Friday, 20 November 2015

FAHAMU HAYA YAHUSUYO NDOA.

"Unajua siku hizi hunipendi” mwanamke ambaye ameishi na mume wake kwa miaka 7 alimlalamikia mume wake.

"Hivi unaongea kitu gani na wewe, kwa nini unasema hivyo?"
Mume naye alimjibu mke wake kwa kushangaa kwa nini mke wake anasema hampendi!

"Ni kweli hunipendi na siku zinavyozidi naona hunipendi zaidi" mwanamke aliendelea kulalamika.
Mshauri wa ndoa akaingilia kati na kumuuliza mume "je, huwa unamwambia mke wako Nakupenda?"

Kwa majivuno mwanaume akajibu kwamba
“anajua nampenda kwani kila jioni nawahi nyumbani kuwa naye, nampa pesa anazohitaji anunulie kitu chochote anataka, nimemjengea nyumba nzuri, nimemununulia gari zuri, Pia nimekubali kuja naye kwako mshauri, je unadhani hadi hapo simpendi?

Mshauri akakaza uzi bado kwamba acha hayo yote je, huwa unamwambia “Nakupenda" mke wako?”
Mume akawa anamwangalia mke wake na mke akawa anatikisa kichwa kukubaliana na maneno ya mshauri wao wa ndoa kuonesha ni kweli huwa haambiwi na mume wake “nakupenda mke wangu.
Mume akajibu akasema “hivi kuna ulazima gani kumwambia nampenda wakati vitu ninavyofanya kwa ajili yake vinaonesha nampenda?"

Hapa wanaume wengi tunaweza kuandamana kumtetea mwanaume mwenzetu na kwamba huyu mwanamke ana lake na kweli hana shukuruni kwani wanawake wangapi wamefanyiwa vile yeye amefanyiwa na wapo kimya, huyu mwanamke pamoja na mazagazaga yote mwanaume mwenzetu amejtajidi kumpa bado anaonekana hampendi.
Hata hivyo linapokuja suala kuonesha mwanamke anapendwa tunatofautiana sana na mitazamo tunayo wanaume wengi.

Mwanamke huhitaji kusikia kwa maneno (tamka) mkiwa wawili au hata mbele za watu kwamba unampenda au “nakupenda”.
Pia inaonekana ni jambo au suala la kawaida sana ingawa mwanzo wa kupendana watu huambiana maneno mengi matamu lakini wanavyoendelea na mahusiano huanza kujisahau.

Kuna maneno zaidi ya 16 ambayo wanandoa ni muhimu sana kuyatamka kila mmoja kwa mwenzake ili kuleta affections na msisimko wa kujisikia unapendwa hasa wanawake.

1.NAKUPENDA.
Ni vizuri kuwambia nakupenda kabla hujaondoka kwenda kazini na wakati ukifika nyumbani baada ya kutoka kazini, mwambie nakupenda kabla hujamaliza kuongea kwenye simu.
Kila ndoa huhitaji dose kila siku na dose mojawapo ya kila siku ni neno nakupenda. Wala usiwe na wasiwasi kusema nakupenda kila si tabia mbaya hata kama mwenzio amekasirika kwa jambo Fulani na kusema nakupenda kunaweza kufungua mlango wa kusamehewa haraka.

2.SAMAHANI.
Uliambiwa unaporudi uwe umenunua maziwa na ile unafika nyumbani kumuona mke wako unakumbuka kwamba maziwa hujanunua, sema nisamehe, wewe ni mke na ulimuahidi mume wako kwamba utafua nguo zake na hana nguo za kuvaa sema unisamehe na maanisha.
Huwa hatumsaidii mtu yeyote tunapojilinda kwa namna yoyote, ila kiburi ndicho hupata faida. Nakuogopa kutumia neno nisamehe lakini, kwani hiyo huua msamaha.

3.UMEPENDEZA.
Wakati tunachumbiana huwa tunapeana sifa kila siku hata hivyo baada ya kuendelea sana kwenye ndoa tunajisahau kupeana sifa.
Labda tunadhani mwenzi anajua jinsi tunavyiojisikia au tunadhani kwamba haina haja tena kuendelea kutoa sifa.
Mwanamke anahitaji kuendelea kuambiwa anapendeza hata baada ya kuzaa mtoto wa kwanza, wa pili hadi mwisho ingawa kuna wakati anaweza hata mwenyewe asikubali hata hivyo wewe umefanya nafasi yako.
Hata wanaume nao wanahitaji la kuambiwa amependeza au leo yupo handsome na pamba zake alizijipiga.
Kupeana sifa huimarisha intimate kati ya wanandoa, kama mke wako hajioni ni sexy kwa nini awe anataka mahaba kwako? Mhakikishie kwamba yupo sexy na akili yake itafunguka kwamba unamuhitaji.

4.NAKUHITAJI.
Wapenzi wetu wanahitaji siyo kufahamu kwamba tuna wa-appreciate tu bali tunawahitaji, tunapaswa kuwaambia kwamba maisha bila wao yangekuwaje? Inakuwaje kila wiki wakijua kwamba tunawahitaji.
Kama kutamka kwa mdomo inakuwa ngumu kumwambia nakuhitaji kila siku basi andika barua, message, email nk.
Mwanamke anahitaji kusikia kwamba anavutia pia wanaume wanapenda kufahamua kwamba mke anamuhitaji pia.

5.ASANTE.
Hivi inakuwaje watu wa nje ndo wanazipata asante zetu kwa wingi kuliko sisi wanandoa wenyewe.
Ukienda sokoni au kazini asante zinatoka bila wasiwasi na mume na mke inakuwa ngumu?
Mwambie asante mke kwa dinner, asante kwa kusafisha nyumba, kwa kukufulia nguo, mwambie asante mume kwa jinsi anavyoweza kuipa familia kipato, mpe asante kwa kuwahi kurudi nyumba.
Kama unashindwa andika email au ujumbe wa simu au vyovyote unaweza.

No comments:

Post a Comment