Wednesday, 9 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO.

Ndoa ni mahusiano yanayoweza na yanayotakiwa kuwa ndiyo kitu kinacholeta raha na kuridhisha katika maisha kuliko kitu chochote.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu walio kwenye ndoa huishi maisha marefu kuliko singles.
Kwa kuwa nusu ya ndoa zinazofungwa huvunjika katika baadhi ya nchi, ni muhimu sana kufahamu vizuri package nzima ya mambo ya ndoa katika pande zote.
Knowledge is power!
Pia ni vizuri kukumbuka kwamba (kama hujaolewa au kuoa bado) yale unakutana nayo muda wote wa uchumba hadi honeymoon ni asilimia 10 tu ya masuala ya ndoa na asilimia 90 ni kazi iliyo mbele yako na hii kazi itakupasa kuendelea kuifanya siku zote unavyoendelea na ndoa.


HATUA YA KWANZA NI KUDONDOKEA KWENYE MAPENZI.
Kibailojia kuna asili ambayo miili yetu huwa msingi katika hatua mbalimbali ambazo hutufanya kuvutiwa na mtu wa jinsia nyingine na kufika hatua tukaona maisha bila huyo mtu hayana maana.
Kuna aina tatu za kemikali (Phenylethylamine, dopamine na norepinephrine ) ambazo huhusika moja kwa moja na kuwafanya wawili wapendanao kwa mara ya kwanza kujikuta wamedondoka kwenye mapenzi (fall in love).

Kwa pamoja hizi kemikali huweza kuzalisha na kutibua matokeo ya kushangaza hadi mtu kuwa na positive attitude na anayempenda, piga ua hukubali kumuacha maana umempenda, watasema usiku watalala kwani nimempata anayenipenda.
Hizi kemikali hutufanya kuwa na nguvu kubwa ya kumpenda mtu na kujisikia tunajisikia very excited na mpenzi mpya.

Hizi kemikali kama nguvu ya hurricane au storm huweza kuufunika ubongo sehemu inayohusika na kutoa tahadhari.
Amygdale huweza kutoa tahadhari au onyo kwamba partner uliyempata anaweza kukuumiza hata hivyo kutokana nguvu iliyopo ya falling in love mhusika hupuuzia.

Mhusika hajui kuonywa ni kitu gani, haogopi watu wanavyosema maana yeye amependa, yupo blind.

Wengi huangukia kwa wapenzi wasiowajua vizuri na hujishangaa kwa nini wanawapenda kwa kasi ya ajabu kiasi hicho.
Kuna powerful attraction kiasi kwamba huweza kusababisha hadi mtu kutoa maamuzi ya ajabu kama vile kukana dini, kukana wazazi kukana ndugu na kukubaliana na huyo amempenda.
Katika hatua hii ya mahusiano wengi hujiona wamefikia na kutimiza ndoto zao.
Kila kitu huwezekana na kukufanya uridhike maana mpenzi anakupa kile unakihitaji ambacho hata wazazi hawawezi kukupa.

Ni hatua natural ambayo mke na mume huvutiana na hupelekea kuoana
Katika hii hatua maisha ni matamu, ahadi kubwa na kedekede kutolewa,
I miss u,
I love u,
You are mine,
I love u from earth to the moon,
Nakupenda kwa moyo wangu wote,
Sina mwingine ila wewe tu.Wakiwa wamelala hukumbatiana kama vile amelala mtu mmoja (mwili mmoja) ni raha ni kuhitajiana kwa kiu ya ajabu.
Wahusika huwa blind na hata kama mwingine ana makosa au vitu fulani anaudhi huonekana si tatizo, na hukubaliana kuoana hivyo hivyo.

Watafiti wengi wanauona huu upendo katika hatua ya kwanza si upendo wa kweli kwani huongozwa na hizo kemikali tatu na kukupa nguvu za attraction za ajabu. Pia haujajaribiwa bado, haujakumbuna na kasheshe bado.

Hii hatua katika mahusiano ya ndoa huitwa hatua ya ghururi (infatuation, self deceit, arrogance, presumption)
Hapa ndipo kunapatikana vitu vinaitwa uchumba na honeymoon
Hii natua huweza kudumu hadi miezi 30 muda ambao hutosha wahusika kuwa na mtoto.

Je, ni hatua zipi hufuata na kupelekea wanandoa kuwa na true love?

Je, mahusiano mengi au ndoa nyingi huvunjika katika hatua ipi?

Na je, ni jambo gani la busara kufanya katika hatua ambayo ndoa nyingi huangukia kwenye shimo?

Endelea kufuatilia....

No comments:

Post a Comment