Thursday, 24 December 2015

SI HAKI YAKO,NI ZAWADI.

Mungu alitoa sex kama zawadi kwa waliooana.
Ametoa zawadi ya sex ili kutufundisha kuhusu yeye na uhusiano wake na sisi.
Utendaji wa sex ni picha ya muunganiko (sharing) kwa kutoa vyote kwa mwenzako (mke au mume) na pia ni picha ya kumkubali kumpokea mwenzako kama alivyo kwako.

Kuna faida wazi kabisa kwa uhusiano wa tendo la ndoa kwa mke na mume kama vile afya ya mishipa, kupunguza maumivu, kufanya MP kuwa stable, kupunguza depression (unyonge wa kihisia), kupunguza (stress) msongo wa mawazo na kuongeza kuridhika kwa mahusiano ya ndoa.

Mungu anawapa uhuru wanandoa kunywa na kufurahi raha ya mapenzi kila mmoja kwa mwenzake kama wanandoa, hata hivyo sababu za kiroho na kisayansi haziwezi kutumika kama silaha ya mwanandoa mwingine kumthibiti mwenzake.
Uwezo wa kimapenzi kati ya mke na mume bado ni zawadi ambayo tunatakiwa kupeana bure na kwa kupenda na kwa moyo wa furaha (kutoa na kupokea kila mmoja kwa mwenzake katika ndoa).
Pale mwanandoa mmoja anapokuwa na mtazamo kwamba tendo la ndoa ni haki basi kunakusinyaa kwa aina fulani katika mahusiano huanza kujitokeza.
Mke hawezi kuwa na raha ya mapenzi katika ndoa kama mume atakuwa ni mtu wa kulazimisha na kutaka kwa nguvu kama haki yake na pia si raha sana pale mke anapotoa tendo la ndoa kwa sababu anawajibika kutoa hata kama hakuwa tayari.

Tendo la ndoa linaloridhisha ni pale kila mwandoa anakuwa amejiadabisha kutoa kwa uhuru mwili wake kwa mwenzake.
Unapotoa kwa uhuru mwili wako kwa mume au mke wako na kupokea mwili wake kwa uhuru unaipa ndoa kitu sahihi cha asili yake na Mungu hufurahia na kutoa kibali.

Wednesday, 23 December 2015

JE"WEWE UNALALA VIPI?

Baadhi ya wanandoa hulala na watoto wao kitanda kimoja, wana sababu zao, ingawa mara nyingi watoto nao huwa na kitanda chao na wanandoa nao huwa na kitanda chao na chumba chao.
Je, unaamini kwamba jinsi wanandoa wanavyolala huonesha afya ya ndoa yao?
Chukulia wanandoa wanalala bila watoto.
Swali la kujiuliza je, wewe huwa unalala vipi na mume wako au mpenzi wako na je, jinsi mnavyolala huelezea mood ya jinsi unavyojisikia huo usiku?




1. THE SPOON STYLE
Huu mara nyingi ni mlalo wa miaka 5 ya kwanza ya ndoa, ukiona mwanamke anapenda sana kuangaliana uso kwa uso maana yake ni mtoaji (giver)
Wanandoa wengi hulala kwa kukumbatiana wote pamoja au mmoja kumkumbatia mwenzake.
Ndoa ipo kwenye miaka ya kwanza ya mapenzi motomoto.

Tuesday, 22 December 2015

MFURAHISHE MUMEO CHUMBANI..

Mwanamke yeyote anayeweza kumfanya mwanaume kuwa mtu wa furaha anastahili pongezi kubwa sana kwa kazi nzuri unayofanya hasa kujitoa ili kuhakikisha ndoa yake inakuwa na afya kila siku.
Wapo wanaume (siyo wote) hata kama mwanamke anajitahidi kwa nguvu zote na ujuzi wake wote kumfurahisha, bado mwanaume haelewi somo anaendelea na maisha yake kama anavyojua yeye, hana muda wa kusikiliza kitu chochote kutoka kwa kiumbe anaitwa mwanamke.


Ili chumbanii kuwe na furaha ni muhimu furaha kuanzia nje ya nyumba kabisa kisha sebuleni na kumalizia chumbani.
Jambo la msingi katika mahusiano ya ndoa; kila mwana ndoa anatakiwa kufanya lile ambalo na yeye anapenda kufanyiwa.
Jitahidi sana kutenga muda kwa ajili ya mume wako kwani maisha ni mafupi sana kuishi kwa kubishana, hasira, gubu, donge, kusemana na kulaumiana hakuna maana zaidi ya kupoteza muda kwani katika vita ya mume na mke anayepata hasara wa kwanza ni ninyi wenyewe kisha watoto.
Muhimu ni kuishi kwa kupeana mambo mazuri sasa hivi kwani huwezi kujua kesho kitatokea nini,
Anza kwanza wewe mwenyewe mwanamke kuwa mtu wa furaha then mwambukize na yeye, hapo mtakuwa mmefungua mlango wa furaha ya nje na ndani ya sita kwa sita.
Furaha ya kwanza kwa mwanaume ni wewe mwanamke unavyoonekana.
Idara ya mwonekano, urembo, uzuri ambao unakufanya uwe mwanamke.
Mwanaume siku zote anapenda sana mwanamke ambaye anapendeza jitahidi kujiweka safi muda wote,
kwa nini uwe rough,
mchafu, hujipendi,
mzembe, hujipambi,
unakuwa kama huishi dunia ya leo.
Kujipamba na kupendeza ni asili ya mwanamke na wanaume huvutiwa na jinsi mwanamke unavyoonekana.
Ni vizuri kumuonesha mume wako jinsi unavyompenda, jinsi unavyomjali na jinsi unavyomuhitaji na kujitengeneza vizuri ni moja ya njia ya kuonesha hayo.
Usitegemeee mwanaume atapata furaha chumbani kama mwanamke mwenyewe ndo huna mpango na uzuri wa mwili wako.

JE,MWANAUME KWA CHAKULA UNAWEZA KUMPA FURAHA?

Ni kweli tupu, Unaweza kumfanya mwanaume ajisikie raha sana na furaha kubwa hadi chumbani hasa kama unajua jinsi ya kumpa mlo wa uhakika (chakula anachokipenda) na kama Mungu amekubariki kupika vizuri basi hiyo ni silaha muhimu sana.
Jaribu angalau kwa weekend mtengenezee chakula maalumu ili na yeye awe moja ya wanaume wenye furaha hiyo hapa duniani.
Hivi umewahi kupanga mkakati wa kuhakikisha kuna siku mume wako anakuwa ni mtu pekee mwenye furaha duniani?
Kama bado sasa ni wakati wake!
Hata kama unajua wewe kupika chakula kitamu ni kilaza, bado unaweza kusoma vitabu au kujifunza kisha ukampikia mumeo.
Wapo wanawake wanajua kabisa mume wake anapenda chakula aina fulani na anajua kabisa akimpikia hicho chakula mume huwa anafurahia lakini who cares, miezi inapita mume hajapata hicho chakula anachokipenda na wakati huohuo mwanamke ana lalamika eti mume siku hizi hanipendi na chumbani mambo si moto, anza kwaza kuwasha moto jikoni then usubiri na yeye awashe moto wa chumbani; thubutu utavuna ulichopanda!
Kama unataka chumbani kuwe na furaha lazima na wewe afanye sehemu yako kwa ajili yake.
Wapo wanawake miezi na miezi, mwaka hadi mwaka kila siku chakula anapika house girl, najua wanaume tunafahamu kabisa kwamba wake zetu mna majukumu makubwa, ila kitendo cha kupikiwa na msichana wa kazi mwezi mzima, mwaka mzima na wewe upo huwa wanaume hawafurahii.
mwanaume hujisikia furaha sana siku akila chakula alichopika na mke wake.

UTAMPAJE FURAHA HUKO CHUMBANI?

Ukisha kuwa umemtengenezea mazingira ya furaha nje ya chumbani, basi lazima hata chumbani atakuwa na furaha tu kwani kazi muhimu umeifanya, kilichobaki ni kuangusha mbuyu kwa shoka moja tu.
Wakati unaingia chumbani tu achana kabisa na mawazo yoyote hasi kuhusu yeye, achana kabisa na mambo usiyoyapenda kuhusu yeye na badala yake jiweke huru na wazi kabisa zaidi jimwage au jiachie kabisa.
Usimfiche kitu chochote unataka kutoka kwake, yaani uwe wazi na jisikie huru fanya kile yeye huwa anapenda hapo hakuna mipaka hakuna kuogopa kufanya kitu, hapo ni uhuru wa ajabu. Mpende kwa maneno,
kwa matendo,
kwa kunusa,
kwa kuonja kwa kugusu na
kwa hisia zote.
Usijilaze kama gogo mbele ya mume wako na kumsubiri yeye afanye kila kitu, participate fanya kile kimekuleta kutoka kwa wazazi wako, kwani kwa wazazi wako ulikuwa huvai, ulikuwa huli, si umemfuata kwa sababu yeye ndiye peke yake anaweza kukupa huduma ambayo wazazi wako hawawezi kukupa, yeye peke yake anaweza kuuhudumia mwili wako na feelings zake, ndiyo maana inabidi uchangamke, ujishughulishe na kuhakikisha unapata kile unahitaji kutoka kwake na kwa kuwa wote mna furaha na mnafanya kile mnapenda basi hapo kutakuwa na furaha kuu.
Mwanamke lazima uwe mtundu!

Monday, 21 December 2015

WIVU ULIOPITILIZA...!!

Wivu mbaya wa kupindukia
Wivu (envy) huu ni wivu ambao mtu anakuwa hana na anakihitaji au anataka mfano pesa, kuwa mshindi, kufanikiwa nk.

Wivu (jealous) huu ni wivu ambao mtu anakuwa na kitu na anaogopa kukipoteza mfano mume, mke, mchumba au mpenzi nk.

Pia kuna wivu mzuri ambao husaidia kuleta maendeleo na mafanikio kwa kila eneo la maisha ya binadamu kama vile kusoma kuhakikisha na wewe una degree, kufanya kazi kwa juhudi ili na wewe uwe na pesa nk

Hapa leo hatuzungumzii ule wivu unaompata mtu baada ya kusikia mume au mke wake au mpenzi wake anafanya mapenzi na mtu mwingine au anauhusiano na mtu mwingine, hapo naamini wivu lazima utakuwepo na kitu cha msingi ni kujihadhari usije ukaua mtu na wewe kufungwa maisha kwani haya tunayasikia kila siku kwenye jamii zetu mara mwanaume kamua mwanamke tena kwenye nyumba ya wageni na wakati mwingine baada ya kufumaniwa.
Masuala ya mahusiano si utani wala masihala, mahusiano hugusa hisia za mtu, huathiri mfumo wa maisha ya mtu hivyo inabidi kuwa makini na mambo unayofanya kwa mume au mke wako.

Hapa tunazungumzia ule wivu wa kupindukia ambao mtu anakuwa na mume au mke au mchumba au mpenzi na kwa kutojiamini kwake anahisi na kuona kwamba huyo mume au mke au mchumba anaweza kuchukuliwa na mtu mwingine au anaweza kumpoteza na wakati huohuo muhusika yupo Innocent.
Kama mtu unayempenda mke, mume au tuseme mpenzi ambaye anaumwa ugonjwa wa wivu, basi inabidi uwe makini kwani wivu katika mahusiano huweza kuharibu kabisa iwe ndoa au uchumba au vyovyote vile, hata kama hayo mahusiano ni mazuri na imara namna gani.
Ndiyo maana wivu ni moja ya dhambi saba zinazoua (deadly sin)


Kumbuka mtu mwenye wivu wa kupindukia kwake kila kitu kinachofanywa na mpenzi wake ni hatari na kitu halisi.
Wivu huweza kuharibu kabisa mahusiano bila kujali partner anafanya juhudi gani kuhakikisha anaweka vizuri mahusiano yenu.
Watu wenye wivu wa kupindukia siku zote wana mihasira isiyo na maana.
Mtu mwenye wivu wa kupindukia anaweza pia kupoteza hata mtu anayejua kupenda au mtu mzuri kwani hakuna mtu duniani anapenda kuishi kwenye kifungo cha mtu mwenye wivu wa kupindukia.

Kumekuwa na kundi kubwa la wanawake au hata wanaume ambao hulalamika kwamba hawapati wapenzi wazuri au kila ninayepata ananikimbia, inawezekana una wivu wa kupindukia hivyo mtu anapima hicho kimo cha maji na anajikuta atazama, hivyo anachoma daraja na kuondoka zake.
Ingawa kila mmoja wetu kwa asili ana wivu Fulani ndani yake, kitendo cha kuwa na wivu wa kupindukia kwa yule unayempenda tena wivu wa kila siku inaweza kuleta matatizo.
Wakati wivu unampata mtu, wapo ambao hujiona tayari mke au mpenzi wake ana taka kumsaliti na hujiona kama vile usalama wao upo mashakani na kwamba mwenzi wake anataka kuchukuliwa na mtu mwingine.
Si kwamba tu wivu ni mbaya bali mtu mwenye wivu hutafsiri vibaya yale mpenzi au mke/mume wake anayafanya au kile kinaendelea katika uhusiano.
Hata kitu ambacho hakipo huwezi kujitokeza na kusababisha kuwa tuhuma kubwa na kuanza kuvurugana ndani ya nyumba hata bila kuchunguza kwanza au kupata ukweli.
Ndiyo maana wapo wanawake na wanaume innocent ambao bado bado hawaaminiwi na waume au wake zao.
Mtu mwenye wivu humfikiria vibaya mwenzake hata bila sababu na kila kitu ambacho wenzake anafanya yeye ni kama anatega tu,
anaangalia utachelewa kazini,
utachelewa sokoni, utaongea na nani nk.
Kwa mfano, mke amepigiwa simu na mume wake mpenzi na simu inaita bila majibu au anaipokea baada ya muda, mwanaume mwenye wivu hapo kapata sababu atasema mengi sana mara hunipendi, au mara ulikuwa na nani au ulikuwa na mwanaume mwingine.
Na hata bila kujua ukweli anaweza kufikia uamuzi kwamba kuna kitu kibaya kinaendelea kumbe hakuna kitu.
Siku nzote ukiwa na mawazo hasi (negative), au mashaka na mtu, au kujisikia hakuna usalama matokeo yake utakuwa unazidi kutengeneza mawazo hasi zaidi, au mashaka zaidi na mwishowe kupoteza usalama kabisa wa ndoa na maisha yako na pia utakuwa mtu asiyeyaamini mahusiano yake.
Kuwa mtu mwenye wivu wa kupindukia katika mahusiano siyo kwamba inakuumiza wewe mwenyewe, bali inaumiza hata yule ambaye unamwonea wivu pia kwani hakuna binadamu anapenda kukaa karibu na mtu ambaye anageuza mazuri kuwa mabaya, anayekupa tuhuma na kutokukuamini wakati huna tatizo.
Ni ngumu sana kuishi na mume au mke mwenye wivu wa kupindukia, kwani hawa watu ni watu wanao penda control mtu kila eneo, ni watu wa kutaka kila kitu kama
anavyotaka yeye, ni watu wa kushambulia na wenye msongo wa mawazo pia, mtu unakuwa mtumwa kwenye ndoa, huna raha na watu wengine, huna raha na maisha nje ya yeye.
Matokeo yake mtu anaona kuolewa au kuoa ni kupoteza uhusu kwa watu zaidi ya yeye na wewe.

Wapo wanamke au wanaume wamepigwa marufuku kupigiwa simu na mtu wa jinsia nyingine au wamepigwa marufuku kuongea na watu wa jinsi tofauti hadi yeye awepo na kwenda mahali hata kama ni dharura bila kumwambia ili na yeye afuatilie.
Wapo wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi maofisini kisa wivu eti watachukuliwa na wanaume wengine nani aliyekwambia wanawake ni rahisi kiasi hicho, kila mtu ana tabia yake na malezi yake.
Wapo wanawake hawaruhusiwi kwenda hata dukani au sokoni kisa wivu, hawaruhusiwi kusafiri kisa wivu, sasa maisha ni nini?
Wivu haufuati kabila unaweza kuwa mhehe, mchaga, au hata mkurya, unaweza kuwa mzungu au mwafrika, unaweza kuwa tajiri au maskini.
Kitu cha msingi jiamini kama huyo mume wako au mke wako amekupenda wewe hadi mkapelekana kanisani kufunga ndoa au mbele ya wanaohusika kisheria kwamba mnataka kuishi pamoja sasa una wasiwasi gani? eti atachukuliwa na mwanaume mwingine au mwanamke mwingine, hakuna kitu kama hicho, jiamini na mpe uhuru na mpende zaidi na kumpa kile anataka na kuhitaji, imarisha mapenzi zaidi badala ya kumlinda na kumchunga kama mbuzi.

Sunday, 20 December 2015

MAKOSA WAYAFANYAYO WANAUME WAKATI WA MAANDALIZI.

1. KUWA NA HARAKA.
Wanaume wengi huwa na haraka ya tendo la ndoa bila kuzingatia umuhimu wa kumuandaa muhusika kwanza.
Wanawake hutumia muda mrefu ili kusisimka ndiyo maana unahitaji kutumia muda bila kuwa na haraka ili uweze kumsisimua na zaidi kuwa na sex nzuri na yenye kuridhishana.
Ni vizuri kutumia muda wa kutosha kumuaandaa na kama unaweza hata kumfikisha kileleni hata kabla ya kumwingilia.


2. KUKOSA KUJUA SEHEMU MUHIMI ZA KUCHEZEA.

Zaidi ya matiti, shingo na midomo na kisimi wanaume wengi hawajui ni sehemu zingine zipi ambazo wanawake huwasisimua zaidi.
Kuna sehemu zingine ambazo mwanamke akiguswa anaweza kusisimka haraka zaidi.
Tumbo, matako, mapaja, nyuma ya shingo, mabega, mgongo, sehemu iliyopo kati ya uke na nyuma.

Hizi sehemu ni muhimu sana kwake kuguswa wakati wa kumuandaa.
Pia lazima uwe mtundu kuweza kusoma lugha yake na jinsi nini anakifurahia na nini hafurahii wakati wa maandalizi.


3. KUWA BUBU BILA KUONGEA MANENO MATAMU NA KUMSIFIA.

Wakati wa tendo zima la kufanya mapenzi wanawake wanategema mwanaume awe anaongea si kuwa bubu na kuongea huanzia kwenye maandalizi na kama wewe ni fundi wa kuongea basi hutachukua muda mrefu kuhakikisha moto umewaka.
Kuna maneno matamu, kwenye mapenzi maneno matamu yapo ya aina mbili, kwanza ni dirty words (mfano uke kwa jina jingine unaitaje vile au uume kwa jina jingine unaitaje vile) na pili maneno ya kumsifia juhudi yake au alivyo na umbo zuri. Dirty words husaidia kumsisimua na kumpa nyege zaidi na maneno ya sifa husababisha atoe juice zaidi.

4.KUBUSU KWA KINYAA AU BILA USTAARABU.

Wakati unambusu usiache mimate kila mahali uwe mstaarabu pia usioneshe kwamba una kinyaa katika kubusu baadhi ya sehemu ambazo yeye anapenda umbusu, huyo ni mke wako na yeye wewe ni mwili mmoja, yeye ni wewe na wewe ni yeye, hivyo unaruhusiwa kubusu sehemu yoyote ndiyo maana usafi ni jambo la kwanza kabisa katika mapenzi.

Niwatakie maandalizi mema ya christmas.

Monday, 14 December 2015

KWANINI HUGOMBANA BAADA YA NDOA?

Mahusiano ni kitu special na maalumu na wakati mwingine hushangaza sana.
Hivi inakuwakeje wapenzi wengi hugombana baada ya kuoana tu?
Ni mara chache sana kuwaona wachumba wakigombana.

Issue hapa ni kwa nini watu hugombana baada ya kuoana na wakati kabla ya kuoana kila mtu alikuwa anamuelewa mwenzake hadi wakafikia hatua kukubaliana kuoana na wakioana tu mambo huanza, yaliyojificha huanza kuwekwa juu ya meza?

Ukiangalia kwa undani sana utakuta kwamba kabla ya kuoana mambo mengi unafanya ni hiari na baada ya kuoana ni wajibu.

Kabla ya kuoana una options kwa maana kwamba unaweza kujitoa au kuendelea naye na baada ya kuoana hakuna options, mwisho wa reli,hakuna njia, unafungwa kwenye box hakuna kutoka.

Pia kabla ya kuoa wengi huwa hawawi 100% honest, kila anachofanya kwa mchumba ni kizuri kwani uchumba huhusicha social activities na romantic interest, so wengi hufungana kamba kwamba everything is ok, hata kama hapendi au anaona kina bore bado atajifanya anakipenda na hakuna shida. Mkioana hakuna kufungana kamba wala kufurahishana ni task oriented institution na deep sharing ya kila kitu na ni real life na kazi.

Mfano:
Jeffy amependana na Anitha (siyo majina halisi) na ni wachumba ambao si muda mrefu watafunga ndoa kuwa mke na mume.
Jeffy anapenda sana kwenda kutazama Soka, imefika siku Yanga na Simba wana mechi na Jeffy hawezi kukosa anamwambia mchumba wake leo naenda kutazama mechi Yanga na Simba wanacheza je tunaweza kwenda?
Anitha hapendi ila kumfurahisha mchumba wake anakuali waende na tiketi zinakatwa wanaenda, wanafurahi na Anitha anashangilia mchezo bega kwa bega na mpenzi wake Jeffy.

Wiki inayofuata Anitha anajiunga na kwaya kanisani na anamuomba awe anamsindikiza kwaya na ikiwezekana wakimaliza anamrudisha nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa Jeffy anataka kuonesha anajali hana shida yupo tayari kukodi hata Tax mpenzi awahi kwaya church au akimaliza kwaya aende nyumbani salama (moyoni Jeffy hapendi kwaya anampenda Anitha tu na anafanya ili Anitha afurahi).

Baada ya kuoana, kuna mechi ya Yanga na Simba na Heffy anamuomba Anitha waende kutazama mechi,Anitha anakataa kata na kutoa sababu kwamba hapendi kwenda kupoteza muda kwa kuangalia Yanga na Simba wakati ana mambo ya msingi ya kufanya.
Jeffy anashangaa kwani kabla ya kuoana alisema anapenda. Anaoana amedanganywa.

Wiki inayofuata Jeffy anaombwa na mke wake Anitha amsindikize kanisani kuimba kwaya, Jeffy anakataa kwa madai kwamba ana kazi za msingi sana kuliko kwenda kumsindikiza mkewe kwaya na hata hivyo si anaweza kwenda mwenyewe na kurudi kwani kwaya si huduma yake (Jeffy anajitetea). Mke wake naye anashangaa inakuwaje kabla ya kuoana alikuwa ananisindikiza hata kunitafutia tax ili niende na kurudi salama leo inakuwaje?

Je, wewe hujawahi kuwa Jeffy au Anitha katika mahusiano yako?

Orodha ya mambo huendelea na inafika mahali kila mmoja anajiona kama amedanganywa kwani Yule alitegemea amebadilika hapo frustration na disappointments huanza na migogoro huanza na kama wajinga wote kunaanza disconnection ya emotions kimwili na kiroho.
Hapa mmoja anajisikia hasikilizwi not understood, valued, loved au appreciated, kila mmoja anapenda mwenzi wake amsikilize, amwelewe na ampe thamani ya kila anafanya.
Kila mmoja anajiona mwenzake haweki msukumo wa kutosha kuhusu Mahusiano yao na kwamba yeye si kipaumbele tena ndipo closeness huanza kupotea.

Ukweli ni kwamba disagreement ni part of marriage, huwezi kukwepa muhimu ni kuzingatia kwamba unahitaji kuwa
Positive,
Fanya kila kitu katika wakati wake,
Uwe unachunga mdomo wako,
Usibishane au kugombana na spouse wako mbele ya public,
Ukikosa kubali na omba msamaha na wote kusameheana na kusahau
Zaidi mawasiliano ni muhimu sana.
Usimlaumu mwenzako badala yake fahamu kwamba sasa unaishi kwenye realm life hivyo changamka na mpende Zaidi ikiwezekana Fanya yale ulikuwa unafanya hata kabla hamjaoana.

NI MUHIMU KUFIKIRI KWANZA.

Inakuwaje watu wawili waliopendana deep idara zote inafika siku wanakuwa baridi na wanajiona ni watu wawili tofauti kabisa kwenye ndoa yao?


Kuna mambo mengi sana husababisha kuanzia na yale yaliyo ndani ya ndoa yao na yale yaliyo nje ya ndoa yao hata hivyo ukweli love is so terrible and is so important, kuna wakati mwingine mpenzi (mke au mume) anaweza kukupa au kukunulia gari au kukujengea nyumba ya uhakika lakini bado ikawa haina maana kama hatatimiza mambo ya msingi kuhusiana na upendo wake kwako.

Kuna aina tofauti za migogoro na jinsi ya kukabiliana nayo, wengine mgogoro ukizuka hata majirani wanajua leo kuna vita kati ya Mr Jeffy na Mrs wake (Anitha) [siyo majina halisi] na baada ya muda wanarudi kwenye mstari. Wengine vita vyao huwa slow, kimya kimya, hakuna kelele ni vita baridi na kila mmoja huanza mbali na mwenzake kihisia, kiroho na kimwili polepole ila matokeo yake ni hatari tupu.


Kama ni mwanandoa mpya ni vizuri kuwa makini katika maamuzi mbalimbali mnayofanya na kufikiria kwa makini huku ukiangalia zaidi ya miaka 5 ijayo, kwa mfano;


Jeffy na Anitha wameamua baada ya kuoana tu wanazaa mtoto haraka iwezekanavyo kwa kuwa kila mmoja ana kazi hivyo shida ipo wapi kama pesa zipo. (Ingawa ukweli pesa huwa hazitatui matatizo yote)

Hata hivyo uamuzi wa kuwa na mtoto haraka kabla hawajajuana vizuri na kufikia mahali wakawa wanafahamiana tofauti na uchumba ni jambo la msingi. (siyo lazima ukubali huu ushauri kwani inatokana mmejuana kiasi gani na mchumba wako)

Kuna watoto wakizaliwa huja na package ambayo mzazi hulali kama vile kulia muda wote na mke kumtumikia huyo mtoto all the time (acha ile ya kumaliza madaktari wote kujua kwa nini mtoto analia usiku mzima na wanakwambia hakuna tatizo) na kufikia mahali mume akawekwa pembeni kwani mtoto kwanza na wakati huohuo ndoa bado changa.

Mke hujikuta mtoto anamuhitaji na mume anamuhitaji na hawawezi kubalance kwani bado ni mgeni na hii institution.


Watoto wengine huwa na matatizo ya kula, kiasi kwamba mama hujikuta hawezi hata kumwachia mtu yeyote amtunzie mtoto na matokeo yake mama hujikuta muda wote anatumikia mtoto na wakati mwingine kuacha kazi (ajira) na pia mume kuwekwa pembeni.


Matokeo yake wanandoa hujikuta wanakuwa mbali na feelings kufa na kila mmoja anaanza kuona ndoa hairidhishi wakati hata miaka 2 haijamaliza.


Jambo la msingi ni mwanamke kufahamu vizuri aina ya mume uliyenaye kwani kuna wanaume ambao wanaweza kuwa baba na kuna wengine ni kazi.

Suala la kulea mtoto linahitaji mke na mume wote kushirikiana kuhakikisha si mmoja ndiye anakuwa na mzigo zaidi.

TATIZO HALIMALIZWI KWA KULIKIMBIA..

Dunia tunayoishi huwezi kukwepa kukutana na tatizo au shida au mkwara au majaribu au mateso au ugumu wa maisha eneo lolote.
Hata hivyo linapokuja suala la ndoa au mahusiano kuna njia mbili tu za kukabiliana na hayo yote hata kama ndoa yako unahisi ni mbaya, hairidhishi au ambayo ndani hakuna kuelewana au unaona kabisa ni kweli inaelekea kwenye shimo.

Njia ya kwanza ni kuachana kabisa kutafuta jibu na njia ya pili ni kukabiliana na tatizo lililopo hadi kuhakikisha unapata jibu.

Hata katika maisha ya hapa duniani njia ni mbili tu, wapo watu wakikutana na matatizo au shida huamua kukimbia au kuruka au kurudi nyuma au kukwepa na kwenda zao na wengine hukabiliana nayo uso kwa uso hadi kieleweke.

Ukweli kukimbia tatizo kuna raha yake (raha ya muda) kwani kuna ahueni ambayo mtu hupata hata hivyo habari mbaya ni kwamba mwisho wa yote ni maumivu makali na kujuta.

Na wale wanaoamua kukabiliana hujikuta katika maumivu makali mwanzoni na mwisho wake ni ahaueni na kupata nafuu ya kudumu au kula kuku kwa mrija hata hivyo hapo kunahitajika imani na kuwa na imani ndipo kwenye tatizo kwani wengi imani huwaota mabawa mapema sana.

Fikiria unaumwa tumbo na unapokumbuka gharama za vipimo pamoja na shughuli nzima ya kumuona daktari unaamua kuachana nalo.
Ukweli ni kwamba maumivu ya tumbo yataendelea kwani ni dalili kwamba afya yako katika tumbo haipo sawa na dawa ni daktari kuchukua vipimo hata kama utatumia gharama na ajue tatizo la tumbo lako ni nini na zaidi akupe tiba kamili mapema.

Tumbo haliwezi kupona kwa sababu umeachana nalo kwani maumivu yataongezeka na gharama ya vipimo na kutibu itakuwa zaidi kwani unapokimbia tatizo linalizidi kuwa kubwa badala ya kumalizika.

Kumbuka ndoa yako ni mfano wa tumbo pale likianza kuuma, fahamu unahitaji kufanyia uchunguzi na vipimo na hatimaye kupata dawa inayotakiwa.
Inawezekana unapita katika ndoa yeny uchungu na maumivu makali na unawaza kwamba kuachana na mume au mke ndo dawa.
Ukweli si dawa dawa ni kupiga magoti na kumuomba Mungu akupe hekima na kukabiliana na tatizo lililopo.

SIKIA HII..!

Wanaume wengi huwa hawaoni umuhimu wa kuwabembeleza wake zao kwa kuwakumbatia, pakata , busu, shikashika nk) baada ya sex.

Kibaolojia mwanaume akimaliza sex anarudi kwenye hatua yake ya kawaida (pre- aroused state) na mwanamke akimaliza sex (baada ya kufika kileleni) huwa anarudi katika yali ya kuwa nusu yaani semi- aroused state) yaani kwake bado moto upo na anaweza kupika tena chakula.

Hii ina maana kwamba mwanaume akimaliza tendo la ndoa anakuwa ameishiwa nguvu au anaenda ICU kwa matibabu ya karibu, hajiwezi wengine ndo huishia kukoroma kiasi kwamba hata vibaka hawawezi kuingia hiyo nyumba, wakati huohuo wanawake wao wakimaliza bado huhitaji kuendelea na tendo la ndoa zaidi na zaidi na kwao cuddling ni kuwapa connection na wakati mwingine y na sex tena na tena.

Hivyo ili mwanamke asiamini kwamba mwanaume huna feelings kama jiwe, inakupasa wewe mwanaume baada ya kumaliza sex fanya hitimisho kwa kuendelea kumkumbatia, busu na kumpa maneno matamu ya sifa na kimapenzi, kumbuka ni mkeo hivyo mpe kila anastahili na utaona mabadiliko.

Pia wanawake wengi wanashangaa kwa nini mwanaume anaweza kutenganisha sex na love.
Wakati wa sex wanawake huzalisha kiwango kikubwa sana cha homoni ya oxytocin ambayo husaidia kuwasisimua katika emotions zao na wanakuwa connected na mume wake wakati wa sex na hii husababisha mwanamke kujihusanisha sex na emotions (love).
Wanaume hawazalishi na kama yupo anayezalisha hiyo homoni basi ni kiwango kidogo sana kiasi kwamba kwake sex na love ni vitu viwili tofauti.
Ndiyo maana ni rahisi kwa mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke ambaye hampendi na kwa mwanamke ni ngumu kwani mwanamke upendo kwanza ndipo huwa tayari kwa sex.

Mume ambaye hamjali mke, hampendi, hampi sifa kwa yale mke anafanya na kumkosesha upendo atajikuta kila siku anaomba sex na mke akijitetea kichwa kinauma.

MICHEZO YA KIMAPENZI..

Katika moja ya misingi ya kujenga mahusiano kati ya mke na mume ni pamoja na mke na mume kuwa na muda wa kucheza pamoja.
Kabla hatujafika mbali hivi ni lini wewe na mume wako au mke wako mmekuwa na muda wa kucheza pamoja?
Kama ni ndiyo basi ubarikiwe na kama hukumbuki ni lini bado hujachelewa ndiyo maana umekuja kusoma hapa ili nikukumbushe.
Kucheza pamoja kwa mume na mke husaidia kujenga urafiki na ndoa kwani ndani ya kucheza kuna interest na vicheko na pia kucheza pamoja maana yake unajali (caring).
Kujenga mahusiano ni pamoja na mke na mume kuwa marafiki na kuwa marafiki ni pamoja na kuwa na muda wa ku-enjoy pamoja kwa kucheza na matokeo yake ni kila mmoja kumuhitaji mwenzake mara kwa mara kwa kuwa kuna kitu mnacho in common.

Tuache kucheza michezo mingine tuangalie kucheza kimapenzi.
Je, ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kucheza mchezo wowote wa kimapenzi (sexual play)
Kwanza, lazima muwe ninyi wawili tu.
Pili, mnahakikisha kuna kuheshimiana katika kuchagua mchezo mnaotaka kucheza.
Tatu, mchezo wenu hauwezi kusababisha maumivu kimwili, hisia na kukwazana kiroho.
Nne, mnahakikisha mchezo wenu una msingi katika mahusiano yenu.
Na tano hakuna kuingiliana kimapenzi

UTAZIDI KUUMIA..!

Tafadhari chukua glass ya maji mkononi, usisome tu naomba kama unaweza chukua glass jaza maji na ishike mkononi.

Swali ambalo naweza kukuuliza ukisha ichukua mkononi ni je, glass ya maji ni nzito kiasi gani?
Naamini jibu ni kwamba haina uzito wowote.
Upo sahihi na umebarikiwa kwa jibu zuri.
Hata hivyo ukweli ni kwamba hata kama uzito wa glass yenye maji si lolote, kama ukiishika kwa zaidi ya saa moja utaanza kusikia uzito wake, unavyozidi kuishika kwa muda mrefu ndivyo utajisikia uzito unaongezeka zaidi ingawa uzito wa glass ya maji ni ule ule.
Utajisikia mkono kuanza kuuma na kulemewa na uzito kama vile umeshika bonge zito la tofali la sementi.

Ndivyo mahusiano ya ndoa yanavyofanya kazi wakati mwingine.

Kuishi wawili ni sharing ya mambo mbalimbali na kuna wakati mwenzako anaweza kukwaza, kukuumiza, kukusema vibaya, kufanya vibaya, kukutukana, kukudanganya nk na kila kitu unafanya kwake au wewe unafanyiwa kina uzito mkubwa au mdogo sana moyoni kwa partner wako.
Hata hivyo unavyozidi kutunza vitu vidogovidogo vinavyokuumiza moyo bila kuviweka wazi kwa mwenzako ili muongee na kuyamaliza. Siku zinavyoongezeka na kwenda itafika siku mkusanyiko ya hayo mambo moyoni mwako utaanza kuwa mzito na kujisikia vibaya kwa mwenzako.


Inawezekana chanzo cha hasira zako au uchungu ulionao au maumivu uliyonayo nk ni matokeo ya vitu ambavyo uliweka moyoni mwako miaka 5 au 10 au 25 iliyopita katika ndoa yako.
Kubwa zaidi hukufanya juhudi yoyote kuhakikisha unaongea bayana na wazi kwa mke wako au mume wako na kutokana na hiyo tabia leo umefika hapa baada ya hayo mambo kujijenga kwenye moyo wako kwa miaka zaidi ya 5 nk.

Huku mwenzi wako akiwa amesahau hayo mambo, wewe umeendelea kuyashika ndani ya moyo wako na ni wewe unayeumia kwani mwenzio hajui kama bado yapo moyoni mwako.

Hata ukimwambia leo anaweza kuwa shocked kusikia kwamba bado ulikuwa umeweka jambo au mambo kama hayo moyoni.
Kwa kuwa umeshindwa kuachilia imefika mahali umeona ndoa haina maana kwako, haikupi furaha na unaanza kufikiria mlango wa kutokea
Unajisikia humpendi tena mume wako au mke wako.
Badala ya kidonda kupona sasa inazidi kuwa fresh.
Na kidonda kinazidi kuliwa na wadudu na damu kutoka bila wewe kujua.

Jifunze kuwa wazi na kuongea kwa mpenzi wako kama amekukosea mwambie na msahemeane na kusahau yaliyopita.

Sunday, 13 December 2015

JENGA MAHUSIANO MAZURI NA MTOTO WAKO.

Mahusiano yako na mtoto wako atakapokuwa mtu mzima huelezea ubora wa mahusiano uliyokuwa nayo wakati yeye angali mtoto mdogo.

Aina mbalimbali za wazazi ambao watoto huwa nao.

Kundi A
Wakali, wasumbufu, wasio na utaratibu, wasio samehe, wakorofu, wanaoweka donge moyoni, wanaopenda sifa, wasioaminika, wasio na subira, wanaowaka wakikasirika, wanakasirika haraka na wanaoshindwa kuwa na kiasi nk.

Kundi B
Wakarimu, wanaojali, wapole, wanaosamehe, wanaoheshimika, ukifanya makosa wanasamehe na kusahau, wanyenyekevu, wakweli, wenye subira, wanahasira lakini wanazihimili, wana kiasi, wacheshi, wanaofurahisha nk.
Je, ungekuwa mtoto ungechagua mzazi wa kundi gani?

Ni yupi kama una matatizo shule ungemwambia?

Ni yupi anaporudi nyumbani ungemkimbilia na kujisikia upo mahali salama?

Ni yupi ukifanya makosa unaweza kukiri wazi kabisa kwamba umefanya makosa?

Kumbuka mtoto hawezi kubaki mtoto miaka yote hivyo wakati akiwa mtoto hakikisha unampa kile anastahili kwa wakati wake.
Kwa mfano usipocheza na mtoto leo usidhani miaka 10 ijayo unaweza cheza mchezo uleule ulitaka kucheza naye miaka 10 iliyopita.

Je, ili kujenga uhusiano na mtoto wako ni mambo gani ya msingi kufanya?

CHEZA PAMOJA NYUMBANI:
Cheza mchezo wowote kama vile kadi, colouring, puzzle nk.
Unatakiwa kubuni mchezo ambao unaweza kucheza na mtoto/watoto wako.

CHEZA NJE YA NYUMBANI:
Unaweza kutembea au kukimbia kwa ajili ya maendelea ya afya ya mtoto. Unaweza kwenda naye kwenye Pak, kutafuta maua au wadudu au kurusha mawe kwenye mto nk.
Kumbuka issue si kwenda naye tu bali na wewe uhusike kucheza nay eye.

PENDA VITU AMBAVYO MTOTO WAKO ANAVIPENDA.
Ni muhimu sana uwe una admire vile vitu mtoto wako anapenda au kuonesha interest na wewe husika na endelea kumsaidia yeye kuwa mbunifu zaidi kwa vitu anavipenda kufanya.
Kama anapenda kutengeneza magari msaidie na kumtia moyo kwani anaweza kuwa designer wa magari baaadae, au kama anapenda kufuga wadudu anaweza kuwa ni conservation officer (wildlife) baadae.

MSAIDIE HOMEWORK NA PROJECT ZA SHULE:
Utakuwa unamtia moyo sana mwanao kwa kuwa kile muhimu kwake na kwako ni muhimu.
Unapofanya hivyo unamsaidia mtoto kuwa organized, pia unaweza kumwingizia ethics zako kuhusu maisha ya shule kama vile juhudi na kutokata tama.

TAFUTA MUDA WA KUJIBU MASWALI YAKE:
Ni muhimu sana kujibu maswali ya mtoto aina zote hata kama atakuuliza swali ambalo ni la mambo ya kikubwa kwani ni mtoto anataka jibu na si kumkemea, kwani hata akiwa na swali mahali popote atajua mzazi wangu ni mtu muhimu nitamuuliza hivyo utamlinda pia.

MTOTO AKIKASIRIKA RESPOND VIZURI:
Hakuna kitu muhimu kama kuwa makini na mtoto akikasirika na jinsi wewe unavyo respond kwani ukiwa na hekima na busara utakuwa unamtengeneza vizuri mtoto wako jinsi yak u-behave akiwa amekasirika hata katika maisha yake baadae akiwa mkubwa kwenye ndoa yake.

MWAMBIE NAKUPENDA:
Hivi ni lini umemwambia mtoto wako nakupenda? Hakuna kitu kizuri kama mtoto kuambiwa anapendwa na wazazi wake na pia ni vizuri mtoto afahamu baba na mama wanapendana.

SHUGHULIKIA TABIA MBAYA MAPEMA
Mtoto wako akionesha tabia mbaya mshughulikie kwa upendo.
Pia kusema HAPANA maana yake bado unampenda, si busara kumwambia ndiyo mtoto hata kitu ambacho unaona hakina faida kwake eti atalia.

UKIKOSEA OMBA MSAMAHA
Wakati mwingine wazazi hukasirika na kuwaadhibu watoto wakati mwingine wakiwa hawana makosa.
Hivyo kama ni kweli umekosea, omba msamaha.

UWE NAO KWENYE SHUGHULI ZAKO:
Ni muhimu sana kuhakikisha unakuwa na mtoto kwenye shughuli zako kama ni ofisini siku zingine nenda naye ili na yeye akakae kwenye kitu chako na kujiona ni boss fulani.
Pia inampa picha nini mzazi anafanya na itampa picha ya maisha na future yake.
Kama ni dereva nenda naye kwenye gari siku moja.
Kama ni forester nenda naye kwenye forest nay eye ajifunze kupanda miti.
Kupika je? Kufua nguo je? Kulima Je?

WAFUNDISHE KUHUSU MUNGU:
Ni muhimu sana watoto wanavyoongezeka na imani yao ya kumjua Mungu iongezeke, imani ya wazazi ina impact kubwa sana kwa mtoto kuliko mahali popote.
Linapokuja suala ma Mungu mtotot huambulia 80% kwa wazazi, asilimia 15 Sunday school (kanisa) na 5% mtaani.
Hivyo mzazi una impact kubwa sana kuhusu Mungu kwa mtoto wako.

TUMIA MUDA PAMOJA KAMA FAMILIA
Kila mtoto ana picha ya wazazi (baba na mama) na kwamba anajisikia raha pale anapokuwa pamoja na wazazi wote.
Pia kama mzazi jifunze kumfurahia mtoto, jitahidi mtoto ajisikia raha kuwa na wewe na si kukukimbia.

MBARIKIWE

Thursday, 10 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA NAHUSIANO. (MWISHO)

HATUA YA NNE NI KUUNGANISHWA.

Jambo linalohuzunisha ni kwamba nusu ya mwanaume na mwanamke wanaoamua kuishi pamoja hushindwa kufikia hii hatua ambayo mateso, maumivu, uchungu na kuvumilia kote huanza kulipa.
Asilimia kubwa ya ndoa zinazovunjika sababu kubwa ni kukosa maarifa hasa kabla ya wawili kuamua kuishi pamoja hivyo huingia kwenye ndoa wakitegemea ndoa itakuwa tambarare kama nyikani au watakutana na vichuguu kumbe kuna milima na mashimo.

Hapa mnakuwa mmeshirikiana kutengeneza historia na kwa pamoja mnakubaliana kwamba kweli ndoa haikuwa rahisi hata hivyo mnajisikia proud kwa kuwa mmeshinda hurricanes na storms zote pamoja.

Kila mmoja anamshukuru mwenzake kwa commitment kubwa na dedication aliyoiweka kuhakikisha ndoa inafika mwisho kwa uvumilivu wa hali ya juu, pia mkiangalia mlikotoa mnajisikia ni kweli ninyi ni wanandoa wa tofauti.
Kila mmoja anajiskia yupo karibu na mwenzi wake na more connected kimwili, kihisia na kiroho, pia kila mmoja hujisikia amepata hamu mpya na kubwa kwa mwenzi wake hasa Kutokana na kupoteza muda mwingi wa kuwa intimate kwa kushughulikia migogoro kila mmoja anajiskia yupo nyumbani tena.

Hujikuta zile qualities ambazo uliziona mwanzo kabisa kumbe bado anazo na unaanza kujiunganisha kihisia upya kwa kuwa sasa mnafahamiana vizuri pande zote za maisha yaani strength na weakness.Hii ni hatua ya furaha, hatua ya mapenzi ya kweli, true love, divine love, unconditional love.

Wanandoa wa hatua hii hata watu wengine huwa-admire kutokana na jinsi walivyoshinda aina zote za majaribu.
Wanakuwa role model kwa jamii.

Kama wanandoa wote wangejua kwamba ndoa huwa katika hatua mbali mbali na kwamba mbele ya safari inalipa, basi wangekuwa tough kuhakikisha wanavumilia na kushinda.

Hata hivyo wengi huamini stage (kama kuna matatizo) waliyopo itakuwa ya kudumu na kwamba watakuwa hapo forever, ni kweli ukiwa na wakati mgumu huumiza na hukatisha tama lakini kumbuka “No situation is permanent” hata kama ndoa imefikia hali mbaya kabisa bado huwa na dalili za kuiokoa ni muhimu kuelekeza nguvu hapo.

Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote za dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.

KUMBUKA;
Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote huku kukiwa na vimsuguano vidogo vidogo kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.

Muwe na Ndoa na Mahusiano Mema Wapendwa.

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO.3

HATUA YA TATU NI MATESO, MAJONZI NA TABU.

Katika hatua hii Wanandoa hushangaana kwa nini kila mmoja amejiweka gundi kwenye njia zake bila kumjali mwenzake.
Na kila mmoja humwambia mwenzake ungebadilika kila kitu kingekuwa kizuri.
Kama ni mlevi basi hujichimbia mizizi na kuwa mlevi wa kupindukia, kama ni mlevi wa kazi basi ataondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi midnight eti ana andaa future.
Hata akirudi nyumbani hukuta mke amelala na watoto wamelala na yeye mwenyewe yupo exhausted kiasi kwamba hawezi hata kumuhudumia mkewe.
Hapa ndipo affair nyingi huzaliwa, na ndoa huwa ni vilio, majonzi, Stress, BP, pressure, kukosa usingizi, Wanasheria wa mambo ya ndoa wengi hutajirika kwenye hatua hii ya ndoa hasa nchi zilizoendelea ambako kuachana ni jambo la kawaida tu.

Watoto wengi huachwa njia panda na kutojua nini cha kufanya maana mara kwa mara baba na mama hawaelewani.
Hapa ndipo tunafahamu kwamba kupigiana kelele, kulaumiana, kusuguana, kutishiana hakuwezi kubadilisha wapenzi wetu bali kukubaliana kwamba kuna tofauti na kushirikiana kutatua tatizo kwa hekima na busara hupeleka ndoa kwenda hatua nzuri zaidi.

Hii ni discovery stage ambayo wanandoa hujuana na ni opportunity ya kujifunza na kuzalisha true love.Wale wanaokimbia au kuomba talaka au kutoa talaka huenda kutafuta wapenzi wapya ambao hujikuta wameangukia the same boat na matatizo mapya na makubwa zaidi.

Na ndoa nyingi huvunjika hapa na kukosa kufikia stage inayofuata ambayo ni true love kati ya wanandoa.
Ndiyo maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba baadhi ya walioachana kwa talaka kuna wakati hutamani kurudiana na wataliki wao au wangejitahidi kuvumilia na hatimaye kutatua matatizo kuliko njia ya kupeana talaka waliochukua.

Wapo ambao huona haina haja kuendelea na hii cold war na huamua kuchukua uamuzi wa kufanya investigation na kuchukua njia sahihi za kujenga mahusiano imara na yenye afya.
Hata hivyo wanaoamua kuchukua huu uamuzi bora wa imani huwa na milima na mabonde ya kupita kufikia hatua ya mwisho ambayo huwapa raha na experience ya ndoa mpya.

Fuatilia hatua inayofuata ambayo ndio hujenga ndoa zaidi..

Wednesday, 9 December 2015

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO. 2

Kila mmoja anajua raha ya falling in love au siku za honeymoon je, nini hufuata baada ya hayo?
Wengi hawajui emotional terrain iliyo mbele au bonde utakayopita katika kuendelea na ndoa yako.
Hapa kuna hatua predictable ambazo ndoa nyingi hupita, naamini ukiijua hii ramani basi utaweza kufika mahali unapoenda.
Tunaendelea na hatua ya pili..
HATUA YA PILI NI MAUZAUZA.
Ile hali ya kudondokea kwenye mapenzi (fall in love) huchakaa na ukweli halisi huanza kuonekana.
Hii ni hatua ngumu kwa sababu unakumbana na anguko kubwa sana la ndoto zako kuhusiana na mpenzi wako.
Zile tofauti na tumakosa tudogo ambato tulikuwa si kitu sasa huanza kusumbua na kuudhi, mfano kama mwenzi wako alikuwa mzembe kupanga vitu hasa nguo chumbani sasa utaanza kuudhika kwani utajisikia umevulia mno, kama anakoroma sasa utaona usumbufu, kama ana kikwapa sasa unaona kinasumbua, kama ana harufu mbaya mdomoni asubuhi itaanza kukusumbua, tayari sasa vitu vidogo vimekuwa mambo makubwa yanayokuudhi.

Kila mmoja huanza kulalamika kwamba mwenzake hawi kama anavyotegemea.
Kunakuwa na disagreement nyingi kuliko agreement na unagundua kwamba mnatofautiana sana katika mitazamo ya vitu vingi.
Wewe unataka kula hotel unaipenda mwenzako anataka mle nyumbani ili ku save pesa, unapenda usikivu usiku nyumbani mwenzako anataka kusikiliza muziku kwa sauti kubwa.

Ule kuwa mwenzi wangu ni perfect huanza kupotea na imani yako kwake huanza kupotea kwamba mmm kumbe ni mkali kiasi hiki, kumbe ni mchoyo kiasi hiki, kumbe hapendi sex kiasi hiki, kumbe anajua kukalia mwenzake kiasi hiki nk.
Hapa tofauti za malezi, tamaduni, dini, kuamini, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza na kuwa wazi.
Katika hatua hii mtu halisi huanza kuonekana na ukweli ni kwamba ndoa huanza kujengwa hapa.
Wengi huanza kujiuliza mbona watu hawakuniambia kwamba ukioa au kutolewa inakuwa hivi kwani anayaanza kuona ni kinyume na matarajio na wengine huanza kujiuliza kwa nini nilioana naye.
Wapo ambao huanza kufikiria wachumba wengine (misri) kwamba labda ningeoana na Fulani alikuwa afadhari kuliko huyu.
Wengi huanza kujiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini hadi nikakubali kuoana naye.
Walio na hekima huanza kumuomba Mungu na kupata ushauri wa watu wanaowaamini...

Hatua ya tatu ni MATESO,MAJONZI NA TABU...Je,huwa vipi...Endelea kufuatilia

HATUA MUHIMU KTK NDOA NA MAHUSIANO.

Ndoa ni mahusiano yanayoweza na yanayotakiwa kuwa ndiyo kitu kinacholeta raha na kuridhisha katika maisha kuliko kitu chochote.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu walio kwenye ndoa huishi maisha marefu kuliko singles.
Kwa kuwa nusu ya ndoa zinazofungwa huvunjika katika baadhi ya nchi, ni muhimu sana kufahamu vizuri package nzima ya mambo ya ndoa katika pande zote.
Knowledge is power!
Pia ni vizuri kukumbuka kwamba (kama hujaolewa au kuoa bado) yale unakutana nayo muda wote wa uchumba hadi honeymoon ni asilimia 10 tu ya masuala ya ndoa na asilimia 90 ni kazi iliyo mbele yako na hii kazi itakupasa kuendelea kuifanya siku zote unavyoendelea na ndoa.


HATUA YA KWANZA NI KUDONDOKEA KWENYE MAPENZI.
Kibailojia kuna asili ambayo miili yetu huwa msingi katika hatua mbalimbali ambazo hutufanya kuvutiwa na mtu wa jinsia nyingine na kufika hatua tukaona maisha bila huyo mtu hayana maana.
Kuna aina tatu za kemikali (Phenylethylamine, dopamine na norepinephrine ) ambazo huhusika moja kwa moja na kuwafanya wawili wapendanao kwa mara ya kwanza kujikuta wamedondoka kwenye mapenzi (fall in love).

Kwa pamoja hizi kemikali huweza kuzalisha na kutibua matokeo ya kushangaza hadi mtu kuwa na positive attitude na anayempenda, piga ua hukubali kumuacha maana umempenda, watasema usiku watalala kwani nimempata anayenipenda.
Hizi kemikali hutufanya kuwa na nguvu kubwa ya kumpenda mtu na kujisikia tunajisikia very excited na mpenzi mpya.

Hizi kemikali kama nguvu ya hurricane au storm huweza kuufunika ubongo sehemu inayohusika na kutoa tahadhari.
Amygdale huweza kutoa tahadhari au onyo kwamba partner uliyempata anaweza kukuumiza hata hivyo kutokana nguvu iliyopo ya falling in love mhusika hupuuzia.

Mhusika hajui kuonywa ni kitu gani, haogopi watu wanavyosema maana yeye amependa, yupo blind.

Wengi huangukia kwa wapenzi wasiowajua vizuri na hujishangaa kwa nini wanawapenda kwa kasi ya ajabu kiasi hicho.
Kuna powerful attraction kiasi kwamba huweza kusababisha hadi mtu kutoa maamuzi ya ajabu kama vile kukana dini, kukana wazazi kukana ndugu na kukubaliana na huyo amempenda.
Katika hatua hii ya mahusiano wengi hujiona wamefikia na kutimiza ndoto zao.
Kila kitu huwezekana na kukufanya uridhike maana mpenzi anakupa kile unakihitaji ambacho hata wazazi hawawezi kukupa.

Ni hatua natural ambayo mke na mume huvutiana na hupelekea kuoana
Katika hii hatua maisha ni matamu, ahadi kubwa na kedekede kutolewa,
I miss u,
I love u,
You are mine,
I love u from earth to the moon,
Nakupenda kwa moyo wangu wote,
Sina mwingine ila wewe tu.Wakiwa wamelala hukumbatiana kama vile amelala mtu mmoja (mwili mmoja) ni raha ni kuhitajiana kwa kiu ya ajabu.
Wahusika huwa blind na hata kama mwingine ana makosa au vitu fulani anaudhi huonekana si tatizo, na hukubaliana kuoana hivyo hivyo.

Watafiti wengi wanauona huu upendo katika hatua ya kwanza si upendo wa kweli kwani huongozwa na hizo kemikali tatu na kukupa nguvu za attraction za ajabu. Pia haujajaribiwa bado, haujakumbuna na kasheshe bado.

Hii hatua katika mahusiano ya ndoa huitwa hatua ya ghururi (infatuation, self deceit, arrogance, presumption)
Hapa ndipo kunapatikana vitu vinaitwa uchumba na honeymoon
Hii natua huweza kudumu hadi miezi 30 muda ambao hutosha wahusika kuwa na mtoto.

Je, ni hatua zipi hufuata na kupelekea wanandoa kuwa na true love?

Je, mahusiano mengi au ndoa nyingi huvunjika katika hatua ipi?

Na je, ni jambo gani la busara kufanya katika hatua ambayo ndoa nyingi huangukia kwenye shimo?

Endelea kufuatilia....

Tuesday, 8 December 2015

SIPATI HISIA..

SWALI.

Mimi ni mwanamke mwenye umnri wa miaka 30 nimeolewa na sasa nina miaka 5 kwenye ndoa, nilikuwa naweza kusisimka mara moja tu hata kwa kupata busu (kissing) lakini sasa hakuna tena.
Je, nifanye nini?



JIBU.

Inaonekana maisha yenu ya sex na mumeo yamekuwa ni mtindo ule ule idara zote kwa muda mrefu bila ubunifu mpya.
Ni muhimu sana kujaribu vitu vidogo vipya kwa ajili ya kuyapa mapenzi au mahaba yenu viungo vipya hasa suala la kuandaana kimwili (foreplay)

Pia jambo la msingi ni kwamba unatakiwa kuwa na focus ya kumsisimua mume wako kuliko kusubiri yeye akusisimue wewe kwani unapojitoa kuhakikisha mwenzako anasisimka utashangaa na wewe jinsi unavyosisimka kirahisi kama maharage ya Mbeya.

Zifuatazo ni tips ndogo ndogo za kuhakikisha mume wako anasisimka na wewe unayegeka na ukifanya baadhi au na wewe kuwa creative zaidi basi utashangaa wewe mwenyewe unavyosisimka hata kwa kushikwa tu acha kupata busu tamu la mumeo.

Kama upo nyumba basi anapoingia mlangoni kutana naye huku umevaa mavazi ya kuvutia (kushawishi kwamba unataka) kama kuna watoto kamtegee chumbani.
Nenda naye kuoga pamoja

Mnong’oneze sikioni kwamba hapo ulipo hujavaa Chupi.
Acha message kwenye briefcase yake, au lunch bag yake au mfuko wa shati au kwenye seat ya gari kile unapenda kufanya naye usiku akirudi mkiwa chumbani au kile unataka yeye afanye kwako.

Mtumie sexy message kwenye simu yake ya mkononi.
Tumia muda mwingi kubusiana kwanza polepole (gentle) then kwa mvuto wakati huo nguo bado zimevaliwa then anza kumvua polepole.
Kama unaweza mfanyie massage na then mwambie na yeye unataka.
Mnong’oneze sikioni kwamba unamtamani na unampenda sana.
Pendeza mfanye sex sehemu nyingine siyo pale mmezoea kila siku
Pia jaribu sex position.
Muulize anapenda kitu gani kipya kujaribu wakati wa sex

Zaidi ya yote ili kusisimka kumbuka mambo yafuatayo:
Ikiwezekana anza wewe kuomba sex usisubiri kila siku akuanze yeye.
Jiandae mwenyewe kwa sex siku nzima.
Wakati wa kubusu busu bila haraka.
Uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya sex.
Focus mawazo yako kwenye tendo (kama kuna mgogoro hakikisha umeisha kwanza)
Jaribu kitu chochote kipya.
Jielimishe mwenyewe kuhusiana na suala la mapenzi katika ndoa
Mtangulize mwenzako (usiwe selfish)

Saturday, 5 December 2015

JINSI YA KUFANYA KTK "KATERERO"

Hii ni kujulisha kwamba mwanamke huweza kukojoa akifika kileleni na hutoa fluid ambayo hujulikana kama divine nectar au amrita au juice.

Wakati mwanamke anasisimuliwa kimapenzi au wakati wa mapenzi glands za Skene hutoa secretions ambayo husukumwa nje kwa speed kupitia urethra (kama mwanaume anavyotoa sperms)
Glands za Skene zimejibana kwenye ukuta wa kibofu cha mkojo na zipo upande wa juu wa ukuta wa uke pia zimetengenezwa kwa erectile tissues.

Divine nectar huweza kumtoka mwanamke baada ya kuponywa eneo la G- spot.
Kila mwanamke anauwezo wa kufika kileleni kwa kupitia G- spot na mwanaume ndiye anayeweza kusaidia.
Wewe mwanaume kwanza lazima uwe na mtazamo kwamba wewe ndiye healer au mtu wa karibu kumsaidia na zaidi wewe ndiye mtu wa ku-guide kwamba lazima mkeo atoe divine nectar.

Pia mwanaume lazima ufikirie pia hicho kipisi cha uume ni kitu ambacho unaweza kuingiza kwenye mwili wa mwanamke na ukishamaliza unatoa na kwenda zako.
Fikiria kwamba uume wako ni Nuru halisi ya kuangaza raha ya mwanamke katika mwili wake na kufungua roho na nafsi yake ili ajisikia ni mwanamke aliyekamilika kimwili, kiroho na kihisia.
Ili mwanamke aweze kuwa kisima cha kutoa divine nectar ni kupata uponyaji halisi wa eneo hili la G- spot au sacred area kwa kufanyiwa massage au kukandwa.

G- Spot ni eneo ambalo lipo upande wa mbele kwa ndani kwenye uke wa mwanamke na unapopitisha kidole utakigundua kwamba ni eneo lenye vimikunjo kama lips za midomo na si smooth
Baadhi ya wanawake huweza kupatikana kirahisi na wengine ni ngumu zaidi ingawa mwanamke akiwa amesisimka huweza kupatikana kirahisi.

Hiki kitendo ni muhimu kifanywe na mwanaume kwa kujitoa kumpa raha mwanamke bila kutegemea kupata return yoyote kwake.
Kwanza mwanaume lazima ajenge trust kwa kumpa mahaba ya uhakika kwanza kwa kuanza naye kwanza kwa mwanaume kuhakikisha kucha za vidole vya mikono zipo safi na zimekatwa vizuri then unaweza kwenda kuoga naye (kumuogesha au kuoga pamoja), pia hakikisha chumba umekiandaa na kuwa na sura ya kimahaba, unambusu passionately hakikisha mnapumua pamoja, huku mkitafakari mapenzi yenu kwa uwazi ili kuunganisha moods zenu na kupeana hamu zaidi kama si kuipa miili joto la kimapenzi.

Anza kwa kumfanyia Massage mapaja, hips, na eneo chini ya kitovu, panda tumboni na kuzunguka matiti, upande wa ndani wa mikono na rudi tena kwenye mapaja huku ukizambaza raha mwili wako wote ukirudi hadi dakika 5 hadi 10 hivi.
Hapo mwanamke atakuwa amerelax na yupo tayari kukuruhusu uendelee kwenye uke wake.
Then kwa upole kabisa anza kuchezea kwa ustadi kabisa kuta za nje za uke wake na kisimi kama vile ni vito vya thamani umepewa mikononi mwako.
Ni vizuri kumuuliza hasa ukiona ameanza kuhema tofauti kama unaweza kuingia kwenye sacred place au kwenye bustani .

Baada ya kuruhusiwa ingiza kidole (kidole cha kati huku kiganja kikiangalia juu) ndani ya uke huku ukichezesha au massage kwa alama kama vile unamuita mtu kwa kidole( njoo).
Ongeza mgandamizo kidogo ili na yeye asikie aina fulani ya mguso, endelea kuchezea kwa kuzungusha kidole chini na juu au kwa vibration, au zigzag au vyovyote hasa kutokana na yeye anavyo respond huku mkono mwingine ukichezea kisimi.
Pia unaweza kuongeza kidole kingine kwani baadhi ya wanawake hujisikia raha au kusisimka zaidi hasa kukiwa na vidole viwili.
Hakikisha macho yako na macho yake yanangaliana huku mkisamabaza umeme wa upendo baina yenu na huku kila mmoja akimsoma mwenzake anaendelea vipi
Pia wakati mnaendelea na hili zoezi ni vizuri mwanaume kuongea maneno mtamu yanayoonesha anafanya uponyaji wa hii sehemu huku mwanamke akimshukuru mwanaume kwa kazi kubwa anayofanya .

Kazi ya mwanamke kwenye hili zoezi la kufanya massage G-spot ni kulala, kuenjoy na kutoa feedback kwa mwanaume (ingawa mwanamke lazima ujiandae kwani unaweza kujisikia unataka kukojoa haja ndogo au unaweza kujisikia unataka kulia au unaweza kujikuta unakumbuka jinsi hisia zako zilivyoumizwa huko nyuma)
Hili kitendo lazima kirudiwe na kufanywa zaidi miezi miwili, mara mbili kwa wiki na kama kila kitu kipo shwari basi mwanamke anaweza kuanza kutoa divine nectar ingawa inatokana na historia yake ya mahusiano ipoje kama amewahi kudhalilishwa kijinsia au kuumizwa wakati wa tendo la ndoa huchukua muda mrefu kupata healing kwenye G spot.

Mambo ya msingi kuzingatia
Mwanamke au mwanaume kufahamu location ya G-spot
Uwezo wa kusababisha mwanamke akijisikia raha anaposisimuliwa au kufanyiwa massage kwenye G spot
Mwanamke kuondoa hofu na mashaka au kujisikia anataka kutoa mkojo hasa anaposisimuliwa G-spot hivyo badala ya kurelax anaweza kuwa na hofu.

Friday, 4 December 2015

HAMU YA SEX HUTOFAUTIANA.

Katika mahusiano mengi mmoja ya wanandoa huwa na hamu ya sex na kutaka sex mara nyingi zaidi kuliko mwenzake kwa sababu binadamu tunatofautiana levels za drive ya sex.

Kama wewe na mwenzi wako mna kiwango kinachofanana cha kuhitaji sex basi ninyi mmebarikiwa.

Ukweli ni kwamba suala la sex ni moja ya eneo ambalo ni tete sana katika ndoa, ndiyo maana kukataliwa sex na mwenzi wako huwa ni jambo linaloumiza sana (hasa wanaume) ingawa wapo wanawake wana drive kubwa ya sex kuliko mwanaume ambaye siku zote anaonekana anahitaji sex 24/7.

Hata hivyo kuna sababu za msingi za kibaolojia zinazopelekea mmoja wa wanandoa kuhitaji sex zaidi ya mwenzake.

*Nini husababisha hamu ya sex?
Hamu ya kutaka sex husababishwa na homoni ambayo kitaalamu huitwa testosterone.
Wote wanaume na wanawake wanayo hii homoni kwenye miili yao.
Wanaume wanayo nyingi zaidi kuliko wanawake kwa sababu wanawake wanayo homoni nyingine inayojulikana kama estrogen.

Msingi ni kwamba kiwango cha testosterone ulichonacho mwilini huweza kuelezea ni kiasi gani au hamu ya sex itakuwaje.
Ukiwa na kiwango kikubwa unakuwa na sex drive kubwa na ukiwa na kiwango kidogo unakuwa na sex drive ndogo.

Mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanaume wana kiwango kikubwa sana cha testosterone na hii husababisha wao kuwa na hitaji kubwa la sex.
Moja ya tatu ya wanaume wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na low sex drive.

Kwa upande mwingine mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanawake wote wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na kiwango cha kawaida cha drive ya sex na moja ya tatu (theluthi moja) tu ndiyo wenye kiwango kikubwa cha testosterone na hawa huwa na sex drive kubwa.

Hii ina maana kwamba mbili ya tatu ya wanaume wenye strong sex drive huishia kuishi (kuoana) na wanawake ambao wana sex drive kidogo na wapo wanawake hujikuta wapo ndani ya nyumba na wanaume (theluthi moja) ambayo sex drive ni ndogo sana.

*Je, ni homoni peke yake husababisha kutokuwa na hamu ya sex?

Siyo homoni peke yake ndiyo inayosababisha mwanaume au mwanamke kuwa na sex drive ndogo kuna vitu vingine vingi huweza kufanya sex drive kuwa ndogo kama vile kuchoka na kazi, kulea mtoto, migogoro katika ndoa, nk.

Pia ni jambo la msingi kutambua kwamba kwa mwanamke suala la maisha huchukuliwa kwa pamoja kwa maana kwamba yupo connected na kila eneo la maisha yake kama vile familia, kazi, sex nk.

Kama mwanamke amekuwa na siku mbaya kazini au amekuwa na wakati mgumu na watoto wake ni ngumu sana kujisikia ana hamu na sex.

Wanawake huhitaji muda wa kuondoa masumbufu au kusafisha mawazo yao kabla ya kujihusisha na sex na hii hufanywa na mwanaume ambaye kwake ni mtu wa karibu.
Mwanamke huhitaji kuwa connected na mume kabla hajawa tayari kujiingiza kwenye masuala ya kuwa mwili mmoja.

NI WEWE NDO WA KUAMUA KWANZA.

Wakati mwingine hata ndoa ambazo huonekana nzuri huweza kushindwa na zile zinazoonekana mbaya hudumu.

Zipo ndoa ambazo wawili huishi kwa mipaka hadi unashangaa sasa kwa nini inaitwa ndoa, kwa mfano mume au mke anatakiwa kuongea kwa mahesabu kwani akikosea neno anaweza kumkasirisha mwenzake na nyumba ikawa haikaliki na hakuna ladha kabisa kuongea na partner wake matokeo yake hata wakiwa wawili hakuna cha maana cha kuongea na kila mmoja hujibakia bubu kwani hujiona ni bora kuwa bubu kuliko ukaongea na ukawasha moto usioweza kuuzima.

Na mwingine hataniwi hata akifika nyumbani kutoka kazini si mama si mume au watoto wanajua kwamba baba amerudi au mama amerudi kila kitu sasa ni moto.
Swali la kujiuliza je, kwa nini uwe hivyo na unapata faida gani kuwa hivyo?
kwa nini familia iwe na nyoka mtu?

Pia wapo wanandoa ambao huwa hawakubali kushindwa hasa pale kukiwa na tofauti ya mawazo au kutoelewana kati yako.
Kila siku wewe ndiye upo sahihi na kila siku mwenzako ndiye anakosea, haiwezekani binadamu wawili wakaishi pamoja na kila siku au mara zote mmoja ndo anayekosea, huo si ustaarabu na ni ubabe tu.

"Ijulikane kwamba ndoa hurekebishwa kwa kuanza na wanandoa wenyewe, wanaweza kwenda kwa wazazi au marafiki au majirani au mchungaji, au padre au washauri maarufu wa ndoa au mtu yeyote mwenye utaalamu wa kushauri masuala ya ndoa, kama wanandoa wenyewe hawataki kujirekebisha na kuweka mambo sawa tangu chumbani mwao, mawazo au ushauri wa wengine hauwezi kupenya kwenye maisha yao ya ndoa na kuleta mabadiliko".

NI NINI MTAZAMO WA NDOA YAKO.

Moja ya tatizo la kawaida kwa ndoa za sasa ni mtazamo wa wanandoa kuamini kwamba ndoa yao haitafika popote au siku moja itashindikana au mmoja wa wanandoa kuwa na wazo kwamba siku moja ataondoka zake au wote kuwa na mtazamo kwamba siku moja nitaondoka na kuanza kivyangu upya.

Ukiwa na wazo la kushindwa ni hakika utashindwa vizuri sana kwani muda wote utakuwa unaangalia matatizo yote (negatives) ambayo yanakuwa alama kwamba sasa kushindikana kumeanza.
Yaani kwa kuwa una mawazo kwamba siku moja ndoa itashindwa basi akili yako hujipanga kusubiri dalili za kushindikana hata wewe mwenyewe kujua.

Wapo wanandoa wanaweza kusimama juu ya paa na kukiri kwamba ndoa zao ni za furaha hata hivyo ukichunguza kwa makini siri ya furaha yao si kwa sababu hawakutani na matatizo au shida au mambo magumu bali ni kwa sababu ya mtazamo wao kwamba wao ni mke na mume hadi kifo kitakapowatenganisha na zaidi sana wanajua sanaa ya kusuluhisha matatizo katika ndoa yao kwa kuanza na wao wenyewe kila mmoja kuamini kwamba anaweza kubadilika kwanza na kuleta mabadiliko na siyo kunyosheana vidole au kila mmoja kujiona yupo right all the time.

Inawezekana wewe unayesoma hapa sasa hivi ni mmoja ya wale ambao likitokea tatizo nyumbani na mumeo/mkeo basi ni kununa tu eti kwa kuwa siku moja utaondoka zako! Au kwa sababu una mipango yako kabambe na murua kabisa ya kumuacha mwenzio kwenye mataa hata hujafikiria watoto na huo uamuzi wako ambao ni kujifaraji tu kwani kuondoka si jibu la mambo yote bali ni njia nzuri ya kwenda kuanza kukutana na tatizo jipya na kubwa zaidi.

Kwani wewe ndo mtu wa kwanza kukutana na tatizo kama hilo kwenye ndoa?
Si kweli, badala ya kuchangamka na kupenda kwa moyo wako wote wewe unafikiria kuondoka au kudhani sasa mwisho wa ndoa umefika.

Eti oooh tupo tofauti sana hatuwezi kuishi pamoja tena! Kwani ni nini kilikuvutia hadi ukakubali kuoana naye?

Eti siku hizi simpendi kabisa! Lini umeanza kutompenda? Si umeamua mwenyewe kutompenda kwani love is a choice, wewe mwenyewe umeamua kutompenda na kweli humpendi ukichagua kumpenda utampenda.

Eti mke wangu ni mchafu sana! Unataka kumuacha kwa sababu ni mchafu? Mbona wakati wa uchumba alikuwa mchafu na ulikuwa una ignore! Nani mchafu kama si wewe uliyechumbia mwanamke mchafu, leo badala ya kutunza kilicho chako king’ae unataka kukimbia?

Unapoingia kwenye ndoa huku ukiwa na ufahamu au mtazamo kwamba ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha hapo tayari umepiga hatua kubwa sana na mbali kukuhakikishia ndoa yako inadumu na kuwa ya furaha kwa sababu unakuwa tayari kukubali kurekebisha kila tofauti zinazojitokeza kwani unajua huyu ni mwenzi wangu na kuna umuhimu wa kuishi kwa furaha kila wakati.

Ukiingia kwenye ndoa huku unategemea kushindwa ni kweli utashindwa vizuri sana na ukitegemea kufanikiwa na kuwa na ndoa ya furaha ni kweli utakuwa na furaha na zaidi utajifunza njia ya kuwa na furaha na utakuwa moja ya wanandoa wenye furaha duniani.

USIFANYE HAYA KWENYE NDOA YAKO.

1. Kumzoea mwenzi wako kiasi kwamba huoni yupo special
2. Kukosa interest kwa kile mwenzi wako anajihusisha kufanya
3. Kuwa mlevi.
4. Kutoshughulikia ndugu wanapoingilia ndoa.
5. Kukosa muda kuwa na mwenzi wako hasa baada ya watoto kuzaliwa.

6. Kujisikia huna kitu common na mwenzako
7. Kukosa kula chakula pamoja angalau mara 3 kwa wiki.
8. Kukosa kulala pamoja
9. Kutojua matokeo ya kuvaa nguo nzuri, usafi, kupendeza kwa mwonekano.
10. Kutosafiri pamoja hasa safari za ghafla na dhalula kwa lengo la kuwa wawili tu.

11. Kuishi pamoja kwa sababu ya watoto tu, na si upendo wa kweli.
12. Kushindwa Kukukubaliana kutokubaliana.
13. Kushindwa kujitunza mwenyewe kimwili, kiroho na kijamii.
14. Kushindwa kuchunga afya yako.
15. Kutumia muda mwingi na jamii badala ya mwenzi wako na familia yako.

16. Kushindwa kuwa na muda wa kuburudika pamoja.
17. Kutokuwa na interest zinazofanana.
18. Kutokubaliana katika pesa.
19. Kutotumia angalau saa moja kwa wiki wewe tu na mwenzi wako kuongea pamoja.
20. Kushindwa kujadili vitu unavyopenda au kutopenda likija suala la mapenzi.

21. Kushindwa kushikana mikono au kukumbatiana huku kila mmoja akiongea na mwenzake au kupeana ndoto za maisha.
22. Kuwa mwema zaidi kwa walio nje ya familia wakati suala hilo hilo unashindwa kufanya ndani ya familia au kwa mwenzi wako.
23. Kukosa kubusu asubuhi unapoondoka kwenda kazini au Unaporudi kutoka kazini.
24. Kukosa kufarijiana.
25. Kushindwa kuuteka moyo wa mwenzi wako.

26. Kufikiri na kuamini kwamba mwenzi wako kila siku yeye tu ndiye anakosea
27. Kukosa tendo la ndoa kwa siku 21 wakati mnaishi pamoja na kulala nyumba moja na hakuna tatizo la kimatibabu.
28. Kuwa na hisia kwamba mwenzi wako ni adui yako na humpendi.
29. Kukosa muda wa kucheka pamoja na mwenzi wako.
30. Kushindwa kwenda kanisani pamoja
31. Kutokujali kuongelea moja ya hayo hapo juu kuonesha kwamba unataka mabadiliko.

USIFANYE MAKOSA HAYA.

Unapotafuta mwenzi wa maisha si suala la kubahatisha kama vile kuwa kwenye chumba chenye giza totoro na kuanza kutafuta sindano sakafuni bali ni suala la kuhakikisha kuna mwanga wa kutosha kupata kabla ya kuingia kutafuta.

Ukweli ni kwamba dalili za ndoa kushindwa huweza kujulikana mapema hata kabla ya ndoa kufungwa hasa kutokana na jinsi mwenzi alivyopatikana

1.USIKUBALI KUOANA HARAKA MNO.

Kuwa wachumba kwa muda mrefu huwezesha ndoa yenye afya.
Hapa unatafuta mtu wa kuishi nawe maisha yako yote ina maana utalala naye chumba kimoja maisha, utakula naye chakula maisha yote, utakuwa naye katika matatizo ya kifedha maisha yako yote, utauguzana naye miaka yako yote, mtakumbana na kukatishwa tamaa pamoja maisha yako yote.
Kuamua haraka haraka kuoana ni kujitengenezea risk kubwa.

2.USIKUBALI KUOANA WAKATI BADO UMRI MDOGO SANA.

Oa au olewa wakati kwanza wewe mwenyewe unajijua vizuri.
Pia hakikisha unamfahamu vizuri yule unaoana naye.
Kuanzia miaka 24 kwenda mbele ni umri mzuri kuoa au kuolewa.
Kuwa na umri mdogo maana yake bado hujatimiza mambo ya msingi kama pamoja na kukomaa kiakili kuishi kama mke na mume.
Tafiti zinaonesha ndoa stable ni zile ambazo wanandoa walioana wakiwa na miaka kuanzia 28.

3.USIKUBALI KITU CHOCHOTE, MAZINGIRA YOYOTE AU MTU YOYOTE KukuSUKUMA KUOLEWA.

Hakikisha umetuliza akili zako ndipo ingie katika biashara za kuoana.
Inawezekana unataka kuoana haraka kwa sababu uliachwa na mchumba mwingine, au unajisikia mpweke, au anahisi ukiolewa suala la uchumi litakuwa limepata jibu.

4.USIKUBALI KUMRIDHISHA MTU YEYOTE NA CHAGUO LAKO.

Ni wewe utakaye pata faida au hasara, raha au machungu, furaha au huzuni, utamu au kuumizwa na si muda mfupi bali hadi kifo kitakapowatenganisha.
Haina haja kuwafurahisha wazazi au marafiki, au mchungaji, au mchumba mwenyewe kwamba unaoa au unaolewa eti wawe very happy.
Hii haina maana kwamba hutakiwa kuwasikiliza katika ushauri wao kuhusu wewe kuoa/kuolewa bali hii ni ndoa ni yako a lifetime opportunity.
Wala usikubali mtu awaye yote akuchagulie au kukufanyia uamuzi hata kama anauzoefu namna gani.
Wewe ndiye unatakiwa kuwa na uamuzi wa busara hata baada ya kupokea ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti

5.USIKUBALI KUOANA NA MTU HADI UWEZE KUMFAHAMU KTK NJIA TOFAUTI.

Unatakiwa kumfahamu vizuri huyo mwenzi wako mtarajiwa, mfahamu tabia zake kwa kadri unavyoweza.
Kutembea mmeshikana mikono miaka 10 ijayo kunategemea sana jinsi unavyomfahamu vizuri kabla ya kuingia naye kwenye ndoa.

6.USIOLEWE AU KUOA HUKU UNA MATARAJIO MAKUBWA SANA.

Ndoa kimbilio la faraja; inahitahiji kazi ya maana ili ikupe faraja.
Usiingie kwenye ndoa umeweka matarajio ya juu sana as if ni solution kwa shida zako zote kifedha, kihisia na kimaisha.
Hata kama sasa kuna mapenzi ya juu sana na una matumaini makubwa uwe makini kwani kila kitu kinaweza kuyeyuka kama barafu kwenye jua.
Kama unataka kuwa an ndoa imara jiandae kwa kazi iliyombele, kujitoa kutakuwa na maumivu, kuvumiliana, utakutana na changamoto ambazo inabidi ushindi na kuthibitishwa ili kuwa na true love kwa mwenzi wako.

7.USIKUBALI KUOANA NA MTU AMBAYE TABIA YAKE UNAHISI HUTAWEZA KUIVUMILIA MAISHA YAKO YOTE.

Kama kuna tabia Fulani ambayo hupendezwi nayo kama wivu, uchoyo, uchafu, hasira, uvivu, kutowajibika, siyo mkweli au msumbufu; jiulize kama utaweza kutumia maisha yako yote na yeye huku ukipambana na hiyo tabia.
Hiyo tabia mbaya kwake haitaondoka, kama unaomba muujiza abadili tabia hakikisha unatokea kabla hujaoana naye lakini si kuoana naye huku unajua kuna tatizo kubwa eti ukioana naye muujiza utatokea.

NI UFUNDI WA KUTATUA MIGOGORO KTK NDOA.

Wapo wanandoa ambao ni kama ua, hata audhiwe vipi anabaki kimya anaogopa asije akasababisha mwenzake kukasirika au kuzozana.
Wengine ni mwewe kitu kidogo tu ni kuzozana hadi yaishe.
Wewe je ni mwewe au ua?

1.MAWASILIANO YALIYO WEZA.
Wanandoa lazima waongee kwa uhakika wao wenyewe kila mmoja kwa mwenzake kuelezea hisia za ndani kabisa na kila mwanandoa lazima amtie moyo mwenzake.

2.KUONESHA UPENDO WA KWELI NA KUJALI
Wanandoa lazima wawe na uwezo wa kuonesha upendo na kujali mwenzake hasa ili kuzuia hali ya kuzolota tabia ya kupenda mwenzake kila wanapoendelea na maisha na kuishi.

3.MAPENZI NA FARAGHA
Wanandoa ni muhimu kila wakati kuchochea mahusiano ya tendo la ndoa linaloridhisha ili kuwa na mahusiano imara na wawili kuwa na faragha pamoja.

4.KUTATUA MATATIZO NA MIGOGORO.
Wanandoa ni muhimu kuwa na ustadi, au busara au hekima na uwezo wa juu sana kumaliza migogoro au tatizo au tofauti yoyote inapojitokeza haraka iwezekanavyo.

5.KUYAMALIZA
Pia ni muhimu sana kwa wanandoa kuwa na hekima ya kujua jinsi ya kumaliza mgogoro kuliko kwenda sambamba kila mmoja bila kuridhika na uamuzi wa mwenzake, kama mmoja amekosa basi akubali amekosa hata kama wewe ni mwanaume na jamii inakuona kama waziri au mbunge au kiongozi mkubwa kwani ndani ya nyumba wote ni kitu kimoja.

6.MGAWANYO WA KAZI
Katika ulimwengu wa sasa ambao wanawake na wanaume wote huondoka asubuhi au muda wowote kwenda kuwinda kwa ajili ya mkate wa familia bila kuwa na mgawanyo mzuri wa kazi nyumbani mmoja huweza kulemewa na zaidi kuzusha migogoro mingine.
Hivyo basi wanandoa lazima wawe wanagawana kazi na kusaidiana vizuri na kila mmoja kumtanguliza mwenzake.

7.JINSI YA KUZOZANA
Ni vizuri kila mmoja kutoa dukuduku alilonalo au kama kuna kitu kinamuudhi au kinamsumbua au haridhiki nacho kwa mwenzake ni vizuri kukiweka mezani na kikamalizwa kwa kujadiliana kuliko kukaa na donge moyoni huku unaangamiza na afaya yako.
Wapo wanandoa ambao hata kama kuna jambo gumu limamuumiza hayupo tayari kumuuliza mwenzake kwa kuogopa wasije wakaanza kuzozana au kuogopa mwenzake asije akakasirika. Ukweli ni kwamba afadhari umwambie akasirike na muyamalize kuliko kukaa nalo moyoni.

TUNAJIFUNZAJE KUHUSU NDOA?

Ndoa huweza kuwa ndicho kitu chenye furaha ya ajabu au kuwa kitu kinacholeta huzuni.
Mungu aliweka ndoa ili kumuunganisha mwanaume na mwanamke ili kila mmoja kati yao ampe mwenzake kila hana hata hivyo hizo tofauti zilizopo zinaweza kuwa sababu kubwa ya hawa wawili kuwa vipande badala ya kitu kimoja.
Kumpenda na kuhishi na mwenzi wako ni kazi ya kujitolea kila siku na zaidi kufanya mema kwa ajili ya mwenzi wako.

Matatizo au migogoro au kutofautiana katika ndoa ni kitu cha kawaida na huweza kuleta matokea mazuri kwani wanandoa wanaotatua matatizo vizuri hujikuta wanafahamiana na matokeo hujuana na hujenga ndoa imara.

Ukweli kama kuna ndoa ambayo wanadai hawana hata tofauti au kupishana kwa njia yoyote basi mmoja ya wanandoa amekufa ni mfu au wameamua kula jiwe tofauti zilizopo huku moyoni kila mmoja akiumia kwa jina la amani.

Kwa migogoro katika ndoa wengine ni faida na wengine huwaangamiza

Mmoja anakuwa ametoka katika familia ambayo wakati wa migogoro na zogo wazazi wake walikuwa wanaishughulikia vibaya kama si kuikwepa au kuiacha.
Hivyo hata baada ya kuishi na mke au mume huamini njia waliyotumia wazazi wake ni sahihi. Unapoamua kuoa au kuolewa unatengeneza ndoa mpya duniani ambayo inahitaji njia sahihi ili kutatua matatizo na migogoro.

Inawezakana mmoja au wote wanaamini kukitokea mgogoro wowote wa ndoa ni kitu kibaya, wanaamini wakijaribu kutatua hawataweza.
Migogoro hutokea kwa sababu ya toafuti za kimawazo na kuijaribu kuitatua kwa upendo na hekima kila mmoja akijaribu kuwa sehemu ya suluhisho hujenga ndoa

Wanaamini amani ni pamoja na kutunza matatizo bila kuyaongelea au kutatua. Wanaogopa kuzungumzia matatizo na tofauti zilizopo kwani wanaweza kuwasha moto wasioweza kuuzima.
Hakuna kitu kibaya kama kutunza jambo moyoni ni sawa na magari mawili ambayo yanaelekea kwenye ahead on collision siku ikifika enough is enough hapatatosha.

Wanafahamiana juu juu tu na hivyo kuyajadili matatizo yanayojitokeza ni kuingilia business ambazo ni kuingilia others stuff.
Ukiingia kwenye ndoa kila kitu ni deep hakuna cha others stuff kwani kujuana ni pamoja na udhaifu na uimara na kwa njia hii hujenga intimacy.

Hawajiamini hivyo mgogoro ukijitokeza wanaongea sana ili kujilinda badala ya kusikiliza na kujua watatue vipi.
Tatizo lolote au mgogoro wowote ukijitokeza ni muhimu kila mmoja kutulia na kusikiliza kwa makini kabla ya kuanza kuongea.
Wapo wanaume (si wote) mke hata kama hajamaliza kuongea yeye hudakia na kusema “najua unataka kusema kitu gani” Mke hujiona hajasikilizwa na mgogoro huweza kupanda kutoka kichuguu na kuwa mlima kilimanjaro.

Kila mmoja analenga kushinda au kwamba yeye ni sahihi kuliko mwenzake matokeo yake wanashindwa kutatua na wanaongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.
Kumbuka hakuna mtu ambaye yupo sahihi kila siku au siku zote; ni muhimu kutambua kwamba kuna wakati tunakosea na tukubali tumekosa na tuombe msamaha.

KWENU WANAUME.

Kuishi na mwanamke kunahitaji mwanaume kuwa makini na jinsi unavyoishi naye pamoja na unavyoongea naye na mawasiliano yote kwa ujumla.
Mawasiliano ni ufunguo kwa mwanamke kumfurahia mume wake.
Ukiongea na mke wako kama mwanamke mrembo naye atajiona ni mrembo ukiongea na mke wako kama vile ni jimama lililopitwa na wakati ni kweli anajiona amezeeka na kupitwa na wakati.

Jambo la kwanza msifie kwa jinsi anavyoonekana yaani nguo alizovaa, nywele, viatu na hata perfume, anyway vitu hivi anavaa kwa ajili yake na wewe pia.
Kwa kumpa compliment basi atakuwa na confidence na kwamba umevutiwa na atajisikia vizuri. Suala la nguo ni kitu muhimu sana kwa mwanamke ndiyo maana hata wenyewe kwa wenyewe huweza kupeana sifa,
je wewe mwenye mali naamini si zaidi?

Unavyozidi kumsifia mwanamke kwa mwonekano wake, jinsi anavyofanya vizuri kitandani, jinsi alivyo, tabia njema na kila kitu anafanya naye atajitoa zaidi kuhakikisha anakupa huduma za uhakika.
Jambo la msingi hapa unaanda akili yake kwa ajili ya kuwa mwili mmoja baadae.

Jambo la pili ni muhimu sana kumuuliza jinsi alivyoshinda hasa ukikutana naye jioni baada ya kazi.
Hata hivyo unatakiwa kuwa makini sana na jibu la swali kwani kama alikuwa na siku mbaya anaweza kukumwagia kopo zima la worms. Pia unatakiwa kuwa na tactics za kuhakikisha unabadilisha mambo mabaya anayokwambia na kuwa mazuri au kubadilisha somo.
Kumbuka lengo lako ni kutaka kutengeneza mazingira ya yeye kuwa na mood nzuri kwa ajili ya kuwa mwili mmoja.

Jambo la tatu hakikisha anajifahamu jinsi unavyojisikia kuhusu yeye na pia ni jinsi gani unajisikia vizuri kufanya mapenzi, tendo la ndoa au kuwa mwili mmoja na yeye.
Kama umezoea kuwa na utaratibu unaojirudiarudia unatakiwa kubadilisha. Ikiwezekana kuanzia sasa kila touch mwilini mwake kuanzia mwanzo hadi mwisho hakikisha unamwambia unavyojiskia raha. Hakikisha amejifunza na anafahamu unavyojisikia unapombusu, mkumbatia, mpenda, mshika, mnusa, muonja nk zaidi mhakikishie jinsi unavyojisikia akikupa mahaba.

Jambo la nne hakikisha unamsifia mbele za watu au mbele za rafiki zako na zaidi sana ukiwa chumbani hakikisha unamuandaa hadi yeye analilia wewe kumuingia ili kuwa mwili mmoja hiyo ina maana kwamba utakuwa umemuandaa vya kutosha, tumia mwendo wa kobe na si cheater.

Jambo la tano, hujawahi ambiwa na mke wako kwamba “ hujawahi nipeleka hata Bagamoyo tu: hii ina maana kwamba anataka siku moja upange muwe na outing ya uhakika wewe na yeye tu, maana yake anataka romance. Hivyo fanya kweli maisha ni sasa!

Hii ilikuwa kwa ajili ya wanaume tu, nashangaa wewe ni mwanamke na umesoma hadi mwisho, ok haina shida muonyeshe ujumbe huu Mumeo.

CHUMBANI..

KUWA NA UTARATIBU ULEULE MIAKA NENDA RUDI.

Kwa kuwa unajua nini hufanyika ukiingia chumbani na mke/mume wako, hivyo unavua nguo zako na zake, unamvuta kwani anajua ukimvuta kwa mtindo huo nini unataka naye anakuacha uendelee, nawe unachukua kiungo A na kuiingiza kwenye kiungo B, unafanya kile unachokijua, baada ya dakika 5 zoezi limeisha, unageuka unalala, hoi folilo!
Unaonaje hapo?

Hapa haijalishi hili tendo ni tamu kiasi gani, unaburudika kwa raha kiasi gani, unapiga kelele za raha kiasi gani, ni dhahiri ya kuwa miaka kadhaa hili zoezi litakuwa nadra sana kufanyika na ikifanyika lazima mmoja atajisikia it is boring.

Kuwa na utaratibu unaofanana kila siku kila mwezi na kila mwaka huhatarisha mahusiano ya kimapenzi kwa mke na mume.
Njia nzuri ya kulinda upendo na connection ya thamani kati ya mke na mume katika mapenzi ni kuwa na kitu kipya baada ya muda fulani hata kubadilisha mazingira tu acha skills.
Ukweli kukiwa na new tips na techniques mtafurahia sana kuwa mwili mmoja kwani mtakuwa hot, na mtahitajiana mara kwa mara na zaidi.
*
Kuogopa kuongelea au kujaribu vitu vipya wakati wa kuwa mwili mmmoja.

Je, umewahi kuwa na wazo zuri au jipya la kutaka kuongeza ladha mpya chumbani ukiwa na mke au mume wako na unashindwa uanze vipi au hujui mwenzi wako ata-respond vipi?
Au unaogopa atakuuliza ulijifunza wapi? Au akaenda mbali zaidi kwa kukuuliza nani amekufundisha?

Ukweli ni kwamba kuna asilimia 90 mpenzi wako atapenda kusikia na pia atashirikiana na wewe kujifunza hizo new skills muhimu tumia hekima na busara kuwakilisha mawazo yako na kila kitu kitakuwa shwari huko chumbani.
Pia ni dalili kwamba mnaogopana na zaid hampo wazi sana kuongea mambo yenu ya ndani ambayo ni muhimu na yanaweza kuwaweka karibu zaidi.
Jiamini na ongea kile unapenda kwa nini ujinyime raha?
*

Kujaribu kumlazimisha mume/mke wako tendo la ndoa.

Kama mke au mume amechoka au hana mood haina haja kuanza kumlazimisha afanye;
Wakati mke au mume anasisimka mwili humwaga kemikali za adrenaline ambazo husaidia kuupa mwili energy ya tendo zima la ndoa hivyo kama amechoka anaweza asisisimke vya kutosha na maana yake atakuwa hana nguvu za kujirusha sawasawa at the maximum ili kuleta matokeo mazuri.

Ikiwezekana kama wewe ni mwanamke na mume usiku amegoma kwa kwua amechoka (kwani huwezi kuisimamisha stick hadi ubongo wake uamue) usijali subiri hadi asubuhi kabla hajaamka kwani kiwango cha testosterone huwa juu kuliko wakati wote hivyo utamfaidi tu na hana ujanja stick itakuwa imesimama na ipo tayaritayari, usifanye kosa tumia busara.

Kama wewe ni mwanaume na mke anasema amechoka kitu cha kwanza ni kutengeneza mood yake ili awe katika hali ya kuwa relaxed, maneno matamu, ongea kile huwa anapenda kusikia, ni vizuri mwanaume kujua nini humfanya ajisikie kunyegeka na kuwa excited hata kama utatumia nusu saa kwani si una mission?
Tumia skills zako zote.
Itafika mahali atajieleza mwenyewe kwa jinsi unavyomwona ila ukishindwa kamwe usimlazimisha na pia usifanye kwa kuwa amesema yupo tayari ni muhimu kufahamu kwamba kukubali kwake ni ni sababu anapenda na siyo ili yaishe utaishia kuulizwa “hujamaliza?”
*

Kuacha au kukwepa kipengele cha kuandaana
kabla ya tendo la ndoa.

Wanandoa wengi (hasa wanaume) hupenda kukwepa kumuandaa mke ili kuwahi kufaidi kitu chenyewe hata hivyo kumuandaa mke humpa faida hata mume mwenyewe.
Kwa kubusu, kumshikashika na mengine yote huweza kusababisha mke kujisikia ameridhika na atajisikia humtumii kwa tamaa zako.
Hivyo slow down, take time!
Lazima mwanaume uwe playful na usiwe na mikono mwepesi bali mikono slow.
*

Kutumia mikanda ya video za X kuimarisha utendaji wa mpenzi.

Wakati maisha ya ndoa yamefikia hali mbaya wapo wanandoa ambao huamua kutumia video (mikanda ya X) kujifunza wakidhania maisha yao ya mapenzi yanaweza kuwa kiwango cha juu kiasi cha kufika kwenye roof.

Ni kosa kubwa,

Kutumia outside source huweza haraka sana kuharibu kuliko kutengeneza au kusaidia.
Ndoa ni mke na Mume pamoja na Mungu mwenye kupokea utukufu unaotokana na uumbaji wake kwa hao wawili.

NI VIZURI KUCHUKULIANA.

Tukioa na kuolewa tunazama kwenye udhaifu na kwenye uchumba tunaona uzuri tu!Kabla ya ndoa au wakati wa uchumba wengi hujikuta wakiwa makini sana katika kuangalia uimara wa wapenzi wao na baada ya ndoa hujikuta wakijikita katika kuangalia udhaifu za mwenzi wao.
Hii ni kwa sababu wakati wa uchumba wawili wanaopendana hujihusisha katika kuburudishana kwa maana kwamba wakati mwingi hutumia kuwa na social activities na kila mmoja huwa na romantic interest.

Wakiingia kwenye ndoa mambo huwa tofauti (waliooa na kuolewa anafahamu na kama hujaolewa au kuoa huwezi elewa kwani hujafika hii hatua) kwani hapa ni uwajibikaji maana wawili hawa sasa wanatakiwa ku-share skills zako in reality.

Kuwa na udhaifu fulani ambao mwenzako inabidi akuchukulie ni hitaji la kila mmoja na halikwepeki kwani ni kitu ambacho kipo kwa ajili ya kutuwezesha kufanya marekebisho ya kujuana kupitia tofauti zilizopo ili kuwa na ndoa iliyo imara zaidi.

Jambo la msingi hapa ni kujifunza tofauti zilizopo na udhaifu uliopo na kuchukuliana, na pia ni jambo lililowazi kwamba huwezi kumpata mtu hapa duniani ambaye hana udhaifu au hana kasoro au amekamilika kila eneo la maisha,
Kama unaota kwamba siku moja unataka umpate partner ambaye hataumiza moyo wako unakosea sana kwani kila kwenye upendo kuumia moyo kupo.

Pia ni vizuri kufahamu kwamba kuna mambo duniani bila kujalisha umesoma kiasi gani, una akili kiasi gani, au una uwezo kiasi gani au jamii inakuamini kiasi gani bila Mungu inakuwa bado ni zero kubwa.

Mwanandoa aliye na hofu ya Mungu yupo tofauti na mwanandoa yeyote duniani hasa linapokuja suala la kuchukuliana udhaifu na mwenzi wake.

Je tofauti hiyo ipoje?

Binadamua tunatabia ya kuona mabaya kwa wengine hata mke au mume badala ya mazuri.
Hivyo ili kukubali udhaifu wa partner wako unahitaji sifa 9 .
Mwanandoa wa aina hii huweza kufurahia ndoa kwa sababu anaweza kushinda kumchukulia mwenzake udhaifu wote kwa kuwezeshwa na Roho.
Kutembea katika roho huweza kufanya udhaifu wa partner wako kuwa si kitu.

Tofauti ya wanandoa haitakiwa kuwa janga kwani kile ambacho wanandoa wanafanya wakati wa mgogoro au tofauti huelezea success au failure ya ndoa.

Ndoa nyingi ambazo leo tunaona nzuri zilipitia conflicts hata hivyo kupitia conflict (siyo zote) zilisaidia wahusika kujuana na kufahamiana vizuri na kupendana zaidi.

KWANINI UKATE TAMAA..!

Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena!
Hawezi kushirikisha kitu chochote ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja.
Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu.
Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina hii bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo.

1;TEMBEA KATIKA ROHO.

Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu.
Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume.
Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kwamba huwezi ukampenda Mungu usiyemuona ukashindwa kumpenda partner wako ambaye unamuona.
Ukiguswa na Mungu lazima na ndoa yako itakuwa ya tofauti.
Kumbuka kutembea katika Roho ni kitu tofauti na kujiita Mkristo.

2.ACHANA NA KUKAA KWENYE LAWAMA,MAUMIVU, UCHUNGU NA KUANGALIA UDHAIFU WA PATNER WAKO.

Yeyote ambaye analalamika kwamba ndani ya ndoa yake hakuna upendo ukichunguza kwa makini utakuta amebeba fulushi zito sana la orodha ya mambo mabaya ambayo partner wake anamfanyia au udhaifu wa partner wake.
Anaongelea huo udhaifu wa partner wake, anasimulia rafiki zake, anauamini, anauwaza, anaukiri kutembea nao kama sala.

Hisia mbaya hata kama ni kweli huwa na matokeo mabaya kwenye feelings.

3.ORODHESHA VITU 10 VIZURI KUHUSU MWENZI WAKO.

Na kiri mara mbili kwa siku kwa siku 21
Shukuru kwa kila jambo.Kulalamika kila siku huweza kuharibu emotions zako bila kujua hata kama mume wako au mke wako hafai kabisa bado unaweza kutumia mambo mazuri aliyonayo kuirudisha ndoa yako kwenye mstari.

Huwezi ukawa na mawazo tele ya udhaifu wa mke wako au mume wako na wakati huohuo ukamfurahia na kumpenda na kuwa na feelings za upendo wa juu.
Vita ya upendo huweza kushinda au kushindwa kwa mawazo yako kwani moyo ni mtumishi wa mawazo yako.

Moyo huamini kile mawazo yako yanakitunza.
Mtu mmoja alikiri kwamba hampendi tena mke wake na kwamba ilikuwa ni miezi mitatu kila mmoja alikuwa analala chumba chake, alipoambiwa aandike mambo kumi mazuri kuhusu mke wake kwenye karatasi.
Akakubaliana kila siku asubuhi anapoenda kazini kuyatafakari hayo mambo mazuri 10 kuhusu mke wake na pia kuyatafakati tena jioni akirudi kazini anapoendesha gari lake.
Baada ya siku kumi akakiri kwamba sasa mambo yameiva kwani tumerudiana, zaidi kulala chumba kimoja sasa tunalala kitanda kimoja.

Na baada ya wiki tatu akakiri kwamba anampenda mke wake kuliko wakati wowote katika maisha yao ya ndoa tangu waoane.
Alipoulizwa je, umeyashika yale mambo 1o mazuri kuhusu mke wako akasema kwamba yale aliyashika siku ya tatu na siku ya nne akaamue kuongeza hadi yakawa 15 na kwa kuwa yalikuwa mtindo wa Cards hivyo alikuwa anayapitia moja baada ya lingine na kuyachanganya na kuyakiri over and over.

Hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa na orodha ya mambo 10 mazuri kuhusu mke au mume wake na akayatamka na kumshukuru Mungu twice a day na kusiwe na kufufuka kwa upendo mpya.

Kumsifu na kumshukuru mke wako au mume wako mbele za Mungu kwa mambo mazuri aliyonayo ni silaha ya nguvu kubwa ili kuwasha upendo na mapenzi mapya katika ndoa.