Wednesday, 9 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO. 2

Kila mmoja anajua raha ya falling in love au siku za honeymoon je, nini hufuata baada ya hayo?
Wengi hawajui emotional terrain iliyo mbele au bonde utakayopita katika kuendelea na ndoa yako.
Hapa kuna hatua predictable ambazo ndoa nyingi hupita, naamini ukiijua hii ramani basi utaweza kufika mahali unapoenda.
Tunaendelea na hatua ya pili..
HATUA YA PILI NI MAUZAUZA.
Ile hali ya kudondokea kwenye mapenzi (fall in love) huchakaa na ukweli halisi huanza kuonekana.
Hii ni hatua ngumu kwa sababu unakumbana na anguko kubwa sana la ndoto zako kuhusiana na mpenzi wako.
Zile tofauti na tumakosa tudogo ambato tulikuwa si kitu sasa huanza kusumbua na kuudhi, mfano kama mwenzi wako alikuwa mzembe kupanga vitu hasa nguo chumbani sasa utaanza kuudhika kwani utajisikia umevulia mno, kama anakoroma sasa utaona usumbufu, kama ana kikwapa sasa unaona kinasumbua, kama ana harufu mbaya mdomoni asubuhi itaanza kukusumbua, tayari sasa vitu vidogo vimekuwa mambo makubwa yanayokuudhi.

Kila mmoja huanza kulalamika kwamba mwenzake hawi kama anavyotegemea.
Kunakuwa na disagreement nyingi kuliko agreement na unagundua kwamba mnatofautiana sana katika mitazamo ya vitu vingi.
Wewe unataka kula hotel unaipenda mwenzako anataka mle nyumbani ili ku save pesa, unapenda usikivu usiku nyumbani mwenzako anataka kusikiliza muziku kwa sauti kubwa.

Ule kuwa mwenzi wangu ni perfect huanza kupotea na imani yako kwake huanza kupotea kwamba mmm kumbe ni mkali kiasi hiki, kumbe ni mchoyo kiasi hiki, kumbe hapendi sex kiasi hiki, kumbe anajua kukalia mwenzake kiasi hiki nk.
Hapa tofauti za malezi, tamaduni, dini, kuamini, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza na kuwa wazi.
Katika hatua hii mtu halisi huanza kuonekana na ukweli ni kwamba ndoa huanza kujengwa hapa.
Wengi huanza kujiuliza mbona watu hawakuniambia kwamba ukioa au kutolewa inakuwa hivi kwani anayaanza kuona ni kinyume na matarajio na wengine huanza kujiuliza kwa nini nilioana naye.
Wapo ambao huanza kufikiria wachumba wengine (misri) kwamba labda ningeoana na Fulani alikuwa afadhari kuliko huyu.
Wengi huanza kujiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini hadi nikakubali kuoana naye.
Walio na hekima huanza kumuomba Mungu na kupata ushauri wa watu wanaowaamini...

Hatua ya tatu ni MATESO,MAJONZI NA TABU...Je,huwa vipi...Endelea kufuatilia

No comments:

Post a Comment