Thursday, 19 November 2015

MFANO WA NDOA.

Ndoa ni mfano wa computer.
Kwani computer hukupa kile kimewekwa tu, huwezi kutumia program ya MS Word kama haijawekwa, huwezi kupata internet kama haijawa connect na internet.
Ndivyo ndoa zilivyo
Ukiweka takataka utapata takataka.

Ukiwekeza katika mke kujisikia vizuri na utavuna mume anayejisikia vizuri.
Usipowekeza upendo ndani ya ndoa hauwezi kupokea upendo.

Hakuna kuwekeza mawasiliano mazuri usitegemee kuwa na mawasiliano mazuri
Ukiilea vizuri ndoa yako itakuwa oasis katikati ya jangwa, na usipowekeza katika kuilea itakuwa jangwa la sahara.

Mke akiwekeza heshima kwa mume wake, atavuna upendo kutoka kwa mume wake.
Mume akiwekeza upendo kwa mke wake; atavuna heshima kutoka kwa mke wake.

Mume akiwekeza kuwa karibu na mke, kuwa waza kwa mke, atavuna tendo la ndoa linaloridhisha.

No comments:

Post a Comment