Tuesday, 9 February 2016

USIWE NA MATARAJIO MAKUBWA.

Wakati wa uchumba noti zinatoka kirahisi, ukiolewa tu bajeti inabana!Baadhi ya wanandoa wapya mwaka wa kwanza wote huwa bado ni wakati wa honeymoon pia, kwa ndoa zingine unapoisha mwaka tayari tofauti huanza kujitokeza na kama si tofauti basi baadhi ya ahadi ziliahidiwa wakati wa ndoa huanza kuota mabawa.

Habari njema ni kwamba kati yao wanandoa hakuna aliye na kosa wote wapo sahihi kwa kuwa hakuna mzoefu wa ndoa wote wanaanza kupata uzoefu mpya hivyo tofauti lazima ziwepo ili wapate uzoefu.
Inawezekana wewe unapenda kusikiliza muziki kwa sauti ya chini na mwenzako anapenda husikiliza muziki kwa sauti kubwa kama vile ni Dj.
Inawezekana wewe unapenda kutazama movie kimya kimya ila yeye anataka kuielezea hadi kila hatua movie inavyoenda hadi inakuwa usumbufu na hakuna maana ya kuangalia hiyo movie. Inawezekana yeye anapenda sex kabla ya kulala na wewe unapenda sex kabla ya kuamka asubuhi sasa inakuwa vurugu maana hakuna maelewano.
Inawezekana yeye anapeda maombi (kuomba Mungu) kabla ya kulala wewe unapenda maombi kabla ya kuanza siku asubuhi.
Inawezekana kabla ya kuoana ulikuwa anajitahidi kujiweka portable lakini sasa amenenepeana kama kitimoto.

Matatizo mengi ya mwaka wa kwanza katika ndoa mpya huweza kuepukika kwa kupunguza matarajio juu ya mwenzako na juu ya ndoa yako na kwamba kila kitu kitakuwa kama unavyotaka wewe.
Pia usitegemee kwa kuwa anakupenda basi kila kitu atafanya na kuwaza kama unavyotaka wewe.
Punguza matarajio!

MFANO.
Jerry alikuwa mwema sana linapokuja suala la pesa wakati wa uchumba kabla hajamuoa Prisca
Alikuwa tayari kumnunulia zawadi yoyote, kitu chochote, na wakati mwingine alimpa pesa Prisca atumie anavyotaka yeye na afanyie kitu chochote anachojisikia kufanya kama vile kwenda saloon kujiweka sawa au kununua pamba anazotaka nk.
Baada ya kuoana ndani ya mwaka mmoja,Jerry amekuwa mchungu wa pesa hadi Prisca anahisi kama ni mwanaume tofauti na yule wa wakati wa uchumba.

Sasa ni mgogoro kila linapokuja suala la matumizi ya pesa na Jerry kila mara aamlaumu mkewe Prisca kwamba hajui kutumia pesa vizuri na anatumia ovyo kwa vitu visivyo na maana kama kwenda saloon kutengeneza kucha na nywele.

Ukweli ni kwamba mwanaume akiwa kwenye uchumba huwa anajitahidi sana kumfurahisha mwanamke ili avutike na hatimaye aoe na akisha oa anaanza kuwaza kuhusu watoto shule, kujenga nyumba, kuwekeza nk. na mipango mingie endelevu ya maisha.

Mwanamke anahitaji kupunguza matarajio otherwise awe na pesa zake mwenyewe kwa ajili ya mambo ya ziada.
Jambo la busara ni kuacha kuzozana kwa issues ndogo kama hizo jaribu kupunguza expectations na jenga familia.
Kumbuka hakua mtu anaweza kuondoa furaha yako au kukufanya ujione inferior hadi uamue mwenyewe so be you.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment