Friday, 4 December 2015

NI KURIDHIKA TU..!

Kuridhika na ndoa huendana na kuridhika kimapenzi hata hivyo suala la kuridhika katika ndoa na kimapenzi ni kama swali la yai na kuku kujiuliza kipi kilitangulia.

Je, kuridhika na ndoa huweza kusaidia kuridhika kimapenzi?

Je, si kuridhika kimapenzi ndiko husababisha kuridhika na ndoa uliyonayo?

Kama mwanandoa mmoja haridhiki kimapenzi katika ndoa hupelekea kujisikia haridhiki na ndoa yenyewe pia kama mwanandoa mmoja haridhiki na ndoa aliyonayo hupelekea kujiona haridhiki na mapenzi katika ndoa.
Hii ina maana kwamba huwezi kuwa na kimoja bila kingine kuwepo.

Mungu ametuamuru kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kumridhisha mke au mume wake kimapenzi na Sayansi nayo inatoa ushahidi kwamba kuna faida kubwa ikiwa wanandoa wataishi maisha ya kuridhishana kimapenzi na hatimaye ndoa yenyewe.

Kama kanisa linaamini talaka ni kitu kibaya na kukaa katika ndoa ni jambo jema basi halina budi kufundisha na kusisitiza kwa nguvu zote au uwezo wote wanandoa kuridhishana kimapenzi kunakopelekea kuridhika katika ndoa zao.

Ni mara ngapi kwa wiki huweza kusababisha kuridhishana katika hisia za mapenzi (sex)?
Mwili wa mwanaume huweza kuzalisha sperms kila baada ya masaa 72 (siku tatu) ndivyo Mungu aliumba.
Mathematically ina maana kwamba tendo la ndoa ni muhimu sana siku 2 au 3 kwa wiki kuweza kufanya connection ya feelings za wanandoa kiroho na kimwili.
Kukiwa na kuridhishana kimapenzi katika ndoa ni ukweli kwamba hata wanandoa wataridhika na ndoa yao kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment