Friday, 20 November 2015

KUWA MAKINI NA MDOMO WAKO.

Sisi wote huwa tunaongea na marafiki na watu wa karibu kuhusu ndoa zetu, hata hivyo mambo tunayowaambia marafiki ni muhimu sana na huweza kuleta matokeo mazuri sana au mabaya sana kwa ndoa zetu.
Pia duniani tunatofautiana sana hasa kutokana na tamaduni zetu kwa mfano mzungu mara nyingi hana siri haijalishi ni siri ya kitu gani anaweza kukwambia kitu kinachohusu mume wake au mke wake kiasi ambacho unaweza kushangaa na tukirudi kwenye jamii zetu za kiafrika nasi kwa kutunza siri tunajua.
Kuna wakati kutunza siri ni upuuzi kabisa kwani ni siri ambazo ukificha mwisho wake kuna madhara makubwa sana.
Kwa mfano kuficha siri kwamba kabla hujaoana na huyo umeoana naye hukuwahi kuwa na mtoto wakati mtoto unaye na yupo na bibi yake kijijini, hiyo ni hatari kwani siku akigundua ni kweli trust kwako itapotea.

Leo tuangalie hili la kuongea siri za nyumbani kwako na mume wako au mke wako na mmoja wenu anaenda kzimwaga kwa marafiki zake, au wafanyakazi wenzake au mama yake au baba yake au ndugu zake kwa kukuzunguka na anaongea hayo mambo kiasi kwamba ungekuwepo asingethubutu kuongea.
Kulinda siri za mume wako au mke wako ni jambo muhimu sana hasa katika kuimarisha trust katika ndoa.
Bahati mbaya ni kwamba wapo wanandoa ambao wao kutoa siri za mke au mume kwa rafiki au watu baki kwake si tatizo ni kama mdomo una washa.

Yaani kitu kidogo tu mfano kuzozana kidogo tu na mume au mke usiku, ile kuamka asubuhi tayari umeshawambia baba, mama, ndugu, majirani na wafanyakazi wenzake kwamba jana mlizozana wakati wala hakuna faida anayopata na anadhani kuwaambia wengine basi yeye anafaa sana kumbe nao huishia kumdharau.

Unapokuwa ni mwanandoa mtoa siri nje unapoteza hadhi yako ya kuwa mwanandoa.
Ni kama unatengeneza kilema kwa partner wako hasa kwa wale unawaambia siri zenu.
Ndiyo, kuna wakati na pia ni muhimu kushirikisha wengine struggles za ndoa hasa mtu wa karibu ambaye unaamini anaweza kukushauri na kukusaidia lakini si kumwaga siri kwa kila mtu.

Ulimwengu wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa anatoka asubuhi na mapema kwenda kutafuta riziki na mke alikuwa na muda nyumbani kuendelea na kazi zake na watoto.

Siku hizi kila mmoja anaaondoka asubuhi na mapema kwenda kazini na huko kazini anatumia muda mwingi kuliko nyumbani, kubwa zaidi ni kwamba kazini anashinda na mke wa mtu au mume wa mtu au wanaume na wanawake ambao si mume wala mke au watoto.

Tafiti nyingi zinaonesha wanandoa wengi sasa wanatumie muda mwingi zaidi kazini kuliko kuwa na familia hii ina maana mwanandoa anatumia muda mwingi wa kazi kushinda na mke wa mtu au mume wa mtu na kama huyo mke wa mtu ndo amekuwa mtu wa kumwagia siri zake za nyumbani au chumbani kwake na mwenzi wake anakuwa ana date na huyo mke wa mtu au mke wa mtu bila kujua.
Kwani ku-share siri ni moja ya kuwa intimate na mtu ndiyo maana sasa tunakuwa na matukio mengi ya ofisi romance kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.

No comments:

Post a Comment