Friday, 20 November 2015

JE,WANAUME WANAPENDA UREMBO TU?

Kuna usemi kwamba jinsi mwanamke anavyovutia kwa mwanaume ndivyo mwanaume humuhitaji zaidi.

Ukweli ni kwamba jinsi usivyokuwa concerned sana na physical appearance ndivyo mwanaume atakuhitaji zaidi na kama ndo dating unaweza kuona mwanaume anakuganda hadi inakuwa ndoa.

Nahisi unadhani hii haijakaa sawa hata hivyo subiri kidogo tuchambue.
Inaweza kuwa kweli kwamba Ukitaka kumvutia mwanaume ni muhimu kujipamba haswaa na kuvaa nguo ambazo zinaweza kumvuta mwanaume yeyote kwani ugonjwa wa wanaume wengi ni kile anaona.

Mwonekano wako unaweza kumvuta mwanzoni lakini hiyo haiwezi kukupa ticket kwamba atadumu na wewe au atakuona unafaa kuwa mke ndani ya nyumba ambaye kila siku atakuwa anasumbua suala la kutojiamini na uzuri wake wa nje.

Wapo wanawake warembo wengi sana wanaojua kujipamba kuanzia kucha za miguu hadi nywele kichwani, bado wapo single na wanaume wamekuwa wakipita na kukimbia.


Kawaida mwanaume huvutiwa sana na mwanamke ambaye emotionally anakuwa kawaida kuhusu anavyoonekana.
Mwanamke ambaye anahitaji sifa na attention kutoka kwa mwanaume kila mara kuhakikishiwa anapendeza wanaume wengi hukwepa kwa kuogopa kuishi nao maana ni usumbufu.
Ni wazi kwamba mwanaume huvutiwa na hupenda kuangalia uzuri wa nje wa mwanamke na wakati huohuo pia mwanaume huwa turned off emotionally na mwanamke ambaye anapenda appended kwa sababu ya uzuri wake.

Mwanamke akiwa ana act au kuonekana anapenda kujisikia vizuri tu kwa sababu ya urembo wake wa nje mwanaume huhisi mwanamke mwenye uhitaji wa aina hii ni usumbufu na mara moja huanza kujitoa au kukimbia kabisa.

Mwanaume huvutiwa na kudumu na mwanamke ambaye kwanza anajisikia vizuri kuhusu uzuri wake awe amependeza au hajapendeza ila anajiamini na kwamba kama alivyo ndiye yeye. Pia kuna mambo mengine yanayofanya mwanaume avutiwe na kubaki na mwanamke kama vile tabia, ufahamu na mitazamo mbalimbali kuhusu maisha na kwamba kama wataishi pamoja huyo mwanamke atakuwa msaada kwa mwanaume kufikia malengo yake ya maisha na mafanikio si urembo tu.

Mwanamke huhitaji kupendeza na kujipamba kwa kadri anavyoweza hata hivyo bila kujiamini kwanza na kutokuwa too much concerned kuhusu urembo wake bado mwanaume huona si good marriage material au good relationship material.

No comments:

Post a Comment