Friday, 26 June 2015

MUHIMU KATIKA NDOA.

Kama wewe ni kizazi cha Adam na Hawa basi suala la ndoa linakuhusu sana na ndoa ni kitu beautiful, Kwani huleta mahusiano ya kutosheleza yanayowaunganisha watu wawili mke na mume.
Inapendeza kwamba Mungu amemuumba mtu maalumu kwa ajili yako.

Kuna mambo muhimu ambayo wakati mwingine wanandoa wanatakiwa kuwa nayo.

10. UJUZI WA KUTATUA MATATIZO.
Kama wanandoa hawana ujuzi wa kutatua matatizo inaweza kusababisha ndoa kuwa ngumu sana hasa miaka 2 ya kwanza katika ndoa.
Kuwa na ujuzi wa namna ya kutatua matatizo katika ndoa ni kufahamu namna ya kuzozana kwa kuelezana ukweli kwa upendo, kufahamu ni wakati gani wa kukaa kimya au kuzungumza.

9. UJUZI WA KUMWEKA MWENZI WAKO NAMBA MOJA
Kumbuka katika ndoa kuna wewe, mwenzi wako na Mungu.
Jambo la msingi ni uhusiano wako na Mungu wako (siyo kazi ya Mungu, au kwenda kanisani bali uhusiano wako na Mungu, then mwenzi wako (mume au mke) ndipo wanakuja watoto na mwisho kazi.
Kama mke wako anafuata baada ya watoto, mama yako au baba yako au ndugu zako au rafiki zako au TV au chochote kile basi ndoa yako haina jipya na ipo siku mwenzi wako ataona hana maana katika ndoa yenu.

8. UJUZI WA KIMAISHA
Ni muhimu sana kila mwanandoa kufanya vitu ambacho vitakuwa msingi wa maisha ya baadae pia kila mwanandoa analo jukumu la kujiuliza ni namna gani anaweza kuwa mwanandoa mwema miaka 10 au 20 ijayo.
Kila mwanandoa analojukumu la kujiuliza nifanye vitu gani ili niwe mwenye mvuto hata miaka 10 ijayo.

7. UJUZI WA KUSAMEHEANA.
Unapokuwa kwenye uchumba, mchumba akifanya kitu cha ajabu unaweza ukaachana naye na kumsahau kabisa, hata hivyo kwenye ndoa unatakiwa kusamehe na kusahau sasa hivi.
Mwenzi wako anapofanya kitu na kujiona amekosea, atakuomba msamaha Kwani ni kweli yeye ni binadamu na ana mapungufu na hayupo sahihi mara zote.
Muda ule ambao unakuwa hutaki kusamehe mahusiano huacha kukua na hudumaa.
Kama huna uwezo/moyo wa kusamehe basi kwenye ndoa usiingie; jibakie single milele.

6. UJUZI WA KUWA MBUNIFU.
Kwenye ndoa tunaishi pamoja na kuonana kila siku, tunalala pamoja, kula pamoja, kuoga pamoja nk.
Bila kuwa mbunifu ndoa huzoeleka na kuchosha.
Tafuta vitu ambavyo mkifanya pamoja vitawafanya kuwa na kitu kipya.
Wapo wanandoa ambao akioa au kuolewa basi Hakuna jipya, Hakuna ubunifu kila mwaka vitu ni vilevile, badilika fanya vitu Tofauti kama hujawahi kwenda sehemu fulani nenda na mkeo au mumeo.

5. UJUZI WA MTAZAMO CHANYA.
Jifunze kuwa na mitazamo chanya kwenye tabia za mwenzi wako. Ni kweli kuna vitu unavipenda kuhusu yeye na kuna vitu ambavyo unavichukia kuhusu yeye, hata hivyo ukweli ni kwamba vitu vizuri unavyovipenda kuhusu yeye ndivyo vimekufanya uoane naye na kwamba vina nguvu kuliko vile ambavyo huvipendi kuhusu yeye.
Weka mtazamo kwenye vile vitu ambavyo vinawafanya ninyi wawili kuwa kitu kimoja.
Ukimnyoshea kidole kimoja mwenzi wako, basi unatakiwa kujinyoshea vidole 5 wewe mwenyewe.

4. UJUZI WA KUJIAMINI.
Lazima uamini kwamba ndoa yenu itadumu na Hakuna kitu kinaitwa talaka na talaka haitakubalika.
Ni muhimu sana ujiamini kwamba mwenzi wako ( mume wako au mke wako) anakupenda sana kama wewe unavyompenda yeye hata kama haoneshi kwamba anakupenda.
Fahamu hivyo na amini hivyo.
Kwa njia hii huwezi kuyumbishwa na upepo wa mashaka na hofu wakati kunapojitokeza kutoelewana.
Kwa njia hii itakuwa rahisi kuirudisha ndoa kwenye mstari.

3. UJUZI WA KUJIFUNZA
Wakati mwingine katika ndoa huwa tunajidanganya sana kwamba tunawafahamu vizuri wenzi wetu hata hivyo baada ya muda tunaanza kushangaa na kujiona tumeoana na mtu ambaye amebadilika sana na Tofauti na wakati ule mnaoana.
Hata hivyo kujisikia mume wako au mke wako amebadilika na kuwa binadamu mwingine si Sababu ya kuachana au kupeana talaka.
Kama huna ujuzi wa kumsoma au kujifunza kuhusu mwenzi wako basi hukutakiwa kuoa au kuolewa au hukustahili kuoa au kuolewa naye.

2. UJUZI WA KUJUA NAMNA WENGINE WANAWAONA/WANAJIFUNZA.
Kama umeoa au kuolewa na unajifanya hujaoa au kuolewa ni kweli dunia na viumbe wake wanakuona ni kweli hujaoa au kuolewa pamoja na umri wako kwenda.
Unatakiwa kuonekana wewe na mwenzi wako ni watu wenye furaha na amani na kweli iwe furaha na amani ya kweli siyo fake.
Mnatakiwa kuwa na smile la kweli na liwe na kweli si fake.
Lazima uwe makini na kufahamu wengine wanawaonaje kama wanandoa na hiyo itakusaidia kujiweka sawa kuhakikisha kunakuwa na kicheko katika ndoa yenu.

1. UJUZI WA NAMNA YA KUGOMBANA.
Hakuna ndoa ambayo wanandoa hawajawahi kupishana au kupingana au kutoelewana au kutokukubaliana katika jambo fulani au tabia fulani.
Pia ni muhimu sana kufahamu kila mnapogombana au Sababu ya kitu kinafanya kuwe na msuguano.
Unatakiwa kuwa na ujuzi wa kufahamu kwamba kugombana kokote kusiwe kwa masaa kadhaa, au siku kadhaa au miezi kadhaa.
Pia ni muhimu sana kuangalia namna unabishana au unaongea wakati wa kutokukubaliana na jambo lolote.
Pia focus katika kulishambulia Tatizo lenyewe na siyo mwenzi wako.

No comments:

Post a Comment