Saturday, 31 January 2015

ZIJUE DALILI ZA UJAUZITO.

Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana
Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.
Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:
>Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
>Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
>Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
>Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
>Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
>Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
>Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya kichwa
>Kizunguzungu
>Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
>Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
>Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
>Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
>Tumbo kujaa au kuvimbiwa
>Kununa na kukasirika haraka
>Kiungulila au kupata choo kigumu
>Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
>Kuongezeka uzito
>Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
>Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
>Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign
>Dalili nyingine ni pamoja na
>Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
>Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
>Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
>Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
>Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto

No comments:

Post a Comment