Friday, 4 December 2015

KWANINI UKATE TAMAA..!

Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena!
Hawezi kushirikisha kitu chochote ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja.
Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu.
Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina hii bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo.

1;TEMBEA KATIKA ROHO.

Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu.
Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume.
Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kwamba huwezi ukampenda Mungu usiyemuona ukashindwa kumpenda partner wako ambaye unamuona.
Ukiguswa na Mungu lazima na ndoa yako itakuwa ya tofauti.
Kumbuka kutembea katika Roho ni kitu tofauti na kujiita Mkristo.

2.ACHANA NA KUKAA KWENYE LAWAMA,MAUMIVU, UCHUNGU NA KUANGALIA UDHAIFU WA PATNER WAKO.

Yeyote ambaye analalamika kwamba ndani ya ndoa yake hakuna upendo ukichunguza kwa makini utakuta amebeba fulushi zito sana la orodha ya mambo mabaya ambayo partner wake anamfanyia au udhaifu wa partner wake.
Anaongelea huo udhaifu wa partner wake, anasimulia rafiki zake, anauamini, anauwaza, anaukiri kutembea nao kama sala.

Hisia mbaya hata kama ni kweli huwa na matokeo mabaya kwenye feelings.

3.ORODHESHA VITU 10 VIZURI KUHUSU MWENZI WAKO.

Na kiri mara mbili kwa siku kwa siku 21
Shukuru kwa kila jambo.Kulalamika kila siku huweza kuharibu emotions zako bila kujua hata kama mume wako au mke wako hafai kabisa bado unaweza kutumia mambo mazuri aliyonayo kuirudisha ndoa yako kwenye mstari.

Huwezi ukawa na mawazo tele ya udhaifu wa mke wako au mume wako na wakati huohuo ukamfurahia na kumpenda na kuwa na feelings za upendo wa juu.
Vita ya upendo huweza kushinda au kushindwa kwa mawazo yako kwani moyo ni mtumishi wa mawazo yako.

Moyo huamini kile mawazo yako yanakitunza.
Mtu mmoja alikiri kwamba hampendi tena mke wake na kwamba ilikuwa ni miezi mitatu kila mmoja alikuwa analala chumba chake, alipoambiwa aandike mambo kumi mazuri kuhusu mke wake kwenye karatasi.
Akakubaliana kila siku asubuhi anapoenda kazini kuyatafakari hayo mambo mazuri 10 kuhusu mke wake na pia kuyatafakati tena jioni akirudi kazini anapoendesha gari lake.
Baada ya siku kumi akakiri kwamba sasa mambo yameiva kwani tumerudiana, zaidi kulala chumba kimoja sasa tunalala kitanda kimoja.

Na baada ya wiki tatu akakiri kwamba anampenda mke wake kuliko wakati wowote katika maisha yao ya ndoa tangu waoane.
Alipoulizwa je, umeyashika yale mambo 1o mazuri kuhusu mke wako akasema kwamba yale aliyashika siku ya tatu na siku ya nne akaamue kuongeza hadi yakawa 15 na kwa kuwa yalikuwa mtindo wa Cards hivyo alikuwa anayapitia moja baada ya lingine na kuyachanganya na kuyakiri over and over.

Hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa na orodha ya mambo 10 mazuri kuhusu mke au mume wake na akayatamka na kumshukuru Mungu twice a day na kusiwe na kufufuka kwa upendo mpya.

Kumsifu na kumshukuru mke wako au mume wako mbele za Mungu kwa mambo mazuri aliyonayo ni silaha ya nguvu kubwa ili kuwasha upendo na mapenzi mapya katika ndoa.

No comments:

Post a Comment