Tuesday, 14 July 2015

FAHAMU HAYA.

Kila Mwanamke ana ndoto za kufanikiwa maisha, kuwa na familia, kuwa na mume atakayempenda n.k

Ni hakika wanawake ni tofauti na wanaume, inawezekana hilo umelijua, kuna mambo ambayo wanaume hufanya kitandani na kumfanya mwanamke ajione ni mwenye furaha duniani na pia kuna wakati kuna mambo yanafanywa na wanaume kitandani na hupelekea mwanamke kujuta na kuumizwa hisia zake.
Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa na mwanaume akiwa chumbani kwani wanawake wengi wanakiri kwamba mambo madogo kama haya wakati mwingine huwafanya kujisikia vibaya hasa linapokuja suala la mahaba.

USAFI
Kuwa msafi ni msingi wa wa mambo yote kitandani, ni vizuri kuoga kabla ya kulala hata kama kuna matatizo ya maji lazima uweke bajeti yako vizuri kuhakikisha unaoga kabla ya kurukia kitandani.
Usafi ni pamoja na sehemu zote za mwili wako, mikono safi na kucha zilizopunguzwa vizuri, pia kunyoa ndevu vizuri, kuna wakati kidevu kikigusa mwili wa mwanamke humkwaruza na kumuumiza, labda uwe na mke anayependa kidevu kama cha Osama.
Pia wapo wanaume ambao huvuta sigara na bila kuwa makini huingia chumbani na harufu ya sigara huku midomo inanuka, hapo unaharibu kila kitu.


KUWEPO
Ni vizuri kuwepo kwenye tendo lenyewe na mhusika mwenyewe kiroho, kimwili na kiakili, kama upo kwenye tendo la ndoa mwanamke hujisikia vizuri kwa kuwa utashirikiana na mwanamke kwa kila hatua na atajiona ni sehemu ya utendaji.
Tamka jina lake, tamka maneno mazuri na kuonekana upo na yeye isiwe kama vile wewe upo na mashine fulani ya kukupa raha.
Pia wapo ambao anaanza then anaacha, mwanamke ni tofauti na mwanaume hivyo basi kama utaacha ujue lazima ukaanze square one from scratch.
Pia wapo wanaume wanajua kabisa mwanamke ni umbo dogo na yeye mwanaume ni umbo kubwa, sasa ukimlalia na kuendelea na shughuli bila kujua hapo chini anaendeleaje si anaweza akashindwa hata kupumua, wewe kuwepo ni pamoja na kujua na kumsoma anauonaje muziki wenyewe.

No comments:

Post a Comment