Monday, 11 July 2016

WANATOFAUTIANA KTK SUALA LA KUFIKA KILELENI.


*Je, kufika kileleni kwa mwanamke anapofanya mapenzi ni tofauti na mwanaume?

Tafiti nyingi zimefanyika na mojawapo ni ile iliyoruhusu Wanawake na wanaume wote kuandika vile wanajisikia wanapofika kileleni na baadae wakaruhusu watu wengine wasome na wapendekeze nani ameandika kati ya mwanamke au mwanaume hata hivyo ilikuwa vigumu kwa wasomaji kufahamu maelezo yaliyoandikwa yameandikwa na mwanaume au mwanamke.
Hii ina maana kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke huhusisha uzoefu unaofanana.
Hata hivyo kuna tofauti ya uzoefu wa kufika kileleni kwa Wanawake na hata mwanamke mmoja na hii tofauti hutokana na aina ya kusisimuliwa ili kufika kileleni kuanzia kisimi, uke, G-spot, matiti n.k

*Je, ni kweli kwamba kinachomfikisha kileleni mwanamke huyu ni tofauti na mwanamke yule?


Ni kweli, na pia hata mwanamke huyo mmoja kinachomfanya asisimuliwe kufika kileleni leo ni tofauti na wiki ijayo na mwezi ujao na hata miaka matano au kumi ijayo.
Wapo wanaopenda kusisimuliwa G-spot na wengine hawataki, wapo wanaopenda kusisimuliwa kisimi wengine hakuna lolote, wapo wanaopenda kusisimuliwa uke na wengine hawataki. Wengine matiti au masikio au shingo nk kila mmoja au hata huyo mmoja uliyenaye anatofautiana kutokana na mzunguko wake wa siku kwa mwezi.
Kama tunavyopenda vyakula tofauti na nguo tofauti na usisimuliwe wapi kwa mwanamke kufika kileleni ni tofauti.
Kuamini kwamba kumsisimua mwanamke Mahali fulani ndipo huweza kumfikisha kileleni bila kuwasiliana naye wakati mwingine huweza kuwa kero.

*Je, mazoezi ya kukaza misuli ya uke huweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kufika kileleni kirahisi?

Mazoezi hayo ni muhimu mno. Uwezo na uimara wa misuli ya PC (puboccoccygeus) unahusiana mno na mwanamke kufika au kufurahia tendo la ndoa.
Wanawake ambao hawawezi kufika kileleni kirahisi wana misuli ya PC iliyodhaifu (loose).
Mwanamke anayeweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa kisimi ana misuli imara hata hivyo mwenye misuli imara zaidi ni yule anayeweza kufika kileleni kirahisi kwa uke wake.


Wanawake huwa na tofauti za kufika kileleni kutokana na aina ya kusisimuliwa pamoja na sababu zingine kama vile anavyojisikia huo wakati, na kiwango cha homoni.
Si suala la kubonyeza button na mwanamke akafika kileleni. Kufika kileleni si conditioned reflex.
Mara nyingi lengo la mume katika sex ni kuhakikisha mke anafika kileleni je kuna tatizo kuwa na mtazamo kama huo?
Kawaida tunapozungumzia maisha huwezi kukwepa kuweka malengo.
Linapokuja suala la sex ni kweli kwamba wanaume huwa goal-directed na Wanawake huwa pleasure-directed.
Tatizo huja pale watu wameshindwa kufahamu hiyo siri na hasa wanaposhindwa kuwasiliana na wapenzi wao.
Mwanamke anaweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa sehemu zingine za mwili kama vile masikio nk hivyo bila kuwasiliana inaweza kuleta shida kwani we are all unique.

No comments:

Post a Comment