Saturday, 27 June 2015

MTAZAME KISHA MSIKILIZE..

Kuna usemi mmoja mzuri sana kuhusu maisha nao ni;
TAZAMA,KISHA SIKILIZA

Kwa kuangalia matendo ya mchumba wako na kusikiliza kile anaongea kwa umakini wa hali ya juu itasaidia kufahamu kama ni kama si mwaminifu (cheating).

Kama wewe ni mwanamke (binti) ambaye una mchumba ambaye umegundua kwamba si mwaminifu au hujajua kama ni mwaminifu au la, unachotakiwa kufanya kwanza ni kumuangalia anayofanya na kumsikiliza anavyoongea na utapata jibu.


Kawaida watu hukwambia na kukuonesha wao ni akina nani muda wote, na ni muhimu sana kuwa makini (pay attention) na nini kinaendelea katika usemi na matendo.

Msikilize kila kitu anachoongea na hakikisha kinaingia kwenye sikio na unakitafakari kwa makini na wakati mwingine unatakiwa kusikiliza hata kile ambacho hasemi (meta message).

Matendo huongea zaidi kuliko maneno yoyote, na kile anafanya mchumba wako huelezea namna anaweza kuwa na wewe.



Hatua muhimu ambayo mwanamke yeyote anaweza kufanya kwa mchumba wake asiyemwaminifu (cheating) kwanza ni kukubali kwamba mchumba wako si mwaminifu. Kubali kwamba kuna mwanamke mwingine zaidi yako ambaye mchumba wako anampenda.

“Huwezi kufanya maamuzi Kama hutakubali kwamba yeye si mwaminifu”


Mara nyingi mwanamke akiwa kwenye mapenzi (love) au mahusiano ya uchumba huwa kipofu wa kufahamu vizuri mwanaume na namna alivyo, unaweza kupewa taarifa kwamba mchumba wako si mwaminifu na ukaendelea kukataa.

Hivyo kukubali kwamba mchumba wako amekuwa si mwaminifu ni hatua ya kwanza na pia kuwa kipofu wa kudhani si mwaminifu wakati unajua kwa matendo yake si mwaminifu haitakusaidia lolote.


Hatua ya pili baada ya kukubali kwamba mchumba wako si mwaminifu ni kutojilaumu wewe mwenyewe.
Kawaida mwanamke anapopata mchumba na mchumba akawa si mwaminifu huanza kujisikia kama amefanya kitu kisicho sahihi au kujisikia ana hatia.
Mwanamke huanza kujimaliza mwenyewe (tearing) na kuanza kujiuliza kuna kitu gani kibaya anacho katika maisha yake au amefanya hadi mchumba wake akaanza kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine.
Lazima ujikubali kwamba hujafanya kitu chochote kibaya hadi yeye akawa si mwaminifu, hakuna uhusiano wa namna wewe ulivyo au unavyofanya na tabia yake ya kuwa si mwaminifu.
Huanza kupoteza kujiamini (self esteem) eti kwa kuwa mchumba wake amepata mtu mwingine.
Wewe ni mwanamke yuleyule ambaye alikuhitaji mara ya kwanza uwe mchumba wake, hujabadilika kamwe!
“Nothing is wrong with you at all”
Pia haina haja kujilaumu kwa kuwa mchumba wako amekuwa si mwaminifu.
Je, utatoa uamuzi gani kwa mchumba asiye mwaminifu?
Kawaida unaweza kuwa na maamuzi katika sehemu mbili tu, kwanza kuendelea naye au pili kuachana naye.
Kama utaamua kubaki au kuendelea na uchumba kwa mwanaume ambaye si mwaminifu lazima umkubali kama alivyo na hakuna kitu utafanya au sema kitaweza kumbadilisha asiwe mwaminifu.
Kumpeleka kwa wazazi wako ukamtambulishe hakuta mbadilisha, kununua simu mpya ili aachane na wanawake anaowasiliana nao haitambadilisha, yeye kukuomba msamaha mara kwa mara haitambadilisha, wema wake kwako hautafanya abadilike, kukununulie gari hakutafanya abadilike, kukununulia kuku na chips hakutafanya awe amebadilika, kumchunga kwa kutumia secret detective agent hakuwezi kumbadilisha kamwe, kupanga siku ya harusi hakutambadilisha, kumuahidi mambo mengi mazuri hakutambadilisha kamwe.
Usiishi kwa kujikana kwamba eti hatarudia au ataacha kutokuwa mwaminifu.
Hivyo kama umemkubali kuendelea naye pamoja na tabia yake ya kutokuwa mwaminifu maana yake unakubali kuendelea naye huku unajua hataacha kutokuwa mwaminifu na hata akiendelea kutokuwa mwaminifu kwako itakuwa sawa tu na haita kuwa tatizo ndiyo maana unaendelea naye.
Ni uamuzi wako umeamua kuishi hivyo na huyo cheater.
Uamuzi wa pili ni kuachana naye; kama umeona huwezi kuishi na mwanaume asiyemwaminifu basi kubali kuacha naye.
Huyu mtu hawezi kukupa kile unahitaji; katika maisha ukweli una haki ya kuishi na mwanaume ambaye ni mwaminifu.
Hata kama unaachana naye kwa mateso, kwa maumivu ni afadhari uteseke kwa miezi kadhaa kuliko mateso ya miaka 20 au 30 au 40 utakayoishi naye kwenye ndoa ambayo kila siku ni “homa ya jiji”

No comments:

Post a Comment