Wednesday, 10 February 2016

HUATHIRI AFYA.

Kuolewa au kuoa ni kitu kingine na kujenga ndoa ni kitu kingine.
Ndoa yenye furaha huwa haijengwi siku ya ndoa au siku ya harusi au siku ya kuvalishana pete tu bali hujengwa kila iitwapo leo.

Ndoa inapokuwa na mgogoro mara nyingi (si zote) wanandoa huathirika zaidi na mara nyingi mwanamke huonekana ni makini na kuelekeza juhudi nyingi ili mahusiano yaendelee na kuwa yenye afya njema ( ingawa si wote)

Katika migogro mingi ya mahusiano (Ndoa au uchumba) mara nyingi mwanamke ndiye huathirika zaidi.
Wanaume hata kama ndoa ina mgogoro bado huonekana wapo physically fit na mentally fit kabisa nakuendelea kujichanganya na wenzao kama vile hakuna linaloendelea ktk ndoa zao wakati wanawake ndoa ikiwa na tatizo basi kwa kumwangalia tu unaweza kupata ujumbe kamili achilia kukoswakoswa kugongwa na magari.

Kwanini?
Wanawake na wanaume hutofautiana sana jinsi ya kukabiliana au kuchimbua hisia (feelings), tukuto (emotions) zinazotokana na mgogoro uliopo.
Wanaume huweza kuvumilia tukuto na hisia zao bila kutegemea mwanamke au kuegemea kwa mwanamke, hii ina maana kwamba mwanaume hujikana, hujiondoa, huwa hajali, hu-withdraw hisia zake au kujisikia kwamba ana mgogoro na matokeo yake haathiriki sana.

Wakati huohuo mwanamke yeye kwanza ni mtu wahisia na tukuto (feelings & emotions ) tatizo likitokea hujihusisha zaidi, huji-engage, hujitoa (dedicate), huji-commit kupata solution, hujiuliza maswali wengine watasemaje? huwaza zaidi kuhusu yeye na mpenzi wake na jinsi ya kusaidia mgogoro uishe, matokeo yake huathirika zaidi na hudhoofisha afya yake na kuweza kukumbwa na magonjwa kama shinikizo la damu, stress, depression, stroke, magonjwa ya moyo nk.

MWANAMKE AFANYEJE?
Jambo la msingi ambalo mwanamke anaweza kufanya ndoa inapokuwa katika mgogoro ni kumuomba Mungu ampe hekima, busara na ushindi ili ndoa iwe katika mstari kwani ni jaribu na lazima ushinde, kila ndoa bora imejaribiwa na kuonekana imara, usione vinaelea vimeundwa.

Pia mwanamke anahitaji kuwa positive, kwamba anaweza na kwamba bado ndoa ipo, mume ni wake na aendelee kumpenda na kutamkia mambo mazuri mume wake kuliko kuwa na mtazamo negative.
Pia mwamke anahitaji kujiamini kwamba chanzo cha furaha yake ni Mungu hivyo hakuna binadamu anaweza kuondoa furaha yake hadi aamue mwenyewe.

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment