Friday, 4 December 2015

NI KURIDHIKA TU..!

Kuridhika na ndoa huendana na kuridhika kimapenzi hata hivyo suala la kuridhika katika ndoa na kimapenzi ni kama swali la yai na kuku kujiuliza kipi kilitangulia.

Je, kuridhika na ndoa huweza kusaidia kuridhika kimapenzi?

Je, si kuridhika kimapenzi ndiko husababisha kuridhika na ndoa uliyonayo?

Kama mwanandoa mmoja haridhiki kimapenzi katika ndoa hupelekea kujisikia haridhiki na ndoa yenyewe pia kama mwanandoa mmoja haridhiki na ndoa aliyonayo hupelekea kujiona haridhiki na mapenzi katika ndoa.
Hii ina maana kwamba huwezi kuwa na kimoja bila kingine kuwepo.

Mungu ametuamuru kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kumridhisha mke au mume wake kimapenzi na Sayansi nayo inatoa ushahidi kwamba kuna faida kubwa ikiwa wanandoa wataishi maisha ya kuridhishana kimapenzi na hatimaye ndoa yenyewe.

Kama kanisa linaamini talaka ni kitu kibaya na kukaa katika ndoa ni jambo jema basi halina budi kufundisha na kusisitiza kwa nguvu zote au uwezo wote wanandoa kuridhishana kimapenzi kunakopelekea kuridhika katika ndoa zao.

Ni mara ngapi kwa wiki huweza kusababisha kuridhishana katika hisia za mapenzi (sex)?
Mwili wa mwanaume huweza kuzalisha sperms kila baada ya masaa 72 (siku tatu) ndivyo Mungu aliumba.
Mathematically ina maana kwamba tendo la ndoa ni muhimu sana siku 2 au 3 kwa wiki kuweza kufanya connection ya feelings za wanandoa kiroho na kimwili.
Kukiwa na kuridhishana kimapenzi katika ndoa ni ukweli kwamba hata wanandoa wataridhika na ndoa yao kwa ujumla.

Thursday, 3 December 2015

NISIKILIZE KWA MAKINI..!

Kuna aina mbili za wanaume, wa kwanza ni wenye HESHIMA na wa pili ni wale WASIO NA HESHIMA.

Usikubali kuolewa na mwanaume kabla hujafahamu tofauti hizi mbili, mwanamke unayemuona kwenye kioo chako cha kujitazama atakushukuru sana.

Mwanaume mwenye heshima atakulinda, atalinda moyo wako na hisia zako, atasimama imara kulinda kiroho chako na mwili wako, kumchagua mwanaume mwenye heshima ni kuchagua maisha bora katika ndoa.
Wewe mwanamke si gari; Ukikutana na mwanaume anayetaka kukujaribu kama gari, palepale mwelekeze kwa wanaouza magari, mwambie kwa heri na usigeuke nyuma.

Ndiyo umekutana na mwanaume handsome, anaonekana ni mwema, mpole na anaonekana ana akili na shule imekubali na katika kuongea naye anakwambia ana mtoto na hana mpango wa kumtunza wala kumuona mama yake huyo mtoto;
Haraka iwezekanavyo mpeleke kwa mama wa huyo mtoto, USIANGALIE NYUMA anza mbele kwa kasi ya ajabu.
Usifanye kosa lilelile ambalo mama wa mtoto alifanya.
Kwani kuna tofauti gani kati ya mama wa huyo mtoto na wewe, kwa taarifa yako wote ninyi ni wanawake!

Jipende mwenyewe kwanza!
Kama huwezi kujipenda mwenyewe na kufurahia maisha mwenyewe, nakwambia upo off the market; usifanye kosa, kama hujipendi mwenyewe hakuna MWANAUME ANAWEZA KUKUPENDA ...

Usiwahukumu wanaume wote kwa sababu ya kosa la mwanaume mmoja; labda kama unataka wanaume wote wakuhukumu wewe kwa kosa la wanawake wengine wasio na adabu.


Je, unajikuta unawavutia wanaume ambao tabia zao ni mbovu?
Basi jichunguze aina ya perfume unatumia kwani wanaume walio na tabia mbovu huvutiwa na aina ya perfume mwanamke anatumia, serious!


Usijidanganye!
Urembo wako, umbo lako, uwezo wako kitandani, ustadi wa kupika chakula, uwezo wa kutetea wanawake wengine hata haiba yako inayovutia haitaweza kumfanya mwanaume abadilike; Never!

Kama mchumba wako anakuahidi kitu na hatimizi, weka rekodi, ukiona hii tabia inajirudiarudia, inawezekana anacheza na feelings zako, pia ni warning signs kwamba huna thamani yoyote kwake na inawezekana hakupendi na hakujali kabisa, Think twice.

Sawa, umekutana na mwanaume si mume wako anakutaka kimapenzi, huna haja kushangaa, huyo hakuheshimu !

Unajiuliza;
“Kwa nini hanipigii simu, kwa nini hana muda na mimi, kwa nini haoneshi kama ananipenda?”
Jibu ni kwamba ni kweli hana mpango na wewe, na kama hutamwacha aende zake na wewe kuendelea na maisha yako basi unachofanya ni kuzuia mtu wa kweli kuja katika maisha yako na kupata penzi la kweli.


Kuna baadhi ya wanaume hupenda kupiga wake zao haijalishi wamesoma au hawajasoma, wanapesa au hawana pesa, kwani kumpiga mke huwapa sense ya kujisikia kwamba wana power/control, na ukijipeleka mwenyewe kwa wanaume kama hawa wanaweza kukufanya wewe ni punching bag.
Ni muhimu sana ukiwafahamu tangu mapema ili uwaepuke.

IKIWAKA MULIKA

KUBADILI JINA BAADA YA KUOLEWA.

Hivi karibuni kumekuwa na kujiuliza kwingi kwa akina dada ambao wanatarajiwa kuolewa kama anaweza kubadilisha jina la ukoo na kulichukua lile la mume wake.
Wengi wamejikuta wakifanya huku hawajafahamu maana au kwa nini wanachukua hatua kama hiyo hata hivyo ni vizuri kufanya jambo ambalo una uhakika na ufahamu wa kutosha kuliko kufuata tu traditions na taratibu ambazo ni kama kufuata mkumbo.

Pia kuna maswali kwamba je, kubadilisha jina baada ya kuolewa ni suala la kibiblia au ni mapokeo tu na zaidi kwa nini wanaobadili majina ni wanawake na si wanaume.

Je, kubadili jina nyakati za leo kuna manufaa yoyote kimaadili na kiimani?

Wanaharakati wa mambo ya wanawake. wanasema haina haja kubadili jina maana mwanamke anapoteza identity yake na kila kukicha wanawake wanaoolewa kwa hiari yao huamua kubadilisha majina yako na kuendelea kufurahia maisha ya ndoa na waume zao wapya.

Kwa nini anayebadilisha jina ni mwanamke na si mwanaume?

Traditions ambazo ni biblical zinaonesha kwamba kwanza Adamu aliumbwa ndipo Eva (Hawa) na Eva alitoka katika ubavu wa Adamu.
Adamu na Eva baada ya kuunganishwa wamekuwa mume na mke yaani mwili mmoja (one couple).
Mungu amewaunganisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kufanya kitu kimoja na mke ndiye amemfuata mume (kipande cha ubavu kilichotolewa ili kumuumba Eva) kuwa kitu kimoja kupitia agano la ndoa.
Mbele za Mungu wanandoa wawili mke na mume huwa ni kiumbe kipya kimoja kinachoitwa ndoa moja, hii ina maana kwamba ingawa mwanaume mmoja ambaye hajaoa huonekana ni mtu mzima kiroho bado huwa nusu na huhitaji kuunganishwa na nusu nyingine ya mwanamke kufanya kitu kimoja yaani ndoa.
Mwanaume huwa hajakamilika hadi anapooa na mwanamke huwa hajakamilika hadi aolewe.
Mwanamke kuchukua jina la mume ni kuipa heshima ndoa na kudhihirisha kuwa kitu kimoja kipya kimezaliwa.
Mke anapoolewa hudhihirisha kwa ulimwengu kuwa amepata identity mpya na anatambua uumbaji wa kimungu kupitia ndoa.
Baada ya kuolewa anaingia kwenye agano jipya kati ya mke na mume na Mungu.

Wednesday, 2 December 2015

NI MUHIMU KUCHUNGUZA KWANZA.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.
Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.

Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.

Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.

Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!

Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).

Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja.

Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia. Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa,

Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!

Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!

EPUKA KUJISAHAU.

Ili ufurahi kuwa mwili mmoja maandalizi hayaanzii chumbani bali huanza tangu asubuhi unavyoamka na yote unafanya siku nzima (communication) na mume wako au mke wako huweza kuongeza hamu na pia kujikuta mpo connected na hatimaye kuwa na usiku wenye raha.

Mbusu wakati unaondoka asubuhi au mnaagana kila mmoja kwenda na kupambana na shughuli za maisha na familia.
Mpigie simu au text au email mchana kwamba una mkumbuka na mwambie kitu chochote kizuri kuhusu yeye.

Hata hivyo kuna mambo madogo lakini muhimu sana ambayo kila mwanandoa ni muhimu kukumbuka ili kuhakikisha akitaka kuwa mwili mmoja na mwenzake mambo yanakuwa motomoto,

Kwanza, kama mke wako (kama wewe ni mwanaume) umeona analalamika kwamba huwa unamshika/mpapasa/gusa/chezea (touch), busu pale tu ukitaka kuwa mwili mmoja na sivinginevyo basi wewe unafanya makosa makubwa sana na unamnyima haki yake ya kuzaliwa ya kupewa non sexual touch.

Pili, kumbuka kukiwa na non sexual touch nyingi zinafumfanya mwili wako kujisikia vizuri na hupeleka feelings hadi moyoni mwake kwamba kuna mtu anamjali na kumbuka pia kuna wanawake touching ndiyo ugonjwa wao so ukimpatia kwako itakuwa paradise kila siku.
Jitahidi angalau gusa bega lake, mshike mikono, mkumbatie nk.

Tatu, watu 100 waliambiwa waandike vitu ambavyo husababisha kuwa turned off na wake zai au waume zao, asilimia 99 waliandika kwamba mwonekano mbaya ni sababu mojawapo.
Usijidanganye eti hata nikivaa ovyo kama ananipenda atanipenda tu, Pole sana anaweza kukupenda lakini asitamani kuwa mwili mmoja na wewe kwani upo rough, mchafu, unanuka, huvutii na mzembe na hufai kabisa.

Nne, kunukia vizuri ni moja ya sifa za kwamba upo sexy.
Ukinukia vizuri mume wako au mke wako anatamani kuwa karibu na wewe na kunuka ni kinyume chake, hata ulalamike na ukajitahidi kumpeleka kisimani kunywa maji hanywi.
Ukiwa na majasho na hujaoga unafunika homoni za pheromones ambazo huvutia na kuwafanya wanaopendana kuwa na bond imara.
Hivyo smell good!

Tano, uwe mzuri na maridadi kwenye mawasiliano hasa kama wewe ni mwanaume, mke wako anaporudi kazini au jioni anapoongea kuhusu yale amekutana nayo siku nzima msikilize na uwe pamoja naye kuhakikisha anaongea maneno yako yote huku ukimsikiliza na ajue unamsikiliza na upo makini na unapenda kumsikiliza kwa njia hiyo unafungua hisia zake na anakuwa open kukuruhusu baada ya mda ufurahia mwili wake.

Thursday, 26 November 2015

KUFIKA KILELENI.

Si utundu na ujanja wa mwanaume tu unaomwezesha mwanamke kupata utamu wa kufika kileleni bali mwanamke pia anahusika.

KUFIKA KILELENI NI NINI?

Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.
Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii

Wengine wakifika kileleni hupiga kelele sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao, wengine hutulia kimya na kupitiliza usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa wananamwona Bwana n.k ilimradi tu ni raha na utamu na ni kweli Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba tena kwa namna ya ajabu.
Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming n.k
Pia wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.

Je mwanaume na mwanamke wote hufika kileleni sawa?

Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic, halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.

Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.

Nini Kitu muhimu kuhsu mwanamke kufika kileleni?
Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke hadi anahitimisha tendo zima angalau kwa dakika 10 au 15 ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye mataa akiugulia kwa kumuondolea utamu na raha.

Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
Lakini pia mwanamke anasehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.

Monday, 23 November 2015

UNENE HUPUNGUZA UUME.

Imethibitika kwamba mwanaume anavyozidi kunenepa uume huliwa na fat na kupungua urefu.
Habari njema ni kwamba kama wewe ni mwanaume overweight (fat) au mnene kupindukia unaweza kuongeza inchi moja ya uume wako kwa kupunguza unene kwa kila pound 35.

Kama umekuwa ni overweight kwa miaka yako yote basi hii ni kumaanisha kwamba hajawahi fikia urefu halisi wa uume wako.
Kama ni mwanamke na mume wako anazidi kunenepeana usishangae siku unaanza kutafuta samaki wake kumbe kaliwa na fat au nyama zembe hivyo saidiana naye kupunguza fat ili abaki na size yake kama kawaida.
Siyo utani wala kichekesho ni kweli unavyozidi kunenepa (hapa nazungumzia unene unaozidi kawaida) ndivyo unavyozidi kupunguza urefu wa uume.