Thursday, 26 November 2015

KUFIKA KILELENI.

Si utundu na ujanja wa mwanaume tu unaomwezesha mwanamke kupata utamu wa kufika kileleni bali mwanamke pia anahusika.

KUFIKA KILELENI NI NINI?

Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.
Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii

Wengine wakifika kileleni hupiga kelele sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao, wengine hutulia kimya na kupitiliza usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa wananamwona Bwana n.k ilimradi tu ni raha na utamu na ni kweli Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba tena kwa namna ya ajabu.
Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming n.k
Pia wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.

Je mwanaume na mwanamke wote hufika kileleni sawa?

Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic, halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.

Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.

Nini Kitu muhimu kuhsu mwanamke kufika kileleni?
Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke hadi anahitimisha tendo zima angalau kwa dakika 10 au 15 ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye mataa akiugulia kwa kumuondolea utamu na raha.

Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
Lakini pia mwanamke anasehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.

Monday, 23 November 2015

UNENE HUPUNGUZA UUME.

Imethibitika kwamba mwanaume anavyozidi kunenepa uume huliwa na fat na kupungua urefu.
Habari njema ni kwamba kama wewe ni mwanaume overweight (fat) au mnene kupindukia unaweza kuongeza inchi moja ya uume wako kwa kupunguza unene kwa kila pound 35.

Kama umekuwa ni overweight kwa miaka yako yote basi hii ni kumaanisha kwamba hajawahi fikia urefu halisi wa uume wako.
Kama ni mwanamke na mume wako anazidi kunenepeana usishangae siku unaanza kutafuta samaki wake kumbe kaliwa na fat au nyama zembe hivyo saidiana naye kupunguza fat ili abaki na size yake kama kawaida.
Siyo utani wala kichekesho ni kweli unavyozidi kunenepa (hapa nazungumzia unene unaozidi kawaida) ndivyo unavyozidi kupunguza urefu wa uume.

Sunday, 22 November 2015

MAHUSIANO YAKO NI YAPI?

Ni vizuri kufahamu kwamba ili mahusiano yadumu kuna umuhimu wa wapendanao kuwa na asilimia kubwa ya kufanana kwa tabia kuliko kuwa tofauti.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za mahusiano ambayo baada ya muda mwanandoa huweza kujikuta ndoto zinayeyuka.

1.MAHUSIANO YA HASIRA.
Hapa mtu anaenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye ni tofauti kabisa na familia yake kwa kila kitu na lengo ni kuikomoa familia yake (wazazi na ndugu) kwa sababu una hasira nao.
Kuna njia za kupamba na hasira lakini si katika kuoa au kuolewa kwani mwenye kuumia ni wewe.
Pambana na hasira zako kwa njia zingine pia jifahamu na uwe na moyo wa kusamehe ndo kuonesha maturity lakini si hasira na kwenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye yupo tofauti na wewe mwenyewe kwa lengo la kuwakomoa wazazi.

2.MAHUSIANO YA KIMISHENARI.
Haya ni mahusiano ambayo mmoja hujaribu kubadilisha dini ya mwenzake ili aoe au kuolewa “Usipobadilisha dini sikuoi au huwezi kunioa”,
Je, akikubali kubadilisha dini then akakuoa na baada ya kukuoa akaacha dini yako itakuwaje? Utajuta!
Ukweli ni kwamba mahusiano ya aina hii hayawezi kuwa na afya mbele ya safari kwani mmoja huwa na agenda ya siri (anaweza kusema ndiyo nimekubali kumbe moyoni hajakubali kabisa anakutaka wewe tu siyo dini yako) na bahati mbaya zaidi ukishaingiza mambo ya dini kwenye ndoa ni ngumu sana kuvunjika.
Unachanganya emotions za mapenzi na dini?
Romance na dini?
Atakukubali kubadilisha ila mbele ya safari (siyo mwisho) mmoja huangukia pua.

3.MAHUSIANO YA KUTOA SADAKA.
Wengi hasa wanawake (si wote) huamua kujitoa sadaka kumpenda mwanaume ambaye hapendeki kwa malengo kwamba siku moja atanipenda asilimia 100.
Huu ni uhusiano kama wa mgonjwa na nesi kwa maana kwamba hujitoa kupenda, kufariji, hata kumtunza mpenzi wake kimavazi, chakula, pesa akitegemea atakuja kupendwa zaidi au kuolewa wakati huohuo anayefanyiwa wala hana mpango.
Mahusiano ya ana hii huwa so exciting mwanzoni hata hivyo mwisho wa safari anayejitoa sadaka huona amedanganywa na kutumiwa.

4.MAHUSIANO EXOTIC
Haya ni mahusiano ya watu ambao kunatofauti kubwa sana ya utamaduni na mila.
Ni kweli mahusiano ya aina hii huwa exciting na adventurous.
Hata hivyo kuna wakati hukosa ladha, hivyo jambo la msingi kabla ya kuwekeza muda wako, nguvu zako, pesa zako kwenye haya mahusiano ambayo unaenda nchi za mbali kubeba exotic species hakikisha umefikiria miaka 50 ijayo.

5.MAHUSIANO YA TOFAUTI YA UMRI ULIOPITA KIASI.
Hapa kunakuwa na tofauti kubwa sana ya umri wa wahusika, ni kweli age is just a number hata hivyo haiko hivyo wakati wote.
Kupishana miaka zaidi ya 20 kuna matatizo yake.

Hata kama unataka kuishi na mama au baba si suala la mke au mume kwani kuna wakati wanandoa huhitaji kuwa na fun ambazo kwa umri kupishana sana ni ngumu.
Hata tukiacha sababu ya kisaikolojia za tofauti kubwa ya umri suala la kupishana sana umri ni moja ya mahusiano yenye tofauti kubwa kuliko kufanana.

Mwanzoni inaweza kuwa raha kwani mwenye umri mkubwa anaweza kuwa amejijenga hata hivyo baada ya muda anaweza kukugeuka kwa hivyo vitu vyake, zaidi anakuwa hana energy kwa baadhi ya shughuli pia kuna kupishana sana katika interest kwani mwingine anakuwa wa miaka ya 47 iliyopita na mwingine kizazi kipya au unaweza kuona mwenzako ni kama mtoto au ana IQ ya kitoto kila siku.

"ONE FOR THE ROAD"!!

Moja ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika suala la tendo la ndoa (kuwa mwili mmoja) ni kitendo cha mwanaume kupenda kufanya mapenzi asubuhi anapoamka na mwanamke kuweka muda maalumu kufanya mapenzi usiku kabla ya kulala.

Kwa mwanaume kupenda sex asubuhi huchochewa na kitendo cha kusimamisha bunduki yake zaidi ya mara tano usiku na anapoamka asubuhi (kitaalamu wanaita Nocturnal penile tumescence – NPT) na wengine huita morning glory au morning wood.
Hii kitendo cha mwanaume kuamka huku amesimamisha kwanza ni kuonesha kwamba ni rijali na pili hupelekea kuwa na sababu nzuri ya kumshawishi mke kuwa na morning glory kabla ya kuwahi kazini.

Hata hivyo mwanaume anahitaji kuwa makini kwani mke anaweza kuwa hata hajafungua macho na mzee anataka, approach unayotumia ni muhimu ili na yeye aweze kukubaliana na kufurahia kupeana one for the road.

Wengine Wanasema kufanya mapenzi asubuhi huweza kuelezea good day na great day.

Ukweli ni kwamba homoni za testosterone huhusika na masuala ya sex kwa mwanaume moja kwa moja na ingawa hizi homoni zinapatikana kwa mwanamke bado mwanamke ana homoni zingine zinazomsaidia masuala ya sex.

Hizi homoni hupenda na kushuka kwa vipindi tofauti yaani mchana usiku na asubuhi, kuongezeka kwa homoni huwa mkubwa wakati wa asubuhi basi utapenda kuwa na sex asubuhi kuliko usiku na kama huongezeka usiku basi utapenda sex usiku na kama huongezeka mchana basi utapenda sex mchana hii ni pale tu kuongezeka kwa homoni kunapokupa hamu.

Ni kwamba binadamu ni complex individuals, hata kama homoni huweza kuathiri tabia zetu linapokuja suala la mapenzi bado si factor muhimu inayotakiwa kuzingatia jinsi tunavyopenda na kuishi na wapenzi wetu.

NI JINSI UNAVYOWEZA KUTUMIA TU.

Wanaume wengi na wanawake wengi huhofia sana size ya baadhi ya viungo vinavyohusika na uzazi.
Wanaume wako concerned na size ya uume linapokuja suala la mapenzi, wakati wanawake wao wako concerned na size ya matiti na uwezo wa uke kuhimili uume mrefu, kwa bahati mbaya ujinga wa aina hii huzalisha hofu, mashaka na woga ambao hupelekea kutojiamini linapokuja suala la mapenzi.

Ukweli ni kwamba haijalishi mwanaume ni mrefu au ni mfupi au ni mnene kiasi gani urefu wa uume huwa si zaidi ya inches 6, na kiasi cha inches 3 tu za urefu wa uume wowote huweza au zinatosha kabisa kumfurahisha mwanamke kimapenzi na akaridhika.
(hapa muhimu ni skills jinsi ya kutumia sticks na si urefu wa sticks).

Pia haijalishi mwanamke ni mrefu kiasi gani au ni mfupi kiasi au ni mnene kiasi gani wanawake wote huwa na uke ambao hauwezi kuwa mpana zaidi au pungufu ya inches 1.

Utafiti unaonesha kwamba mwanaume mrefu sana akioana na mwanamke mfupi sana wanaweza kufurahia mapenzi (sex) sawa na wale ambao mwanaume na mwanamke wana urefu sawa.
Tofauti ya urefu wa kimo kati ya mwanamke na mwanaume huweza kuleta shida au matatizo wakati wa kupeana kisses wakati wa kuwa mwili mmoja.

Pia suala la mwanamke kuwa na matiti makubwa sana au madogo sana huwa na usumbufu wa aina yake kwa wanawake hasa wale wambao hawajaolewa.
Hata hivyo jambo la msingi ni kujiamini kwamba na kufahamu kwamba kuwa na matiti makubwa sana au kidogo sana maana yake huna tatizo na unaweza kuvutia na kuwa sexy sawa na wengine tatizo ni attitude yako.

Saturday, 21 November 2015

Nilipata swali hili nami nikaamua kulijibu na kwa wengine wafahamu.

SWALI;
Je, Ni kweli kwamba kisimi, kinembe ni kiungo pekee ambacho mume ni lazima aguse (chezea) ili mke asisimke na kuwa tayari kuwa mwili mmoja?

JIBU;

Si kweli.
Mwanamke si Channel za radio kwa maana kwamba ukibonyeza kitufe pale station inapatikana basi utapata frequency na kuanza kufaidi matangazo yake (muziki au habari).
Mwanamke ni kiumbe cha tofauti ambacho hutawalaliwa na hisia (emotions, mood na feelings).
Pia wanawake wote hutofautiana na hata huyo mmoja huweza kuwa tofauti kila siku hii ina maana kwamba kama jana alisisimka sana ulipomchezea kisimi si kanuni kwamba na leo atasisimka kwani inaweza kuwa katika mzunguko wake basi matiti ndiyo yanasisimka zaidi au G-Spot ndo anasisimka zaidi nk.
Ni jukumu la wewe mwanaume kuwa sensitive na smart kujua hitaji lake au ni kiungo gani kwa huo anasisimka zaidi.

Kuchezea kisimi chake si kanuni au sheria au utaratibu ambao umewekwa na kwamba usipofanya basi hakuna kusisimka, ingawa ni kweli mwanamke huweza kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi zaidi wakati mwingine kuliko kutwanga na kupepeta kwenye kinu.
Mwanamke anahitaji maandalizi kwanza, anahitaji busu, caring, anahitaji mwanaume mwororo, gentle, loving, anayebembeleza, mwanaume mwenye mikono slow na mwenye mwendo wa kobe kuzunguka (kumtembelea) kiwanja kizima cha mwili wake kabla ya kufika huko kwenye kisimi.

Ni muhimu kwenda sehemu zingine za mwili kwanza kama matiti (chuchu) na sehemu zingine kuanzia zile ambazo zinasisimka kidogo hadi zile ambazo ukimgusa mwili wake unapata joto kiasi cha yeye kutoa ukelele ambao utajua kweli tumeanza kupanda mlima na kileleni tutafika.
Wanawake wengi (siyo wote) hulalamikia kitendo cha mwanaume kuwa na full speed kwenda kwenye kisimi bila kupita maeneo mengine kiasi ambacho huwa ni kuumia au kuumizana kwani kisimi huwa hakijawa tayari kupokea msisimko.

Kumbuka hili eneo lina zaidi ya nerves 8,000 hivyo ni muhimu kuguswa wakati ambao eneo lipo tayari na evidence kwamba kupo tayari ni eneo zima la south pole kuwa wet.
Kupeleka vidole vyako vikavu na bado kukavu huweza kuumiza badala ya kutoa raha.

NI MUHIMU KUJADILI SUALA HILI.

Sex ni somo au kitu ambacho ni exciting duniani, hata hivyo ni kitu kigumu sana na husumbua sana kujadili na hii inatokea mara nyingi kwa wale walio kwenye ndoa.

Mwanaume na ujanja wake wote kuna wakati hujikuta ananywea kuongelea suala la sex au kumshirikisha mke mpenzi nini wafanye ili wanapokuwa mwili mmoja kuwa na kuridhika kwa kila mmoja.
Pia wapo wanawake huogopa kuongea bayana na wazi kile wanahitaji kwa mume au mahusiano na kwa kuwa kuna stima kubwa kwa mwanamke kuwa passive kwenye ndoa matokeo kila mmoja anakula jiwe na wote huishia kuumia na kuugulia wakati wanandoa wengine duniani wanaongea na kuweka sawa mambo yao chumbani bila woga.

Kawaida unavyochelewa au kuacha kuongelea issue hii ya sex kwenye kuta nne za chumba chenu ndivyo inazidi kuwa ngumu zaidi na huzidi kuwapa disconnection ya feeling kwenu wawili.

Jambo la msingi ni kufanya haya Yafuatayo:-
Omba Mungu akupe hekima na busara ili uweze kujadiliana na mume wako au mke wako kwa upendo na wazi issue hii, wewe unadhani uliondoka kwa wazazi wako kuja kwake ili iweje kama si kupata mtu ambaye atakupa hitaji la mwili wako.
Hii issue ni muhimu kuijadilia kama mnavyojadili mipango mingine ya familia kama fedha na miradi.

Tafuta muda ambao wewe na mwenzi wako mnaweza kukaa chini na kujadili, tafuta sehemu ambayo imetulia na hamuwezi kusumbuliwa na kitu chochote.

Muhakikishie kwamba unampenda na onesha msingi wa upendo ulio nao kwake, elezea hisia zako halisi na kwamba kuna kitu ambacho hukipati katika maisha ya ndoa, na kwamba ungependa muongelee na ukipate.

Hatua kubwa na ya msingi ni kwa wote kukubali kwamba kuna tatizo.
Ukweli ni kwamba ukiona unashindwa kuongelea issue za sex kwenye ndoa, maana yake mnashindwa kuongelea mambo mengi ya msingi.
Pia kuongelea suala la sex ndani ya ndoa huweza kuwaweka karibu zaidi na wanawake hupenda sana hii topic kwani huonesha kwamba mwanaume anajali.



MKIHUDUMIANA VIZURI,UGOMVI UTAPUNGUA

Wakati mwingine mwanaume hujikuta amekuwa mkali, majibu ovyo na mkato, violent na mwenye hasira kumbe tatizo ni kutotoshelezwa kimapenzi na mke wake, acha wale wanaume ambao ukali kwao ni nature.
Pia wapo wanawake ambao huwa violent maofisini hasa kama ni boss (siyo wote lakini) hata kitu kidogo tu kwake inakuwa issue.

Moja ya matokeo ya kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha, mke na mume kuridhishana na kila mmoja kuridhika na mwenzake ni kupunguza misuguano katika ndoa.
Mwanaume ambaye anapata huduma inayomridhisha kimapenzi huwa ni mwanaume aliyetulia
Hii haina maana kwamba matatizo makubwa yatatoweka yenyewe au kwa kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha basi ada ya shule watoto itapatikana haraka au itasaidia budget kuwa shwari.

Wapo wanaume wengi hawafahamu kwamba baadhi ya matatizo yanayokuwa nayo nyumbani na kazini yanaweza kuwa traced kwa kutokana na utoshelevu wa tendo la ndoa wanavyopeana mke wake pia mke mwenye hekima na busara huweza kutambua namna mume wake ana-behave nyakati tofauti na anajua dawa yake ni ipi.

Katika ulimwengu wa ndoa wakati mwingine matatizo madogo madogo huweza kupungua size kutokana na hali nzuri ya utendaji kitandani.
Hii ina maana kuna mizozo mingi ingekuwa haisikiki katika ndoa kama kila mmoja angejua kwamba kumridhisha mpenzi kimahaba inaweza kuwa dawa tosha.

Kuridhishwa kwa tendo la ndoa pia husaidia nervous system ya mwananmke kuwa relaxed.
Wapo wanawake kutokana na kukosa huduma au kuhudumiwa vizuri na waume zao hadi kuridhika kimapenzi wamekuwa wakali, wenye vurugu, visilani na hata maofisini kama ni boss kuwaka moto kwa kila mfanyakazi pasipo sababu ya msingi acha wale wanawake ambao ni wakali by nature.

Mfumo wa fahamu wa mwanamke umeunganishwa moja kwa moja na viungo vya uzazi na kila mwanamke kutoka kila aina ya maisha duniani ameumbwa kuwa na uzoefu wa kupokea furaha ya Ku-relax kupitia kitanda cha ndoa (sex).
Hivyo basi mwanaume anayejua raha ya mwanamke kuwa relaxed anakuwa mjanja kuhakikisha kitanda kinakuwa na moto wa kutosha.

Friday, 20 November 2015

JE,WANAUME WANAPENDA UREMBO TU?

Kuna usemi kwamba jinsi mwanamke anavyovutia kwa mwanaume ndivyo mwanaume humuhitaji zaidi.

Ukweli ni kwamba jinsi usivyokuwa concerned sana na physical appearance ndivyo mwanaume atakuhitaji zaidi na kama ndo dating unaweza kuona mwanaume anakuganda hadi inakuwa ndoa.

Nahisi unadhani hii haijakaa sawa hata hivyo subiri kidogo tuchambue.
Inaweza kuwa kweli kwamba Ukitaka kumvutia mwanaume ni muhimu kujipamba haswaa na kuvaa nguo ambazo zinaweza kumvuta mwanaume yeyote kwani ugonjwa wa wanaume wengi ni kile anaona.

Mwonekano wako unaweza kumvuta mwanzoni lakini hiyo haiwezi kukupa ticket kwamba atadumu na wewe au atakuona unafaa kuwa mke ndani ya nyumba ambaye kila siku atakuwa anasumbua suala la kutojiamini na uzuri wake wa nje.

Wapo wanawake warembo wengi sana wanaojua kujipamba kuanzia kucha za miguu hadi nywele kichwani, bado wapo single na wanaume wamekuwa wakipita na kukimbia.


Kawaida mwanaume huvutiwa sana na mwanamke ambaye emotionally anakuwa kawaida kuhusu anavyoonekana.
Mwanamke ambaye anahitaji sifa na attention kutoka kwa mwanaume kila mara kuhakikishiwa anapendeza wanaume wengi hukwepa kwa kuogopa kuishi nao maana ni usumbufu.
Ni wazi kwamba mwanaume huvutiwa na hupenda kuangalia uzuri wa nje wa mwanamke na wakati huohuo pia mwanaume huwa turned off emotionally na mwanamke ambaye anapenda appended kwa sababu ya uzuri wake.

Mwanamke akiwa ana act au kuonekana anapenda kujisikia vizuri tu kwa sababu ya urembo wake wa nje mwanaume huhisi mwanamke mwenye uhitaji wa aina hii ni usumbufu na mara moja huanza kujitoa au kukimbia kabisa.

Mwanaume huvutiwa na kudumu na mwanamke ambaye kwanza anajisikia vizuri kuhusu uzuri wake awe amependeza au hajapendeza ila anajiamini na kwamba kama alivyo ndiye yeye. Pia kuna mambo mengine yanayofanya mwanaume avutiwe na kubaki na mwanamke kama vile tabia, ufahamu na mitazamo mbalimbali kuhusu maisha na kwamba kama wataishi pamoja huyo mwanamke atakuwa msaada kwa mwanaume kufikia malengo yake ya maisha na mafanikio si urembo tu.

Mwanamke huhitaji kupendeza na kujipamba kwa kadri anavyoweza hata hivyo bila kujiamini kwanza na kutokuwa too much concerned kuhusu urembo wake bado mwanaume huona si good marriage material au good relationship material.

JE,NINI SIRI YA MWANAMKE KUWA HODARI KITANDANI.

Kwenye suala la mahusiano (kufanya mapenzi katika ndoa au kuwa mwili mmoja au tendo la ndoa kwa mwanamke kuwa na IQ kubwa au vipaji au umri mzuri katika ndoa havina maana sana ukilinganisha na mental attitude uliyonayo kuhusiana na suala la kufanya mapenzi.

Wapo wanawake walioolewa (si wote) ambao ni warembo, wamesoma, ni portable, matiti katika size inayong’ang’aniwa na wanaume, wana vipaji vya ajabu na umri sahihi wa kuwa kwenye ndoa na sifa zingine kedekede zinazofanya aonekane mwanamke wa nguvu, lakini linapokuja suala la mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja wamekuwa si lolote na aibu tupu kama si kukatisha tamaa kwa waume zao.

Kwa upange mwingine wapo wanawake (si wote) kwenye ndoa wapo wapo tu na sura zao, hawajasoma, IQ ni ndogo, wapo overweight, vifua flat kama wanaume, hawana hata uwezo wowote katika jamii; hata hivyo linapokuja suala la mapenzi au kitandani ni moto wa kuotea mbali na wanawapa waume zao vitu vya uhakika kitandani.

Na wapo ambao anaweza kuwa kwenye kundi lolote hapo juu na akawa zero kitandani au akawa moto kitandani.

Je, ni nini siri ya mwanamke kuwa moto kitandani na mume wake?
Ukweli si size wala shape wala appearance ya mwanamke ndiyo inayo dhihirisha ufundi wake kitandani bali mtazamo kuhusu tendo la ndoa (sex) ndio msingi unaoweza kuelezea mafanikio na kushindwa kitandani.

Kama mwanamke anaamini kufanya mapenzi ni uchafu au ni kitu kibaya au mtazamo wowote potofu katika ndoa hataweza kuleta furaha ya kweli.
Kama anaamini mapenzi katika ndoa ni legalize rape basi hata siku moja hataweza kufurahia mapenzi atakuwa anajiona anabakwa kila siku.

Kama anaamini matiti yake ni madogo sana au makubwa kupita kiasi ambacho hawezi kufurahia kufanya mapenzi ni kweli hataweza kufurahia na anaweza kukosa feelings za kweli kuhusu mapenzi ndani ya ndoa.
Kama anaamini skills zake katika kufanya mapenzi ni pungufu basi hataweza kufurahia raha ya kuwa mwili mmoja.
Kama anaamini mwili wake upo ovyo kiasi kwamba hawezi kuwa uchi mbele ya mume wake basi ni dhahiri faragha na mumewe imeingiliwa.

Katika utafiti ambao ulihusisha wanaume ambao sehemu zao za siri ziliondolewa testicles (mapumbu) na wanawake ambao waliondolewa visimi na kuwachunguza wanavyofanya mapenzi na partners wao; ilikuja kujulikana kwamba walifurahia kufanya mapenzi sawa na wengine ambao wapo salama.
Hii ni kudhihirisha kwamba organs (kisimi na pumbu) hazikuwa msingi wa wanandoa kufurahia mapenzi bali jinsi wanavyofikiria au mtazamo wao kuhusu tendo la ndoa.

Hii ina maana unaweza kuwa na size, shape na appearance tofauti au yenye hitilafu kwa mtazamo wa jamii lakini ukiwa na mtazamo (binafsi) mzuri kuhusu mapenzi unaweza kufurahia tendo la ndoa kwa njia ya ajabu sana na unaweza kuwa moto kitandani na mumeo kukufurahia.

KWANINI IMESISITIZWA WANAUME TU!

Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake.
Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume.

Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana.

Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama,
Wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali.

Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa!
Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume.

Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali.

Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa!

Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume.

Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake.

KUWA MAKINI NA MDOMO WAKO.

Sisi wote huwa tunaongea na marafiki na watu wa karibu kuhusu ndoa zetu, hata hivyo mambo tunayowaambia marafiki ni muhimu sana na huweza kuleta matokeo mazuri sana au mabaya sana kwa ndoa zetu.
Pia duniani tunatofautiana sana hasa kutokana na tamaduni zetu kwa mfano mzungu mara nyingi hana siri haijalishi ni siri ya kitu gani anaweza kukwambia kitu kinachohusu mume wake au mke wake kiasi ambacho unaweza kushangaa na tukirudi kwenye jamii zetu za kiafrika nasi kwa kutunza siri tunajua.
Kuna wakati kutunza siri ni upuuzi kabisa kwani ni siri ambazo ukificha mwisho wake kuna madhara makubwa sana.
Kwa mfano kuficha siri kwamba kabla hujaoana na huyo umeoana naye hukuwahi kuwa na mtoto wakati mtoto unaye na yupo na bibi yake kijijini, hiyo ni hatari kwani siku akigundua ni kweli trust kwako itapotea.

Leo tuangalie hili la kuongea siri za nyumbani kwako na mume wako au mke wako na mmoja wenu anaenda kzimwaga kwa marafiki zake, au wafanyakazi wenzake au mama yake au baba yake au ndugu zake kwa kukuzunguka na anaongea hayo mambo kiasi kwamba ungekuwepo asingethubutu kuongea.
Kulinda siri za mume wako au mke wako ni jambo muhimu sana hasa katika kuimarisha trust katika ndoa.
Bahati mbaya ni kwamba wapo wanandoa ambao wao kutoa siri za mke au mume kwa rafiki au watu baki kwake si tatizo ni kama mdomo una washa.

Yaani kitu kidogo tu mfano kuzozana kidogo tu na mume au mke usiku, ile kuamka asubuhi tayari umeshawambia baba, mama, ndugu, majirani na wafanyakazi wenzake kwamba jana mlizozana wakati wala hakuna faida anayopata na anadhani kuwaambia wengine basi yeye anafaa sana kumbe nao huishia kumdharau.

Unapokuwa ni mwanandoa mtoa siri nje unapoteza hadhi yako ya kuwa mwanandoa.
Ni kama unatengeneza kilema kwa partner wako hasa kwa wale unawaambia siri zenu.
Ndiyo, kuna wakati na pia ni muhimu kushirikisha wengine struggles za ndoa hasa mtu wa karibu ambaye unaamini anaweza kukushauri na kukusaidia lakini si kumwaga siri kwa kila mtu.

Ulimwengu wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa anatoka asubuhi na mapema kwenda kutafuta riziki na mke alikuwa na muda nyumbani kuendelea na kazi zake na watoto.

Siku hizi kila mmoja anaaondoka asubuhi na mapema kwenda kazini na huko kazini anatumia muda mwingi kuliko nyumbani, kubwa zaidi ni kwamba kazini anashinda na mke wa mtu au mume wa mtu au wanaume na wanawake ambao si mume wala mke au watoto.

Tafiti nyingi zinaonesha wanandoa wengi sasa wanatumie muda mwingi zaidi kazini kuliko kuwa na familia hii ina maana mwanandoa anatumia muda mwingi wa kazi kushinda na mke wa mtu au mume wa mtu na kama huyo mke wa mtu ndo amekuwa mtu wa kumwagia siri zake za nyumbani au chumbani kwake na mwenzi wake anakuwa ana date na huyo mke wa mtu au mke wa mtu bila kujua.
Kwani ku-share siri ni moja ya kuwa intimate na mtu ndiyo maana sasa tunakuwa na matukio mengi ya ofisi romance kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.

KELELE ZA MAHABA KITANDANI.

Kwa mwanaume hakuna kitu kinakuwa sexy kama mwanamke ambaye anakuwa loud kitandani na si kuwa na vikelele tu bali kujihusisha moja kwa moja kwa mwanamke katika kuongea maneno matamu
au sweet words).

Mwanaume akiwa kwenye game anapenda sana kujua mke wake anajisikia vizuri kwa kile anafanya na kwamba mwanamke anaonesha total participation, pia vile mke unatamka jina la mume wako kwa manung'uniko ya kimahaba huleta raha sana pamoja na vikelele vingine kama vile ooooh! aaah! mmmh! nk humpa uwezo zaidi mume kuendelea kukurusha kwa namna ya ajabu na kuweza kukuridhisha inavyotakiwa.

Kawaida mume huaanza kukuuliza kama kile anafanya unakipenda na kwa njia hii ni vizuri wewe mwanamke kumweleza vile unajisikia na unaweza kuji-express kwa uwezo wako wote na hapa ndipo unaweza kuongea sweet word zote (ulizojufunza au kadri feelings zako zinavyokupa taarifa kwenye kiungo kile kinapata raha au kinaguswa kwa mguso mtamu zaidi) si unajua mapenzi ni sana na msanii mzuri anajua nini aongee na aongee namna gani na mwanamke umejaliwa kuwa na sauti ambayo kwa miguno na kulalamika kimahaba mnaweza kuwa na sherehe nzuri sana ya kuwa mwili mmoja.

Kuwa kitandani ni nafasi kubwa sana mke kuweza kuonesha umaridadi wake haina haja kushona mdomo au kubaki kimya kama vile mume amelala na gogo badala jitume kwa maneno na matendo, huu ni uwanja wako, mume wako, jipe raha na enjoy raha ya mwili.
Piga kelele kwa raha zako na unaweza kutamka kitu kizima kizima bila woga maana huyo ni mume wa ujana wako.

Wanaume nao wakati mwingine huwa insecure kama wanawake wakiwa kitandani hivyo kumtia moyo kwa miguno na vikelele vya kimahaba huweza kumpa ushahidi kwamba una-enjoy kile anafanya na kwamba skills zake na utaalamu wake mke unampa credit naye atajisikia vizuri na kufanya zaidi na hata kujifunza siku nyingine afanye kwa ufundi zaidi.
Hivyo usiogope kuwa mbunifu, lazima uwe mshangiliaji mzuri kwenye mechi na mumeo na hiyo itakuhakikishia furaha zaidi wakati wa kuwa mwili mmoja.
kama ni shule basi maksi zako ni zaidi ya 95%

Mambo ya kuzingatia
Hata kama wanaume huwa tunafurahia sana mke kuwa noise kitandani ni muhimu kuwa makini na sauti kwani kupiga kelele kama unapigwa na majambazi si ustaarabu kwani mtaa mzima unaweza kuhamaki na kuja kutoa msaada kumbe watu mnapeana raha zenu au mnaweza ku-attract mijitu inayopenda kupiga chabo bure.
Ni vizuri hakikisha chumba kina Mfumo mzuri wa kuchuja sauti kwani mnaweza kushtakiwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria cha Antisocial behaviour order kwani baadhi ya nchi zinafuata na mnaweza kuishia jela au mkajenge nyumba yenu huko shamba mpigiane mikelele yenu.


Wanasayansi katika utafiti wao wamegundua kwamba mwanamke anapokuwa na kelele kitandani wakati wa kuwa mwili mmoja mwanaume huwa na asilimia 59 za kukojoa (siyo mkojo) tofauti na asilimia 2 kwa mwanamke kuwa kimya na pia mwanamke huwa na kilele zaidi kitandani akiwa fertile na kwa mwanamke kuwa na kilele speed ya mwanaume na uwezo wa kusugua huongezekana maradufu wakati wa kuwa mwili mmoja.

FAHAMU HAYA YAHUSUYO NDOA.

"Unajua siku hizi hunipendi” mwanamke ambaye ameishi na mume wake kwa miaka 7 alimlalamikia mume wake.

"Hivi unaongea kitu gani na wewe, kwa nini unasema hivyo?"
Mume naye alimjibu mke wake kwa kushangaa kwa nini mke wake anasema hampendi!

"Ni kweli hunipendi na siku zinavyozidi naona hunipendi zaidi" mwanamke aliendelea kulalamika.
Mshauri wa ndoa akaingilia kati na kumuuliza mume "je, huwa unamwambia mke wako Nakupenda?"

Kwa majivuno mwanaume akajibu kwamba
“anajua nampenda kwani kila jioni nawahi nyumbani kuwa naye, nampa pesa anazohitaji anunulie kitu chochote anataka, nimemjengea nyumba nzuri, nimemununulia gari zuri, Pia nimekubali kuja naye kwako mshauri, je unadhani hadi hapo simpendi?

Mshauri akakaza uzi bado kwamba acha hayo yote je, huwa unamwambia “Nakupenda" mke wako?”
Mume akawa anamwangalia mke wake na mke akawa anatikisa kichwa kukubaliana na maneno ya mshauri wao wa ndoa kuonesha ni kweli huwa haambiwi na mume wake “nakupenda mke wangu.
Mume akajibu akasema “hivi kuna ulazima gani kumwambia nampenda wakati vitu ninavyofanya kwa ajili yake vinaonesha nampenda?"

Hapa wanaume wengi tunaweza kuandamana kumtetea mwanaume mwenzetu na kwamba huyu mwanamke ana lake na kweli hana shukuruni kwani wanawake wangapi wamefanyiwa vile yeye amefanyiwa na wapo kimya, huyu mwanamke pamoja na mazagazaga yote mwanaume mwenzetu amejtajidi kumpa bado anaonekana hampendi.
Hata hivyo linapokuja suala kuonesha mwanamke anapendwa tunatofautiana sana na mitazamo tunayo wanaume wengi.

Mwanamke huhitaji kusikia kwa maneno (tamka) mkiwa wawili au hata mbele za watu kwamba unampenda au “nakupenda”.
Pia inaonekana ni jambo au suala la kawaida sana ingawa mwanzo wa kupendana watu huambiana maneno mengi matamu lakini wanavyoendelea na mahusiano huanza kujisahau.

Kuna maneno zaidi ya 16 ambayo wanandoa ni muhimu sana kuyatamka kila mmoja kwa mwenzake ili kuleta affections na msisimko wa kujisikia unapendwa hasa wanawake.

1.NAKUPENDA.
Ni vizuri kuwambia nakupenda kabla hujaondoka kwenda kazini na wakati ukifika nyumbani baada ya kutoka kazini, mwambie nakupenda kabla hujamaliza kuongea kwenye simu.
Kila ndoa huhitaji dose kila siku na dose mojawapo ya kila siku ni neno nakupenda. Wala usiwe na wasiwasi kusema nakupenda kila si tabia mbaya hata kama mwenzio amekasirika kwa jambo Fulani na kusema nakupenda kunaweza kufungua mlango wa kusamehewa haraka.

2.SAMAHANI.
Uliambiwa unaporudi uwe umenunua maziwa na ile unafika nyumbani kumuona mke wako unakumbuka kwamba maziwa hujanunua, sema nisamehe, wewe ni mke na ulimuahidi mume wako kwamba utafua nguo zake na hana nguo za kuvaa sema unisamehe na maanisha.
Huwa hatumsaidii mtu yeyote tunapojilinda kwa namna yoyote, ila kiburi ndicho hupata faida. Nakuogopa kutumia neno nisamehe lakini, kwani hiyo huua msamaha.

3.UMEPENDEZA.
Wakati tunachumbiana huwa tunapeana sifa kila siku hata hivyo baada ya kuendelea sana kwenye ndoa tunajisahau kupeana sifa.
Labda tunadhani mwenzi anajua jinsi tunavyiojisikia au tunadhani kwamba haina haja tena kuendelea kutoa sifa.
Mwanamke anahitaji kuendelea kuambiwa anapendeza hata baada ya kuzaa mtoto wa kwanza, wa pili hadi mwisho ingawa kuna wakati anaweza hata mwenyewe asikubali hata hivyo wewe umefanya nafasi yako.
Hata wanaume nao wanahitaji la kuambiwa amependeza au leo yupo handsome na pamba zake alizijipiga.
Kupeana sifa huimarisha intimate kati ya wanandoa, kama mke wako hajioni ni sexy kwa nini awe anataka mahaba kwako? Mhakikishie kwamba yupo sexy na akili yake itafunguka kwamba unamuhitaji.

4.NAKUHITAJI.
Wapenzi wetu wanahitaji siyo kufahamu kwamba tuna wa-appreciate tu bali tunawahitaji, tunapaswa kuwaambia kwamba maisha bila wao yangekuwaje? Inakuwaje kila wiki wakijua kwamba tunawahitaji.
Kama kutamka kwa mdomo inakuwa ngumu kumwambia nakuhitaji kila siku basi andika barua, message, email nk.
Mwanamke anahitaji kusikia kwamba anavutia pia wanaume wanapenda kufahamua kwamba mke anamuhitaji pia.

5.ASANTE.
Hivi inakuwaje watu wa nje ndo wanazipata asante zetu kwa wingi kuliko sisi wanandoa wenyewe.
Ukienda sokoni au kazini asante zinatoka bila wasiwasi na mume na mke inakuwa ngumu?
Mwambie asante mke kwa dinner, asante kwa kusafisha nyumba, kwa kukufulia nguo, mwambie asante mume kwa jinsi anavyoweza kuipa familia kipato, mpe asante kwa kuwahi kurudi nyumba.
Kama unashindwa andika email au ujumbe wa simu au vyovyote unaweza.

FAHAMU MAHITAJI YA MWENZAKO.

Kama ni mwanandoa ambaye unataka kuwa na ndoa yenye furaha, inaweza kuwa ndiyo kwanza unaanza maisha ya ndoa, au unaweza kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu na ndoa ipo hali mbaya kiasi kwamba unajuta kwa nini upo kwenye ndoa au inawezekana wewe ni mmoja ya wanandoa ambao wanafurahia kuwa kwenye ndoa na unapenda kujifunza zaidi na kuwa na ndoa yenye kumpa Mungu utukufu zaidi.

Jambo la msingi ni kwamba unaweza kuijenga ndoa imara kama utajifunza kufahamu mahitaji ya mwenzako na kuyatumia.

Bila kutimizwa kwa haya mahitaji muhimu wanandoa wengi hujikuta katika matatizo makubwa baina yao.
Mahitaji ya mwanaume na mwanamke ni tofauti hivyo basi kila mmoja anahitaji kuwa makini kujua upande mwingine unahitaji kitu gani na si kuhitaji tu bali kutimiza.

Mahitaji matano muhimu ya mwanaume katika ndoa.

1.Kuridhishwa kimapenzi.

2.Mtu wa kuandamana naye.

3.Mke anayevutia.

4.Msaada nyumbani.

5.Kuwa na mwanamke anayemuhitaji.

Mahitaji muhimu ya mwanamke katika ndoa.

1.Upendo.

2.Mtu wa kuongea naye

3.Uwazi na ukweli

4.Kutimiziwa hitaji la fedha.

5.Mwanaume anayejali familia.

Kwa mwanandoa kukosa moja ya hayo mahitaji muhimu huweza kutengeneza kiu ambayo lazima ipate maji.
Baada ya mwanandoa kukosa mahitaji hayo muhimu anaweza kushawishika kuanza kutafuta kutimizwa nje ya ndoa yake.

MUHIMU.
Hata kama mwanandoa mmoja anashindwa kutimiza mahitaji muhimu kwa mwenzake kutoka nje ya ndoa bado si jibu au jawabu kwenda kukipata kile unakosa.
Njia sahihi ni kukaa pamoja na kuelezana kwa upendo kila mmoja kueleza kile anakosa na kuendelea kuijenga ndoa kwa pamoja kwani huko nje kuna foxes ambao kama si kuweza kukutafuna mzima mzima basi unaweza kuangamiza familia nzima.

HAYA HUMNYIMA RAHA MUME.

Kama kufanya mapenzi kati ya mke na mume huweza kuwaunganisha wanandoa kiasi kwamba hata kama kuna bad relatioship huweza uwa nzuri na mpya pia suala la kufanya mapenzi mke na mume huweza kuua mahusiano mazuri kama timing na utendaji unakuwa tofauti.

Mambo yanayomnyima raha mume kutoka kwa mke wake.

Mke mvivu kitandani,
Mume hapendi kabisa mke ambaye wakiwa kitandani anaonesha kutofurahia kile mume anafanya au kufanya mapenzi pamoja.
Kuna usemi kwamba zamani za kale wanawake walifundishwa wakati wa kuwa mwili mmoja walitakiwa kulala tu na kusikilizia hizo siku zilishapita.
Mume hahitaji Mke ambaye ni submissive tu bali yule anajishughulisha na kufurahia kile Mume anafanya.
Kuwa kama gogo kitandani hakumridhishi mume na Mume hujiona ni foolish.
Mume huhitaji mke ambaye ni active na anaye enjoy sex pamoja.

Mke ambaye hata siku moja haanzishi suala la kuhitaji sex.
Kama hakuna hata siku moja ambayo mke anajisikia kumtamani mume na hatimaye kumuomba tendo la ndoa basi Mume hujiona hahitajiwi na mke wake na inampa maswali why.
Hata hivyo hapa ni Mke kuwa initiator na si demanding.

Mke asiyejichunga kuhusu mwonekano wake:
Rahisi kabisa, wanaume huvutiwa na kile wanaona hivyo physical attractiveness ya Mke ni muhimu sana kwa mume wake, generally Mke huangalia sifa za ndani za Mume kama tabia za ndani zinazomfanya Mke kujiona safe na secure.
Hivyo mke ni muhimu kujitahidi kuonekana attractive, kutumia common sense kuhusiana na masuala ya usafi, pamoja na kula vizuri, kufanya mazoezi na just taking good care of your body.

Mke ambaye hupo so concerned kuhusu appearance yake.
Ingawa wanaume huvutiwa sana na Mke ambaye ni naturally pretty, hali ni tofauti kwa Mke ambaye anajiona urembo wake ndiyo kitu cha msingi kwake.
Mke ambaye anakuwa obsessed na urembo wake au vipodozi vyake ambavyo ameweka kwa mwili wake hadi anafanya tendo zima la ndoa kuwa gumu eti anaweza kuharibu iwe nywele zake au vipodozi alivyoweka huweza kufanya turn off ya uhakika kwa mume.

Mke ambaye hawezi kuhudumia vizuri stick ya mume wake kwa raha zake.
Mke yeyote ambaye hana skills za kumhudumia mume wake kiungo muhimu ambacho kinatumika kumpa yeye mwenyewe raha ya mapenzi kwa kujitoa na kuonesha ni kiungo special huweza kuwa turn off kwa mume.

Mambo yanayompa raha mume kutoka kwa mke wake?

Mke anayefurahia sex
Kila Mume anapenda Mke ambaye anapenda sana kuwa na Mke ambaye anafurahia sex na mume wake mara kwa mara anapohitaji.

Mke ambaye anaweza kuwa initiator wa sex sometimes.
Mume anapenda kujua mke anamuhitaji yeye mume kama yeye mke anavyomuhitaji mume.
Mke anayemsifia mume wake kwamba ni the best lover in the world hasa linapokuja suala la kuwa mwili mmoja.
Mume hufurahia mke ambaye anamsifia, anamshukuru kwa raha anayompa na jinsi alivyo great.
Hata hivyo haina haja mke kudanganya kwamba anapata raha kama hakuna lolote.

Mke ambaye anamshirikisha mume vitu ambavyo vinamsisimua katika positive way siyo critical.
Kwa kuwa wanaume ni sensitive sana hivyo basi positive message huwa inafanya kazi kubwa kuliko negative na kitandani suala hili ni muhimu mno.
Unachotakiwa ni kuwa loving partner kitandani na si kutumia maneno ambayo mume anaweza kusababisha hata stick yake kurudi ground zero.
Badala ya kutoa sauti kubwa na kwa ukali kwamba “usifanye hivyo” unaweza kusema “unaonaje ungefanya hivi”

Mke anayeweka kipaumbele kuwa na sex kama mume anavyoweka kipau mbele suala la kufanya sex na mke wake.
Mume anapenda mke ambaye ana share hamu yake ya mapenzi kwa mume na kwamba mke yupo attracted kwa mume.

MKE HUPENDA MUME WA AINA HII

Mambo yanayomnyima raha mke kutoka kwa mume:

Mwanaume ambaye hana ufahamu wa kimapenzi.
Hajui ni nini na wapi kipi kinapatikana na kinafanywa vipi.
Kwa mfano hajui kisimi nini, kipo wapi na kina manufaa gani na hana mpango wa kujua au kujifunza lolote kuhusu mapenzi.

Mume ambaye hana hamu ya kujifunza jinsi ya kumridhisha mke zaidi.
Kutokuwa na hamu ya kutaka kujua skills na mambo mapya inaweza kuwa ni turn off kwa mke kwani kila mwanamke ni tofauti na katika mapenzi (kuwa mwili mmoja) huwezi kukoma kujifunza haijalishi unajua kiasi gani bado kuna vitu vingi sana vya kujifunza .

Mume ambaye ni mbinafsi kujipa raha yeye mwenyewe.
Kama unahitaji kujua maana ya tendo la ndoa linalowaridhisha wote basi jifunze kumtanguliza mwenzako na kumridhisha kwanza yeye.

Mwanaume asiyeuliza hata swali wakiwa kitandani.

Mke huhitaji mume ambaye ni initiator anayejua kuutumia uwanja (mwili wa mke wake) na kuuliza anajisikiaje kila sehemu anayogusa au kukanyaga.

*
Mambo ambayo huwa yanampa raha mke kutoka kwa mume wake:

Mume ambaye amejaa ufahamu kuhusu mwili wa mkewe.
Kwa mfano mume anaejua kisimi kipo wapi, kipoje, kina sifa gani, kina respond vipi, kinafanywa vipi kitoe raha na anajua ni namna gani mke atakuwa amepata raha anayohitaji kupitia hapo nk hapo ni kila kiungo ambacho mke anaweza kusisimka na kupata raha ya mwili kutoka kwa mume wake na kuridhika.

Mume ambaye focus kubwa ni kumpa raha mke na si kutimiza wajibu.
Hana haraka na kufanya na kumaliza na kutimiza wajibu bali ana mikono slow kiasi cha kufamfanya mke ajione ni mke anayeridhishwa na mume kuliko mwanamke yeyote duniani.
Ni mume ambaye mke akikumbuka jinsi wanavyofanya huko faragha basi kama mume amesafiri anaanza kutamani mume arudi haraka maana hakuna muda mzuri kwake duniani kama kuwa na mume faragha na kufaidiana.

Mume anayemfanya mke kujiona ni beautiful chumbani na nje ya chumbani.
Anampa sifa na kumfanya mke akione ni kweli ni mzuri na anapendeza chumbani na nje ya chumbani.

Mwanaume anayejali kuridhika au kutoridhika kwa mke katika sex.
Mwanamke yeyote hupenda kujua au kuona mume wake anakuwa completely involved kuhakikisha anampa raha ya kimahaba na mume anakuwa na mtazamo au anajitahidi kuongeza ujuzi ili kuhakikisha mke anapata raha zaidi kila wakiwa pamoja chumbani.
Siyo mwanaume ambaye hawezi hata kujua hali ya zoezi zima la tendo la ndoa lipoje zuri, kawaida au wanaelekea kwenye cliff.
Anapenda mwanaume anayetaka kujua ni kitu gani kinampa raha live, siyo kuwa selfish na baada ya kumaliza mke anaendea kuugua na kujiona ametumiwa tu.

Mume anayemfanya mke kujiona yeye ni namba moja kwake kwa kila kitu.
Mke hapendi tu kujiona yeye ni factor kwa mume bali anapenda kuona ni very important factor kwa maisha ya mume wake.
Mke lazima ajisikie salama na huru katika kile anatenda katika ndoa na mume wake.
Mume anahitaji kuwa creative jinsi ya kufanya mke vipi ajisikie.
Ni kweli sex ni kitu kizuri sana na huweza kumpa raha mume na mke hata hivyo Mungu amempa mume uwezo wa kufanya kazi apate pesa hata aweze kumnunulia mke vitu vidogo vidogo kama massage oil ili wakiwa wawili wapeane raha katika miili yao.

MWISHO.
Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe.
Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.

FAHAMU UTOFAUTI HUU WA MWANAUME NA MWANAMKE.

Hivi kwa nini wanaume huwa hawahangaikii upendo kama wanawake?

Jibu limelalia zaidi kutokana na walivyoumbwa wiring yao ipo tofauti.
Wanawake huanzia kwenye romance, mawasiliano mazuri na hatimaye sex wakati wanaume husafiri kwa opposite direction.

Ukichunguza kwa undani zaidi utagundua kwamba mwanaume anapokuwa na uhitaji mkubwa au hamu kubwa ya sex huwa anakuwa anataka kujiunghanisha emotionally na mwanamke, ndiyo maana kwa mwanaume sex ni mhimu sana wakati kwa mwanamke romance ni muhimu sana.

Kuwa na uelewa mdogo kuhusu hii tofauti hufika mahali wanawake waka –underestimate umuhimu wa sex kwa mwanaume na wakati mwingine wamewahukumu kwamba mwanaume anachotaka ni kitu kimoja tu nacho ni sex.

Hata hivyo mwanaume kusisimka kimapenzi na kuhitaji sex ni njia ya kujiunganisha na mwanamke kihisia na ili ajifahamu kihisia kwamba anakupenda.
Ni kupitia sex moyo wa mwanaume hufunguka na kumruhusu kupata hisia za upendo (love) kwa mke wake.

Ni kupitia sex mwanaume hupata feeling za kupenda ingawa kwa mwanamke sex huja baada ya kutoa na kupokea upendo (romance)

Wanawake huhitaji mawasiliano mazuri na kujisikia wanapendwa ili kufungua moyo kwa ajili ya sex wakati huohuo mwanaume huguswa na upendo wa mwanamke kupitia sex.
Kama mwanamke anavyohitaji mawasiliano mazuri na mwanaume (partner) ili ajisikia anapendwa, mwanaume huhitaji sex ili ajisikie anapendwa.

Sex drive ya mwanaume mara nyingi si rahisi kuweza kuifanya iwe turned off, yupo designed kuwaza kuhusu sex na kuhitaji sex muda mwingi na ni mara chache sana mwanaume hujikuta amechoka au yupo stressed kuhitaji sex.

Hii haina maana kwamba mwanaume huwa anaoa ili kupata sex tu na haina maana pia kwamba anaoa ili asipate sex, Bali sex ni moja ya sababu muhimu za yeye kuoa na jambo la msingi ni kwake kuwa na mwanamke special ambaye yeye kama mwanaume atakuwa anapata hitaji lake la sex maisha yake yote.

Wanaume wengi (siyo wote) likija suala la sex ni 24/7!

UMUHIMU WA KULALA VIZURI.

Wanawake ambao hujimyima usingizi hawapo sexy, hivyo kabla ya kufikiria kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi na mke wako au mume wako zingatia kwanza kuwa na muda mzuri wa kupumzika.

Mwanamke asiyelala huwa mchovu hivyo kushindwa kujishughulisha vizuri na suala la tendo la ndoa kwani mwili wake huwa mchovu na zaidi ya yote kukosa usingizi husababisha kutokuwa na furaha.
Hakikisha mke wako au mume wako anapata usingizi wa kutosha ili kupumzisha mwili vizuri kwa faida ya ndoa yenu.
Kumbuka usiporidhika kimapenzi (tendo la ndoa) utajisikia ndoa hairidhishi na usiporidhika na ndoa yako ni mwanzo wa kuanza matatizo ya ndoa yako.

KUWENI MAKINI,NI MALI YENU

Tunapooana kama wanandoa tunakubaliana kwamba tutakuwa tunafanya tendo la ndoa sisi wawili tu maisha yetu yote haijalishi tunafanya kwa kufikiria, au kwa kutofikiria, au tunafanya bora liende au kwa ufanisi, tunafanya kwa kupenda au kulazimishwa, tunafanya kwa ubunifu au kwa uchoyo au kwa kubania au kwa hiari au vyovyote vile kitabu kimefungwa na lazima kila mmoja apate kile mwenzake anampa iwe nusu au kitu kizima au kunyimwa kabisa au kupewa kila ukihitaji.
Hakuna kuangalia kushoto wala kulia ngoma ni ninyi wawili tu kuicheza hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ukweli wengi wetu huwa tunachukua kila kitu for granted, hakuna efforts zozote tunaweza kuziwekeza kuhakikisha mwenzako anapata the best kutoka kwako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa kwani ni wewe tu ndiye mwanamke au mwanaume duniani ambaye amekubali kuishi na wewe na kushirikiana kupeana hiyo zawadi ya mwili ambayo ni mali ya ndoa yenu na si vinginevyo.
Naomba ujiulize ndani ya moyo wako tena ukiwa na akili nzuri kabisa kama Mungu alivyokujalia kuoana na mwanaume au mwanamke special kama huyo uliyenaye.

Je, ni kweli unataka leo kumbariki mke wako au mume wako kwa mwili wako kwa kuwa hakuna kwingine anaweza kupata hii huduma?

Je, una hamu ya kumpa kitu cha uhakika (mapenzi, mahaba) kwa sababu ya jinsi anavyokupenda, anavyokujali na jinsi alivyoshirikiana na wewe hadi hapa mmefika?

Au umefika mahali umechoka, huna hamu tena ya kuhakikisha mume wako anapata kile mlikubaliana wakati mnaoana?
Au unasubiri hadi umpoteze ndipo ujue thamani yake?

Je unajua huko nje ya ndoa yako kuna wanawake au wanaume wengi kiasi gani wanamtamani sana huyo mume wako au mke wako?

Je, kwa nini huweki juhudi yoyote kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa mahali bora kukimbilia kama mke na mume?

Sex ni mali ya ndoa na ndivyo Mungu alivyo design, hivyo kama upo kwenye ndoa ina maana suala la tendo la ndo lisichukuliwa just for granted, panga, andaa na wekeza kwa uwezo wako wote kuhakikisha mke wako au mume wako anaridhika na wewe na utendaji wako.

Thursday, 19 November 2015

MUHESHIMU,AKUPENDE.

Katika ndoa si upendo tu bali kuheshimiana.
Mke huhitaji upendo na mume huhitaji heshima.

Niheshimu nami nitakupenda!

Sex kwa mwanaume na love kwa mwanamke ni two way street.
Mwanaume anapoihudumia roho yako ili akubaliwe na mwili wako wewe mwanamke (sexual release) maana yake wewe mwanamke unahitajika kumhudumia mwili wake ili na yeye akupe upendo wake.
Kuheshimiwa au heshima ni hitaji la msingi kwa mwanaume kama ilivyo kupendwa au upendo ulivyo hitaji la msingi la mwanamke.
Hii haina maana kwamba mwanaume hahitaji upendo au mwanamke hahitaji kuheshimiwa bali ukimheshimu mwanaume hujiona unampenda na ukimpenda mwanamke hujiona unamheshimu.
Wanaume huona afadhari usipendwe na uwe mpweke kuliko kuonekana hufai na kutoheshimiwa na mtu yeyote duniani.

Hii ina maana roho ya mwanaume inajiona afadhari kutopendwa kuliko kutokuwa respected.

Mwanamke hujisikia vizuri kihisia kutokana na maongezi mazuri na mume wake na kwa kutimiziwa hitaji lake la kuwa karibu na mume wake kwa maongezi hujisikia anapendwa.
Mume akigoma kuongea na mke wake hii ina maana kwamba mke hupata signal kwamba hapendwi na mume wake na pia mume hamjali.
Na mume naye akinyimwa sex na mke wake hupata signal kwamba mke hamjali na hamheshimu katika kumtimizia mahitaji yake.
Ni kama mume analalamika kwamba mke wake hupo unfair kumwambia
“Niangalia kwa macho tu na sex hapana”
Mke huonesha respect pale anapomtimizia mume wake hitaji la sex na mume huonesha upendo pale anapomtimizia mke wake hitaji ya emotions zake.
Kuna mambo mawili ambayo mke anahitaji kufahamu kuhusu mume wake linapokuja suala la sex.

KWANZA
Linapokuja suala la sex kuna tofauti kubwa kati ya mke na mume.
Mwanaume ni visually oriented, hamu ya mapenzi hupenda kwa kuona.
Akimuona mwanamke mrembo sura ya umbo anakuwa stimulated.
Mwanamke hasisimki kimapenzi kwa kuona kama mwanaume.

PILI
Anahitaji tendo la ndoa (sexual release) kama wewe unavyohitaji upendo (emotional release)
Bila sex anajiona mke hamheshimu na anaanza kuonesha tabia zisizo za kiupendo.
**
Kama ni mwanaume umefika Mahali mke analia kwa sababu ya kukosa upendo unahitaji kujitazama upya na kama ni mwanamke imefika Mahali unamsema mumeo hadi anajiona si lolote au hana tofauti na watoto basi jitazame namna unavyomkose heshima.

Kumbuka maandiko yananena wazi kwamba
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda NAFSI yake mwenyewe, naye mke LAZIMA amheshimu mumewe.
Efeso 5:33

MFANO WA NDOA.

Ndoa ni mfano wa computer.
Kwani computer hukupa kile kimewekwa tu, huwezi kutumia program ya MS Word kama haijawekwa, huwezi kupata internet kama haijawa connect na internet.
Ndivyo ndoa zilivyo
Ukiweka takataka utapata takataka.

Ukiwekeza katika mke kujisikia vizuri na utavuna mume anayejisikia vizuri.
Usipowekeza upendo ndani ya ndoa hauwezi kupokea upendo.

Hakuna kuwekeza mawasiliano mazuri usitegemee kuwa na mawasiliano mazuri
Ukiilea vizuri ndoa yako itakuwa oasis katikati ya jangwa, na usipowekeza katika kuilea itakuwa jangwa la sahara.

Mke akiwekeza heshima kwa mume wake, atavuna upendo kutoka kwa mume wake.
Mume akiwekeza upendo kwa mke wake; atavuna heshima kutoka kwa mke wake.

Mume akiwekeza kuwa karibu na mke, kuwa waza kwa mke, atavuna tendo la ndoa linaloridhisha.

Wednesday, 18 November 2015

KISIMI/KINEMBE.

Kuchua / kusugua baadhi ya sehemu za mwili kunaleta raha na kumaliza ashki ya tendo takatifu la ndoa.
Kwa wanawake wengi kinembe/kisimi ndiyo sehemu haswa inayoleta raha.
Hii ni kwa sababu sehemu hii ina mishipa mingi ya kusisimua mara ikiguswa.
Njia moja ya kupata raha na kumaliza ashki ni kuchua taratibu sehemu hii.
Hii ni njia moja ya kutoshelezana kimahaba.

Kinembe au kisimi au clitoris au clit au joy button, hot spot nk ni moja ya kiungo ambacho humsisimua mwanamke zaidi kuliko kiungo chochote katika mwili wake unaovutia. Hiki kiungo kipo eneo la juu zinapounganika kuta za ndani za uke (Labia minora).
Ni rahisi kukipata kiungo hiki kwa macho na kwa kugusa au kupapasa.
Kisimi hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, wengine ni kidogo sana na wengine huwa kikubwa zaidi.

Kipoje?
Kisimi kina sehemu muhimu 18 na kile tunaona na kugusa kwa nje ni kitu kidogo sana ukilinganisha na siri iliyofichwa ndani.
Kwa nje kisimi kimejigawa katika sehemu kuu tatu kichwa, msukano (shaft) na mfuko ambao hufunika kichwa na msukano.
Mwanamke akisisimka kimapenzi kisimi hudinda au huongezeka au kutuna na kimfuko hurudi kwa nyuma na kichwa ambacho ni very sensitive hujitokeza na kuwa kigumu.
Kisimi kipo eneo la juu baada ya tundu la kibofu cha mkojo na chini ya tundu la kibofu cha mkojo kuna tundu la uke.
Ngozi laini inayofunika kisimi huwa na stimulation ya uhakika na kuna baadhi ya milalo huwezesha kusugua hii ngozi na mwanamke hujisikia raha zaidi wakati wa sex.

Kazi yake ni nini?

Kisimi ni powerful organ kwa ajili ya raha ya sex kwa mwanamke, kina nerves zaidi ya 8,000 kuliko sehemu yoyote katika viungo vya binadamu; why? Ukweli ni kwa ajili ya kumpa mwanamke raha kimapenzi.
Kisimi kazi yake ni moja tu kumpa mwanamke raha ya mapenzi.
Na wanasayansi wamegundua kwamba chini ya kisimi kuna network ya tishu za msisimko, misuli, nerves na mishipa ya damu ambayo kwa pamoja huitikia na kujikunja wakati wa sex na kupelekea mwanamke kufika keleleni.

Tofauti na uume ambao hutoa mlipuko mmoja wa kufika kileleni kwa sekunde chache, kisimi hutoa mlipuko wa muda mrefu wa aina zaidi ya 100 za raha, Hii ina maana kisimi ni zaidi ya uume kwa kutoa raha ya kimapenzi.
Ole wenu mnaowafanyia ukeketaji wanawake, mna kesi ya kujibu! Kwani mnawanyima haki yao ya kuzaliwa kupata raha ya kimapenzi.

Je, wengi wanajua umuhimu wa kisimi katika raha ya tendo la ndoa?

Wanaume na wanawake wengi tunapozungumzia suala la sex huchukulia kwa mtazamo wa kiume (mfumo dume) kwa maana kwamba sex ni nzuri sana kwa wanaume na si wanawake na kwamba jukumu la nani aanze ni mwanaume na kwamba wanawake hawapo powerful kwenye sex kama wenzao wanaume.

Hata hivyo mwanamke akifahamu utendaji wa mwili wake kiungo baada ya kiungo anaweza kugundua na kuimarisha furaha ya tendo la ndoa akisaidiana na mume wake na moja ya viungo muhimu ni kisimi.
Na pia anaweza kufahamu ni namna gani anaweza kufika haraka kileleni kwa kujua kisimi kilivyo muhimu kwake.

Je, nini umuhimu wa kisimi wakati wa tendo la ndoa?

Wanawake wengi ili kufika kileleni (orgasm) ni muhimu sana kusuguliwa, kuchezewa kisimi.
Hii ni kwa sababu uke hauwezi kumpa direct stimulation wakati wa sex na pia mwanaume hawezi kusugua uke kiasi cha mwanamke kufika kileleni bali uke huweza kumpa mwanaume msuguano ambao humuwezesha yeye mwanaume kufika kileleni haraka.

Hii ina maana mwanaume anatakiwa kuelekeza nguvu nyingi kuhakikisha anasisimua kisimi kwa muda wa kutosha kuliko uume wake kuwa kwenye uke na kuusugua kwa skills zote badala ya kuelekeza skills zote kwenye kisimi.

Hii ina maana kwamba kama mwanaume anataka kufika kileleni haraka ni kwa mwanamke kumruhusu mwanaume kuingiza uume wake kwenye uke na mwanaume akitaka kumfikisha mwanamke haraka kileleni ni kumshughulikia mwanamke kisimi kwa skills zote.
Hii haina maana kwamba mwanamke hawezi kufika kileleni bila kisimi la hasha kwani anaweza kufika hata kwa busu, au kumpa mguso kwenye sehemu zingine za mwili, hapa tunazungumzia kisimi

Itaendelea...

KISIMI/KINEMBE 2

Kabla ya wiki 8 za kwanza za mimba sehemu za viungo vya uzazi; mtoto wa kike na kiume huonekana sawa kimaumbile katika uzazi, baada ya hapo mtoto wa kiume huanza kutoa testosterone ambazo husaidia huwezesha uume kujitokeza zaidi kuliko mtoto wa kike.
Hivyo basi kilivyo kisimi na uume hufanana na vyote hufanya kazi sawa kutoa raha ya mapenzi na kufika kileleni linapokuja suala la mahaba.

Kama kisimi ni zaidi ya uume kwa raha ya mapenzi kwa nini baadhi ya wanawake wakisisimuliwa kisimi bado huwa hawajisikii raha?
Utangulizi:

Jibu:
Hakuna tatizo lolote na hao wanawake ingawa ni kweli kisimi/kinembe ni kiungo maalumu na cha tofauti sana kwenye mwili wa mwanamke.
Ila kumbuka kila mwanamke na mwili wake ni tofauti na mwanamke mwingine, wengine hupenda na kujisikia raha kisimi kikiguswa kwa nguvu, wengine si kwa nguvu sana, wengine kubusiwa, wengine kunyonywa, wengine kikilambwa, wengine kikisuguliwa na wengine hawawezi kupata raha hadi kifanyiwe mazoezi kwa muda zaidi (baada ya miezi na miaka kadhaa).

Pia kumbuka wapo wanawake ambao huwa hawasikii raha hasa mwanaume akiwahi kisimini kabla ya kusisimuliwa sehemu zingine kama matiti nk kwani huko kuna nerves 8,000 so ukigusa haraka anaweza kurusha rocket mwezini.
Pia kuna wanawake ambao ni mbumbu kuhusu sexuality na miili yao mfano kama anaamini unampotezea muda kuhangaika na kisimi chake, je unadhani atapata raha yoyote?

Sex huanza kwenye mind kama ameweka password kwenye mind yake utafungua vipi?
Kumsisimua mwanamke huhusika moja kwa moja na ubongo wake au nini unaongea naye wakati mwingine hata kabla ya kuingia chumbani au kitandani.
Ili asisimke inategemea sana nini unaongea kwenye sikio lake, kile unamnong’oneza kina maana sana katika kuuandaa mwili wake, kama hujajua kuongea maneno fulani fulani ambayo huongelewa kwenye sikio la mwanamke kabla ya sex basi huna budi kujifunza.
Jinsi unavyoweza kumsisimua kabla hata nguo hajavua utakuwa na kazi rahisi sana wakati akiwa hana hata nguo moja na hii itakurahisishia yeye kutaka zaidi.

Kama umeoa mwanamke ambaye hajijui mwili wake na kisimi kina kazi gani kwake jaribu hii na unaweza kuwa mbunifu zaidi ukiongeza skills inazozijua wewe.
Kwa kuwa unajua kisimi ni nini na kipo wapi hongera maana umeshapiga hatua kubwa on this game, hakikisha ame-relax, ungana naye kuhakikisha miili inapata joto la mahaba kimwili, kiroho na kiakili.
Jisikia comfortable, hakikisha unapumua vizuri na ukitaka hakikisha mnapumua pamoja sare na deep , ukiweza mfanyie massage mwili mzima kuanzia kichwa hadi vidole vya miguu, anza kwa kutumia ncha za vidole vyako na baadae kwa kupalaza viganja na mikono yote.
Sasa hakikisha unalishikilia vizuri hekalu lako, uso, shingo, masikio, mabaga, mikono, kifua, matiti, tumbo, mgongo, mapaja na miguu hadi vidole.
Huku ukimchunguza kama vile umewahi fanya kazi FBI angalia kama yupo relax na amesisimuka ( anapumua kwa nguvu zaidi, chuchu zimesimama, na south pole kunalowa kimbiza mikono yako kwenye kuta za uke na kisimi.
Ukiaona bado hajisikii raha kwenye kisimi chake, rudi ground zero kichwani tena kwa kumbusu sawa kama ulivyompa massage.
Then rudi tena kwenye kuchezea kisimi kwa skills zote
Then fanya unachojua wewe!

Jinsi ya kusisimua kisimi.

1.VIDOLE.

Kwanza mikono lazima iwe safi na kucha fupi zilizokatwa vizuri zisizo na mikwaruzo yoyote wala ncha mpya kali.
Na kabla hujatujuliza vidole au kidole chako hapo hakikisha unapita kwanza kusalimia sehemu zingine kama mapaja na eneo zima la uke.
Kujua ni pressure kiasi gani utumie wewe si bubu muulize mkeo anaweza kukujibu kwa kukunong’oneza au kwa kukupa signal, kumbuka kuna aina ya kuchezesha vidole au kidole iwe duara au square na kama hukusoma geometry au vector basi rudi shule maana hapo ndo application yake.
Kumbuka hilo ni eneo sensitive kuliko eneo lolote katika mwili wa binadamu hivyo usicheze rafu.

2.KINYWA.
Wapo ambao kwao sex si uchafu na huweza kutumia viungo vyao nyote katika mwili na kwao kufanya hivyo ni kuwa karibu zaidi kati ya mke na mume na ni mwili mmoja na zaidi tendo la ndoa ni kuwaunganisha wawili kimwili, kiakili na kiroho hivyo si kuingiliana tu bali kuwa kitu kimoja.
Kwa kuwa ulimi ni kiungo au msuli imara kuliko yote katika mwili wa binadamu basi kisimi kikikutana na ulimi mbingu hufunguka na watu kurushwa International Space Station bila kujijua basi kama umejazwa Roho Mtakatifu unaweza kunena kwa lugha kwa raha inayotokea.
Lubricant ya asili iliyopo kweny ulimi na joto la kinywa hutoa sensation ambayo ni kama dream team pamoja na kuzungusha ulimi kwa skills zote mke wako atakutana na lift itakayomnyenyua hewani kuelekea kileleni.


3.UUME.
Uume ni toy la mwanamke yeyote ambaye ameolewa, uume unaweza kuingia kwenye game la kuchezea kisimi.
Ila jiangalie usije maliza haraka kwani kusugua kisimi kwa uume huweza kuupa uume sensation za kupelekea kumaliza haraka.

MWISHO.
Kufahamu kuhusu kisimi kwa mwanaume au mwanamke ni kuonesha kwamba ume-invest vya kutosha kuhusiana na raha ya mapenzi ya mke au mume wako, kitu cha msingi ukijua utakuwa na tendo la ndoa ambalo linaridhisha na zaidi kila mmoja atamuhitaji mwenzake kila mara.

Kumbuka ukiwa na mwanamke anayeridhika kimapenzi na yeye atahakikisha anakuwa na mwanaume anayeridhishwa kimapenzi pia na hutauliza hili kwake maana anajua.

bila kujua geography ya mwanamke huwezi kumfikisha pale anahitaji kufika kimapenzi.

MAHUSIANO.

Eti mahusiano mazuri hayana sexual problems?

Wanandoa wote kuna wakati hupitia matatizo kuhusiana na sex na hii haina maana kwamba uhusiano wako na mume au mke basi umeota mabawa.
Hata hivyo kama tatizo linabaki kwa kula jiwe kati yako na mwenzako ni kweli linaweza ku ruin ndoa yenu na mahusiano.
Signal yoyote ya kuwepo tatizo katika mahusiano linapokuja suala la sex si alama ya kuwa ninyi ni failure ni sehemu katika mahusiano.
Inawezekana sexual needs za mume wako au mke wako zimebadilika, hasa katika dunia ya leo ambayo watu wanakimbizana na maisha bila mafanikio.
Umenunua gari ukimbize maisha lakini wapi, umejenga nyumba ukimbize maisha lakini wapi, umeoa mke mzuri kukimbiza maisha lakini wapi na wewe unayesoma hapa umeolewa na mwanaume mzuri lakini maisha wapi bado ni kukimbizana tu, mimi simo!
Hata hivyo kubadilika kwa hamu, kuridhika nk vinahitaji muda ili muweze kufanya adjustment na kurudi kwenye mstari na kuendelea na maisha kwa raha zenu.

Eti mwanamke lazima afike kileleni kwa intercourse peke yake (uume kuingia kwenye uke)

Wanawake wengi hawawezi kufika kileleni kwa hicho kitendo peke yake hata kama unatumia ukuni mkubwa kiasi gani au jogoo anawika kwa muda mrefu kiasi gani kwa sababu uume hauwezi kutoa stimulation ya kutosha hadi kufika kileleni isipokuwa kisimi.
Pia kutumia milalo ya aina tofauti hasa ile inayoweza kusisimua kisimi au G- spot huweza kusaidia kwa wengine.
Pia kumbuka foreplay ni muhimu kuliko sex yenyewe na hilo ni muhimu kuhakikisha kila mmoja anafika kileleni kwa raha zake hata hivyo muhimu zaidi ni mood hasa kwa mwanamke.
Ni busara ya hali ya juu kwa mwanaume kuacha kufanya sex kama mwanamke unahisi hana mood.

Eti mke wangu au mume wangu atajua mwenyewe tu jinsi ya kunipa raha hata nisipomwambia wakati wa mahaba.

Mkeo au mumeo si mind reader hana scanner yoyote ya kujua unajisikia raha wapi na aongeze efforts kwenye hilo eneo huku wewe umelala kama gogo.
Kukosa mawasiliano wakati wa sex ni moja ya factor kubwa inayochangia kuwa na tendo la ndoa lisiloridhisha kwa kila mmoja.
Kila mmoja anajua sex ni kitu gani kila mtu hili eneo ni genius hata hivyo kila mtu ana sexual needs tofauti na mwingine.
Ni lazima umwambia partner wako nini unahitaji, acha aibu tena mwambia kwa details na kuwa huru hata kama yeye huwa bubu au huchanganyikiwa kabisa ukishamwambia twende south pole.

NITAJUAJE NI YEYE?

Uchumba ni mtamu acha kabisa, ila kumbuka ndoa ni kitu halisi!

Yupi anaweza kuwa mchumba halisi ambaye atakuwa mke au mume wako?

Ukizingatia kwamba kuoa au kuolewa ni uamuzi ambao unaweza kupelekea kuwa mtu wa furaha katika maisha yako au mtu wa huzuni na kujuta siku zote katika maisha yako.
Mambo ya msingi kuangalia ni haya:

MAHUSIANO HUWA RAHISI TANGU SIKU YA KWANZA:

Tangu siku ya kwanza nilipojikuta naonana uso kwa uso upendo uliokuwa kati yangu na yeye ulikuwa natural, nilijihisi nimemuona mwanamke ambaye namfurahia kila kitu, namkubali kama alivyo, nilihisi kama tulizaliwa tuishi pamoja na sasa nimempata mtu ambaye nimekuwa namtafuta, nilijiona atanitosheleza kimwili na kiroho, ninapoongea naye naridhika kwa mvuto alionao.
Kila kitu katika mahusiano na urafiki wetu kilikuwa natural na kutupa hisia mpya kabisa hapa duniani.

Wapo ambao katika safari ya uchumba hadi ndoa hufikia kuzipiga na kugombana mara nyingi sana, leo wanazipiga au kununiana au hugombana na kesho wanapatana tena na kurudiana.
Wanaendelea na kasheshe hizo hizo mara kwa mara hadi wanaoana.

Inawezekana unarudiana naye labda kwa kuogopa ukiachana naye hutapata mtu mwingine wa kuoana naye, au umri unaona umeenda sana, au unataka kuondoa nuksi ili na wewe ujulikane uliolewa, au rafiki zako watakucheka au una hamu sana na sex, Kumbuka ni busara kuachana wakati wa uchumba kuliko kuachana ikiwa ndoa.
Ukiingia kwenye ndoa utakumbana na storm ambayo itakuja kupima kama sababu zako za kuoana zilikuwa strong kuliko storm yenyewe na kama zilikuwa weak storm itakuchukua bila huruma.

UHUSIANO MZURI NA FAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI:

Inaweza kuwa tofauti kidogo hasa linapokuja suala la dini, kabila, nk kwani mara nyingi wazazi na familia nyingi huwa na lao kuhusu kabila au dini.
Ikitokea kwamba mchumba wako ni kabila moja, dini moja na bado ndugu zako, familia yako au marafiki zako hawaelewani naye ni vizuri kufikiria upya.
Wewe umelelewa na familia na kutokana na hayo malezi ndivyo ulivyo na umempata huyo mchumba kutokana na tabia yake aliyokulia au kulelewa na hiyo familia na kama bado hakubadilika maana yake hapo kuna bendera nyekundu inawaka na inaashiria kuna kitu hakipo sawasawa.

Kawaida ukishaingia kwenye mapenzi (fall in love) huweza kupunguza uwezo wako wa kuamua na kuona kasoro ndiyo maana wanasema love is blind.
Hii haina maana kwamba unatakiwa kuvunja mahusiano eti kwa sababu ya ndugu, familia au marafiki hawakubaliani na huyo mchumba wako ila ni kawaida kwamba inawezekana kuna kitu ndugu zako na familia yako wanakiona na wewe hukioni ambacho mbele ya safari mkiwa kwenye ndoa unaweza kukumbana nacho na bahati mbaya umewakana wazazi ndugu na marafiki.
Utaenda kwa nani kuomba ushauri maana umekuwa kichwa ngumu.

Jaribu kuchunguza kile ambacho ndugu zako au familia au marafiki wanasema vibaya kuhusu huyo mtu wako inawezekana ni kweli.
Ni kawaida kama umepata mtu wa kufanana na wewe basi huweza kujichanganya kirahisi sana na ndugu zako, familia yako na marafiki zako.

HUTAONA KITU KIKUBWA CHA KUMBADILISHA:

Kawaida, hata kama mnapendana kuliko binadamu yeyote chini ya jua, bado tofauti ndogondogo zitakuwepo; hata migogoro itajitokeza pia.
Ila kama kuna jambo kubwa sana unaona ni muhimu sana yeye abadilike basi hiyo ni ishara kwamba fikiria kwa makini.

Tatizo ukishashambuliwa na chemicals za love unaweza kujikuta unadhania kwamba haina shida kwa tatizo au kasoro alizonazo na utavumilia.
Ukiingia kwenye ndoa chemistry ya mapenzi hushuka na kupanda kutokana na jinsi mnavyojitahidi kuimarisha ndoa yenu; hapo ndipo sasa utagundua kwamba ulichemka and too late.
Usiingie kwenye ndoa ukidhania utambadilisha mtu sana sana wewe ndo utabadilishwa.
Kama umegundua kuna kitu ambacho ni tatizo kubwa sana mbele ya safari na hutaweza kuishi nacho ni vizuri ku move out kuliko kupoteza muda wako na kujifariji na baada ya miaka 3 ya ndoa ujikute upo kwenye jehanamu yako mwenyewe na upweke uliokithiri.
Watu hupata upweke lakini upweke wa kwenye ndoa ni mbaya kuliko upweke mwinghine wowote duniani.

NI RAFIKI
Mvuto wake ni kitu muhimu sana katika mahusiano.
Ndani ya mahusiano lazima kuwa na mzizi mkuu wa urafiki ambao hata mkiwa wawili sehemu yoyote duniani bado mnajiona hamjapungukiwa na pia bado mnajiona ndiyo marafiki bora duaniani.
Je, unajiona unahitaji kutumia muda na yeye tu?
Je, unajisikia raha kuwa na yeye wawili tu?
Je, unahisi yeye ndiye anastahili wewe kumwambia siri zako na kwamba ni yeye tu anakufahamu kuliko mtu yeyote duniani, kama ni NDIYO, basi mshike vizuri.
Kuwa best friends hata baada ya kuoana ni raha sana, na ndoa hudumu, maana hakuna anaye bore mwenzako.

UNAPOFIKIRIA KUOANA NAYE HAIKUPI SHIDA:

Kama unajikuta unapofikira kuoana naye huna wazo lingine la kuhisi ndoa inaweza kuwa na matatizo na unajisikia amani ya kweli moyoni na kwamba future yako na yeye itakuwa sawa basi umepatia.

Mwisho Kumbuka Kumuomba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mtu wako maana yeye ndiye anajua liubavu lako lipo wapi.

“Marriage is not about finding a person you can live with, it’s about finding the person you can’t live without.”

MWANAUME HUMTENGENEZA MWANAMKE.

Wakati wa sex Mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi.Inatokea mwanaume anafika nyumbani kutoka kazini anamkuta mke naye yupo nyumbani anamsalimia then anaenda zake chumbani kubadilisha nguo za kazini.
Anapata chakula cha usiku then anaanza kutazama TV au kupitia magazeti yake na kuyasoma.
Muda wa kulala umefika anaenda kuoga na kuvaa pajama zake; mke naye anaenda kuoga na kufanya sawa na mume.
Wanapanda kitandani, mume anampapasa mke, mke naya anajua mzee anataka maana ndiyo sex code yake akinigusa kwa mtindo huu maana yake anataka tuwe mwili mmoja na anajisikia kama kusumbuliwa maana alikuwa hajui kama mzee atataka kutokana na kutowasiliana hata hivyo anamkubalia.
Baada ya dakika chache wamemaliza, wapo kimya na mzee anapiga usingizi.
Mke anajiona kama ametumiwa tu kwani hakukuwa na raha yoyote ni kuumizwa tu kwani mwili haukuwa connected hisia.

Kuna tofauti gani na chura hapa?
Kuwa na mahusiano na kimapenzi kwa mtindo huu ni sawa na kuiba akili ya asili ya chura.

Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati mwanamke huhitaji kusisimuliwa. Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona wakati nwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo wa mwanaume.

Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.

Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnong’oneza mkewe kwamba “vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda anaweza jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neno lingine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.

Kwa mawasiliano mazuri na kupeana quality time mwanamke huweza kufunguka kiakili, kimwili na kiroho na kuwa tayari kwa usiku wa kufurahisha na kuridhishana.
Ndiyo maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa “baba nanii leo kichwa kinaniuma sana” au “nimechoka sana” au “unapata zero participation na kuambiwa maliza haraka” au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.

Jifunze kuwa mwanaume mwororo (tenderness) wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mpe mgusu (touch), mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.

Mwanaume humtengeneza mwanamke!

MWILI MMOJA.

Kuambatana!
Wanahitaji kuongea uso kwa uso!

Tumeona kwamba mwanamke anatakiwa (lazima) amheshimu mume ili mume naye ampende na matokeo yake kila mmoja aridhike na mwenzake na hatimaye kuwa na uhusiano mzuri idara zote.

(Efeso 5:33)

Mke anahitaji mume anayempenda na kumuonesha upendo kuanzia asubuhi, mchana na jioni wakikutana mume anahitaji kuwa karibu na mke wake ili mke ajisikia anapendwa na hatimaye ajisikie relaxed na kuwa tayari hata kwa activities zingine usiku.

Je, mume kuwa karibu na mke wake ina maana gani?

Maana ya kuwa karibu kwa mke na mume ni kuambatana, shikamana, kushikana, ng’ang’aniana, fungamana, kaa jirani jirani, songamana, karibiana, kuwa pamoja (cleaving, cling or intimate)
Kuwa karibu ni kuungana uso kwa uso na kuwa mwili mmoja.

“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”.
(Mwanzo 2:24)

Katika uimbaji wa Mungu ni Binadamu peke yao ambao huweza kuwa karibu kimapenzi uso kwa uso.
Kuambatana kati ya mke na mume ni zaidi ya kuwa mwili mmoja.
Kuambata kwa mke na mume ni kuwa karibu au mwili mmoja kiroho na kimwili.
Kama wewe ni mwanaume inakupasa ufahamu kwamba mke wako hufurahia na kujiona anapendwa na wewe pale unapomkaribia na kufanya ajione unataka kuwa karibu kwa namna unavyomtazama, unavyomgusa, unavyomkumbatia, unavyotabasamu na kumbusu na kumwambia NAKUPENDA.

Katika ulimwengu wa sasa ni rahisi sana kwa mke na mume kuchukuliwa na kuwa busy na kujisahau kujenga ukaribu ambao ndiyo msingi wa mwanamke kujisikia anapendwa na mume wake.
Wanandoa wenye busara huchukua dakika si chini ya 15 kila siku wakikutana jioni baada ya kazi; huhakikisha kila mmoja anajihusisha na mwenzake kwa ukaribu wa kimaongezi na sharing ya information za namna siku ilikuwa kwao wote na matokeo yao jioni na usiku vinakuwa exciting.
Mke akirudi anataka connections, anataka involvement na mume, anataka face to face talks na Mume akirudi kazini anataka kwenda pangoni hata hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuhakikisha anapata muda wa kutosha ili kufanya connection na mke na hasa kama unataka mambo yawe safi kuanzia jikoni, sebuleni hadi chumbani huo usiku pia usigande kwa TV au Gazeti au pangoni bila kuongea na mke na kusaidia kazi ndogondogo hapo nyumbani.
Kuna ubaya gani kama utakuwa unapiga story na yeye anaandaa dinner au na wewe unasaidia kupika (kama hamna wafanyakazi wa ndani)

KUMBUKA KUWA KARIBU NA MKE SI GHARAMA BALI MUDA:

Mke atafurahi kama mara kwa mara:
Utamshika tu mikono,
Utamkumbatia na kumbusu wakati wowote,
Unapokuwa affectionate bila wazo la sex,
Kufanya kitu kinachosaidia kuwa na “togetherness”
Pale unapomwambia unampenda, yeye ni mwanamke mzuri (mrembo).
Kumbusu mke kwa sababu unataka sex tu ni turn off.
Pale mnapoangaliana na kupeana story zinazowafanya kuwa na kicheko.
Unapotumia muda wa kutosha kuwa na yeye katika kazi ndogondogo kama kupika, kufua nguo, kuogesha watoto, kusafisha nyumba nk.
Pale unapomfanya ajisikie unafurahia kujadili vitu mbalimbali na yeye.
Pale unapoendelea kuongea naye, au mkumbatia na mbusu baada ya tendo la ndoa.

SEX NI KITU CHA AJABU SANA.

SWALI
Kaka Jeffy,
Kwanza nashukuru sana kwa hii blog kwani nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na masuala ya mahusiano.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 29 na ni mwaka wangu wa 3 kwenye ndoa hata hivyo nilitaka kuuliza swali lifuatalo kama unaweza kunisaidia.

Mume Wangu anatabia ya kunikaba au kunikwida shingo wakati tukifanya mapenzi (sex) sijajua tabia kama hii ina maana gani.

Nimevumilia kwa muda mrefu hata hivyo imefika Mahali sijisikii kuwa comfortable na hii tabia yake.

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa bila kuleta madhala yoyote?


JIBU:

Asante sana kwa swali zuri na pia kupita hapa ili kujifunza tips mbalimbali za maisha ya mahusiano.

Swali lako la msingi linasema

Je, ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kukukwida shingo wakati wa tendo la ndoa?

Ukweli ni kwamba linapokuja suala la mapenzi (sex) Binadamu (mke na mume) huonesha tabia nyingi ambazo hushangaza sana (binadamu ni kiumbe wa ajabu sana).

Wapo ambao wakati wa sex hufanya vitendo au kuonesha tabia zifuatazo;
kama vile kufinyana, kuumana kwa meno, kupiga kelele na wengine yowe as if kuna msiba (hadi majirani wanawajua), kupeana matusi ya nguoni, kupigana makofi (kuzabana vibao), kufungana kamba au pingu na kuchapana viboko, wapo wanaume akilifuma kufuli la mke wake hulifakamia na kulinusa kwa dakika kadha na kujisikia raha, wapo ambao hukomalia kunusa kwapa, wengine ni kupeana ahadi kama kununuliana magari au kujengeana ghorofa Mbezi beach (wakiamka asubuhi wanajikuta wapo nyumba ya kupanga manzese jijini Dar es Salaam), sijawasikia hao wa kukwidana shingo na viungo mbalimbali vya mwilini (hii naona inahatarisha maisha zaidi)
Tabia zote hizi wao wanasema ni “to have fun” na kusherehekea mapenzi, hata hivyo inawezekana kwako zisikubalike na kwao zikakubalika.
Usiige!
Napenda ufahamu kwamba kuvumilia tabia au kitu ambacho hukipendi siyo jambo zuri katika uhusiano wa mapenzi kati ya mke na mume, uwe wazi na mweleze ukweli wa vile unajisikia.


Ni muhimu Sana kuweka mipaka kwa vitu ambavyo huvifurahii katika tendo la ndoa na pia muulize mume wako naye ni vitu gani anavipenda na vitu gani havipendi.
Otherwise, nilitakiwa kumuuliza huyo mume wako huwa anasukumwa na kitu gani hadi anakukwida wakati sensitive kama huo au ndo kuzidiwa na mahaba!

NI VIZURI KUFAHAMU HAYA.

Ili Mke awe available kwa mume kimwili na kiroho inampasa mume awe sifa zifuatazo:
Ukaribu, uwazi katika mambo yake, anayeeleweka, mtu wa amani, anayempa uhakika mke kwamba ni yeye peke yake ndiye anapendwa na mume wake na pia kumpa uhakika kwamba yeye ni mwanamke mwenye sifa anazozipenda kimwili (beauty) na kiroho.

Je, unawezaje kuwa mume ambaye mke anakuelewa (understanding)?

Ili mke akuelewe mume unahitaji kutumia secret weapon ya sikio lako.
Kumsikiliza tu mke huweza kuonesha kwake kwamba umemuelewa kuliko hata kabla hajamaliza kuongea wewe unamkatiza na kusema ulikuwa unajua anataka kusema kitu gani.

Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume ni kwamba mwanaume kawaida yupo wired kusikilizwa na si kusikiliza, na mara nyingi mwanaume hupenda kutatua tatizo au matatizo au kutoa jibu kwa ajili ya tatizo lolote, hivyo anapoongea na mke wake kwa kutomfahamu anakuwa na haraka ya kutaka kutoa majibu badala ya kusikiliza tu.
Narudia tena;
Si mara zote mwanamke anapouliza swali au kukwambia kitu anahitaji majibu, mara nyingi anakuwa katika harakati ya kujihusanisha (connection) na wewe na anachahitaji ni sikio lako tu na si namna ya kupata majibu.
Unachotakiwa kufanya ni kumsikiliza na kushiriki katika kuzungumzia hiyo shida yake na kuliona kama tatizo lenu wote.
“The first duty of love is to listen”.
Mwanamke huhitaji mtu wa kumsikiliza tu na sikio lako wewe mume ndilo analihitaji na si uwezo wako wa kutatua tatizo.
Ukimsikiliza, atajisikia vizuri tofauti na ukirukia kukatiza kile anaongea au kuanza kupendekeza solutions kwa kile anakwambia.

Wanaume kujitahidi kutoa solutions za kile mke anaongea au hata kukatiza kile anaongea kwa mume kujifanya anajua mke alitoka kuongea kitu gani ni moja ya matatizo sugu ya kwenye ndoa.
Hata kama wewe ni mwanaume maarufu kutatua matatizo ya wanaume wenzako bado ukiwa na mke wako unatakiwa kumsikiliza tu na sikio lako hadi aridhike.