Friday, 20 November 2015

KUWENI MAKINI,NI MALI YENU

Tunapooana kama wanandoa tunakubaliana kwamba tutakuwa tunafanya tendo la ndoa sisi wawili tu maisha yetu yote haijalishi tunafanya kwa kufikiria, au kwa kutofikiria, au tunafanya bora liende au kwa ufanisi, tunafanya kwa kupenda au kulazimishwa, tunafanya kwa ubunifu au kwa uchoyo au kwa kubania au kwa hiari au vyovyote vile kitabu kimefungwa na lazima kila mmoja apate kile mwenzake anampa iwe nusu au kitu kizima au kunyimwa kabisa au kupewa kila ukihitaji.
Hakuna kuangalia kushoto wala kulia ngoma ni ninyi wawili tu kuicheza hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ukweli wengi wetu huwa tunachukua kila kitu for granted, hakuna efforts zozote tunaweza kuziwekeza kuhakikisha mwenzako anapata the best kutoka kwako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa kwani ni wewe tu ndiye mwanamke au mwanaume duniani ambaye amekubali kuishi na wewe na kushirikiana kupeana hiyo zawadi ya mwili ambayo ni mali ya ndoa yenu na si vinginevyo.
Naomba ujiulize ndani ya moyo wako tena ukiwa na akili nzuri kabisa kama Mungu alivyokujalia kuoana na mwanaume au mwanamke special kama huyo uliyenaye.

Je, ni kweli unataka leo kumbariki mke wako au mume wako kwa mwili wako kwa kuwa hakuna kwingine anaweza kupata hii huduma?

Je, una hamu ya kumpa kitu cha uhakika (mapenzi, mahaba) kwa sababu ya jinsi anavyokupenda, anavyokujali na jinsi alivyoshirikiana na wewe hadi hapa mmefika?

Au umefika mahali umechoka, huna hamu tena ya kuhakikisha mume wako anapata kile mlikubaliana wakati mnaoana?
Au unasubiri hadi umpoteze ndipo ujue thamani yake?

Je unajua huko nje ya ndoa yako kuna wanawake au wanaume wengi kiasi gani wanamtamani sana huyo mume wako au mke wako?

Je, kwa nini huweki juhudi yoyote kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa mahali bora kukimbilia kama mke na mume?

Sex ni mali ya ndoa na ndivyo Mungu alivyo design, hivyo kama upo kwenye ndoa ina maana suala la tendo la ndo lisichukuliwa just for granted, panga, andaa na wekeza kwa uwezo wako wote kuhakikisha mke wako au mume wako anaridhika na wewe na utendaji wako.

No comments:

Post a Comment