Friday, 7 August 2015

NI MAMBO MADOGO LAKINI NI MUHIMU SANA.

Weekend ni wakati mzuri kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa na muda mzuri na mpenzi wako, mke wako, mume wako, mchumba wako, soul mate wako, partner wako, honey au sweetie wako nk.
Naaamini utasema kwamba dunia ya leo mambo muhimu ni uchumi, kazi zetu nk, kitu cha msingi bila amani, upendo na furaha ktk nyumba zetu bado hata kama tutakuwa na pesa nyingi.

Kama wewe ni mwana ndoa jitahidi hii weekend kufanya mambo tofauti kabisa na jinsi unavyofanya kila siku hasa weekdays.

Kitu cha msingi ni wewe kuwa mbunifu kufanya vitu vidogo vidogo (kama unaweza kufanya makubwa fanya) ambavyo vitasababisha mwenzi wako akuone unamjali na unawajibika katika mahusiano.
Kama ni mwanaume unaonaje hii weekend angalau unasaidia kazi ndogondogo pale home kama vile
kutandika kitanda,
kupika kama unaweza,
kuwaandaa watoto,
kufanya usafi, kusaidia kufua nguo nk
Fanya hivyo kwa upendo..

Na ukitoka leo kazini unaonaje pia kama utaenda kununua zawadi yoyote kwa ajili yake, ingawa hii weekend zawadi muhimu ni wewe mwenyewe kuwa na muda na yeye.

Na kama ni mwanamke naamini utakuwa mbunifu zaidi kufanya vitu vipya kwani wanaume siku zote wanataka kitu kipya katika mahusiano.
Unaonaje ukihakikisha chumbani kunakuwa tofauti kabisa kuanzia
Kitanda na mashuka yake nk
marashi mbalimbali chumbani
na pia wewe mwenye kuhakikisha una nukia vizuri kwani smell of your body affects emotions, jipambe sawaswa tofauti na siku za kawaida kwa ajili yake,
Tafuta time kuwa naye yeye tu na kama hukupika wewe mwenyewe wiki nzima jaribu weekend hii kumpikia mwenyewe kwa mikono yako chakula cha uhakika.
Pia usisahau kumuombea mkeo au mumeo maana (maombi) ndiyo yatawahakikishia kwamba kitanda chenu shetani hapati nafasi kulala maana akilala, kuangalia TV kunakuwa raha kuliko faragha ya chumbani kwenu.

Kama wewe ni single na ndo upo kwenye process za Uchumba najua hii weekend umepanga mkutane mkaongee mipango yenu, nahisi tangu mmekutana wiki iliyopita umeona kama siku haziende, Mungu ni mwema weekend ndo hiyo.
Jitahidi unapokuwa na mke/mume wako mtarajiwa unatumia jina lake vizuri kwani kuna raha yake mtu ukimtaja kwa jina lake mwenyewe kama vile Mungu anavyojitambulisha kwetu kwa jina lake na kututaja majina yetu.
vijana wa siku hizi Badala ya jina mnatumia maneno kama ‘
"Oya twende zetu!"
"Hey nikununulie nini!"
Tumia jina lake hiyo inakupa point kwamba ni presentable
Pia tumia huo muda kumfurahisha kwa maneno matamu, yanayotia moyo ili kumsahaulisha na yale amepitia wiki zima, kwani hapo ndo mnaanza kutoa picha ya nyumba yenu jinsi itakavyokuwa.
Pia ni muhimu unapokutana naye Ongea mambo muhimu; siyo mambo ya watu wengine au ku-discuss michezo ya kwenye TV, muda mnaotumia kukaa pamoja na kuongea ni muhimu sana mtakuja kuukumbuka mbele ya safari


Nawatakia weekend njema na Mungu awabariki sana

Thursday, 6 August 2015

KUFICHA SIRI..!

"Ndoa ni institution ambayo ni takatifu na hujengwa kwa msingi wa kuaminiana.
Huu msingi wakati mwingine hujikuta una hofu ya kubomoka na kusambaratika kwa vitu vidogo vidogo kama suala la siri katika ndoa.

Siri katika ndoa huweza kuharibu msingi wa ndoa ambayo imejengwa vizuri na kuonekana mbele za watu ipo imara.
Ni kweli inawezekana mke wako au mume wako hatakiwi kujua kila kitu kuhusu wewe vile umefanya ana unajua kila siku inayopita duniani hata hivyo ukiangalia kwa undani zaidi siri unazoficha kwa mume wako au mke wako zinaweza kukupeleka pabaya.
Iwe siri nzuri au siri mbaya kumbuka kwamba inaweza kuweka madoa mabaya sana kwenye ndoa yako.

Jambo la kujiuliza ni je, kwa nini unaficha hizo siri?
Kumbuka kiapo (vow) namna ulivyoahidiana wakati mnaoana kwamba ninyi ni kitu kimoja na kama unajikuta unajitahidi kuficha siri basi unaelekea kwenye big trouble.

Je, unaficha matumizi ya pesa?
Kumbuka siri katika ndoa mara nyingi ni hatari kwani itafika siku utaangukia pua, kwa mfano kama unaficha namna unatumia pesa na madeni yanazidi kuingiliana ipo siku wanaokudai watakuja kuuza nyumba ndipo mke au mume atajua kulikuwa na tatizo na utakuwa umeshachelewa!
Inawezekana unamficha mchumba wako kwamba huna mtoto wakati mtoto unaye, siku akigundua hata kama mmeoana miaka 5 au 10 gharama ya kurudisha trust itakuwa kazi ya ziada, Utajuta!

Inawezekana unaficha siri kwamba mtoto uliyenaye si wa huyo mume wako na umeamua kula jiwe, hata hivyo siku akigundua hapata tosha!

Je, ni siri kiasi gani unamficha mke wako au mume wako au mpenzi wako?
Kumbuka mahusiano ya kweli hujengwa kwa trust, kuficha siri ni moja ya bleach ya trust na zaidi kuliko yote hakuna siri duniani.

Wednesday, 5 August 2015

MWANAUME,PUNGUZA SPEED UNAPOKUWA KIFUANI..

Ni kama ua hivyo handle with care!
Unachotakiwa kujua ni kwamba inches mbili za kwanza kwenye uke wa mwanamke ndiyo ina hold raha ya sex kwa mwanamke (ni sehemu yenye nerves za raha ya sex kuliko ndani ya uke.

Na kuna factors 3 muhimu za kuzingatia

MWENDO
Lazima ziwe katika kipimo ambacho mwanamke anaweza kujisikia.
Wanaume wengi hufanya makosa ya kwenda kwa nguvu kama mbio za hasira.
Hii ni kupoteza muda otherwise iwe imefanywa muda sahihi
Kwa wanawake wengi isipokuwa muda mfupi kabla ya kufika kileleni suala la kutumia miguvu ni style ambayo huwaacha katika maumivu na boring kwani kawaida hakuna feeling za utamu wa tendo.
Ngozi huweza kubeba feelings za sex mara 10 zaidi iwapo mwanamke atakuwa anasisimuliwa polepole.
Kufahamu siri hii kutaweza kukupeleka mbele zaidi na kukufanya mwanaume lovable kutimiza kile mke wako anahitaji.

Kumbuka ngozi yetu kama wanaume linapokuja suala la sex (uume) ipo nje na kavu ukilinganisha na mwanamke ambaye organs zake zipo ndani, wet na zipo nyororo kama ua la roses.
Huhitaji kuwa genius ili kufahamu jinsi unaweza kusababisha maumivu bila kwenda polepole.
Jinsi mwanaume anavyoumia akipigwa teke kwenye balls ni sawa na mwanamke huumia wakati mwingine mwanaume akiwa rough ndani ya uke.
Weka akilini kwamba muda wote unapomuingilia mke wako unatakiwa kuwa na movement polepole hatua kwa hatua kama vile unawasha moto ili aweze kupata feeling kwenye ngozi yake.
Hivyo hata kama ni ile ya Quickie au whole night mwanaume kumbuka kuwa passionate na loving huku ukiwa na self control kuhakikisha skin on skin ipo tender.

Iangalie sex kama riadha kwa kuanza polepole na baadae unaongeza mwendo kidogo na mwisho mwenda wa kufa mtu na kushinda hizo mbio.
Exception ya hii kanuni ni pale tu mwanamke anapokuwa ana nyege kuliko kawaida na ana ugulia kwa hamu au kiu ya sex hivyo inabidi amalizwe kiu haraka iwezekanavyo.

PEMBE YA KUINGILIA
Angle muhimu kwa ajili ya kumpa raha na ridhiko katika kiwango cha juu kwa mwanamke kwanza ni muhimu kwa uume kucheza kiasi cha inches 1-1/2 hadi 2 ndani ya uke.
Pia fikiria mke wako amelala chali na wewe unamwangalia akiwa mbele yako na ukachukua saa na kuiweka juu ya uke wake basi pale inaonesha 12 (12 o'clock) ndipo kwenye vaginal orgasmic trigger.

Ili kumsisimua kiwango kinachotakiwa unahitaji ufahamu wa hili eneo na pia angle ambayo mwanaume anatakiwa thrusting.
Ndiyo maana love making position nzuri ni ‘Doggy Style', huu mlalo ni fantastic kwa sababu
Kwanza mwanaume anapofanya thrusting uume hugusa moja kwa moja kwenye vaginal trigger (G-spot)
Pili huwaruhusu mwanamke na mwanaume huwa huru kujielekeza kule kunasisimua zaidi, pia mwanamke anaweza kusaidiana na mwanaume kuwa na movement za mzunguko kwa mwanamke kuzungusha kiuno (hips) kutoka upande wowote chini, juu, pembeni au vyovyote anataka.
Tatu kunakuwa na uwezo wa kuthibiti kiasi gani uume uingie.

Faida kubwa ya face to face ni kwamba inakuwa rahisi kwa mke na mume kubusiana na hii ni factor ambayo inatakiwa isichukuliwe kwa mzaha hasa pale anataka kufika kileleni.

KINA
kichwa cha uume hakikuumbwa kwa ajili ya kuweza kuingia kirahisi au kwa ajili ya mwanaume kufurahia sex bali kwa ajili ya kumuwezesha mwanamke kufurahia tendo la ndoa (awe crazy).

Hivyo basi kuingia kwako ndani yake kunatakiwa kuwa kitu kizuri kwake kujisikia.
Kuna baadhi ya wanawake huwa ngumu sana kufika kileleni kwa uke kusuguliwa na uume hata hivyo kama mwanaume anajua namna ya kutumia tool yake basi anaweza kuondoa hivyo vaginal climax barrier.

Kuanza kwa strokes za kwanza very slowly na shallowly!
Hii husaidia kwani mwanamke huhitaji kuingiliwa slowly, tenderly kama ua linavyofunguka asubuhi wakati wa kiangazi.
Kufungua kwa haraka huweza kusababisha ua kukauka (wilt)
Kuwa na haraka kuingia huweza kumuumiza hivyo kabla ya kuiingia ni vizuri kutumia kichwa cha uume kusugua polepole eneo zima kuanzia juu kwenye kisimi hadi urefu wote wa uke kwa nje.
Waingereza huita ni style ya “Sausage & Bun" au nah ii ipo designed kwa ajili ya kuwafikisha keleleni wanawake ambao hufika kileleni kwa njia ya kisimi tu.

Baada ya hapo unaweza kuwa na penetration ndani kidogo hata kama anakuomba uingie zaidi kwani wewe ndiye kiranja wa hicho kipindi si yeye.

Polepole ongeza kuingia ndani hadi mwisho na hapo unaweza kuongeza speed kwa kadri unavyojisikia na bila kusahau skills za kujizuia usimalize mapema.

Ukihisi anataka kufika kileleni unaweza kupunguza moto au kuchochea zaidi in full speed huku ukiwa na movement za aina tofauti.

EPUKE HAWA,UNAPOTAFUTA MWENZI WA MAISHA YAKO.

Nyumba ikijengwa kwa msingi imara huweza kusisimama kila aina ya dhoruba, hata suala la mahusiano ni kitu kilekile ukijichanganya wakati wa kutafuta mchumba utaishia kwenye ndoa inayochanganya.
Hata hivyo ni muhimu sana kuwa makini na ishara ambazo unaziona kwa yule unaamini anaweza kuwa mke au mume baadae.

Je, yafuatayo ni sehemu ya maisha yake?

Msumbufu:
Anasumbua ingawa ana kazi nzuri.
Jinsi mtu anavyokufanya ujisikie ukiwa naye ni muhimu mara mia kuliko vile asivyokuonyesha ukiwa naye.
Hii ina maana kama ni msumbufu itafika mahali utamchoka hata kama ana kazi nzuri.

Mficha vitu:
Ingawa umekuwa naye kwa muda mrefu lakini unajiona humfahamu yeye halisi.
Anakuficha mambo mengi kuhusu yeye na kila kitu kuhusu yeye.
Anayefaa anakuwa wazi, anakushirikisha mambo mazuri na mambo mabaya yanayotokea katika maisha yake.
Anakwambia vitu vinavyomhusu yeye mwenyewe bila wewe kuchunguza.

Ahadi tupu:
Anaendelea kukuahidi na kukuahidi kwamba atafanya hivi na vile, ila ukimuuliza ni kwanini hatimizi anatoa sababu zaidi ya mia moja na moja.
Anakuahidi kukununulia gari wakati yeye mwenyewe anatunzwa.
Anakuahidi kukutafutia kazi wakati yeye mwenyewe hana kazi.
Ipo siku hasira na kukatishwa tamaa kutakufanya ujute.
Kumbuka anayefaa anatimiza ahadi zake na anayetimiza kile anasema na kuahidi anafaa zaidi kuliko yule wa maneno matupu na asiye timiza ahadi zake.

Mtu wa kupenda sifa:
Kawaida mtu mwenye hekima na busara husifiwa na wenzake na asiye na busara (mjinga) hujisifu mwenyewe.
Matokeo ya kujipa sifa mwenyewe inafika mahali anadharauliwa na kuonekana mtu mdogo sana asiye na maana.

Mtu wa kulaumu:
Kila kitu kibaya kikitokea anakulaumu wewe; mtu wa aina hii hajui responsibility ni kitu gani.
Hata kama ni yeye amefanya makosa atapindisha ili uonekane wewe ndiye uliyekosa.
Hupenda kulaumu kila kitu kama vile chakula, ndugu, marafiki, hali ya hewa, Rais, Boss wake, jua, baridi, mvua nk.

Mwongo:
Kama ameweza kukudanganya jambo kubwa, basi ujue upo na mtu ambaye hushughulikia mambo makubwa kwa kudanganya.

USIACHE HASIRA ZIKAJAA..

Kutoweza thibiti hasira husababisha kutokuelewana katika ndoa.
Kila mwanandoa anahitaji kuwa makini na hasira zake ambazo wakati mwingine hupelekea kuwa mtu wa kukefyakefya, mtu wa vijembe na kejeli, pia mtu wa kulaumu kila wakati na vitu kama hivi ni moja ya alama kuonesha kwamba ndoa imeanza kuchimbika.

Tunahitaji constructive ways za ku handle hasira katika ndoa.

Siku zote binadamu hupenda ku-fight back, kitu kidogo huwa issue kubwa kabisa hata hivyo mtu mwenye busara anafahamu fika kwamba kusamehe na kusahau nia kuishi katika mapatano ni sehemu ya gharama ya amani na upendo katika ndoa imara.

Mwanamke mwenye busara husema:-
"Ingawa mume wangu hutupa nguo na soksi huko na huko anapobadilisha namuona ni mume mzuri kwani ananijali, who care! Kama ananitimizia mengine mengi tu hili ni kitu gani linisumbue!"

Mwanaume mwenye busara husema:-
"Hata kama mke wangu hapendi kusafisha nyumba mara kwa mara hivyo jinsi anavyopika chakula kitamu na alivyo mwema kwangu ninampenda na ninaridhika na ndoa yangu".

Ingekuwa wengine kwa matatizo yaliyoelezwa hapo juu basi ingekuwa shughuli nzito kwani wanandoa wengi huangalia negatives badala ya positives na ukweli ni kwamba ukiwa unaangalia negatives maana yake unaweka sumu katika mahusiano yako.

Kumbuka mke na mume wanapoanza kuzozana ni kama kutoboa matundu kwenye bwawa na baada ya muda bwawa zima hupasuka na kutoa maji ya fujo hivyo kuhimilia hasira ni jambo la msingi.

Pia si busara sana kusubiri hasira zijazane kwani itafika mahali intensity itakuwa kubwa sana na mkaanza kulipuana kama mabomu.


Kama ikitokea mnabishana kwa ajili ya kitu chochote si vema kumwambia mke wako au mume wako “hoja yako ni rubbish”
Uwe makini na kile unaongea ukiwa na hasira

Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.
Mithali 15:1-2

JE,IPI NI NZURI..NDEFU au NENE?

Je, urefu wa uume ni suala muhimu kwa mwanamke kuridhika kimapenzi?

Hii ni imani potofu ambayo imewafanya wanaume wengi kujiingiza kufanya surgery za gharama kubwa na wengine kupoteza pesa zao kwa ajili ya kutafuta dawa za kienyeji ili kuongeza maumbile kuwa marefu zaidi.
Huko ni kupoteza muda na pesa.

Ingawa urefu wa uume hauna umuhimu kama imani potofu inavyodai bado suala la msingi ni uimara wa misuli ya uume; kwani misuli ya uume ikiwa imara basi mwanaume huwa na uwezo ambayo itaweza kumpa sifa mume kwa mke wake kuliko kushabikia kuwa na jumbo size.
Hii ina maana bila kujali una urefu kiasi gani au ufupi kiasi gani, kama una misuli imara hilo ndilo jambo la msingi kwa mwanaume.

Tuweke suala la hiyo imani potofu pembeni hivi ni kitu gani mwanamke huhitaji physically ili afurahie tendo la ndoa?

Suala la muhimu ni kuwa na ufahamu wa anatomy kuhusu mwanamke (uke); ukweli ni kwamba nerves nyingi zipo within inches mbili kutoka mlango wa uke na asilimia kubwa ya nerves zipo katika mzunguko wa mlango wa uke.
Hii ina maana mwanaume yeyote mwenye uume wa inches mbili kama anajua namna ya kumfikisha mke kuridhika au kufika kileleni kupitia uke (vaginal climax) basi ataweza kumfikisha mke wake kileleni.

Je, unene wa uume huweza kumridhisha mwanamke kimapenzi?

Ni kweli unene unaweza kuwa ni factor hasa kutokana na uwezo wa mwanamke alionao kukaza misuli ya uke.

Je mwanamke ana umri gani, amekuwa na partners kiasi gani na amezaa watoto wangapi na zaidi amefanya kitu gani kuhakikisha misuli yake (uke) inakuwa imara.

Bahati mbaya ni kwamba tamaduni nyingi za Africa, ulaya na Amerika hazina mazoea ya kuwa na mazoezi ya kukaza misuli ya uke au uume.

Hivyo thickness ni muhimu kwa mwanamke ambaye uke wake ni loose na weak pia kama misuli yake ipo hoi.

Je, inakuwaje kama mwanaume ana uume mkubwa (unene na urefu) zaidi ya wastani ambao wanaume wengi huwa?

Tafiti nyingi zinaonesha wanawake wengi hulalamika pale mwanaume anapokuwa na uume mkubwa zaidi ya kawaida na hasa kama hajui namna ya kuutumia.
Wanawake wengi huona ni huge barrier kwa ajili ya ku-enjoy sex kama mke na mume na wakati mwingine mwanamke hujisikia uncomfortable na huishia kukwepa.
Pia wanaume wenyewe ambao wana uume mkubwa tafiti zinaonesha kwamba wengi hujikuta katika huzuni na wanaombolezo kwa sababu partners wao kujisikia maumivu na kuumia na hata imesababisha mahusiano ya kimapenzi kati ya mke na mume kuzolota.

Je, hutokea nini pale mwanaume mwenye jumbo size akakutana na mwanamke mwenye uke uliobana?

Na wanaume ambao ukubwa wa uume ni zaidi ya kawaida wanapokutana na mwanamke ambaye ana size ndogo ya uke, au hakuwa wet sawasawa au hajazaa mtoto kabisa au bikira suala la sex linakuwa shughuli nzito kuihimili kwani lazima mwanamke akubaliane na pressure na pain za kuta za uke zinapochanwa.

Na pia kama mwanaume ana urefu unaozidi inches 6 ambayo ni average size kwa wanaume basi mwanamke anaweza kujikuta anajuta kwani anaweza kuhisi mwanaume anagonga hadi kwenye kizazi (internal reproductive organs).
Na matokeo yake mwanamke hujikuta anakaribisha magonjwa kama cysts ambayo huhitaji surgery na pia huweza kupata infections ambazo huweza kusababisha kukosa watoto.


Nini kifanyike?
Jambo la msingi ni kwa mwanaume kufahamu namna ya kutumia tool yake vizuri, hii ni pamoja na kuwa caring, kufanya maandalizi ya kutosha.

Je, nini faida ya kuwa na uume mkubwa au uume mdogo?

Kama mwanamke ana uke ambao ni loose na hawezi kuthibiti mwendo (misuli imelegea) basi tool kubwa kama hiyo huweza kumsaidia kupata feelings za kufurahia mapenzi hapa haijalishi mwanaume ana skills zozote au la.
Na mwanaume ambaye ana uume mdogo kuliko kawaida anaweza kuwa na faida kwa mwanamke ambaye ana uke mdogo (tight).

Hii ina maana mwanaume mwenye uume mkubwa ana match na mwanamke mwenye uke loose na hii combination huwezesha hao wawili kuwa na ridhiko kimapenzi.
Na mwanaume mwenye umbile dogo ana match na mwanamke mwenye uke tight.

UPENDO KATIKA NDOA.

Mapenzi katika ndoa huweza kugawanywa katika sehemu mbili yaani upendo wa ndani (internal) na upendo wa nje (external).

Tunapozungumzia upendo wa ndani tuna maana jinsi tunavyoonesha katika emotions kama vile tendo la ndoa, kuwa pamoja karibu, pamoja kimawazo, kujieleza katika feelings, maneno matamu yanayoonesha kujali na kupenda, kupeana busu, kukumbatiana, kupeana zawadi nk.

Tunapozungumzia upendo wa nje huu hujikita zaidi katika huduma kama vile kupika chakula, kuzaa watoto, kujenga au kukarabati nyumba, kufua nguo, kupiga pasi nguo, kuogesha watoto na kazi (ajira) ambazo zinatupa vipato.

Hapo zamani (mababu na mabibi) wao upendo external ulikuwa na maana zaidi kuliko internal na kizazi cha leo ni kinyume chake.

Ndiyo maana ni rahisi sana leo kuishi kama mke na mume zaidi ya miaka miwili na ikafika siku mke au mume akamuuliza mwenzake
“je, unanipenda?”
Hata kama wamefanikiwa kujenga nyumba au kuwa na gari au familia na maisha mazuri kwa ujumla.

Kuuliza je, unanipenda ina maana something is wrong kwenye upendo wa ndani (internal) inawezekana ni tendo la ndoa au ukaribu kimapenzi au maneno ya kutia moyo na sifa kimoja au vyote havipo sawa.

Leo wanawake wanategemea sana mume alete zawadi kuliko kuleta mkate.
Mke anataka mwanaume ambaye anaongea maneno matamu na si anayefanya kazi nzuri tu.

Mwanaume kiasili ni bread winner na anapenda mke atambue kwamba kwa kazi anayofanya maana yake anampenda mke na familia sasa baada ya kazi kutwa nzima na kurudi nyumbani na mkate na mke akamuuliza
“Je, Unanipenda?"
Eti kwa sababu asubuhi wakati anaondoka hakuaga kwa busu na hug kwa mwanaume bado ni kitu kinachoshangaza.

Hata hivyo industrial revolution imeleta mabadiliko ambayo wanaume na wanawake wote sasa wanafanya kazi (mchanganyo wa duties na responsibilities za mke na mume) na leo tupo kwenye information society kwa maana kwamba information zina flow ajabu na kila mwanandoa anataka Mapenzi (romance/intimacy) bila kujali sana kazi anayefanya mwenzake.

Je, siri ya ndoa imara ni ipi?

Siri ya ndoa iliyobarikiwa na imara ni ile inayohakikisha upendo wa ndani (internal) unaenda sawa na ule wa nje (external), ni ile ndoa ambayo inachanganya tendo la ndoa na majukumu kuwa kitu kimoja na kukipa nafasi sawa.

Mwanandoa halisi ni yule ambaye leo anaweza kumsaidia mwenzake anayeumwa kwa kufuta matapishi yake na baadae akaendelea kumpa kisses za kutosha.

Mke halisi ni yule anayeweza kuwa mama mchana na kuwa mpenzi usiku chumbani na kumfurahia mume wake kimapenzi kwa kwenda mbele.
Ndoa iliyo imara ni ile ambaye wanandoa ni waaminifu katika kutekeleza uhitaji wa ndani na nje katika ndoa.