Baada ya muda katika ndoa kila kitu kinaweza kuwa katika ratiba isiyobadirika, huwa vilevile, routine, predictable, uniform, sare jana juzi, leo na kesho maongezi ni yaleyale, ratiba ya kuwa mwili mmoja ni vilevile hakuna kipya na hakuna raha.
Inawezekana hawa wewe msomaji kile kinachotokea kwenye ndoa yako kinakupa wakati mgumu na unajiuliza hivi nitaishi bila kuridhika kiasi hiki hadi lini.
Hata hivyo kabla hujaanza kumlaumu partner wako ni vizuri ukajiuliza maswali yafuatayo huku ukitafakari kwa undani wewe mwenyewe bila kumnyoshea mwingine kidole
Hivi wakati mnachumbiana (let say dating) ni vitu gani ulikuwa unavifanya ili huyu partner wao aonekane yeye ni special kwako?
Je, hapa karibuni au wiki hii umefanya kitu gani kwa partner wako aonekane yeye ni special?
Je, unakumbuka ni kitu gani na lini mmekuwa pamoja na mmefanya kitu special na mkawa na wakati mzuri nje ya hapo nyumbani mnapoishi?
Je, ni mara ngapi mnakuwa wote kufanya kile kila mmoja anakifurahia kufanya?
Ukiulizwa utaje vitu vitano ambavyo partner wako anavipenda au anaviona vya maana sana katika maisha yake na kujisikia vizuri katika maisha unaweza kutaja? Na je umehusika vipi kuhakikisha anavipata?
Je, mume wako au mke wako yupo namba ngapi kwenye list yako ya vitu vya thamani duniani?
Haya maswali yakipata majibu yake inaweza kuwa njia sahihi kwako kuanza kutengeneza mahusiano yenye direction mpya kuelekea furaha na amani.
Najua mtu yeyote akikuuliza je, unampenda huyo partner wako jibu utakalo toa ni “ndiyo nampenda” hata hivyo ulivyo busy na kazi na watoto na kazi zingine ni dhahiri kwamba humpendi na kama unampenda basi hujaweka efforts zinazotakiwa.
Ni kweli hivyo vitu ni muhimu sana hata hivyo ndoa ni zaidi ya vyote, hata kama umekuwa unasema nitafanya hivyo karibuni hata hivyo karibuni yako sasa ni mwaka hakuna kitu.
Wakati uliokubalika ni sasa, sasa ni wakati wa kuwekeza kiasi cha kutosha kwa partner wako, na utatakiwa kurekebisha ratiba yako ili partner wako aingizwe kiuhakika katika ratiba yako ngumu.
Ukweli ni kwamba hata watoto hufurahia kuwa na wazazi wanaopendana kuliko wao kufurahia kuchezea gitaa linalotoa sauti nzuri au kufunga goli anapopelekwa na mzazi kucheza soka kuliko wazazi ambao hawapendani ndani ya nyumba.
Ndoa yako ni muhimu sana, na mke wako au mume wako ni muhimu sana kumbuka Mungu aliumba ndoa, kabla ya kazi na kabla ya watoto.
No comments:
Post a Comment