Friday, 26 June 2015

FAHAMU HAYA KUHUSU WANAWAKE.

Sababu za kuwa na migogoro kati ya mume na mke mara nyingi ni kwa sababu wanaume hawawaelewi kabisa wanawake na wanawake wanawaelewa vibaya wanaume .
Kibaya zaidi wanaume mara zote huendelea kufanya kinyume na vile wanawake wanategemea wafanyiwe na waume zao.
Na wanaume nao wanawashangaa wanawake namna wanavyobadilika kila mara kwani unaweza kumkuta mke dakika moja yupo na furaha na kicheko na baadae kidogo anajikunyata na kuhuzunika na wanaume huwaona wanawake ni viumbe wa ajabu sana chini ya jua.
Linapokuja suala la kutafuta mpenzi (mume mtarajiwa) wanawake wanatabia ya kumkubali na kumshika mwanaume mzima mzima. Na hutumia akili kuhakikisha anamnasa hata kwa kujipitisha sehemu au njia ambazo anaamini anaweza kukutana naye.
Kama anajua mwanaume yule hupatikana maeneo fulani na anampenda basi hujipeleka hilo eneo ili wakutane ili iwe coincidence fulani.
Atasubiri hako kanafasi ili wakutane ghafla.
Mwanamke hutumia njia ya hisia anapoingia kwenye suala la mapenzi na kuwa karibu na kifua chake (moyo) si mwonekano kama wanavyofanya wanaume.
Kawaida mwanamke huchelewa sana kufungua moyo kwa mwanaume na akishaufungua huufungua kwa asilimia 100 na akimpenda huyo mwanaume (fall in love) basi huwekeza kila kitu maishani mwake kwa ajili ya huyo mwanaume.

Wanawake huhitaji mwanaume ambaye atamhakikishia upendo na kwamba anapendwa kila siku, wanapenda kupokea sifa kwa mavazi, namna anaonekana na kila kitu, wanawake wapo sensitive sana katika issue za mapenzi na huumizwa kirahisi.
Wanawake wanapompata mwanaume wa kupendana naye huwekeza kwa muda mrefu na kwao mahusiano huwa na maana sana kama pumzi anayovuta.
Huwekeza katika kufahamu sifa za ndani za mwanaume kuliko uzuri wa sura ndiyo maana wanawake wengi wazuri kwa sura huishia kuoana na wanaume wenye sura zisizovutia hata kidogo.
Pia wanawake huwa wazi kimahusiano, kama kuna kitu kinamsumbua huongea waziwazi tofauti na wanaume. Pia wanawake ni wazuri kusoma mwanaume akiwa na tatizo au kumshtukia kama kuna kitu kinaenda ndivyo sivyo.

Mwanamke anapoongea na mpenzi wake hutegemea mume wake huyo kuacha kila kitu na kumsikiliza kwa makini.
Pia mwanamke hupenda kufanya kazi kama timu na ushirika ndiyo maana hata kama mume amempa rafiki yake pesa na akagundua bila kuambiwa, kwake ni issue ingawa tatizo si zile fedha bali kwa nini hakuambiwa.
Pia wanawake hupenda surprise leo na kesho au mara kwa mara, hufurahia kufanyiwa vitu vidogovidogo kama vile mkienda restaurant mwanaume anachukua jukumu la kumuagizia chakula na kumletea ale (kuhudumiwa kama queen au princes)

Pia wanawake huwa hawapendi mwanaume kuongelea habari za mwanamke mwingine labda huyo mwanamke awe na sifa pungufu kuliko yeye kila idara.

No comments:

Post a Comment