Monday, 29 June 2015

NINI MKE ANAHITAJI ?

Ili Mke awe available kwa mume kimwili na kiroho inampasa mume awe na sifa zifuatazo:

Ukaribu, uwazi katika mambo yake, anayeeleweka, mtu wa amani, anayempa uhakika mke kwamba ni yeye peke yake ndiye anapendwa na mume wake na pia kumpa uhakika kwamba yeye ni mwanamke mwenye sifa anazozipenda kimwili (beauty) na kiroho.

Je, unawezaje kuwa mume ambaye mke anakuelewa?

Ili mke akuelewe mume unahitaji kutumia secret weapon ya sikio lako.
Kumsikiliza tu mke huweza kuonesha kwake kwamba umemuelewa kuliko hata kabla hajamaliza kuongea wewe unamkatiza na kusema ulikuwa unajua anataka kusema kitu gani.

Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume ni kwamba mwanaume kawaida yupo wired kusikilizwa na si kusikiliza, na mara nyingi mwanaume hupenda kutatua tatizo au matatizo au kutoa jibu kwa ajili ya tatizo lolote, hivyo anapoongea na mke wake kwa kutomfahamu anakuwa na haraka ya kutaka kutoa majibu badala ya kusikiliza tu.

Narudia tena;
Si mara zote mwanamke anapouliza swali au kukwambia kitu anahitaji majibu, mara nyingi anakuwa katika harakati ya kujihusanisha (connection) na wewe na anachohitaji ni sikio lako tu na si namna ya kupata majibu.
Unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza na kushiriki katika kuzungumzia hiyo shida yake na kuliona kama tatizo lenu wote.

Mwanamke huhitaji mtu wa kumsikiliza tu na sikio lako wewe mume ndilo analihitaji na si uwezo wako wa kutatua tatizo.
Ukimsikiliza, atajisikia vizuri tofauti na ukirukia kukatiza kile anaongea au kuanza kupendekeza solutions kwa kile anakwambia.

Wanaume kujitahidi kutoa solutions za kile mke anaongea au hata kukatiza kile anaongea kwa mume kujifanya anajua mke alitoka kuongea kitu gani ni moja ya matatizo sugu ya kwenye ndoa.
Hata kama wewe ni mwanaume maarufu kutatua matatizo ya wanaume wenzako bado ukiwa na mke wako unatakiwa kumsikiliza tu na sikio lako hadi aridhike.

KUCHEPUKA..(PART 2)

Moral standard za ndoa sasa zimeshuka kiasi kwamba
si ajabu tena kuona bibi harusi na vazi la harusi huku ana mimba kubwa!

Karibu watu wote wanaokamatwa na suala la kutokuwa waaminifu katika ndoa zao hukubali kwamba ni kweli wamekosea na wengine husema ni shetani tu aliwaingia.
Tafiti zinaonesha kwamba katika jamii yoyote duniani asilimia 25 ya wanaume huchepuka nje ya ndoa zao na asilimia 10 ya wanawake hukiri kuchepuka kwenye ndoa zao hii haina maana wanandoa wenzao hujua suala ni kwamba huwa wanakiri kwamba wamewahi kutoka nje ya ndoa zao.

NINI HUSABABISHA WENGI KUCHEPUKA

Kutoridhika na ndoa zao idara zote na kuanza kutafuta mtu wa nje ili kuridhishwa.

Matatizo ya familia.
Wengine hujikuta amempenda mtu mwingine.

Kutengana kwa muda mrefu mume na mke inaweza kuwa masomo au kazi nk.

Kushuka kwa kiwango cha kiroho cha wanandoa.
Kuhitaji kuridhishwa zaidi kimapenzi; kuna watu wana libido la ajabu!
Kutafuta Kujiamini na kutambuliwa kwamba yeye ni nani katika jamii
Kuikata kweli ya Neno la Mungu.

Ukaidi na uhuni.
Hitaji la kupendwa baada ya kutelekezwa.
Kuzaliwa mtoto wa kwanza katika ndoa; Feelings za kumpa mume huhamia kwa mtoto na wanandoa hujikuta wapo emotionally distant.


NINI HUSABABISHA WENGI KUGOMA KUCHEPUKA.

Kujitoa kwa ndoa na kulinda ahadi na agano (covenant)
Kuaminiana kwa wanandoa.

Sababu ya dini yaani wokovu (uhusiano binafsi wa mwanandoa na Mungu).

Kuogopa matokeo ya kuchepuka kama vile magonjwa (UKIMWI) na crisis zingine.

Kujifahamu na kukomaa kiakili na Kujiamini.

Kupenda mke na watoto na kuwapa heshima iliyotukuka na kuishi kwa mfano kimatendo na kimaneno.

Uadilifu (moral standard)

KUCHEPUKA

Linapokuja suala la ndoa au mahusiano huu usemi wa kingereza usemao “How Far is too Far’ una maana kwamba je, ni namna gani au utajuaje au ni kufanya kitu gani hueleza kwamba hujawa mwaminifu kwa mke wako au mume wako.
Kujua hujawa mwaminifu ni pale kile unafanya au yale unaongea na mwanaume mwingine au mwanamke mwingine huwezi kumwambia mke wako au mume wako.

MFANO
Jeffy ni kijana smart sana kazini na nyumbani na kwa sasa anajiona yupo bored nyumbani hasa kutokana na yale yanayoendelea katika maisha na mkewe Jane.
Hivyo anaamua kutaniana na kujihusisha zaidi na mwanamke anayeitwa Lily ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisini.
Katika kutaniana kwao urafiki unazaliwa na wanajikuta wanakuwa muda mwingi pamojana kuvutiana zaidi; sasa iwe lunch, au kinywaji baada ya muda wa kazi Jeffy yupo na Lily.

Baada ya siku na miezi kadhaa wanajiona karibu zaidi na Jeffy anajikuta anamwambia Lily siri zake za nyumbani na mkewe na Lily naye anamwambia Jeffy siri ambazo hajawahi kumwambia mtu yeyote.
Sasa wakikutana wakiwa wawili ni kupeana kisses na hugs kwa kwenda mbele ingawa bado hawajavuliana nguo.
Yote haya yanapotokea Jeffy hajamweleza mke wake.

Je, Jeffy amekuwa si mwaminifu kwa mke wake? Au kwa ndoa yake?
Je ungekuwa wewe ni Jeffy ungemwambia mke wako huo urafiki na mwanamke Lily?
Au ungekuwa ni mwanamke Lily ambaye umeolewa Ungemwambia mume wako urafiki wako na Jeffy?

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA NI NINI?
Kukosa uaminifu katika ndoa ni utendaji unaoanzia ndani ya moyo kuvunja trust na ahadi ya ndoa kimwili, kiakili, kimawazo na kihisia na siri zote za ndoa.
Ni kuvunja agano na pia ni kumsaliti mwenzi wako.

Je, unaweza kujihusisha na mtu mwingine nje ya ndoa kihisia na ukabaki mwaminifu kwa ndoa yako?

Jibu ni hapana kwani ulipokubali kuoana naye ulikubali kwamba mtakuwa mwili mmoja (one flesh); kuwa mwili mmoja ni pamoja na emotions, feelings, mawazo na maisha yote ya ndoa kwa ujumla.
Unatakiwa kuwa kwa mwenzi wako kimawazo na kimwili.

Uzinzi wa emotions upo serious sawa na ule wa kimwili
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini'.
Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
(Mathayo 5:27-28)

Uzinzi ni sehemu ya infidelity ( kukosa uaminifu katika ndoa) infidelity ni kutimiza hitaji la mwili na hisia nje ya ndoa wakati adultery ni sex nje ya ndoa.

Kama ninyi ni wachumba na mmoja si mwaminifu huo unaitwa ni uasherati na ni vizuri kuachana kwani mchumba asiyemwaminifu huja kuwa mwanandoa asiyemwaminifu.

Washauri wa mambo ya ndoa wanafahamu fika kwamba katika matatizo mengi ya wanandoa suala la kukosa uaminifu (infidelity) kawaida ni nusu ya matatizo yote katika ndoa.

Ujue au usijue kwamba kuna kuchepuka metokea katika ndoa yako ukweli unabaki kwamba matokeo ya mwanandoa mmoja kuchepuka nje ya ndoa yake ni mabaya sana kwa yeye mwenyewe, ndoa yake na huweza kuleta crisis kubwa ya familia na hata jamii kama si taifa.
Fikiria suala la UKIMWI tu.

VITUKO VYA KUCHEPUKA NJE YA NDOA.

Kawaida mwanandoa anayechepuka akikamatwa na kupewa talaka mara nyingi hawezi kuoana na yule aliyekamatwa naye.
Hivyo kama upo kwenye affair na mwanaume wa mtu au mke wa mtu kumbuka kwamba hupati point yoyote au kukuongezea uwezekano wa yeye kuoana na wewe ikitokea amepata talaka.

Affair ni dalili za huzuni iliyopo kwa wanandoa na maana yake mmoja anakosa hisia sahihi kwa mwenzake na matokeo yake husukumwa kuchepuka nje na akishachepuka huongeza matatizo mengine zaidi ya ndoa kama vile kuchelewa kurudi nyumbani, matumizi ya pesa na magonjwa.

Si sahihi kwamba kuwa na affair ni kupata great sex, kutoka nje ni vibaya kwa sababu ni kweli kwenye ndoa kuna great sex na "we need to spread the word" kwamba kwenye ndoa sex ni tamu zaidi.

Si kweli kwamba mwanandoa anayechepuka hufuata mwanamke mrembo zaidi kuliko aliyekwenye ndoa yake au mwanaume maridadi zaidi kuliko aliye kwenye ndoa yake, wengi huvutwa na feelings zile wanakosa ndani ya ndoa zao.

Affair nyingi zina base kwenye urafiki na kuungana kihisia na sharing ya siri na feelings mbalimbali na wakati mwingine sex huwa si sababu ya kuwa na affair bali urafiki wa karibu kwa jinsia tofauti.

Tamaduni nyingi humwangalia vibaya mwanamke kuliko mwanaume linapokuja suala la mwanandoa kuchepuka nje.

Kubwa zaidi ni kwamba uwezekano wa kutolewa talaka ni pale mwanamke akionekana ametoka nje ya ndoa (cheating) kuliko mwanaume akitoka nje ya ndoa.

DALILI KWAMBA ANACHEPUKA.

Dalili za mwanaume anayechepuka

1. ANATUMIA MUDA MWINGI NJE NA NYUMBANI
Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja na kila mmoja ukampa muda sawa, it is impossible.
Wengi huanza kubadilika na kukwepa kuwepo nyumbani na mke wake hata kabla ya affair (astray).
Mwanaume kutumia muda mwingine nje ya nyumbani haina maana kwamba ana-cheat bali inaweza kuwa dalili kwamba ana cheat hasa kukiwa na dalili zingine.
Hata hivyo ukigundua mapema unaweza kuzuia na kuepuka maumivu ya cheating.
Wakati mwingine “hawa wanaume” huwafunga kamba wake zao kwamba
“Nikitaka kutoka nje, naweza hata muda wa kawaida hivyo nikichelewa haina maana na-cheat”
uwe makini na huo usemi kwani ukweli ni kwamba wanaume wengi hutumia muda wa ziada na si muda wa kazi kufanya cheating zao.
Ukiona mume ana dalili za kukwepa kuwepo nyumbani kama ilivyokuwa kawaida, basi inabidi uwe makini na kuchunguza kujua nini kinaendelea.

NINI CHA KUFANYA:
Ni vizuri kukaa pamoja na kujadili pamoja kuangalia kama kuna issues ambazo haridhiki nazo zirekebishwe haraka ili arudi kwenye mstari.

Pia jiulize:
Je, hapo nyumbani kuna amani, heshima, upendo, na utulivu?
Na je, namna unaongea na mume wako kuna respect? Au ni kulalamika, hasira, huzuni na yeye anajiona ni failure na loser?
Inawezekana huko anaenda kunampa kile anakikosa hapo nyumbani au kwako wewe mke.

2. TENDO LA NDOA MARA CHACHE
Kupunguza kwa kiwango cha sex kati ya mke na mume ni dalili mojawapo kwamba kuna kitu hakipo sahihi na mojawapo inaweza kuwa mume anachepuka kwa “yule mwanamke”.
Pia unaweza kuijua hii dalili mapema na ukazuia huzuni kutokea katika ndoa yako kwa kupiga gia ya reverse kwa kuongeza frequency za sex kati yako na mumeo.
Wapo ambao ni wajanja zaidi ambao huendelea na sex kama kawaida ili wasishtukiwe hata hivyo kutokana na kuwekeza kwa “yule mwanamke” automatically akiwa na mke wake hamu hupungua na matokeo ni kupungua kwa uhitaji na kiwango cha sex hushuka.

NINI CHA KUFANYA:
Kwanza jiulize swali hili:
Je, kiwango cha sex ni mara chache kuliko kawaida? Kama ni chini ya kiwango ni vizuri wewe mwanamke pia kulianzisha uone nini kinatokea.
Kama mwanamke Jitahidi kutengeneza mazingira ambayo yatakufanya usijisikie kuchoka sana na kama inawezekana unaweza kumuomba mume wako kukusaidia kazi ndogondogo za pale nyumbani.
Pia fikiria ni kitu gani unaweza kuongeza (kipya) ili kuimarisha sex na kama inawezekana mnaweza kwenda nje ya hapo nyumbani kwa ajili ya kuwa na intimacy zaidi.

3. ANAANZA KUKUKWEPA WEWE MWENYEWE MKE WAKE
Anaweza kukukwepa kwa njia zile mnatumia kuwasiliana iwe mchana au usiku huanza kupunguza.
Unaweza kujikuta simu hazijibiwi, sms hazipewi majibu na mara simu imefungwa.
Kama ana simu ya mkononi anaanza kutembea nayo hadi anapenda kuoga, anapoi-charge kama ni nyumbani basi ataisimamia kama FBI wanaomsimamia terrorist aliyekamatwa kabla ya kujilipua.
Na kuna simu akiipokea No matter what ataenda kuongelea nje au kwenye uchochoro wowote.
Kama upo makini utajua tu something is not right!
Kikubwa zaidi hapendi kuwa na wewe “closer” kitendo hiki hufanya muwe mbali kihisia.

NINI CHA KUFANYA:
Jaribu kuchunguza kama simu unazompigia sinamsumbua kazini au ni jeuri yake tu na ukorofi kwa sababu ya “yule mwanamke”
Ongea naye namna ya kuwa na muda pamoja kwa kila wiki.
Wakati mwingine mpigie simu ya kumpa appreciation kwa ajili ya kitu chochote amefanya badala ya simu za kulalamika na kumfanya ajione failure na loser.
Kama una hints chunguza simu yake ya mkononi na kama huna hints achana nayo kwani hakuna mwanaume anapenda kutembea huku amefugwa video camera usoni kuchunguzwa kila kona anayopita.

4. ANAKUWA CRITICAL
Alikuwa anapenda mapishi yako, unavyoonekana (sura na maumbile), mapenzi yako, namna unapenda bajeti; ghafla from nowhere anaanza kulalamika na kukulaumu kwa kila unachofanya.
Inawezekana tatizo ni yule mwanamke!
Kiti kidogo kikikosewa inakuwa kama kapatia sababu ya kuanzisha mgogoro au vita ya tatu ya dunia.
Wakati mwingine anaweza kuwa mwonezi.

NINI KIFANYIKE:
Jadili kwa nini mume wako anakuwa critical na wewe muulize kwa upendo bila wewe kuwa critical pia.
Pia jadili kujua tatizo lipo wapi ili lirekebishwe huku wote mkiwa positive.

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA.

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA HUUMIZA SANA
Mume wa Jane alipokiri kwamba ni kweli “Nilikuwa na uhusiano na yule mwanamke”.
Jane alipata mshituko ambao hauelezeki ni zaidi ya shock ya umeme.

Kwanza alijiuliza
“Imekuwaje sikuweza kujua dalili kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea na nilikuwa mjinga kiasi gani nisijue;
je, nilikuwa sioni matatizo ya ndoa yangu hadi mume wangu anafikia hatua hiyo, nilikuwa kipofu kiasi gani?
Na huyo mwanamke ametumia mbinu gani hadi kumpata mume wangu nami nisijue?”
Alijiuliza hayo maswali huku machozi yakibubukika kutelemka kwenye mashavu kama mvua za Alnino.

Jane alijikuta yupo katika wimbi kubwa la msongo wa mawazo mazito, hasira na kutojiamini kukaongezeka.
Wakati mwingine alikuwa anafua nguo na ghafla anajikuta anaishiwa pumzi na mapigo ya moyo kubadilika na viganja kuanza kutoa jasho nyembamba kama vile amakutana na simba ghafla.

Wakati mwingine hata kama anatazama TV ili kupoteza mawazo, ikitokea kukawa na program inaonesha affair yoyote ya ndoa basi hujikuta hasira zinampanda na kuzima Tv na kuanza kulia kwa machozi.

Zaidi ya miezi miwili usingizi umeota mabawa na hakuwa na hamu ya chakula na matokeo yake afya yake ikaanza kuzorota na kila mtu akajua Jane anaumwa kwani ule uchangamfu wake na afya yake vinaleta maswali zaidi ya majibu.

Ingawa mume wake alikiri kwamba hawasiliani tena na yule mwanamke, bado Jane alijikuta bado anawaza na kupata picha ya mume wake akiwa anafanya mapenzi ya yule mwanamke na akajikuta anamthibiti mume wake kila movement anayofanya maana haaminiki tena na kitu kidogo tu kilimchukiza mno Jane.
Jane alijitahidi sana asiwaze kuhusu huyo mwanamke hata hivyo alivyokuwa anajitahidi kusahahu ndivyo alivyozidi kukumbuka na kuwaza zaidi na alijikuta mawazo kuhusu huyo mwanamke yanazidi kujirudia na kulata hasira zaidi.

Tukumbuke kwamba ni kweli affair huumiza sana na maumivu yake ni makali kimwili, kiroho na kihisia.
Kukiwa na affair huwezi kukwepa kuwa na msongo mawazo kama ya Jane.
Jambo la msingi ni kwamba Jane si mtu wa hasira za kupigana na kelele kama sisi wengine kwani angekuwa mwingine hapa pasingekalika kabisa.

Msongo wa mawazo huja na mawazo huja kutokana na issue kwamba yule unayemwamini kuliko mtu yeyote duniani anakuwa amekusaliti kirahisi hivyo tena bila wewe kujua.

Wanandoa ambao wanapambana na issue ya affair huwa na kiwango kikubwa cha depression kuliko matatizo mengine ya ndoa.

Ni kweli affair ni dhambi na chukuzo kwa Mungu na ni kitendo kinacholaaniwa kwa nguvu zote hata hivyo hata kama umeumizwa sana jambo la msingi ni kukumbuka kwamba huwezi kujisia hivyo (msongo na mawazo na hasira) milele.
Ukweli ni kwamba kujisikia hivyo upo sahihi na unatakiwa kuweka malengo mapya ya kurudi katika hali yako ya kawaida kitu ambacho naamini ni kigumu sana.
Unatakiwa kuhimili hali uliyonayo ili hayo maumivu na feelings ulizonazo zisikufanye kilema hata ukajiumiza zaidi kama vile kujinyonga au kunywa sumu kwani hapa ndipo utasikia mapenzi yanaua.

Ni muhimu kuchukua hatua Zifuatazo ili kurudi kwenye hali yako ya kawaida;
Jiruhusu mwenyewe kujisikia vile unajisikia, kama ni kulia, lia tena kwa machozi mazito, kama kukasirika basi kasirika na muuliza maswali anayehusika kadri ya unavyotaka ili kujua ukweli. Zaidi jikubali na ukubali kwamba ni kweli yametokea.

Tafuta mtu unayemwamini (mshauri, mchungaji nk) akusaidia kuhimili maumivu na uchungu ulionao kwani kwa kuongea na mtu unayemwamini maumivu huondoka.

Jitoe, jikabidhi (moyo) kwa Mungu.
Yeye peke yake ndiye anajua maumivu.
Mungu ametuahidi kutupa faraja wakati wa dhiki na maumivu hata kama shetani ana mpango wa kuharibu ndoa zetu bado tukiishi katika blueprint ya ndoa kama Mungu anavyotaka tutaishi maisha ya furaha amani na ushindi.

MAMBO YA KUZINGATIA BAADA YA KUJIFUNGUA.

Wanawake wengi huwa katika wakati mgumu kufahamu ni lini wanaweza kurudi kwenye maisha ya kuendelea na tendo la ndoa na waume zao baada ya kujifungua.
Pamoja na kuwa na imani potofu zinazozuia mwanamke kujihusisha na sex baada ya kuzaa mtoto bado hakuna uthibitisho wa kitaalamu (scientific research) kuelezea ni muda gani muafaka wa kuanza sex baada ya kujifungua au hatari za kuendelea na tendo la ndoa baada ya kujifungua.
Mke anao uhuru wa kuamua ni wakati gani anajiona yupo huru kuanza tena kushiriki katitka sex na mume wake.

Je, ni muda gani hasa hutakiwa?

Inapendekezwa kwamba ni kiasi cha wiki sita uterus huwa katika hali ya kawaida baada ya mtoto Kuzaliwa hiki ndicho kimekuwa ni kipimo cha wakati wote jamii nyingi duniani.
Ingawa wapo wanawake huwa tayari kihisia na kimwili kushiriki sex na waume zao kabla ya hizo wiki sita, pia lini mwanamke aanze inatokana na complications za wakati wa kujifungua (delivery).
Jambo la msingi ni pale anapojisikia yupo comfortable.
Kwa wanawake wengine inachukua zaidi ya wiki sita kuwa tayari kufanya mapenzi.
Mambo ambayo huhisiana na kuanza kwa kufanya mapenzi mapema ni maumivu kutokana na kisu wakati wa kuzaa, kuvuja kwa damu nyingi, kuchoka Na pia mwanamke kuwa mkavu (chini) kutokana na kiwango kidogo cha estrogens hasa baada ya kujifungua.
Wanawake ambao kuzaa kwako kulikuwa na labour ya muda mrefu, au upasuaji au kuzaa kwa kusaidiwa (vacuum extraction, forceps or caesarean) ni vizuri kusubiri hadi wiki kati ya 8 hadi 12 au zaidi.
Na wale ambao kuzaa kulitokana na kuchanwa (perineal tearing) wanaweza kusubiri hadi miezi kadhaa baada ya kupona kabisa.

Je, kuna tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa?

Ndiyo kuna kufanya mapenzi baada ya mtoto Kuzaliwa.
Kawaida kabla ya kujihusisha na tendo la ndoa ni vizuri kuwasiliana na daktari wako kukagua kama kumetokea healing ya kutosha kwa uterus na perineum ambayo mara nyingi huchukua wiki 6 baada ya kujifungua mtoto.
Baada ya daktari kuwapa go ahead, basi unahitaji kuwa wazi wewe na mume wako kusema namna gani kila mmoja anajisikia kimwili na kihisia.
Kukimbilia kuanza sex mapema kabla mmoja hajawa tayari inaweza kusababisha mambo kwenda vibaya.
Pia hofu ya kuumizwa kwa mke huweza kutawala ubongo na pia mtoto kulia inaweza kuwa ni kizuizi cha mahaba.
Ukiona sex ni painful, ni vizuri kwenda polepole na Kumbuka kuhakikisha huko chini (mwanamke) yupo lubricated hata kwa kutumia KY jelly.
Pia inabidi mke azingatie kwamba maziwa huweza kuchuluzika wakati wa tendo la ndoa.
Hili si tatizo na si kiwango Kikubwa kuweza kuathiri uwingi wa maziwa ya mtoto.
Mara nyingi hii hutokea miezi miwili ya kwanza kwa wanawake wengi na Baadhi huendelea hadi miezi 8 kama ananyonyesha mtoto maziwa.
Jambo la kuzingatia kwa mwanamke ni kuhakikisha baada ya kushiriki tendo la ndoa na mume wake ahakikishe anajisafisha matiti yake na mikono yake (kuzingatia usafi) kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto.

Tips kwa mwanamke!
1. Usikimbilie na kuwa na haraka kwa ajili ya kuanza sex, take your time.
2. Panga njia ya mpango wa uzazi kabla ya kujihusisha na tendo la ndoa, uwe makini unaweza kujikuta una mimba miezi miwili tu baada ya kujifungua mtoto.
3. Ni vizuri kuwa pamoja kama wazazi hivyo panga mipango mingi zaidi kuhusiana na mtoto.
4. Inabidi kuwa na ratiba mpya ya sex kwani si kweli kwamba kila muda kwa kwenda kulala unaweza kuwa muda mzuri wa sex hasa kutokana na mahitaji ya mtoto.
5. Kumbuka wakati huu sex ni quality na si quantity.
6. Zungumza kama kuna hofu na mashaka yoyote ya wewe mke kujihusisha na tendo la ndoa.

STYLE NZURI YA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI?

Kuna wanandoa wengi hata kama hawaridhishwi inavyotakiwa katika ndoa zao kimapenzi bado wamekuwa wagumu kuzungumzia suala la sex kati ya mke na mume au kuomba ushauri.
Pia suala la sex ni muhimu sana katika ndoa kwani ukiridhika katika sex na ndoa utaiona inakuridhisha.

Aina ya mlalo si dawa ya kukusisimua ingawa ni moja ya vionjo ambavyo vinaweza kukufanya uwe na tendo takatifu la ndoa linakuridhisha.
Hata hivyo kutokana na uzoefu pamoja na tafiti nyingi na medical reports nyingi dhahiri kwamba mlalo wa Rear Entry au Doggie Style ni moja ya mlalo unaomridhisha mwanamke na kumhakikishia kufika kileleni (orgasm) bila shaka.

KWANINI?
Kitendo cha uume kukuingia kwa nyuma husaidia kumpa uwezo mwanaume kuweza kukupa thrusting inayokupa raha pia uume huweza kusugua G-spot na kuweza kukumfikisha mwanamke katika utamu na raha isiyotamkika.
Ili uume kufikia G spot ni lazima uume uingie huku uke ukiwa angled na hii doggie style ndiyo mlalo perfect.
Pia ukifika kileleni kwa kuguswa G spot utataka zaidi na utaingizwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa raha ya mapenzi.

Zaidi pia ni kwamba mwanaume anakuwa na uwezo wa kuwa huru kuendelea kuchezea (rub) kisimi, kuchezea matiti (chuchu) hasa kama hivi vyote vinakusisimua na kama mpo portable mnaweza kuendelea kupeana kisses huku kila kitu kikiwa kinapaa kwenda hewani.

Hii ni deep penetrative sex ambayo mwanaume huwa dominant na mwanamke huwa submissive hivyo ni mlalo natural.

Pia muungano wa miili miwili kugusana kimahaba husaidia mwanaume kuona mwili wa mwanamke kwa nyuma na kama mwanaume ni mgonjwa wa kuona matako ya mke wake (fahari ya mwanamke) basi itakuwa dawa sahihi kwake kukupeleka mwendo wa mbali zaidi kwa yeye mwenyewe kusisimka kwa kuona vitu au kitu.

Zaidi pia shaft ya uume wa mume huweza kutoa sensation ya ajabu kwenye vulva kiasi cha mke kupata raha ya ajabu.

Kawaida mwanamke huweza kufika kileleni kwa njia ya kisimi, G-spot na uke wenyewe, hivyo hii style inaweza kukupa vyote kwa wakati mmoja. Kutofika kileleni kwa sytle ya aina hii ni kweli hapo kutakuwa kuna tatizo kubwa.

Pia wakati wa kupeana mahaba mwanaume hujikuta balls zake zinagusa uke au kisimi na hii inaweza kukupa raha kama si kukufanya uwe wet zaidi na zaidi hahaha over and over!
Je kuna mlalo mwingine zaidi?
Ni kweli tendl la ndoa ni sanaa hivyo ubunifu ni kitu cha msingi kabisa, mlalo mwingine ni ule wa front to back/spoons (mke na mume kulala kama vijiko vinavyopangwa kwa maana kwamba wote mnalala (kiupande)kuelekea upande mmoja kwa mume kulala nyuma ya mke na kumwingia kiubavu kwa nyuma).
Hii pia huweza kuleta matokeo sawa na ile ya doggie style au rear entry.

MUHIMU.
Jambo la msingi ni kwamba ili kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha kuwa na maandalizi ya kutosha ndiyo jambo la msingi (foreplay) si suala la kukimbilia haraka doggie style wakati hamjasisimuana vya kutosha.
Na mawasiliano ni jambo la msingi kabisa.

KUSISIMULIWA KIMAHABA

Kila mtu ana maeneo yake muhimu kusisimka akiguswa.
Weka kwenye akili zako kwamba forepaly kawaida ni dakika 20 ili kufikia uwezo Mnaouhitaji kwa ajili ya tendo la ndoa linaloridhisha.
Usiwe na haraka, tumia muda kuenjoy pamoja na mpenzi wako.
Pia ifahamike kwamba si kila mtu husisimka sehemu sawa na mtu mwingine, kila mtu anasehemu zake maalumu ambazo zina msisimko kuliko sehemu zingine hivyo ni vizuri kuwa na mawasiliano mazuri ili kila mmoja afurahie maandalizi ya tendo la ndoa

MAENEO MUHIMU KTK MWILI WA MWANAMKE

KICHWA
Kwenye kichwa kuna homoni za endorphins zinazofanya kazi ya kutoa raha (pleasure) hivyo mwanamke kuchezewa nywele zake hapo atayeyuka tu, ingawa si wote hujisikia raha.

MIDOMO (LIPS)
Kubusu ndiyo mlango wa kwanza katika kuingia katika mwili wake. Lips ndipo mahali ambapo ni kiini cha ubongo kumsisimua mwanamke (Brain’s arousal center).
Kama unajua vizuri jinsi ya kumbusu kwa utundu wote basi ni dhahiri kwamba busu analopata linaenda mbali zaidi na kumpa raha ya ajabu.
Ni vizuri ukajua jinsi ya kutumia ulimi na meno yako vizuri kumfikisha pale anahitaji kufika.
Wanawake wengi hupenda busu na unaweza kutumia muda wa kutosha kubusu kwa kadri anavyotaka, na mwanaume akisisimka rangi ya lips hubaridika na kuwa red zaidi.

SHINGO
Usisahau kutumia mikono yako pia, tumia ulimi wako na meno kugusa shingo yake huku ukiongea maneno matamu.
Pia unaweza kubrush lips zako kwenye kidevu chake.

MASIKIO
Baadhi ya wanawake hupenda sana kunyonywa masikio, kubusiwa, na kulambwa pia na unaweza kubusu na kunyonya sikio kama vile unavyonyonya chuchu zake ni dhahiri kwamba kama yeye yupo sensitive kwenye masikio basi atapata raha ya ajabu.
Na kile kitendo cha yeye kujisikia unapumua kwenye masikio yake basi ananyegeka.

KIUNO
Kiuno ni hot spot kwa mwanamke, busu kiuno na tumia mikono yako kukipa mgusu wa kimahaba, tumia ncha za mwisho za vidole kumgusa kama vile una reki.
Usiwe na mikucha mirefu maana unaweza kumuumiza.

MATITI NA CHUCHU
Hapa kila mtu anajua sana, matiti husisimka sana hasa kama utayachezea vizuri kwa kuyabusu, kuyalamba, kuyanyonya; ingawa ni vizuri kuwa makini na jinsi yeye anavyojisikia na uwe makini kujua yeye anataka ufanye vipi.
Wataalamu analinganisha kusisimka kwa chuchu ni sawa na kisimi hivyo ni muhimu kutumia utundu wote kumpa raha mpenzi wako hasa kama chuchu zake ni sensitive na zinampa raha zaidi.

TUMBO
Wakati unaendelea kumbusu kila sehemu ambazo unaona anapenda, unaweza kuendelea kuchezesha ncha za vidole vyako kwenye tumbo lake huku ukichora duara kwenye kitovu chake na kwa utundu na kuzunguka tumbo, wapo wanawake hupata raha sana kwa kitendo hiki.

NYUMA YA MAGOTI NA MAPAJA
Nyuma ya magoti kuna nerves na unaweza kushangaa mwanamke anavyojisikia raha kwa kupata busu, hasa busu la kipepeo.
Pia sehemu za mapaja ni sensitive kama utabusu, massage na kupitisha vidole kwa utundu (caress) wa kumpa raha.
Usipokuwa makini unaweza kuona anakulazimisha upeleke mkono kwenye machimbo haraka iwezekanavyo kwani atakuwa tayari ameshaanza kuzidiwa.

MIGUU
Wanawake wengi hupenda miguu yao kuguswa (touch) massage na wengine kubusu au hata kuinyonya.

MATAKO
Wanawake wengi hufurahia kuchezewa matako kwa kuyafinyangwafinyangwa.

MGONGO
Wapo wanawake hufurahi sana kufanyiwa massage na caress kwenye mgongo, anaweza kulala au wewe kuwa nyuma yake na tumia ncha za vidole vyako kuhakikisha unampa mguso wa uhakika kama vile una reki kutoka juu ya mgongo mabegani hadi chini kabisa kiunoni.

SEHEMU ZA SIRI
Hapo kuna uke na kisimi na ni dhahiri unajua nini kinatakiwa kufanywa hapo

MAENEO MUHIMU KTK MWILI WA MWANAUME.

Wengi hudhani mwanaume ana sehemu moja tu ya kusisimuliwa kimapenzi yaani uume, labda kwa sababu wao mara nyingi umeme huwaka haraka mno na kusababisha sehemu zingine zisivumbuliwe, unahitaji kuwa mbunifu ili uweze kuwasha moto unaotakiwa hasa kwa ajili ya foreplay.

KICHWA
Hapa tunazungumzia kichwa kilichopo juu ya shingo, wapo wanaume ambao unapopitisha vidole vyako laini ndani ya nywele zake kichwani hujisikia kusisimka sana hata kama anakipara wapo ambao ile kuguswa tu (massage) hupata raha kubwa sana.
Kibaolojia kwenye kichwa kuna homoni inaitwa endorphions inayohusika na kutoa raha kwa kuguswa (massage) hufanya kazi unapofanya hicho kitendo.

MASIKIO
Unaweza kubusu au kunyonya masikio yake taratibu kisha angalia ana respond namna gani. Pia unaweza kumnong’oneza au kutoa sauti yoyote unayoijua wewe ndani ya masikio yake na chunguza kama anapata raha au la.

MIDOMO YAKE.
Si kubusu tu bali pia unatakiwa kuienzi na kuendelea kuvumbua kuona ni jinsi gani anaweza kupata utamu zaidi kwa hizo lips zake.

SHINGO.
Busu shingo yake pande zote na pia unaweza kubusu kama unanyonya vile shingo yake, hakika atapenda.

MGONGO.
Wanawake wengi hupenda wanaume wenye misuli ya uhakika mgongoni na kifuani, lakini wakiwa faragha hawaifanyii chochote hivyo kifua na migongo yenye misuli, unahitaji kumpa massage au kumbusu mgongo wote kuanzia juu ya mgongo kupitia uti wa mgongo hadi chini.
Uti wa mgongo una nerves nyingi na ukifanya kwa ubunifu basi raha atakayopata ni ya ajabu.

MIGUU.
Wanaume wengi huwa hawajisikia vizuri kubusiwa au kufanyiwa massage miguu yao, hiyo inatokana na yeye mwenyewe alivyo, kitu cha msingi uliza kama anapenda au la kwani kuna wengine hujisikia raha sana.

SEHEMU ZA SIRI.
Huko unajua nini kinatakiwa na malizia mwenyewe!

UNAKIFAHAMU KISIMI/CLITORIS?

Kuchua / kusugua baadhi ya sehemu za mwili kunaleta raha na kumaliza ashki ya tendo takatifu la ndoa.
Kwa wanawake wengi kinembe/kisimi ndiyo sehemu haswa inayoleta raha.
Hii ni kwa sababu sehemu hii ina mishipa mingi ya kusisimua mara ikiguswa.
Njia moja ya kupata raha na kumaliza ashki ni kuchua taratibu sehemu hii.
Hii ni njia moja ya kutoshelezana kimahaba.

Kinembe au kisimi au clitoris au hot spot nk ni moja ya kiungo ambacho humsisimua mwanamke zaidi kuliko kiungo chochote katika mwili wake unaovutia. Hiki kiungo kipo eneo la juu zinapounganika kuta za ndani za uke (Labia minora).
Ni rahisi kukipata kiungo hiki kwa macho na kwa kugusa au kupapasa.
Kisimi hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, wengine ni kidogo sana na wengine huwa kikubwa zaidi.


Kisimi kina sehemu muhimu 18 na kile tunaona na kugusa kwa nje ni kitu kidogo sana ukilinganisha na siri iliyofichwa ndani.
Kwa nje kisimi kimejigawa katika sehemu kuu tatu kichwa, msukano (shaft) na mfuko ambao hufunika kichwa na msukano.
Mwanamke akisisimka kimapenzi kisimi hudinda au huongezeka au kutuna na kimfuko hurudi kwa nyuma na kichwa ambacho ni very sensitive hujitokeza na kuwa kigumu.
Kisimi kipo eneo la juu baada ya tundu la kibofu cha mkojo na chini ya tundu la kibofu cha mkojo kuna tundu la uke.
Ngozi laini inayofunika kisimi huwa na stimulation ya uhakika na kuna baadhi ya milalo huwezesha kusugua hii ngozi na mwanamke hujisikia raha zaidi wakati wa sex.

KAZI YAKE NI NINI?

Kisimi ni powerful organ kwa ajili ya raha ya sex kwa mwanamke, kina nerves zaidi ya 8,000 kuliko sehemu yoyote katika viungo vya binadamu; Ukweli ni kwa ajili ya kumpa mwanamke raha kimapenzi.
Kisimi kazi yake ni moja tu kumpa mwanamke raha ya mapenzi.
Na wanasayansi wamegundua kwamba chini ya kisimi kuna network ya tishu za msisimko, misuli, nerves na mishipa ya damu ambayo kwa pamoja huitikia na kujikunja wakati wa sex na kupelekea mwanamke kufika keleleni.

Tofauti na uume ambao hutoa mlipuko mmoja wa kufika kileleni kwa sekunde chache, kisimi hutoa mlipuko wa muda mrefu wa aina zaidi ya 100 za raha, Hii ina maana kisimi ni zaidi ya uume kwa kutoa raha ya kimapenzi.
Ole wenu mnaowafanyia ukeketaji wanawake, mna kesi ya kujibu! Kwani mnawanyima haki yao ya kuzaliwa kupata raha ya kimapenzi.

Je, wengi wanajua umuhimu wa kisimi katika raha ya tendo la ndoa?

Wanaume na wanawake wengi tunapozungumzia suala la sex huchukulia kwa mtazamo wa kiume (mfumo dume) kwa maana kwamba sex ni nzuri sana kwa wanaume na si wanawake na kwamba jukumu la nani aanze ni mwanaume na kwamba wanawake hawapo powerful kwenye sex kama wenzao wanaume.

Hata hivyo mwanamke akifahamu utendaji wa mwili wake kiungo baada ya kiungo anaweza kugundua na kuimarisha furaha ya tendo la ndoa akisaidiana na mume wake na moja ya viungo muhimu ni kisimi.
Na pia anaweza kufahamu ni namna gani anaweza kufika haraka kileleni kwa kujua kisimi kilivyo muhimu kwake.

Je, nini umuhimu wa kisimi wakati wa tendo la ndoa?

Wanawake wengi ili kufika kileleni ni muhimu sana kusuguliwa, kuchezewa kisimi.
Hii ni kwa sababu uke hauwezi kumpa direct stimulation wakati wa sex na pia mwanaume hawezi kusugua uke kiasi cha mwanamke kufika kileleni bali uke huweza kumpa mwanaume msuguano ambao humuwezesha yeye mwanaume kufika kileleni haraka.

Hii ina maana mwanaume anatakiwa kuelekeza nguvu nyingi kuhakikisha anasisimua kisimi kwa muda wa kutosha kuliko uume wake kuwa kwenye uke na kuusugua kwa skills zote badala ya kuelekeza skills zote kwenye kisimi.

Hii ina maana kwamba kama mwanaume anataka kufika kileleni haraka ni kwa mwanamke kumruhusu mwanaume kuingiza uume wake kwenye uke na mwanaume akitaka kumfikisha mwanamke haraka kileleni ni kumshughulikia mwanamke kisimi kwa skills zote.
Hii haina maana kwamba mwanamke hawezi kufika kileleni bila kisimi la hasha kwani anaweza kufika hata kwa busu, au kumpa mguso kwenye sehemu zingine za mwili, hapa tunazungumzia kisimi.

FAHAMU UTAMU HUU WA MWANAMKE..(PARTY 2)

Taratibu za mwanaume kumsaidia mwanamke kutoa divine nectar:

Divine Nectar huzalishwa na glands zinazojulikana kwa jila la Skene sawa na zile za Prostate ambazo hutengeneza sperms kwa mwanaume.
Fluid inayozalishwa na Skene si mkojo lakini hufanana na mkojo ingawa yenyewe huwa na glucose na prostatic acid.
Muundo wa kikemia wa hii fluid hufanana zaidi na semen za mwanaume ila hakuna sperm kuliko mkojo ingawa huwa majimaji kama mkojo.

Hii ni kujulisha kwamba mwanamke huweza kukojoa akifika kileleni na hutoa fluid ambayo hujulikana kama divine nectar au amrita au juice.

Wakati mwanamke anasisimuliwa kimapenzi au wakati wa mapenzi glands za Skene hutoa secretions ambayo husukumwa nje kwa speed kupitia urethra (kama mwanaume anavyotoa sperms)
Glands za Skene zimejibana kwenye ukuta wa kibofu cha mkojo na zipo upande wa juu wa ukuta wa uke pia zimetengenezwa kwa erectile tissues.

Divine nectar huweza kumtoka mwanamke baada ya kuponywa eneo la G- spot .
Kila mwanamke anauwezo wa kufika kileleni kwa kupitia G- spot na mwanaume ndiye anayeweza kusaidia.
Wewe mwanaume kwanza lazima uwe na mtazamo kwamba wewe ndiye healer au mtu wa karibu kumsaidia na zaidi wewe ndiye mtu wa ku-guide kwamba lazima mkeo atoe divine nectar.

Pia mwanaume lazima ufikirie pia hicho kipisi cha uume ni kitu ambacho unaweza kuingiza kwenye mwili wa mwanamke na ukishamaliza unatoa na kwenda zako.
Fikiria kwamba uume wako ni Nuru halisi ya kuangaza raha ya mwanamke katika mwili wake na kufungua roho na nafsi yake ili ajisikia ni mwanamke aliyekamilika kimwili, kiroho na kihisia.
Ili mwanamke aweze kuwa kisima cha kutoa divine nectar ni kupata uponyaji halisi wa eneo hili la G- spot au sacred area kwa kufanyiwa massage au kukandwa.

G- Spot ni eneo ambalo lipo upande wa mbele kwa ndani kwenye uke wa mwanamke na unapopitisha kidole utakugundua kwamba ni eneo vimikunjo kama lips za midomo na si smooth
Baadhi ya wanawake huweza kupatikana kirahisi na wengine ni ngumu zaidi ingawa mwanamke akiwa amesisimka huweza kupatikana kirahisi.

Hiki kitendo ni muhimu kifanywe na mwanamke kwa kujitoa kumpa raha mwanamke bila kutegemea kupata return yoyote kwake.
Kwanza mwanaume lazima ajenge trust kwa kumpa mahaba ya uhakika kwanza kwa kuanza naye kwanza kwa mwanaume kuhakikisha kucha za vidole vya mikono zipo safi na zimekakatwa vizuri then unaweza kwenda kuoga naye (kumuogesha au kuoga pamoja), pia hakikisha chumba umekiandaa na kuwa na sura ya kimahaba, unambusu passionately hakikisha mnapumua pamoja, huku mkitafakari mapenzi yenu kwa uwazi ili kuunganisha moods zenu na kupeana hamu zaidi kama si kuipa miili joto la kimapenzi.

Anza kwa kumfanyia Massage mapaja, hips, na eneo chini ya kitovu, panda tumboni na kuzunguka matiti, upande wa ndani wa mikono na rudi tena kwenye mapaja huku ukizambaza raha mwili wako wote ukirudi hadi dakika 5 hadi 10 hivi.
Hapo mwanamke atakuwa amerelax na yupo tayari kukuruhusu uendelee kwenye uke wake.
Then kwa upole kabisa anza kuchezea kwa ustadi kabisa kuta za nje za uke wake na kisimi kama vile ni vito vya thamani umepewa mikononi mwako.
Ni vizuri kumuuliza hasa ukiona ameanza kuhema tofauti kama unaweza kuingia kwenye sacred place au kwenye bustani .

Baada ya kuruhusiwa ingiza kidole (kidole cha kati huku kiganja kikiangalia juu) ndani ya uke huku ukichezesha au massage kwa alama kama vile unamuita mtu kwa kidole( njoo).
Ongeza mgandamizo kidogo ili na yeye asikie aina fulani ya mguso, endelea kuchezea kwa kuzungusha kidole chini na juu au kwa vibration, au zigzag au vyovyote hasa kutokana na yeye anavyo respond huku mkono mwingine ukichezea kisimi.
Pia unaweza kuongeza kidole kingine kwani baadhi ya wanawake hujisikia raha au kusisimka zaidi hasa kukiwa na vidole viwili.
Hakikisha macho yako na macho yake yanangaliana huku mkisamabaza umeme wa upendo baina yenu na huku kila mmoja akimsoma mwenzake anaendelea vipi
Pia wakati mnaendelea na hili zoezi ni vizuri mwanaume kuongea maneno mtamu yanayoonesha anafanya uponyaji wa hii sehemu huku mwanamke akimshukuru mwanaume kwa kazi kubwa anayofanya .

Kazi ya mwanamke kwenye hili zoezi la kufanya massage G-spot ni kulala, kuenjoy na kutoa feedback kwa mwanaume (ingawa mwanamke lazima ujiandae kwani unaweza kujisikia unataka kukojoa haja ndogo au unaweza kujisikia unataka kulia au unaweza kujikuta unakumbuka jinsi hisia zako zilivyoumizwa huko nyuma)
Hili kitendo lazima kirudiwe na kufanywa zaidi miezi miwili, mara mbili kwa wiki na kama kila kitu kipo shwari basi mwanamke anaweza kuanza kutoa divine nectar ingawa inatokana na historia yake ya mahusiano ipoje kama amewahi kubakwa au kudhalilishwa kijinsia au kuumizwa wakati wa tendo la ndoa huchukua muda mrefu kupata healing kwenye G spot.

Mambo ya msingi kuzingatia
Mwanamke au mwanaume kufahamu location ya G-spot
Uwezo wa kusababisha mwanamke akisijia raha (pleasure) anaposisimuliwa au kufanyiwa massage kwenye G spot
Mwanamke kuondoa hofu na mashaka au kujisikia anataka kutoa mkojo hasa anaposisimuliwa G-spot hivyo badala la kurelax anaweza kuwa na hofu

FAHAMU UTAMU HUU WA MWANAMKE.

Divine nectar ni
Kama maji vile ila ni fluid inayotokana na mfumo urogenital pamoja na glands za prostatic za mwanamke.
Huitwa divine nectar au Amrita au the foutain of youth.
Wapo wanawake ambao akifika kileleni (G- spot stimulation) huweza kutoa fluid mfano wa mkojo kupitia urethra huwa na sweet smell, huweza kujaa hata kikombe cha chai na huruka umbali wa futi hata 8 na kugonga ukuta wa chumba.

Huu si mkojo na ni haki ya kuzaliwa ambayo mwanamke amepewa na muumba wake hasa linapokuja suala la kufurahia mapenzi na mumewe.
Pia haya maji maji huitwa Amrita au Divine Nectar, au Fountain of Youth huu si mkojo hata kama hutoka kupitia njia ya mkojo ya kawaida.

Hiki ni kitu cha kawaida kwa mwanamke yeyote ambaye anapata mapenzi ya kweli na kukubali hisia zake na kufahamu mwili wake unavyofanya kazi akisaidiana na mpenzi wake.
Hii divine nectar imefahamika pia huweza kutokea hata pale mwanamke akifurahi jambo lingine na si lazima iwe mapenzi tu.
Hujasikia mwanamke alifurahia jambo akacheka na kutoa machozi na kukojoa?

Kila mwanamke anayo potential ya kutoa amrita au divine nectar ila ni pale tu atakapojifunza ku-surrender mwenyewe na kuwa na furaha ya kweli.

Wataalamu wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi wanandoa wameweza kuhusanisha suala la sex kwamba ni kimwili, kihisia na kiroho.

Mwanamke huweza kufikishwa kileleni kimapenzi kwa kusisimuliwa kisimi (clitoris), uke au G- spot.

Tofauti ya mwanamke kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi ni kwamba ile raha huja ghafla kama mwanaume anapofika kileleni,wakati kufika kileleni kwa uke au G-spot mwanamke hujisikia raha kama mawimbi (waves) kwenda mwili mzima.

Ndani ya uke sehemu ya juu ndani ya ukuta kati ya kufunguka kwa uke na cervix kuna eneo ambalo huitwa G spot na hili eneo liligunduliwa na Gynecologist Ernst Grafenberg mwaka 1944.

Hili eneo huweza kukua na kuhama ambalo wengi huliita ni sacred spot kwa mwanamke huweza kutunza kumbukumbu na hisia za kuumizwa (hurts and pains), infections, abortion, sexual abuse, magonjwa na kitendo cha kutotaka sex na kama hakuna healing huweza ku-shut down na kushindwa kutoa divine nectar.

Ili mwanamke aweze kutoa divine nectar ni lazima hili eneo liweze kuponywa au kuwa activated upya na mwanaume.
Activation hufanywa kwa mwanaume kumfanyia massage zaidi ya mwezi kwa kwa muda usiopungua nusu saa kila wakifanya mapenzi huku mwanaume akimpa mpenzi wake gentle and compassionate love making.

Sunday, 28 June 2015

KUBEMENDA NI NINI?

Kubemenda ni imani potofu (myth) na hakuna uhusiano wa sperms na maziwa ya mama katika kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa kushirikiana tendo la ndoa au kumshika mtoto baada ya sex.

Je, nini maana ya kubemenda mtoto?

Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto.
Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.
Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (sex) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu kama hicho.

kuhusu tendo la ndoa jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya kujifungua.

Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu

Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa kama suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.

Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa?

Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu.
Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?

Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote.
Ni jukumu la baba na mama wa mtoto kuhakikisha wanatumia muda wao kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua na kuwa na afya njema na si kujinyima kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia mtoto kuonekana amebemendwa.
Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto anapoishi (vyombo vya kutumia kwa chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa mtoto na mama na baba pia) ni muhimu sana kwani baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa mume na mke kuhakikisha wanakuwa safi tena bila kujihusisha na kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au kuoga.

Saturday, 27 June 2015

AINA ZA CHEATING.

Kama wanandoa wapo katika kufanya matengenezo ya damage iliyofanywa na mwanandoa mmoja kuchepuka basi ni muhimu kufahamu kitu ambacho wanashughulika nacho kwani bila kufahamu ni sawa na kumpa mgonjwa wa Malaria dawa za kutuliza maumivu ya meno.
Watu wanaotoka nje ya ndoa wamegawanyika katika makundi makubwa matatu ambayo ni:
1. KUCHEPUKA KWA USIKU MMOJA.

2. KUCHEPUKA KWA KUNASWA NA KUFUNGAMANA.

3. KUCHEPUKA KWA URAIBU.

UFAFANUZI ZAIDI:

1. KUCHEPUKA KWA USIKU MMOJA.

Hutokea katika jamii ambayo masuala ya sex yameilemea, kukosa uadilifu, kukosa nidhamu na kuheshimiana.
Katika modern world ambapo watu wanasafiri (business trips) sana basi cheating za usiku mmoja kwa wanandoa zimekuwa nyingi kuliko watu wanavyofikiria hasa baada ya wanawake kuingia kwa wingi katika ajira zinazowafanya wasafiri mara kwa mara.
Hii hutokea kwa kufanya sex kwa usiku mmoja (au mara moja) bila hata kuwa na uhusiano na baada ya sex wahusika hawajuani tena.
Wakishamaliza haja zao kinachofuata ni kumpiga chini huyo mhusika kama vile hawajuani.
Hutokea ghafla kutokana na kushindwa kuhimili tamaa za kimwili au kuwaka kwa tamaa.
Ni rahisi mhusika kurudi kwenye mstari kama vile Daudi alipokuwa confronted na Nabii Nathani aliutubu dhambi yake (2 Samuel 12)
Wanaume au wanawake wa hili kundi akibanwa na kukomaliwa anaacha na kugeuka.
Hii haina maana kwamba cheating kama hii haina damage kwani isiposhughulikiwa vizuri huweza kuzaa affair nyingine.
Kama umefanya affair kama hii na umeficha fahamu kwamba hilo ni bomu ambalo muda wowote linaweza kufumka na kuleta madhala katika ndoa iwe kukosekana kwa ukaribu na partner wako au kujiingiza zaidi kwa mwingine nje ya ndoa.

2. KUCHEPUKA KWA KUNASWA NA KUFUNGAMANA:

Hapa cheating huanza kwa mahusiano na urafiki na hatimaye kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa kudumu kwa muda mrefu na kuvunja hii bond huhitaji kazi ya ziada.
Hutokea polepole na baadae baada ya urafiki kukomaa kutokana na mazingira ya kufanya kazi pamoja au kuhusiana katika shughuli mbalimbali na kujenga urafiki na mahusiano.
Wanakuwa wame-fall in love kama mahusiano ya ndoa yanavyoanza.
Wanapokuwa pamoja hujikuta wanatimiza lile hitaji ambalo mmoja au wote wanakosa kwenye ndoa zao.
Hapa ndipo tunakutana na neno “nyumba ndogo”.
Huwa kazi sana kuvunja mahusiano kama hayo kwani watu hawa huwa na uhusiano unaohusisha mioyo na hisia zao.
Pia ili kuvunja uhusiano wao lazima mwanandoa ajue “hitaji” ambalo lilikuwa linakosekana nyumbani au katika ndoa hadi mwenzake akanasa kwa huyo mwanamke au mwanaume.

3. KUCHEPUKA KWA URAIBU:

Hutokea kwa kusukumwa hisia zake kwa kuwa hana uwezo wa kuhimili emotions ni kama mvuta sigara au mlevi wa pombe.
Haya ni mahusiano tofauti kabisa na kundi la kwanza na la pili hapo juu.
Kwa kuwa ana hisia zinazomsukuma anaweza kuathiri hata maisha yake kwani huwa Huyu huwa na msululu wa partners kila port meli yake inatua au mji.
ladha kutoroka kazi na kujiingiza katika sex haramu kama vile ukahaba, ubakaji, pornography na anaweza kukamatwa na polisi mara kwa mara kutokana na addiction aliyonayo kuhusiana na ngono.
Pia anakuwa na risk kubwa kupata magonjwa ya zinaa (bila kusahau UKIMWI) kutokana na tabia zake, wakati mwingine huuawa kutokana na kuwa violent.
Wakati mwingine anakuwa mwizi, mwongo ili kukamilisha kiu yake.
Pia huendana na tabia chafu na za ajabu zinazohusiana na masuala ya sex kama kubaka, sex kinyume na maumbile, kupigana nk.
Ili kuvunja tabia kama hii huhitaji ushauri kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya addictions ambaye anaweza kutumia approach tofauti na aina zingine.

FAHAMU HAYA KUHUSU CHEATERS

Katika asilimia 100 ya wanaume wanaotoka nje ya ndoa zao, asilimia 12 ya hao wanaume wanao cheat hufanya hivyo kwa sababu ni cheaters, wao hutoka nje ya ndoa zao No matter what!
Hata kama wanaridhishwa na wake zao zaidi ya kawaida bado akikutana na mwanamke mwingine bila kujali ana sura inayofanana na chimpanzee kwake ni mistress na atafanya kila analoweza ili kutembea naye (sex).
Ndoa iridhishe isiridhishe wao hutoka.
Wao hutoka nje ya ndoa zao kwa sababu ni cheaters tangu mwanzo.
Kama ni mwanamke utafanya kila ambacho mwanaume duniani anatakiwa kufanyiwa na bado atatoka; hawa ni vilema, hawana hisia, hawaijui kuumiza mke ni kitu gani, hawana adabu, hawana heshima, wameshindika.
Hawajali utu wao, vyeo vyao, umuhimu wao katika familia na jamii, wanatoka nje.
Je, tusemeje kwa ile asilimia 88 ya wanaotoka nje?
Hapa kuna kitu cha kujifunza, nacho ni kwamba kuna matumaini makubwa kwa wanawake wengi kwamba efforts wanazofanya katika kuhakikisha ndoa zao zinakuwa na afya ni jambo zuri na la msingi sana kwani hawa wa asilimia 88 huwa na sababu kamili inayowafanya kutoka nje ya ndoa zao. Hivyo mwanamke anayejituma kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri kwa mume wake kuridhika nyumbani husaidia kumlinda ndoa.
Mwanamke mwenye busara huwekeza efforts nyingi katika:
A. Kumfanya mwanaume ajisikie si mpweke katika ndoa yake.
B. Kumpa heshima (appreciation & respect) katika mahitaji yake kimwili na kiroho.

UMUHIMU WA TIMING KTK SEX

Moja obstacle ya kuridhishana kimapenzi kwa wanandoa ni suala la timing.
Tunaposema timing tunamaana kwamba badala ya jambo kufanyika katika wakati sahihi na hufanyika kinyume chake.
Mke anaweza kuanza kumsisimua mume (manually & orally) na baada ya mume kusisimka sawasawa wanaendelea moja kwa moja kwenye intercourse.
Kwa kuwa mume amesisimka zaidi kuna uwezekano mkubwa kwa mume kufika kileleni haraka sana na Kumwacha mke bila kuridhishwa.
Matokeo yake mke anakuwa frustrated kwani pamoja na juhudi zake za kumsisimua mume wake haikuchukua hata dakika 3 mume kumaliza.
(Kufika kileleni wakati mke kwanza bado ndo alikuwa anaanza kufurahia).
Je, ushauri muhimu ni upi?
Jawabu rahisi ni kuwa na timing nzuri; baada ya mke kumsisimua mume kwa uhakika inatakiwa mume apumzike huku mume akiendelea kumsisimua mke kwa kiwango cha kukaribia au hata kumfikisha mke kwa mara ya kwanza kileleni (manually & orally) na ndipo mume aanze kumuingia mke (intercourse).
Kwa njia hii mwanamke huwa tayari yupo njiani au tayari kufika kileleni na mume atakuwa anaanza upya kusisimka (amezitunza risasi zake) na inamchukua muda zaidi kufika kileleni na anaweza pia kufika kileleni wakati mmoja na mke wake.
Pia ni muhimu kwa mke kuwa wazi kwa mume wakati wa intercourse kumwelekeza mume namna na kiwango cha thrusting anayohitaji kutokana na msisimko anaoupata kwa kupunguza au kuongeza speed.

MKE MMOJA,MUME MMOJA.

Kuna neno moja ambalo ni neno la msingi na muhimu sana linapokuja suala la ndoa hasa katika lugha ya kingereza nalo ni loyalty.
Maana ya hili neno ni kuwa mtiifu, au mwaminifu kwa hali ya juu iwe katika biashara au mahusiano nk.
Ni neno linalofanana na neno allegiance, truth, faithfulness.
Mke wako anafahamu kwamba yeye ni mke wa mume mmoja, anajijua kwamba yupo committed kwako 100%
Lakini kuna wakati mke wako Hujiuliza maswali kama ni kweli wewe ni mume wa mke mmoja, hasa pale anapokuona unavutiwa na mrembo/warembo unaokutana nao mtaani au hata kwenye TV.
Ni kweli ulikubali kwenda mbele ya kanisa ili kukubali kwamba unataka kuwa na ndoa ya mke mmoja hata hivyo namna unaishi na yeye inampa wasiwasi kwamba wewe ni mume wa mke mmoja.
Mke wako amekuwa insecure kwenye eneo hili na anahitaji reassurance na si wewe kumtania au kuleta dhaka au kuleta mahoka au kufanya masihara au kuleta mizaha au jokes au kuleta matani au kutumbuiza au kufanya Vichekesho au michezo.
Yupo serious anahitaji umuhakikishie kwamba wewe ni mume wa mke mmoja kama ulivyomuahidi hata ukaamua kufunga naye ndoa takatifu ya mke mmoja na mume mmoja.

Je, umewahi kufikiria namna ilivyo ngumu kwa mke wako kukuamini kwamba wewe ni mume wa mke mmoja hasa kutokana na wanaume wengi wanavyo- cheat, dunia inavyopambwa na kila aina ya warembo, dunia ilivyojaa wanawake wanaoshawishi wanaume kwa kuvaa wanavyotaka wao, namna Tv, Radio na internet zinavyopotosha watu kuishi kwa uadilifu katika ndoa?
Unahitaji kumhakikishia kwamba wewe ni mume wa mke mmoja!


Wanaume wote tunahitaji kujifunza kuwa

Mke anapokuwa na uhakika kwamba mume wake amefanya agano (covenant) na Mungu kwamba atajitahidi kumfanya Mwokozi wa maeneo yote ya maisha yake pamoja na ndoa yake mke hujisikia salama.

Mke anapokuwa na uhakika wa upendo na uaminifu wa mume wake kwake anajisikia kuwa na nguvu na kuhamasika kuhakikisha ndoa inakuwa bora zaidi.

Hii ni kutokana na namna Mungu amemuumba mwanamke na ndiyo maana agano la ndoa lina msingi wa kuaminiana (loyalty) hadi kifo kwa wawili (mke na mume) wanapooana.


Mke hujisikia mume anaonesha loyalty pale;

Anapomuongelea vizuri mbele za watu,

Anapojihusisha na mambo mazuri kuhusu mke wake,

Anapomsaidia kutoa maamuzi yanayohusiana na watoto wake,

Anapokuwa hamsahihishi mbele za watu.


Pale anapokuwa hawatamani wanawake wengine,

Pale anapofanya ndoa kuwa kitu cha kwanza,

Anapokuwa hamlalamikii (critical) mke mbele za watoto na watu wengine,

Pale anapohusishwa katika mambo ya jamii hata kama wengine wanaona aibu kwenda na wake zao,

Pale anapowaambia watoto wanatakiwa kumheshimu mama yao,

Pale anapoongea positively na si negatively.

NB:
Mke uliyenaye anakutosha

KWANINI WANAWAKE HUBADILIKA?

Wanaume wengi walio katika ndoa hulalamika kwamba hawapati sex kiasi cha kutosha kutoka kwa wake zao kama ilivyokuwa zamani au mwanzo wa ndoa zao.
Wanaume hawa hushangaa ni kitu gani kimetokea kwa wake zao ambao si suala la kupoteza hamu ya sex tu bali hujisahau na kuacha kuwa na mwonekano unaovutia kimapenzi.
Ni kweli wanawake wanafahamu sana namna ya kumvutia mwanaume wanayemhitaji na hii hujidhihirisha pia siku za uchumba au mwanzo za ndoa ambapo mwanamke hupendeza kimavazi na hata kunukia.
Enzi zao wakati wa uchumba au ndoa ilipokuwa mpya huweza mwanamke alivalia nguo zinazovutia na kuonekana ni mke na si mama, alichagua nguo za kuvaa chumbani (sexy) na za kuvaa sebuleni au kazini. Alijipamba kwa makeup za uhakika kuanzia kwenye kucha za miguu hadi nywele.
Alijipulizia delicious perfumes kama moja ya strategy kuhakikisha mume anavutiwa na anatulia ndani.
Ukirudi kwa namna alikuwa anaongea kwa sauti ya Urembo basi mwanaume alijiona kama ni ndoto za kumpata mwanamke anayemtaka zimetimia.
Hata hivyo baada ya miaka kadhaa na watoto kuzaliwa mke badala ya kuwa mke sasa amekuwa mama, na mama kwelikweli kwani kuoga kwenyewe kazi hadi muda wa kwenda kulala, mwili mzima ni maziwa ya mtoto ndo imekuwa perfume, kajichokea mwenyewe kama kuolewa ameolewa who cares!
Mume anashangaa hivi ndo huyu mwanamke wa wakati ule mboni sasa hata kuoga hadi nimkumbushe!
Sex ndo usiseme ni kuvutana kama manati!
Sex ilikuwa mara 3 au 4 kwa wiki sasa ni mara moja napo lazima mwanaume akomae maana bila kukumbushia mwezi unapita.
Mwanaume anajikuta thamani yake ni sawa na kipande cha furniture
Kila kitu sasa kimekuwa watoto kwanza na wewe mume ni mtu mzima subiri.
Hata hivyo tukumbuke kwamba:
Kuwa mwanamke katika ulimwengu huu wa kisasa ni kazi sana kwani mwanamke huyohuyo mwenye mtoto ndiye Anafanya kazi zote za nyumbani na ndiye anaenda ofisini na ndiye Anahakikisha mume ametimiziwa mahitaji yake yote. Mke akifika muda wa kwenda kulala anakuwa amechoka na hatazamiki.
Hivyo kukosa hamu ya sex huja bila yeye kuwa na uwezo wa kufanya chochote kwani majukumu na kuwajibika ndiko kumemfanya kujisikia hivyo.
Na wapo wanaume huchukulia wake zao “for granted” na huhitaji sex wakati siku nzima hajafanya jambo lolote kumsaidia mke na hata kuwasiliana naye acha kuonesha upendo.
Ukweli ni kwamba:
Ndoa ni kazi (hard work) ambapo mume na mke wote kwa pamoja hawatakiwi kuanza kulaumiana badala ya kushirikiana pamoja kwanza kusaidiana kazi za nyumbani na mume kumtengenezea mke wake mazingira mazuri ambayo atajisikia hajachoka.
Binadamu ni wepesi sana kulaumu mwingine pale mambo yakiwa yanaenda visivyo na wanandoa kwa hili ndo wenyewe.
Kuimarisha afya ya uhusiano wa kimapenzi kati ya mke na mume ni kazi inayoendelea maisha yao yote ya ndoa.
Kuonesha upendo kwa vitendo na mawasiliano mazuri ni mambo muhimu sana kwa ndoa imara.
Ndiyo kuna wanawake ambao baada ya kuolewa na kuzaa watoto hujisahau, hata hivyo wengi ni kutokana na wanaume wenyewe wanavyochukulia ndoa zao.
Kama ni mwanaume unahitaji mke awe na hamu ya sex basi unahitaji kumjengea mazingira ya kuhitaji sex na si kulaumu tu.

MTAZAME KISHA MSIKILIZE..

Kuna usemi mmoja mzuri sana kuhusu maisha nao ni;
TAZAMA,KISHA SIKILIZA

Kwa kuangalia matendo ya mchumba wako na kusikiliza kile anaongea kwa umakini wa hali ya juu itasaidia kufahamu kama ni kama si mwaminifu (cheating).

Kama wewe ni mwanamke (binti) ambaye una mchumba ambaye umegundua kwamba si mwaminifu au hujajua kama ni mwaminifu au la, unachotakiwa kufanya kwanza ni kumuangalia anayofanya na kumsikiliza anavyoongea na utapata jibu.


Kawaida watu hukwambia na kukuonesha wao ni akina nani muda wote, na ni muhimu sana kuwa makini (pay attention) na nini kinaendelea katika usemi na matendo.

Msikilize kila kitu anachoongea na hakikisha kinaingia kwenye sikio na unakitafakari kwa makini na wakati mwingine unatakiwa kusikiliza hata kile ambacho hasemi (meta message).

Matendo huongea zaidi kuliko maneno yoyote, na kile anafanya mchumba wako huelezea namna anaweza kuwa na wewe.



Hatua muhimu ambayo mwanamke yeyote anaweza kufanya kwa mchumba wake asiyemwaminifu (cheating) kwanza ni kukubali kwamba mchumba wako si mwaminifu. Kubali kwamba kuna mwanamke mwingine zaidi yako ambaye mchumba wako anampenda.

“Huwezi kufanya maamuzi Kama hutakubali kwamba yeye si mwaminifu”


Mara nyingi mwanamke akiwa kwenye mapenzi (love) au mahusiano ya uchumba huwa kipofu wa kufahamu vizuri mwanaume na namna alivyo, unaweza kupewa taarifa kwamba mchumba wako si mwaminifu na ukaendelea kukataa.

Hivyo kukubali kwamba mchumba wako amekuwa si mwaminifu ni hatua ya kwanza na pia kuwa kipofu wa kudhani si mwaminifu wakati unajua kwa matendo yake si mwaminifu haitakusaidia lolote.


Hatua ya pili baada ya kukubali kwamba mchumba wako si mwaminifu ni kutojilaumu wewe mwenyewe.
Kawaida mwanamke anapopata mchumba na mchumba akawa si mwaminifu huanza kujisikia kama amefanya kitu kisicho sahihi au kujisikia ana hatia.
Mwanamke huanza kujimaliza mwenyewe (tearing) na kuanza kujiuliza kuna kitu gani kibaya anacho katika maisha yake au amefanya hadi mchumba wake akaanza kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine.
Lazima ujikubali kwamba hujafanya kitu chochote kibaya hadi yeye akawa si mwaminifu, hakuna uhusiano wa namna wewe ulivyo au unavyofanya na tabia yake ya kuwa si mwaminifu.
Huanza kupoteza kujiamini (self esteem) eti kwa kuwa mchumba wake amepata mtu mwingine.
Wewe ni mwanamke yuleyule ambaye alikuhitaji mara ya kwanza uwe mchumba wake, hujabadilika kamwe!
“Nothing is wrong with you at all”
Pia haina haja kujilaumu kwa kuwa mchumba wako amekuwa si mwaminifu.
Je, utatoa uamuzi gani kwa mchumba asiye mwaminifu?
Kawaida unaweza kuwa na maamuzi katika sehemu mbili tu, kwanza kuendelea naye au pili kuachana naye.
Kama utaamua kubaki au kuendelea na uchumba kwa mwanaume ambaye si mwaminifu lazima umkubali kama alivyo na hakuna kitu utafanya au sema kitaweza kumbadilisha asiwe mwaminifu.
Kumpeleka kwa wazazi wako ukamtambulishe hakuta mbadilisha, kununua simu mpya ili aachane na wanawake anaowasiliana nao haitambadilisha, yeye kukuomba msamaha mara kwa mara haitambadilisha, wema wake kwako hautafanya abadilike, kukununulie gari hakutafanya abadilike, kukununulia kuku na chips hakutafanya awe amebadilika, kumchunga kwa kutumia secret detective agent hakuwezi kumbadilisha kamwe, kupanga siku ya harusi hakutambadilisha, kumuahidi mambo mengi mazuri hakutambadilisha kamwe.
Usiishi kwa kujikana kwamba eti hatarudia au ataacha kutokuwa mwaminifu.
Hivyo kama umemkubali kuendelea naye pamoja na tabia yake ya kutokuwa mwaminifu maana yake unakubali kuendelea naye huku unajua hataacha kutokuwa mwaminifu na hata akiendelea kutokuwa mwaminifu kwako itakuwa sawa tu na haita kuwa tatizo ndiyo maana unaendelea naye.
Ni uamuzi wako umeamua kuishi hivyo na huyo cheater.
Uamuzi wa pili ni kuachana naye; kama umeona huwezi kuishi na mwanaume asiyemwaminifu basi kubali kuacha naye.
Huyu mtu hawezi kukupa kile unahitaji; katika maisha ukweli una haki ya kuishi na mwanaume ambaye ni mwaminifu.
Hata kama unaachana naye kwa mateso, kwa maumivu ni afadhari uteseke kwa miezi kadhaa kuliko mateso ya miaka 20 au 30 au 40 utakayoishi naye kwenye ndoa ambayo kila siku ni “homa ya jiji”

NAMNA YA KUMSAHAU MPENZI ULIECHANA NAE.

Namna ya kumsahau mpenzi uliyemwacha kwa sababu za kukosa uaminifu na namna ya kuuponya moyo ulioumizwa.
Na pia namna ya kurudi katika hali ya kawaida baada ya kuachana.

Mahusiano ya uchumba yanaweza kuwa complicated kiasi cha kuweza kufikia hatua ya wawili waliopendana kuachana.
Kibaya zaidi ni kwamba wakati wawili waliopendana wakiachana mmoja wao huvunjwa moyo na kupata maumivu yasiyoelezeka kiasi cha kuwa na wakati mgumu kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Huumiza sana kusahau mambo yote (story, memories, ndoto na plan za maisha) ambayo walifanya pamoja.

TUKUMBUKA KWAMBA:
Kuuponya moyo ulioumizwa huchukua muda na uvumilivu.

Tuangalia hatua zifuatazo ambazo zinaweza kuwa mwongozo katika kuponya moyo wako ulioumizwa na kusahau kabisa yale yaliyotokea.


1:-Toa machozi kwa kadri unavyoweza na lia kwa kila sababu unazoamini zimefanya uumie.
Ukiwa umeumizwa ni kawaida au vizuri kulia machozi kwa uwezo wako wote.
Usifikirie kabisa kwamba eti kulia machozi ni kuonesha wewe ni dhaifu, kulia machozi ni kitu cha kawaida na vizuri sana kulia machozi baada ya kuumizwa.
Unapolia machozi unaondoa hasira na kuumia na kujiona umetua mzigo mzito.
Kama unaweza jifungie chumbani, jifungie weka muziki wa sauti ya chini, halafu ruhusu maumivu uyasikie na lia kwa machozi hadi unahisi mzigo kuwa mwepesi.
Jambo la msingi hapa ni kuondoa maumivu na ruhusu maumivu yaondoke.


2:- JISHUGHULISHE. (busy)

Ukitaka kumuondoa mtu kwenye kichwa chako lazima uweke vitu vingine humo kichwani mwako.
Fanya kitu chochote kinachoweza kufanya ubongo wako ujishughulishe ili kuharibu wazo la kuanza kumfikiria yeye.
(fanya kazi yoyote, angalia movie [siziwe movie za mapenzi], safari, shiriki michezo yoyote)
Tafuta kitu ambacho unakipenda kufanya, kitu kinachofanya akili yako kuwa busy ili kuziba nafasi ya kumfikiria mtu ambaye unajitahidi kumsahau katika maisha yako.


3:- TUMIA MUDA WAKO NA RAFIKI ZAKO.

Marafiki ni muhimu sana hasa katika hatua au nyakati kama hizi.
Kwani wanaweza kukufanya ujisikie vizuri na kukufanya wazo la huyo mtu kutokuja kirahisi.
Marafiki huweza kukufanya ucheke na kujiona wewe ni muhimu sana kwao.

ONYO
Waambie mapema rafiki zako wasiongelee kabisa kuhusu huyo mtu ambaye unajitahidi kumsahau.
Wakifanya kosa la kumtaja mara kwa mara unaweza kujikuta badala ya kucheka unaweza anza kutoa machozi.
Hivyo uwe mkweli na waambie wasimtaje kamwe.

Step 4:
4:-MKWEPE, EPUKANA NA HUYO MTU.

Usiende sehemu ambazo unaweza kukutana naye.
Kama unataka kumsahau mtu na unaendelea kukutana naye, huwa ngumu sana kumsahau.
Ukikutana naye Mahali uwe mwema tu, ila haraka iwezekanavyo mpige chenga na kwenda zako kama vile wametangaza kwamba kuna terrorist bomb limefichwa hilo eneo.
Kama unafanya naye kazi ofisi moja au unasoma naye darasa moja (chuo) basi inabidi usiwe unamwangalia sana na kuongea naye, uwe mwema tu na busy na mambo yako.


5:-USIJIFUNGIE NDANI, TOKA NJE KUTANA NA WATU WENGINE WAPYA.

Kujifungia ndani kwa muda mrefu huweza kusababisha process kuwa ngumu zaidi, hata kama unajisikia huna mood unachotakiwa kufanya vaa vizuri (pamba za uhakika, viatu cha uhakika, smile la uhakika) waite rafiki zako na mnaweza kwenda sehemu mkafurahia maisha (siyo kuutwika na uhuni) bali mambo mazuri.
Ukirudi nyumbani baada ya kuwa na rafiki zako na kuonana na watu wengine wapya utagundua kwamba yule uliyeachana naye kumbe si peke yake mwenye smile zuri au sauti, wapo na wengine.
Mungu apewe sifa kwani kuna watu wengine wenye sifa nzuri kuliko huyo unayetaka kumsahau wapo huko nje wanatafuta watu wenye misimamo mizuri kama wewe.


6:-EPUKA VITU VINAVYOHUSU MAPENZI.

Kama unataka kumsahau mtu ni muhimu sana kujiepusha na kusikiliza miziki inayoimba mambo ya mapenzi, movie zinazohusu mambo ya mapenzi kwani huweza kukufanya ujisikie vibaya na kuanza kumkumbuka yule mtu ambaye kwanza ndo unataka kumsahau.
Haijalishi ni Wimbo unaoupenda kiasi gani kama unaimbwa Radioni badilisha channel, na weka nyimbo za furaha (gospel songs ni nzuri sana)
Jambo la msingi unatakiwa kuepuka ni kitu kinaitwa mapenzi kwa wakati huu.


7:- JIFUNZE, JILINDE, JIPE FURAHA.

Wanawake wengi baada ya kuumizwa huanza kujimaliza wenyewe.
Si busara kuacha kujipamba na kuanza kujinenepesha kwa chocolate na sukari eti kwa sababu huna mtu, au kumkomoa uliyeachana naye.
Kinachotokea unakuwa huvutii na unapoteza kujiamini (self confidence).
Usiruhusu maumivu ya kuachwa au kuachana kukumaliza wewe mwenyewe.
Fanya mazoezi, kula chakula bora, fanya kazi, jipambe zaidi ya zamani ili ujisikia mzuri na ujiamini.


8:-KUBALIANA NA HATUA ULIZOCHUKUA.

Unaweza kuwa upo imara sana katika haya maamuzi ya kuamua kuachana na kuponya moyo wako na bado moyo ukaendelea kuumia.
Kumbuka hizi ni hatua na hatua hizi huchukua muda na uvumilivu na lazima ukubaliane.
Huwezi kumsahau mtu kwa siku 5 kama ulipendana naye kwa miaka 3.
Huwezi kujifanya upo imara na huwezi kulia machozi, kubali na kabiliana na hiyo hali hata kama itachukua muda.
Unapokuwa na subira, mambo huwa rahisi sana baadae.

UNATAKA MUME AKUPENDE.

Haijalishi ni kazi gani mume anafanya anastahili kupewa appreciation!

Wanaume wakikutana wenyewe kwa wenyewe kama hawafahamiani swali la kwanza kuulizana ni “unafanya kazi gani?”
Sababu ya msingi ni kwamba wanaume wengi suala la kazi ni kitambulisho (identity)
Ndivyo walivyoumbwa na Mungu na hiki ni kitu wanachozaliwa nacho kujikuta ni mtu wa kwenda kuwinda, kulima, kufanya kazi kwa ajili ya familia yake.
Kufanya kazi ni jambo la msingi kwake.
Akipata ugonjwa anaweza kupigana na kuhimili kila aina ya msongo wa mawazo au mgandamizo wa damu hata hivyo linapokuja suala la kazi kwake huwa maumivu ni makubwa kiasi cha kuwa na stress au depression.
Mwanaume anaweza kusimama imara hata katika ugonjwa unaoleta mauti kama cancer lakini si suala la kupoteza kazi au business.
Mwanaume mmoja baada ya kufanya deal la uhakika kwa kutengeneza Mamilioni ya pesa, kwa furaha akaenda nyumbani kwa mke wake kumwambia hizo habari njema na mke wake akamjibu kwa mkato “sawa nimekusikia” kisha akaendelea na kazi zake pale nyumbani.
Mume alikatishwa tamaa na kuvunjwa moyo kiasi cha kutoa maamuzi kwamba kuanzia hapo hatamshirikisha mke wake jambo lolote au maamuzi yoyote kwani hakutegemea kama mke wake angejibu kwa mkato vile na kuonekana alichofanya hakina maana.
Wanawake wengi hawafahamu umuhimu ambao wanaume wameuweka katika kazi zao na kwamba ukimshukuru kwa kazi anayofanya basi anaweza kukuonesha upendo wa ajabu.
Fikiria wewe ni mwanamke sasa umegundua kwamba ni mjamzito na unaenda kumweleza mume wako naye anakujibu “sawa” kisha anaendelea kuangalia TV utajisikiaje?
Basi ndivyo mume wako hujisikia pale Unapokuwa hutambua kazi yake hata kama wewe unafanya kazi na kupata fedha kubwa zaidi.
Mwanamke anaweza kuamua au kuchagua kufanya kazi au kuwa nyumbani na kulea watoto, hata hivyo mwanaume anaweza kuchagua kufanya kazi au kwenda jela.
Ni kweli mwanamke mwema huolewa kwa sababu ya UPENDO na si FEDHA, hata hivyo mwanamke huyu mwema huwa na hekima na maarifa ya kufahamu sifa ya ndani ya huyu mwanaume kama anaweza kujenga kiota na kuhudumia vifaranga kwa chakula, mavazi na malazi maisha yao yote.

Je umewahi kumshukuru Mume wako kwa kazi anayofanya?
Kwa mwanamke ambaye anataka kuonesha respect kwa mume wake anaweza kujaribu kuandika hata message au note na kuiweka hata kwenye Lunch box yake na kumwambia “ mpenzi mume wangu nashukuru sana kwa namna unajituma kufanya hiyo kazi kwa ajili ya familia” au vyovyote unavyotaka wewe.
Pia unaweza kumshukuru kwa uhuru aliokupa wewe mwanamke kufanya kazi au kukaa nyumbani na yeye kufanya kazi.
Wapo wanawake ambao huwaza mara kwa mara kwamba wangewashukuru waume zao kwa kufanya kazi, hata hivyo kuwaza peke yake si lolote unachotakiwa kufanya ni kumshukuru au kumwambia.
Je, utajisikiaje mume ambaye anasema kwamba huwa anafikiri mara kwa mara kukwambia anakupenda na hajawahi kukwambia anakupenda!
Ukweli mahusiano ni two way street, mume anatakiwa kukwambia “ANAKUPENDA” na wewe unatakiwa siku moja kumwambia mumeo “Asante sana nashukuru kwa kazi unayofanya ambayo inatupa fedha na maisha”
Nakuahidi atafanya mambo ya ajabu sana kuhusiana na kukupenda wewe kwa sababu ataamini wewe ni mwanamke ambaye unaamini katika yeye.
Mume wako anajiona unamshukuru kwa kazi anayofanya pale tu
Pale unapomwambia kwa maneno au maandishi kwamba kile anafanya kina maana kwako na familia.
Unaelezea imani yako katika taaluma yake.
Unasikiliza stories mbalimbali kuhusu kazi zake na taaluma yake, inaweza kuwa ni magari, ualimu, Computer, forestry, nk.
Kumsaidie kukamilisha ndoto zake kama wakati ule wa kuchumbiana.

Friday, 26 June 2015

WAFAHAMU WANAUME

Kwa nini wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.

wanaume huwa frustrated na wanawake kwa kuwa hawapendi sex na wanawake huwa frustrated na wanaume kwa kuwa kila mara wao ni sex tu.
Wanawake wanawalaumu sana wanaume kwa kuwa hawajui kupenda na wanaume wanawalaumu sana wanawake kwa kuongea tu kuhusu upendo lakini hawataki kuonesha vitendo (kufanya mapenzi).

Sababu inayofanya binadamu kujihusisha na sex ni kutokana na hormone ya testosterone, ambayo kwa kiwango kikubwa ni hormone ya wanaume.
Mwili wa kawaida wa mwanaume huzalisha mara 20 zaidi ya mwili wa mwanamke.
Kwa maneno mengine, hamu ya sex kwa mwanaume katika siku moja ni sawa na hamu ya sex kwa mwanamke baada ya kukosa sex kwa siku 20 au hamu ya kuhijitaji sex kwa mwanaume katika siku 20 ni sawa na hamu ya mwanamke kukosa sex kwa mwaka mzima.

Kwa kufahamu hizo tofauti hadi hapa unaweza kufahamu maumivu ambayo jinsia nyingine inayapata.

Kumbuka wanaume kuhitaji sex hadi kupitiliza hawajasababisha wao au ni kitu wanajitakia bali ndivyo wameumbwa na hizi ni sababu zinazofanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke.
Wanaume na wanawake ni tofauti.


Mwanaume anaweza kuzalisha au kusababisha mimba kwa mwanamke kila anapofanya sex, lakini mwanamke anaweza kuzaa mtoto kila baada ya miaka 2; hii ina maana mwanamke lazima awe makini kuchagua sana mwanaume wa kuoana naye ili kuzaa naye watoto.
Lazima achague the best seed.
Kwa miaka mingi (generations) wanawake wamekuwa wakilipa gharama kutokana na kuchagua wanaume wasiofaa (mbegu dhaifu); kwani wanawake waliochagua wanaume wenye udhaifu wa genes wamesababisha kuwa na watoto ambao imekuwa si rahisi kuishi (survive); wanawake waliochagua wanaume wenye genes imara wamezaa watoto imara ambao waliishi, na hawa ndio wanabeba genes za mama zao za kuwa wachaguaji wa kupitiliza linapokuja suala la kuoana hadi leo.

Kwa asili wanaume huhitaji sex mara kwa mara ili kusambaza kizazi wakati wanawake huhangaika kutafuta the best seed ili kuwa na maamuzi bora ya kupata mbegu bora ya kuwa na kizazi bora.

Ndiyo maana wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.

Upendo ni uhakika ambao wanawake huhitaji kwa mwanaume ili kuhakikisha atashikamana naye kusaidia kulea watoto na kuhakikisha wanakua, na sex kwa mwanamke ni kitu cha ziada anachotoa kwa mwanaume ili awe committed kwake.

Kwa mwanaume sex ni kitendo cha kimwili ambacho husaidia kupunguza msukumo wa hormone ya testosterone ndani ya mwili wake na baada ya kufanikisha ndipo mwanaume huanza kuhisi upendo kwa mwanamke au hujikuta mwanamke huyo hana thamani tena kama hakuna commitment (ndoa)
Ndiyo maana wanaume wengi hupotea baada ya kukipata kile walikuwa wanakitafuta kwa mwanamke kwa kuwa issue nzima ilikuwa ni testosterone na si upendo.
Ndiyo maana mwanamke kumpa mwili mwanaume mapema kabla ya ndoa ni hatari sana kwani wanawaume wengi huwa hawajawa tayari kupenda (huwa anakuwa bado hajampenda mwanamke bali ni msukumo wa testosterone).
Mwanaume huhitaji muda ili feelings zake ziwe developed na njia sahihi ambayo mwanamke anaweza kufanya ni kukaa mbali na maombi yake ya sex.
Kama ataweza kujizua kufanya sex maana yake ataweza kujenga upendo wa kweli ambao ndiyo msingi wa mahusiano, kinyume na hapo baada ya sex ataishia na mwanamke atajikuta anakuwa mtumwa.

sababu ya wewe kuwepo hapa leo ni kwa vile ancestors, wanaume na wanawake walifanya maamuzi sahihi na wakaweza kuvutia partner sahihi (best seed) ambaye leo wewe upo.
Hivyo haina haja kujisikia uchungu sana kwa mume kuhitaji sex mara kwa mara na mke kuhitaji upendo au kupendwa mara kwa mara.

FAHAMU HAYA KUHUSU MWANAUME

Wakati mwingine ni vigumu sana kwa wanawake kufahamu ni kiasi gani hamu ya kufanya mapenzi ilivyo kwa mwanaume.
Ingawa wanaume hutofautiana katika kiwango cha hamu ya mapenzi bado wanaume wanaonekana wapo juu katika hamu ya mapenzi kuliko wanawake.
Wataalamu wa masuala ya mapenzi (sex) wanasema kwamba mwanaume ni mtu wa mzunguko wa siku tano ( kwa maana kwamba huhitaji sex kila baada ya siku tano) na wakati huohuo mwanamke ni mtu wa mzunguko wa siku kumi ( kwa maana kwamba huhitaji sex kila baada ya siku kumi), kuna kaukweli fulani katika hili.
Hata hivyo kuna wanaume wengi sana hasa vijana wao hupenda kupata sex ikiwezekana kila siku na pengine wangependa iwe zaidi ya hapo kama miili yao ingeruhusu.
Je, hii ina maana gani kwako mwanamke?
Hii ina maana kwamba mume wako anapenda sana sex.
Pia anawaza sana kuhusu sex kila mara kuliko wewe unavyowaza kuhusu sex.
Haijalishi ni gentle and romantic kiasi gani lakini mwisho wa siku anachowaza ni kufanya sex na wewe.
Kwa kuwa ana drive kubwa ya sex kuliko wewe na anajisikia kufanya mapenzi na wewe, ukimzungusha anaweza kuchukua risk kubwa sana ya masuala ya sex bila kujali consequences zitakazompata (kutokuwa mwaminifu kwako, kulipa fedha apate sex nk).
Pia fahamu kwamba mwanaume humpenda mwanamke kwa mtindo wa vipande vipande kwa maana kwamba anaweza kuvutiwa na namna mwanamke anaonekana sura yake, miguu yake, matiti yake, meno yake akicheka, kiuno chake, makalio yake na wakati mwingine hata perfume ambayo mwanamke amejipiga.
Hivyo basi kama wewe ni mwanamke unasoma hapa hata siku moja usitanie kuhusu nguvu aliyonayo mume wako kuhusu sex.
Unatahadhalishwa!

FAHAMU HAYA KUHUSU WANAWAKE.

Sababu za kuwa na migogoro kati ya mume na mke mara nyingi ni kwa sababu wanaume hawawaelewi kabisa wanawake na wanawake wanawaelewa vibaya wanaume .
Kibaya zaidi wanaume mara zote huendelea kufanya kinyume na vile wanawake wanategemea wafanyiwe na waume zao.
Na wanaume nao wanawashangaa wanawake namna wanavyobadilika kila mara kwani unaweza kumkuta mke dakika moja yupo na furaha na kicheko na baadae kidogo anajikunyata na kuhuzunika na wanaume huwaona wanawake ni viumbe wa ajabu sana chini ya jua.
Linapokuja suala la kutafuta mpenzi (mume mtarajiwa) wanawake wanatabia ya kumkubali na kumshika mwanaume mzima mzima. Na hutumia akili kuhakikisha anamnasa hata kwa kujipitisha sehemu au njia ambazo anaamini anaweza kukutana naye.
Kama anajua mwanaume yule hupatikana maeneo fulani na anampenda basi hujipeleka hilo eneo ili wakutane ili iwe coincidence fulani.
Atasubiri hako kanafasi ili wakutane ghafla.
Mwanamke hutumia njia ya hisia anapoingia kwenye suala la mapenzi na kuwa karibu na kifua chake (moyo) si mwonekano kama wanavyofanya wanaume.
Kawaida mwanamke huchelewa sana kufungua moyo kwa mwanaume na akishaufungua huufungua kwa asilimia 100 na akimpenda huyo mwanaume (fall in love) basi huwekeza kila kitu maishani mwake kwa ajili ya huyo mwanaume.

Wanawake huhitaji mwanaume ambaye atamhakikishia upendo na kwamba anapendwa kila siku, wanapenda kupokea sifa kwa mavazi, namna anaonekana na kila kitu, wanawake wapo sensitive sana katika issue za mapenzi na huumizwa kirahisi.
Wanawake wanapompata mwanaume wa kupendana naye huwekeza kwa muda mrefu na kwao mahusiano huwa na maana sana kama pumzi anayovuta.
Huwekeza katika kufahamu sifa za ndani za mwanaume kuliko uzuri wa sura ndiyo maana wanawake wengi wazuri kwa sura huishia kuoana na wanaume wenye sura zisizovutia hata kidogo.
Pia wanawake huwa wazi kimahusiano, kama kuna kitu kinamsumbua huongea waziwazi tofauti na wanaume. Pia wanawake ni wazuri kusoma mwanaume akiwa na tatizo au kumshtukia kama kuna kitu kinaenda ndivyo sivyo.

Mwanamke anapoongea na mpenzi wake hutegemea mume wake huyo kuacha kila kitu na kumsikiliza kwa makini.
Pia mwanamke hupenda kufanya kazi kama timu na ushirika ndiyo maana hata kama mume amempa rafiki yake pesa na akagundua bila kuambiwa, kwake ni issue ingawa tatizo si zile fedha bali kwa nini hakuambiwa.
Pia wanawake hupenda surprise leo na kesho au mara kwa mara, hufurahia kufanyiwa vitu vidogovidogo kama vile mkienda restaurant mwanaume anachukua jukumu la kumuagizia chakula na kumletea ale (kuhudumiwa kama queen au princes)

Pia wanawake huwa hawapendi mwanaume kuongelea habari za mwanamke mwingine labda huyo mwanamke awe na sifa pungufu kuliko yeye kila idara.

MUHIMU KATIKA NDOA.

Kama wewe ni kizazi cha Adam na Hawa basi suala la ndoa linakuhusu sana na ndoa ni kitu beautiful, Kwani huleta mahusiano ya kutosheleza yanayowaunganisha watu wawili mke na mume.
Inapendeza kwamba Mungu amemuumba mtu maalumu kwa ajili yako.

Kuna mambo muhimu ambayo wakati mwingine wanandoa wanatakiwa kuwa nayo.

10. UJUZI WA KUTATUA MATATIZO.
Kama wanandoa hawana ujuzi wa kutatua matatizo inaweza kusababisha ndoa kuwa ngumu sana hasa miaka 2 ya kwanza katika ndoa.
Kuwa na ujuzi wa namna ya kutatua matatizo katika ndoa ni kufahamu namna ya kuzozana kwa kuelezana ukweli kwa upendo, kufahamu ni wakati gani wa kukaa kimya au kuzungumza.

9. UJUZI WA KUMWEKA MWENZI WAKO NAMBA MOJA
Kumbuka katika ndoa kuna wewe, mwenzi wako na Mungu.
Jambo la msingi ni uhusiano wako na Mungu wako (siyo kazi ya Mungu, au kwenda kanisani bali uhusiano wako na Mungu, then mwenzi wako (mume au mke) ndipo wanakuja watoto na mwisho kazi.
Kama mke wako anafuata baada ya watoto, mama yako au baba yako au ndugu zako au rafiki zako au TV au chochote kile basi ndoa yako haina jipya na ipo siku mwenzi wako ataona hana maana katika ndoa yenu.

8. UJUZI WA KIMAISHA
Ni muhimu sana kila mwanandoa kufanya vitu ambacho vitakuwa msingi wa maisha ya baadae pia kila mwanandoa analo jukumu la kujiuliza ni namna gani anaweza kuwa mwanandoa mwema miaka 10 au 20 ijayo.
Kila mwanandoa analojukumu la kujiuliza nifanye vitu gani ili niwe mwenye mvuto hata miaka 10 ijayo.

7. UJUZI WA KUSAMEHEANA.
Unapokuwa kwenye uchumba, mchumba akifanya kitu cha ajabu unaweza ukaachana naye na kumsahau kabisa, hata hivyo kwenye ndoa unatakiwa kusamehe na kusahau sasa hivi.
Mwenzi wako anapofanya kitu na kujiona amekosea, atakuomba msamaha Kwani ni kweli yeye ni binadamu na ana mapungufu na hayupo sahihi mara zote.
Muda ule ambao unakuwa hutaki kusamehe mahusiano huacha kukua na hudumaa.
Kama huna uwezo/moyo wa kusamehe basi kwenye ndoa usiingie; jibakie single milele.

6. UJUZI WA KUWA MBUNIFU.
Kwenye ndoa tunaishi pamoja na kuonana kila siku, tunalala pamoja, kula pamoja, kuoga pamoja nk.
Bila kuwa mbunifu ndoa huzoeleka na kuchosha.
Tafuta vitu ambavyo mkifanya pamoja vitawafanya kuwa na kitu kipya.
Wapo wanandoa ambao akioa au kuolewa basi Hakuna jipya, Hakuna ubunifu kila mwaka vitu ni vilevile, badilika fanya vitu Tofauti kama hujawahi kwenda sehemu fulani nenda na mkeo au mumeo.

5. UJUZI WA MTAZAMO CHANYA.
Jifunze kuwa na mitazamo chanya kwenye tabia za mwenzi wako. Ni kweli kuna vitu unavipenda kuhusu yeye na kuna vitu ambavyo unavichukia kuhusu yeye, hata hivyo ukweli ni kwamba vitu vizuri unavyovipenda kuhusu yeye ndivyo vimekufanya uoane naye na kwamba vina nguvu kuliko vile ambavyo huvipendi kuhusu yeye.
Weka mtazamo kwenye vile vitu ambavyo vinawafanya ninyi wawili kuwa kitu kimoja.
Ukimnyoshea kidole kimoja mwenzi wako, basi unatakiwa kujinyoshea vidole 5 wewe mwenyewe.

4. UJUZI WA KUJIAMINI.
Lazima uamini kwamba ndoa yenu itadumu na Hakuna kitu kinaitwa talaka na talaka haitakubalika.
Ni muhimu sana ujiamini kwamba mwenzi wako ( mume wako au mke wako) anakupenda sana kama wewe unavyompenda yeye hata kama haoneshi kwamba anakupenda.
Fahamu hivyo na amini hivyo.
Kwa njia hii huwezi kuyumbishwa na upepo wa mashaka na hofu wakati kunapojitokeza kutoelewana.
Kwa njia hii itakuwa rahisi kuirudisha ndoa kwenye mstari.

3. UJUZI WA KUJIFUNZA
Wakati mwingine katika ndoa huwa tunajidanganya sana kwamba tunawafahamu vizuri wenzi wetu hata hivyo baada ya muda tunaanza kushangaa na kujiona tumeoana na mtu ambaye amebadilika sana na Tofauti na wakati ule mnaoana.
Hata hivyo kujisikia mume wako au mke wako amebadilika na kuwa binadamu mwingine si Sababu ya kuachana au kupeana talaka.
Kama huna ujuzi wa kumsoma au kujifunza kuhusu mwenzi wako basi hukutakiwa kuoa au kuolewa au hukustahili kuoa au kuolewa naye.

2. UJUZI WA KUJUA NAMNA WENGINE WANAWAONA/WANAJIFUNZA.
Kama umeoa au kuolewa na unajifanya hujaoa au kuolewa ni kweli dunia na viumbe wake wanakuona ni kweli hujaoa au kuolewa pamoja na umri wako kwenda.
Unatakiwa kuonekana wewe na mwenzi wako ni watu wenye furaha na amani na kweli iwe furaha na amani ya kweli siyo fake.
Mnatakiwa kuwa na smile la kweli na liwe na kweli si fake.
Lazima uwe makini na kufahamu wengine wanawaonaje kama wanandoa na hiyo itakusaidia kujiweka sawa kuhakikisha kunakuwa na kicheko katika ndoa yenu.

1. UJUZI WA NAMNA YA KUGOMBANA.
Hakuna ndoa ambayo wanandoa hawajawahi kupishana au kupingana au kutoelewana au kutokukubaliana katika jambo fulani au tabia fulani.
Pia ni muhimu sana kufahamu kila mnapogombana au Sababu ya kitu kinafanya kuwe na msuguano.
Unatakiwa kuwa na ujuzi wa kufahamu kwamba kugombana kokote kusiwe kwa masaa kadhaa, au siku kadhaa au miezi kadhaa.
Pia ni muhimu sana kuangalia namna unabishana au unaongea wakati wa kutokukubaliana na jambo lolote.
Pia focus katika kulishambulia Tatizo lenyewe na siyo mwenzi wako.