Kinyongo,
Kuumia hisia na
huweza kusababisha mwanandoa mmoja kujiondoa katika muungano wa kindoa uliopo
(kuanza kuishi kivyake katika kufikiria na kutenda).

Zifuatazo ni dalili mbaya sana ambazo zinaonesha ndoa inayoelekea kwenye kifo

KUFIKIRIA MAISHA KIVYAKO BILA MKE AU MUME KUMUHUSISHA
Ukiona unaanza kufikiria uzuri wa maisha utakavyokuwa bila mwenzi wako kwa maana kwamba kuwa na yeye unaona asilimia mia moja anakulostisha, au hana maana kabisa ni dalili kwamba hiyo ndoa inaelekea kwenye kifo cha ghafla.
Na kama unasongwa sana na mawazo kutaka kuishi mwenye au na mtu mwingine zaidi ya huyo uliye naye na kujiona utakuwa na amani zaidi basi unaelekea kubaya kwani inaonesha umeshapoteza nafasi yake ndani ya moyo wako na kitu cha msingi waone washauri wa mambo ya ndoa ili waweze kukusaidia.

MAMBO MABAYA NI MENGI KULIKO MAMBO MAZURI KWENYE NDOA YAKO
Kama mnajikuta ndoa yenu ina mambo mabaya mengi zaidi kama vile
kutokuelewana, k
ila mtu ana hasira,
mnapishana lugha kila mara,
hakuna kucheka wala kufurahishana na
mambo mazuri kama kucheka pamoja,
kufurahi pamoja,
kujisikia bila mwenzako siku haiendi
basi hiyo ni dalili kwamba hiyo ndoa inahitaji msaada na bila kuifanyia ukarabati basi itasombwa na mafuriko na hatimaye kufa.

UNAJISIKIA VIGUMU SANA KUWASILIANA NA MKE AU MUME WAKO
Je, unajisikia kupatwa na hofu au mashaka kuongea na mke au mume wako kuhusu matatizo ya ndoa yako au maisha yenu kwa ujumla?
Mawasiliano ndiyo njia pekee ya kuondoa stress za ndoa na maisha kwa ujumla na hatimaye kujenga ndoa yenye afya kwa wanandoa.
Kama mkiwa pamoja mnakuwa kimya bila kuongea chochote na hakuna dalili ya kutaka kuongea na mwenzako basi kuna tatizo kubwa sana, hasa kama ni tofauti sana na kawaida yenu hasa jinsi ilivyokuwa katika siku za kwanza wakati mnachumbiana.
Kama hujisikii vizuri kuwasiliana na mwanandoa mwenzio basi hiyo ni dalili kwamba tayari umekosa imani kwake na ndoa huwa inakuwa katika wakati mgumu kukiwa kauna kuaminiana (trust)
Pia kama wewe ni mtu wa mwisho kujua kitu chochote muhimu au kuzuri kuhusu yeye, basi hapo kuna tatizo kwani ni kawaida wanandoa kuelezana vitu vizuri vinavyotokea kwa mmoja wao.

KILA MMOJA KUKATAA KUHUSIKA NA MATATIZO AU MIGOGORO YA NDOA INAPOJITOKEZA
Kama kila mmoja anajilinda na kutothamini hisia za mwenzake hasa linapotokea tatizo na kuanza kumrushia mwenzake lawana kwamba ndiye muhusika na wote mnakuwa na msimamo huohuo, fahamu kwamba hapo ndoa inapitiliza hata tiba za uangalifu zinazopatikana ICU.
Ikiwa migogoro au matatizo yanapojitokeza kuna kuwa na kushindana kwa kila mmoja kukwepa kuhusika na badala ya kupata suluhisho mnajikuta mgogoro unazidi kuongezeka basi hiyo ni dalili kwamba sasa mmeanza kubusu kifo cha ndoa.

KUJIKUTA NI WEWE PEKE YAKO TU UNAHUSIKA KATIKA KUTATUA MIGOGORO AU MATATIZO YA NDOA.
Je, umekata tamaa, au kujisikia vibaya kuongea masuala ya matatizo ya ndoa yako kwa sababu mwenzako anakurudisha nyumba, au imefika mahali na wewe umeamua kunyamaza na kuachana kabisa na kujishughulisha na tatizo lolote katika ndoa na matokeo yake hakuna hata mmoja anajali tena kushungulikia matatizo ya ndoa?
Kama mpo kwenye matatizo na kila mmoja amenyamaza kimya katika kuhakikisha mnamaliza tatizo lililopo basi hii ndoa ipo ICU na kama mtabaki kimya bila kila mmoja wenu kuhusika ili kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari basi ni kama bomu lililotegwa ardhini na siku mtu akikanyaga hakuna kitakachosalia.

TENDO LA NDOA
Kama mmoja wenu sasa hana hamu kabisa na tendo la ndoa, au wote kwa pamoja hamna hamu kabisa ya tendo la ndoa hiyo ni dalili kwamba somethings is wrong.
Kukosa faragha ya pamoja (intimacy and affection) itawafikisha mahali ambapo ndoa inaweza kufa au kuwa na ndoa isiyokidhi haja au kukosa kuridhishana inavyotakiwa.
Je mnaishi tu kwa sababu ya watoto ndo wamewafanya msiachane?
Kama ni ndiyo basi mnahitaji kupata msaada wa washauri wa mambo ya ndoa kwani hakuna tatizo lolote kwenye ndoa ambalo halina jibu.
Kama hakuna hamu ya mapenzi kwa mmoja wenu au wote maana yake hisia zenu zipo mbali sana na hiyo ni dalili kwamba kila mmoja anaenda njia yake.

KUBISHANA AU KUGOMBANA KWA KITU KILEKILE KILA MARA
Kama kubishana, kupishana, kugombana, kuanzisha zogo kila mara kunatokana na issue ileile moja bila kupata suluhisho basi hiyo ndoa imesimama haikui wala kuelekea kwenye uimara zaidi bali inatelemka kwenda kwenye shimo.
Kama hakuna kitu kipya kinatokea ili kupata ufumbuzi wa hiyo hali basi tafuta mshauri wa mambo ya ndoa ili awasaidie.
HITIMISHO
Hakuna tatizo la ndoa ambalo halina jibu hapa duniani kuna washauri wa mambo ya mahusiano na ndoa, wazazi ambao hupenda mafanikio ya watoto wao, kuna wachungaji ambao wana hekima na busara walizopewa na Mungu kwa ajili ya kuwashauri hivyo hata kama kuna tatizo kubwa namna gani jibu lipo na tiba ipo.
Anza kwa kuzungumza na mwanandoa mwenzako then ikishindikana nenda kwa watu mnaona wanaweza kuwasaidia, usiwe mbishi wala mbabe ndoa ni kuchukuliana na kuelewana.

No comments:

Post a Comment