Sunday, 25 January 2015

ETI UKIMPA MPENZI WAKO KINYUME NA MAUMBILE NDIO ATAKUPENDA DAIMA?

Kuna siri moja ambayo nahisi ipo kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa na hata wale walio kwenye uhusiano wa kawaida kwamba, wanafikia hatua ya kutoa aina hiyo ya penzi eti ili wapenzi wao wasiwasaliti. Jamani hii inaingia akilini kweli?

Unafikia hatua ya kuhatarisha maisha yako kisa unataka kukamilisha ile sentesi ya kwamba unampa mumeo kila anachokitaka? Huo ni ulimbukeni na kama wapo wanaoendelea kufanya hivyo, wanajitafutia matatizo yatakayowafanya waje kujuta baadaye.

Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampatiliza katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?
Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?

Ni kamchezo ka’ nyumba ndogo

Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaoongoza kwa mchezo huo mchafu ni wale wezi wa mapenzi ambao hufahamika kwa jina la nyumba ndogo.
Hawa eti wanatumia mbinu hiyo kuwashika waume za watu. Kimsingi hii ni aibu na wanaokubali kufanyiwa hivyo wanajidhalilisha na hawawezi kudumu na wanaume wao.

Usithubutu kabisa

Mapenzi kinyume na maumbile licha ya kwamba yamekatazwa hata na vitabu vitakatifu, madhara yake kiafya pia ni makubwa. Wapo wengi ambao sasa wanajuta kwa kufanya mchezo huo kutokana na kupata matatizo wakati wa kujifungua lakini pia wengi wao imekuwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa ukiwemo Ukimwi.

Ni laana

Wanaofanya hivyo wamelaaniwa na wanaweza kushangaa uhusiano wao unakumbwa na matatizo kisha kusambaratika kwani Mungu hawezi kuubariki ule unaokwenda kinyume na maagizo yake.
Ni suala tu la kukaa na kujiuliza, wewe mwanamke unapata raha gani kufanya mapenzi kwa njia ambayo haijaruhusiwa? Wakati mwingine nashindwa hata kuwaelewa hawa wanaofikia hatua ya kujisifia kuwa eti wanawaachia waume zao ‘wajisevie’ wanachotaka kwa kuwa wanawapenda.
Hivi watakuwa na akili timamu? Kumpenda mtu ndiyo uwe tayari kuhatarisha maisha yako kiasi hicho? Tena kwa taarifa yako wale wanaowakubalia wapenzi wao mapenzi kunyume na maumbile wanaonekana wajinga na wanadharaulika. Hakuna mwanaume anayeweza kumheshimu mwanamke anayeweza kuuweka rehani mwili wake kwa njia hiyo.
Nimalizie makala haya kwa kusema kuwa, kanuni ya kwamba unatakiwa kuhakikisha unampatia mpenzi wako kile anachokipenda inabaki palepale lakini umkubalie katika yake yasiyo na madhara kwako. Yale ambayo unaona yatakuletea matatizo, mkatalie kwa kumpa sababu za msingi. Kama ni muelewa atakuelewa, asipokuelewa kuwa tayari akuache lakini usihatarishe maisha yako.

1 comment:

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.

    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.

    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyeyajua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%.

    Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.

    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.

    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.

    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.

    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.

    Nitaendelea kushukuru milele.

    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp Ikiwa unahitaji msaada wowote kati ya haya.

    WhatsApp yake: +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete