Thursday, 4 February 2016

MWANAMKE HUCHUKULIA SAWA TU.

Wanaume wengi (si wote) hudhani kwamba kumpa mwanamke zawadi kubwa, au kumnunulia kitu cha thamani kubwa kama gari au nyumba au kumfanyia jambo kubwa kunampa alama kubwa na ni kuonesha mapenzi makubwa na kwamba kwa kufanya hivyo basi mwanamke hastahili kutokuwa na furaha.

Ukweli ni kwamba kila zawadi au jambo unalofanya kwa mwanamke lina nafasi sawa au maksi moja tu kati ya mia, hivyo basi ukimnunulia gari unapata maksi moja, ukimjengea nyumba unapata maksi moja, ukimnunulia pipi unapata maksi moja, ukimbusu unapata maksi moja, ukimsaidia kufua nguo unapata maksi moja, ukimpeleka vacation nje ya nchi unapata maksi moja, ukimkumbatia unapata maksi moja, ukimpa neno la kumtia moyo unapata maksi moja nk.
Ukiongea naye kwa kumsikiliza unapata maksi moja, ukimununulia chocolate unapata maksi moja, ukimnunulia kiatu cha kisasa unapata maksi moja pia.
Kwa mwanamke zawadi zote zina thamani sawa, iwe kubwa au ndogo, kumfanyia vitu vidogo vina thamani sawa na kumfanyia mambo makubwa, hii ina maana kwamba kumpa zawadi kubwa au zawadi ndogo humpa furaha sawa.

MFANO.
Jeffy ni Daktari kwenye hospitali moja kubwa jijini DSM Tanzania na kazi yake ina pesa nyingi sana kiasi kwamba familia yake imeweza kujenga nyumba, kusomesha watoto, kununua gari na kulipa bills kwa ajili ya mahitaji muhimu ya familia yao.
Daktari Jeffy anaamini Mkewe Suzy anastahili kuwa na furaha kwa sababu fedha anazopata zinawezesha wao kuwa na maisha bora na pia haoni umuhimu wa yeye kusaidia mkewe kazi ndogondogo na kuwepo nyumbani kwa ajili ya kukaa na familia, hivyo wakati mwingie huchelewa nyumbani kuendelea kufanya kazi ili apate pesa nyingi mke afurahi zaidi.

Mkewe Suzy ni mama wa nyumbani, yeye hufanya kazi za pale nyumbani na zaidi huhakikisha kila kitu pale nyumbani kipo in order.
Mkewe Suzy analalamika kwamba mumewe kwanza anachelewa nyumbani, pili hasaidii kazi ndogo ndogo za pale nyumbani, hana muda na mumewe anajisikia upweke na anajisikia mumewe hamjali.

Daktari Jeffy naye haoni sababu kwa mkewe kulalamika na Kutokuwa na furaha kwani yeye anapata pesa nyingi kuipa support familia na ameshajenga nyumba na kuinunulia familai gari.
Anaamini kuwa na pesa nyingi ni zawadi tosha kwa mke na mke anastahili kuwa na furaha.
Pia Jeffy anaamini kuwa anapofanya kazi kubwa ya udaktari na kupata pesa nyingi hastahili kufanya kazi ndogo ndogo pale nyumbani kumsaidia mkewe.

Anaamini pay cheque yake ina point nyingi (maksi 80) kuliko pengine kumsaidia mkewe kutandika kitanda (maksi 1) hajui kwa mwanamke kuwa na pay cheque kubwa kuna maksi moja na kumsaidia kutandika kitanda kuna maksi moja tu.

Unapotaka kumuelewa mwanamke huhitaji kuwa logical bali emotional, mwanamke yupo after romance, jinsi unavyompenda, unavyomsaidia vitu vidogo, unavyomsikiliza, unavyombembeleza, unavyompa muda wa kuwa pamoja na kufurahia, unavyombusu, unavyomkumbatia, unavyomtia moyo, unavyocheza naye nk, kwake ni muhimu kuliko kununua gari au nyumba na kuamini kwamba hapo mwanamke atakuwa na furaha na hana sababu ya Kutokuwa na furaha.
Unaruhusiwa kumfanyia mambo makubwa sana lakini kumbuka anza kwa kumfanyia mambo madogomadogo kwanza.

Kwa kuwa umefanya mambo makubwa haina maana kwamba hutakiwi kufanya mambo madogo na kwamba mambo makubwa au zawadi kubwakubwa ukimpa hana sababu ya Kutokuwa na furaha na kuona unamjali.

No comments:

Post a Comment