Wednesday, 2 December 2015

NI MUHIMU KUCHUNGUZA KWANZA.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.
Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.

Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.

Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.

Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!

Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).

Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja.

Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia. Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa,

Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!

Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!

No comments:

Post a Comment