Tuesday, 9 February 2016

HATUA MUHIMU ZA NDOA.

Binadamu yeyote aliyezaliwa na mwanamke mara nyingi maisha yake huathiriwa sana na muamuzi yake na uchaguzi anaofanya, na moja ya uchaguzi na maamuzi ni suala la ndoa.
Tangu wawili mume na mke wanapooana ndoa hupitia hatua mbalimbali hadi mmoja anapokufa na baadae mwenzake kufa baadae na ndoa kuwa historia.
Zifuatazo ni hatua muhimu ambazo ndoa nyingi hupitia si lazima ndoa ipitie kila hatua bali ni ukuleles cha hatua mbalimbali ndoa hupitia na kama upo kwenye ndoa unaweza kujua ndoa yako ipo stage ipi kati ya hizi nne muhimu.

1. MAHABA:
Wanandoa wote wamepitia hatua hii, kwani ndiyo hatua iliyowapa sababu ya kuamua kuoa kwa kupeana ahadi za kuishi pamoja hadi kifo kitakapo watenganisha.
Hapa maisha ni matamu, kupendwa ni kutamu na bila mwenzako (partner) maisha unaona hayana maana kabisa.
Kila mmoja yupo romantic ni raha.
Kila mmoja hutoa maneno matamu yenye Kuonesha mapenzi ya kweli kama vile "I mis you baby!" "You are mine", I love u nk, pamoja na kupeana vizawadi vya kila aina.
Hupeana ahadi za kushinda hata wanasiasa wanapongombea vyeo utasikia “nitakupenda milele‘, ‘hakuna mwanamke mzuri kama wewe‘, ‘hakuna mwanaume wa maana kama wewe”

Huwa kunakuwa na tofauti lakini tofauti hazionekani kwani humezwa na “fall in love”
Hata wakilala hukumbatiana kama wote ni mwili mmoja.
Wanandoa wengine hii hatua hudumu kwa muda wa kuanzia miezi sita hadi miaka mitano ya kwanza.

2. MAUZAUZA:
Katika hatua hii ya pili zile tofauti ndogondogo ambazo zilikuwa hazionekani sasa huanza kujitokeza na kwa mbali huanza kukera na kusumbua na kuudhi.
Vitu vile vile ambavyo Mwanzoni vilikuwa havina maana au vilikuwa havisumbui wala kuudhi sasa huanza kuudhi na kusumbua wanandoa.
Mmoja au wote huanza kulalamika kwamba mwenzake sasa hawi kama anavyotaka, hii ina maana sasa tofauti zinaanza kujitokeza na kuonekana.

Sasa spouse anaanza Kuonekana si perfect kama ulivyokuwa unadhani.
Ndoto za kuwa ulikuwa na bonge la partner zinaanza kuyeyuka kama barafu kwenye jua, unaanza kulinganisha na wengine.
Unaanza kujiuliza na kama kuna mtu alikushauri kwamba partner anatatizo unaweza kuanza kukumbuka ushauri wake hata kama hakuwa sahihi.
Wengine kwa hatua hii tu huanza kuwaza kuhusu talaka ingawa walio na hekima na hofu ya Mungu ndani yao huanza kuchukua hatua ili kupata solution.

3. MAJONZI, MATESO NA TABU

Hapa kama mtu ni mlevi basi hujikita nakuweka mizizi na hali kuwa mbaya zaidi.
Hapa wengine ndo huanza extra marital affairs, na wengine husikia maneno yanayoumiza kutoka kwa spouse wao kiasi kwamba hujiuliza hivi huyu ndo Yule nilikubali kuishi naye?

Ndoa huingia kwenye majonzi, majuto, mawazo, stress, BP, depression, kukosa usingizi, katakana, kudundana, ngeu, kulala mzungu wa nne, wengine vyumba tofauti.
Hapa ndo talaka nyingi hutokea, ni hatua ambayo imeumiza watoto wengi sana ambao walikuwa na wazazi wawili na kujikuta wakiishi na single parent.
Ndoa huwa katika mtihani, ndoa huwa katika maumivu makali kama ya jino ambayo huathiri mwili mzima.

Inaweza kutokea Mwanandoa mmoja akawa anataka talaka au ndiyo huyo mmoja analeta kasheshe zote na mwingine ndo anataka mambo yaishe na kupata suluhu.
Hapa ni mahali ambapo mwanamke au mwanaume anahitaji Kuonesha uwezo,hekima ubunifu, moyo mkuu, kutokata tama, kuwa imara, kusimama imara ili kuhakikisha anabadilisha machungu yote kuwa furaha, amani, na upendo na ndoa kuwa imara kuliko mwanzo.
Wengi wanaoachana (talaka) kwenye hii hatua wakioa mwanamke mwingine au kuolewa na mwanaume mwingine baada yamuda hujikuta anaingia kwenye matatizo yaleyale na kuanza kujiona ana mkosi au bahati mbaya kupata aina ileile ya partner, ukweli ni kwamba hajui jinsi ya kupambana na matatizo ili kupata solution.

4. KUAMKA, KUCHANGAMKA NA FURAHA MPYA
Kumbuka wote wanaoishia hatua ya 3 na kuamua kutengana si watu wabaya, bali tatizo kubwa ni kwamba walikosa tools au walikosa kujua tools zinazotumika kujenga ndoa imara.
Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote na dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.
Hata kama ndoa imekondeana na kubaki mifupa ambayo hata mtoto wa chekechea anaweza kuhesabu mifupa, bado inaweza kutiwa stake na kuwa nene ikapendeza zaidi kuliko mwanzo.
Ndoa si romance kama tunavyoangalia kwenye magazeti na TV ndoa ni maisha halisi pamoja na kukutana na setback na kuzigeuza kuwa viungo vitamu kuifanya ndoa kuwa na furaha, amani na upendo kila siku.

Kwenye hii hatua Mwanandoa huanza kuaminiana kuliko kawaida kwa sababu wanajuana na pia wametoka mbali na wamepitia mengi na wamejifunza.

NB:
Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment