Saturday, 31 January 2015

SABABU HIZI ZINAWEZA KUSABABISHA KUACHIKA KWENYE MAPENZI.

KUPENDA SANA AU KUMGANDA MTU;

Kwenye mahusiano
mmojawapo anapokuwa anaelekea kumpenda mwenzake sana na kumganda husababisha mmoja wapo kumchoka mwenzake. Wote mkiwa kwenye mahusiano pendaneni sawa ili kutopelekea kuchokana.
Kukata tamaa kwenye mahusiano: Unapoonyesha namna ya kukata tamaa kwenye mahusiano au hali ya kusikiliza ya watu ni rahisi kupelekea mahusiano kuvunjiaka. Wengi kwenye mahusiano wanakaa kufikiria kuwa hadi kwenye ndoa. Hivyo unapokuwa na hali ya kukata tamaa kutokana na mazingira ni dhahiri kupelekea kuona bora mahusiano yaishe.
Kuwa mkali kwenye mahusiano: Hii ikiwa inawahusu zaidi wavulana/Wanaume wenye tabia hii kuwa kutokujali hali y ampenzi wako na kuwa mkali kwenye mahusiano. Kuto thamini kila hali ya shida au udhaifu wa mpenzi wako. Pia kuna wasichana/Wanawake ambao huwa na hali hii.

UTOTO KWENYE MAPENZI. Hakuna masichana anayependa mvulana ambaye ana tabia za kitoto. Kama mvulana ukiwa na tabia za kitoto kama kuto kujiheshimu au kuwa mchafu kama mtoto inapelekea kupunguza mapenzi na hata kuachika.
Mavazi na Muonekano: Hakuna mtu ambaye ni mabaya, Ila unaweza kujiona ni mbaya kutokana na muonekano wako wa mavazi na unavyo ishi. Ni vyema kujiweka nadhifu kwenye mavazi ili kuto hatarisha penzi lako.
Uchafu wa Kucha na Vidole: Shughuli unazozifanya zinaweza zikawa ni zakuchafuka ila nivyema kuhakikisha baada ya hapo unaweka vidole vyako nadhifu na visafi. Kuwa makini kuzitunza kucha maana nimahususi kwenye kuamsha hisia za ngono. Hivyo unapokuwa mchafu wa kucha na vidole mpenzi wako anaweza kuku acha na kama ni wakike, mvulana kuogopa hata chakula chako.

KUONYESHA HISIA.
Kuwa na muonekano wa hisia za kumpenda mpenzi wako ni muhimu na unaposhindwa unahatarisha mahusiano yako hata kama unampenda.
Tamaa: Kwenye mahusiano jiepushe kuwa na tamaa ya vitu vingi. Kuwa na kiasi sio kila unachokiona au kukisikia basi uhitaji. Mpenzi wako atakuona unamchuna na kukuchoka mwishowe kukutupilia mbali.

MIZOZO YA MARA KWA MARA.
Unapokuwa na mzozo au kila mara kugomba na kumpiga mpenzi wako ni dhahiri hata kama unampenda atakuwa hana uhitaji kwako tena. Jiepusha kuwa na mzozo hata kama mwenzio amekosea mrekebishe taratibu.
Heshima kwenye mapenzi ni kitu muhimu, Haijalishi hali aliyonayo. Nidhamu ni jambo linaloweza kukufikishia malengo yenu.

ZIJUE DALILI ZA UJAUZITO.

Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana
Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.
Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:
>Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
>Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
>Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
>Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
>Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
>Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
>Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya kichwa
>Kizunguzungu
>Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
>Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
>Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
>Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
>Tumbo kujaa au kuvimbiwa
>Kununa na kukasirika haraka
>Kiungulila au kupata choo kigumu
>Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
>Kuongezeka uzito
>Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
>Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
>Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign
>Dalili nyingine ni pamoja na
>Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
>Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
>Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
>Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
>Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto

MAMBO MUHIMU YANAYOMSHAWISHI NA KUMPA RAHA MWANAMKE KUFANYA NGONO.

Leo tuzitazame dalili za mwanamke anapotaka ngono.

Kwanza kabisa nikujulishe kuwa kitaalam mwanaume huwa anawaza ngono kila baada ya sekunde sita huku akiwaza mahala pa kufanyia tendo hilo wakati mwanamke huwaza ngono kila baada ya sekunde tisa na akikubali kuvua nguo ni lazima awe na sababu za msingi.

‘’Mimi sijisikii kufanya mapenzi’’ hii ni moja kati ya kauli ambazo wanaume huambiwa na ukisikia hivyo ujue si peke yako unayeambiwa hivyo na hii ni kauli inayolalamikiwa sana na wanaume wengi ambapo baadhi yao wamediriki hata kuchepuka wakidhani wenzi wao wamewachoka.

Wanawake wanapagawa na huhitaji kufanya mapenzi kuliko wanaume wengi wanavyodhani na ukijua mazingira hayo hautamwacha mwanamke wako,naye hatatamani mwingine kwasababu wanawake wanajieleza wazi kuwa katika mazingira nitakayoyataja hapa chini yakifuatwa wanajisikia raha mno…

1.      Mfurahishe
Hali yeyote ya furaha kupita kiasi inamfanya mwanamke kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufanya mapenzi bila kizuizi chochote.

2.     Baada ya kuzozana
Kugombana ninakozungumzia hapa ni kule kwa pande mbili mnakwazana na baadaye kila upande ukatoa dukuduku zake hata kama kwa kufikishana kwa wakubwa kwa nia ya kupata muhafaka na baada ya hapo hakuna kitu kizuri cha kubadilisha upepo huo zaidi ya kukumbatiana, kubusiana kwa huba huku mkiziamsha hisia zenu.

Ukiona hata kama mwanamke wako analia au ameghafirika kwelikweli, mwache anyamaze au mnyamazishe huku ukimbembeleza hata kumfuta machozi kisha …….hapo tatizo linaisha na wakati huo wote kwa pamoja mtafurahia tendo hilo.

3.     Siku ya 14 (Heat Period)
Wataalam husema kuwa hiki ni kipindi cha joto kwa mwanamke, ni kipindi cha aina yake katika mahusiano ambapo mwanamke anakuwa na hisia nyingi wakati mayai yanapotungwa.

Hivyo zikiwa zimepita wiki tatu baada ya kumaliza Afya yake ya ‘’uchinjaji kisha damu kukauka’’ wakati huu ni muhafaka kufanya mapenzi na hata kama mwanaume ni mbishi kiasi gani au umechoka mwanamke atakuamsha na kukutega na mara nyingine atakueleza kuwa anataka.

4.     Mapenzi ya Mbali.
Mapenzi ya mbali yanaweza kuwafanya mkawa na maisha yasiyokuwa na migogoro ya mara kwa mara huku kila mmoja akiwa anamtamani mwenzake na kitu pekee kwa wakati huu wa utandawazi kinachoweza kuwaunganisha zaidi ni simu na internet.

Mkikutana siku hiyo kila mmoja anamtamani mwenzake na kama ni asubuhi mtaona siku haiendi haraka hasa kwa wale wenye familia na kama mtakuwa wawili katika chumba ama nyumba hiyo aaaaaaahhhhh hiyo niwape hongera kwasababu hamtakawia hata sebuleni.......

5.     Wivu
Ninachozungumzia hapa si ule wivu wa kijinga bali nazungumzia wivu wa mwanamke anayejitambua na kujiamini kuwa anamtii, kumnyenyekea na kumshauri kwa hekima mwanaume wake lakini anapata wivu anapoona mwanaume huyo yupo na mwanamke mwingine hata kama si katika mahusiano. Si unajua kila mtu ana moyo wa nyama? Hasa ukipenda, weeeeeee acha tu!

Mwanamke anapoona mwanaume wake ananyemelewa na mwanamke mwingine na kumshawishi kimapenzi huona wivu sana na wanawake wanaojitambua badala ya kufoka huamua kuwaonyeshea wanaume wao kitandani kwa kuwapa mapenzi motomoto huku wakionyesha stahili na kuonyesha kujiamini kuwa ni wazuri kila upande yaani sura, maumbile na hata kitandani kuliko wale wanaomnyemelea.

Hapa siruhusu wanaume kuwa vicheche ama kuambatana na wanawake wengine bila sababu eti tu unataka mwanamke wako akuonee wivu hapana hii ni mbinu ya kuotea maana kumrusha roho mtoto wa mwanaume mwenzako si vema.

6.     Mwanamke kujinyima
Kadri mwanamke anavyozidi kukaa muda mrefu bila kufanya usodoma na ugomora, ndivyo anazidi kupata ashki ‘’Nyege’’ na mwanaume unapompata mwanamke aliyekaa muda mrefu hakika utafaidi na yeye pia atakuweka kwenye historia maana atajisikia raha sana baada ya tendo hilo.

Na mwanamke wa namna hii haitoshi kuwa mmefanya tendo la ndoa siku moja huyu atahitaji walau siku mbili vinginevyo ukimwacha atachepuka ingawa ni wachache wanaoamua kufa kisabuni na kuamua kutumia maji ya moto kujikanda.

7.     Mawazo
Mwanamke ambaye amekuwa na mawazo kwa muda mrefu akihitaji faraja na akakosa hatimaye Mungu na malaika wake wakamwangazia nuru na kujikuta mikononi mwa mwanaume anayeweza kumpa mapenzi yatakayomfariji hakika mwanamke hufurahia tendo hilo ambalo anahisi linakata kiu yake na kushusha pumzi.

8.     Mbunifu wa Mazingira
Wanaume wengi wanawanyima uhuru wa mazingira wanawake zao huku wakihoji ‘’ameyapata wapi haya’’ nakushindwa kujua kuwa huo ni moja ya mtego wa kutaka mapenzi.

Mwanamke anaweza kukutaka mfanye mapenzi jikoni, bafuni, sebuleni kwenye kiti au popote pale na kama amekupagawisha vizuri katika penzi la jikoni kuna siku mnaweza kujikuta mkiacha chakula kikiungulia huku nyie mkiwa mnatoa jasho la Afya na hapo mwanamke atafurahi kwasababu mtego wake wa kwale haujanasa chui.

9.     Muziki na Kinywaji
Kucheza muziki na wengine wale ambao wanapata kidogo kinywaji ni moja ya mambo ambayo yanasisimua mwili na kuamsha hisia za mahaba kwa mwanamke.

Hapa kwa mwanaume unaweza kumchukua mwanamke wako na kwenda naye kwenye kumbi za muziki.

Wakati mnacheza jaribu kugusana ama kupapasana taratibu hapo mwanamke yeyote mradi akikubali kupapaswa, mambo yanakuwa si mambo.

Thursday, 29 January 2015

NJIA MUHIMU ZA KUSAFISHA UKE.

Awali nilikuwa nikidhani kuwa kila mwanamke anapaswa na anafahamu jinsi ya kujisafisha ndani ya uke mara tu baada ya kuondolewa bikira (kuanza mahusiano ya kimapenzi na hatimae ngono), lakini nimekuja kugundua ukweli kwamba wanawake wengi hawajui uke unasafishwa vipi?
Baadhi huofia kuwashwa na sabuni na wengine hudhani utokwaji wa utoko ni kawaida hivyo hawana budi kuacha kama ilivyo na badala yake hutumia “pads” ndogo au “wipes” zenye manukato ili kuzuia harufu/shombo ya uke na vilevile kuzuia uchafukwaji wa “vyupi” vyao.
Huitaji kuficha(Bali punguza) harufu ya asilia ya uke kwa kutumia bidhaa zenye mahukato hasa ukiwa na mpenzi wako kwani hiyo harufu ndio uanamke wenyewe na ikikutana na ile ya kiume ndio raha ya kufanya mapenzi na ikiwa mpenzi wako ni “aliyejaaliwa” atakuwa akiipenda harufu hiyo na hubaki akilini mwake hali inayoweza kumfanya akupende zaidi au kutoweza kufanya ngono na mtu mwingine bali wewe.

Hujawahi kusikia wanaume wanashindwa kutoka (date) wanawake wengine baada ya wapenzi wao kufariki dunia? Au mwanaume kushindwa kuendelea na maisha yake ya kimapenzi bila wewe na matokeo yake hata mkiachana lazima atarudi tu kwako….sababu moja wapo ni hiyo.
Kujiswafi ili kupunguza ukali wa shombo/harufu ya uanamke:
Utoko hujikusanya ikiwa mwili umetulia (usiku) hivyo hakikisha unajisafisha kila asubuhi kabla hujaanza kuoga.
Kwa wale tunaoishi Bongo wengi tunatumia maji ambayo usalama wake ni wa utata, sasa ili kuepuka maambukizo hakikisha maji ya kujisafishia sehemu zako za siri yamechemshwa vizuri. Unaweza kutenganisha maji ya kuoga na ya kusafishia uke ukitaka.
*Kabla hujaguza uke wako hakikisha umesafisha mikono yako vizuri kwa sabuni (ukiweza tumia sabuni yenye dawa) na wakati huo huo pitisha sabuni juu ya uke wako ili kuondoa vijidudu kama vilikuwepo, safisha mahali hapo(juu ya uke kwa maji na hakikisha hakuna sabuni).
*Kisha kwa kutumia kidole chako cha kati, ingiza taratibu pale ambapo uume unaingia, kwa kuanzia huitaji kwenda mbali sana. Zunguusa kidole hicho taratibu huku ukijimwagia maji kwa kutumia mkono wa pili, kisha kitoe (kitatoka na weupe mzito) safisha kidole na maji yako.
*Rudia tena na sasa kiingize ndani zaidi na ukizunguushe tena (huku ukijimwagia maji) na kukitoa utaona “utoko” mwingi zaidi kidoleni, rudia hatua hizo mpaka uhakikishe kidole kinatoka bila weupe(utoko) na utahisi hali ya usafi, hakuna utelezi.
UTOKO huwa na madhara kama
1.Kukufanya uwe unatoa harufu/shombo kali ukeni haswa wakati wa kungonoka.

2.Utoko ukibaki ukeni haswa ule wa usiku huwa una tanua kuta za misuli ya uke kwa hiyo utajikuta uke wako unakuwa karai/beseni
Ni muhimu kujiswafi
Unapojimwagia maji ukeni huku kidole kiko ndani maji huingia pia ukeni na ndio maana mwishoni kabisa utahisi umesafishika vema kabisa na utoko huo hautotoka tena siku nzima na uke wako hautokuwa na shombo kali kama ambavyo siku zote ambazo ulikuwa hujisafishi.
Kwa wale wanaotumia bath unafanya kama nilivyoeleza ila tofauti ni kuwa maji yataingia vizuri zaidi ikiwa unapata “bath” hivyo hakikisha “bath” sio ya kuchangia, maji ni salama(safi), usiweke sabuni (bath cream) au bidhaa yoyote yenye kemikali kwenye “bath” yako ili kuepuka matatizo ya kiafya na maambukizo mengine.

Tuesday, 27 January 2015

JINSI YA KUMPATA MSICHANA ANAEONEKANA MGUMU.

MWANAMUME yeyote anapotaka kumtongoza mwanamke hulazimika kwanza kumwonesha – japo kwa matendo – kuwa anampenda, au kwamba amevutiwa naye, hata kama ni kimwili tu. Hatua hii ndiyo yenye changamoto kubwa zaidi kwa mwanamume, maana ndipo wakati anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe kwa mlengwa huku yeye mwenyewe akijihakikishia kuwa haharibu mambo.
 
Mwanamume anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe wa “nakupenda” kwa mwanamke, mapigo ya moyo yanaweza kumwenda mbio, hususan kama mwanamke mwenyewe anaonekana kuwa “maji marefu”. Hata hivyo, ni kazi ambayo kila mwanamume hulazimika kuifanya.

Kazi hii ya kufikisha ujumbe kwa mara ya kwanza huhitaji umakini. Bahati njema, shughuli yenyewe ina sayansi yake, ambayo ina misingi katika mahusiano ya kijamii. Ukifahamu sayansi hii inaweza kuwa rahisi zaidi kwako kufikisha ujumbe kwa mtarajiwa wako – na kufanikiwa.

1. KUKUTANISHA MACHO NI MUHIMU
Kawaida, mambo yote huanzia – na pengine kuishia – katika kukutanisha macho. Mwanamke atakapobaini kuwa hujajaribu kumwangalia japo kwa sekunde mbili mfululizo, ataondoa mawazo na hisia zake kwako hata kabla hujasema neno lolote.

Macho ndizo zana muhimu zaidi mtu anapokuwa anataka kufikisha ujumbe kwa mwenzake kuwa anampenda, au amevutiwa naye. Hii ni kwa sababu macho ndiyo vipitisho na visambazaji muhimu vya ishara baina ya mtu na mtu, hata kama si katika masuala yanayohusiana na mapenzi.

Kukutanisha macho na mtu wa jinsia nyingine unayevutiwa naye au anayevutiwa nawe ni jambo lenye nguvu za ajabu katika kuanzisha uhusiano. Kwa sababu hiyo, hata unapofanikiwa kumtazama moja kwa moja machoni mwenzako hutarajiwi kutumia zaidi ya sekunde mbili, kutokana na nguvu iliyomo katika mawasiliano haya.

Katika hili, wanaume mahiri hufahamu ni wakati gani wa kumwangalia mwanamke na ni wakati gani wa kutomwangalia. Mara nyingi, ni vizuri zaidi kumwangalia zaidi mwanamke wakati anapozungumza, huku ukikwepesha macho kidogo pale unapozungumza wewe.

2. UNATAKIWA UWIANO, UKWELI KATIKA MAZUNGUMZO
Ni jambo lisilopingika kwamba wanaume na wanawake wanatofautiana katika maana ya dhana ya mawasiliano. Hata hivyo, bado inawezekana kuendesha mazungumzo shirikishi na yenye kuburudisha ukiwa na mwanamke, bila kuonekana wa bandia.

Watu wa jinsia zote mbili wanaweza kutuhumiwa kwa kupindisha ukweli na kujaribu kuficha tabia na mienendo yao wanapozungumza na wapenzi watarajiwa. Naam, katika mazungumzo ya kwanza baina ya wapenzi au wachumba watarajiwa uwongo – ukiwemo ule usiotarajiwa – huwa mwingi.

Katika mazungumzo ya kwanza ni kawaida kwa mwanamume kubadilisha matendo yake na mtindo wake wa kuzungumza kwa maslahi ya kumpata mwanamke, jambo ambalo huifanya hulka yake ya wakati huo kuwa ya bandia. Lakini pia wasichana/wanawake husema “Nakupenda” bila kumaanisha, pengine kwa ajili ya kumfurahisha mwanamume, au kusikia mwanamume atasemaje.

Jambo la muhimu katika mazungumzo ya awali baina ya mwanamume na mwanamke ni kuepuka michezo ya kudanganyana na kukwepana, badala yake, yafanye mazungumzo kuwa rahisi na halisi. Hapo ndipo mwanamume hujitofautisha na wanaume wengine na kupendwa kwa sababu hiyo.

3. USIPUUZE NGUVU YA LUGHA YA MATENDO
Wakati mtu anapokuwa akijaribu kuwasilisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mwenzake, lugha ya matendo yake huzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno yake. Hili limeweza kuthibitishwa kwa nyakati mbalimbali kutokana na tafiti mbalimbali.

Katika muktadha wa kujaribu kufikisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mlengwa, lugha ya matendo ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi. Kwa hakika, asilimia kubwa ya ujumbe unaowasilishwa kwa mlengwa huwasilishwa kwa njia ya matendo ya mwili na si maneno. Ni asilimia ndogo tu ya ujumbe inayowasilishwa kwa maneno – na wakati mwingine maneno huweza kuleta matatizo maana katika kuzungumza kuna kujikwaa kwingi, kwani ulimi hauna mfupa.

Ili uweze kufanikiwa katika kueleza nia yako kwa mwanamke, lazima ujue jinsi ya kutumia lugha ya matendo yako. Na pengine hutatumia nguvu, maana watu husema penzi kikohozi – kama unalo litaonekana tu machoni pa mlengwa.

Ukitafakari kwa makini utabaini kuwa huhitaji kusema sana ndipo uweze kupendwa, kwani maneno huchangia asilimia kidogo tu. La muhimu ni kuhakikisha kuwa mlengwa wako anakusoma na kukuelewa vizuri kwa kuangalia matendo ya mwili wako.

4. ACHA ASILI ICHUKUE MKONDO WAKE
Katika nadharia mbalimbali za kijamii na kidini ni jambo la kawaida kusikia kuwa binadamu wote ni sawa. Hata hivyo, katika muktadha wa kimapenzi, kila mtu mmoja mmoja anafahamu kabisa kuwa si kila mwanamume/mwanamke ni sawa na mwenzake.

Methali yenye asili ya kimagharibi husema “Uzuri wa mtu uko katika macho ya yule anayemtazama.” Hii ina maana pia kwamba, kila mtu anavyo vigezo vyake vya uzuri kwa kuzingatia maumbile yake. Pia jamii zinavyo vigezo vya uzuri, lakini hutangulia kwanza vigezo binafsi.

Unapokuwa umekaa na mwanamke ambaye anakuvutia kwa mwonekano wake, sauti yake na kadhalika, si rahisi sana kujizuia kuonesha kuwa anakuvutia. Hii ni kwa sababu si wewe, bali ni nafsi yako inayokusukuma. Na yeye mwenyewe atakusoma kwa kuangalia lugha ya matendo yako na kukwelewa, utakaobaki ni uamuzi wake tu.

Katika jamii kuna vigezo kuhusiana na kiuno, miguu, maziwa, makalio na kadhalika. Wengi wa wanajamii huvizingatia na kuongeza vyao. Huu ni ukweli wa kibiolojia ambao hauwezi kupingika. Mwanamke mwenye vigezo vinavyokubalika zaidi katika jamii yake atawavutia wanaume wengi zaidi. Hapa mwanamume hahitaji kutumia nguvu nyingi – asili ya maumbile itamsaidia humtambulisha mwanamke kuwa amempenda.

5. TUMIA CHANGAMOTO YA WALAKINI
Mara nyingi changamoto kubwa katika suala zima la mtu kubainisha nia yake kwa mwanamke hutokana na ukweli kwamba katika mchakato mzima huwa kuna wasiwasi na walakini. Kwa hakika, jambo hili ni la “pengine” au “labda” kutokana na kutoweza kufahamu kirahisi mwenzako anawaza nini.

Unapoonesha nia yako ya kumpenda mwanamke, ni kama unaamsha hisia zake kwako na ni kama vile unamuuliza: “Ungependa kuwa nami?” Kwa njia hii ni kama utakuwa unafungua mlango wa kupata jibu la “ndiyo” au “hapana” kwani huyo unayemwonesha kuwa unampenda na yeye ana matakwa yake na mapendeleo yake.

Kimsingi hakuna kanuni wala sheria rasmi unazopaswa kuzingatia wakati wote. La muhimu ni wewe mwenyewe kujiachia na kuingia katika maji usiyofahamu kina wala mwisho wake, bali wewe nenda na mkondo wake huku ukitarajia kuwa lolote linaweza kutokea. Hiyo ndiyo sehemu ya raha yake.

6. DHIBITI HISIA, MIHEMKO
Tofauti na mwanamke, mwanamume anayejaribu kuonesha nia yake hatakiwi kujiweka katika mkao wa mwanamitindo. Wanawake ndio hufahamika zaidi kwa mikao yao “ya kula” wanapokuwa katika mawindo (japo wengi hubisha), lakini si mwanamume. Wanawake ndio hutarajiwa kujieleza zaidi kwa njia ya matendo na mikao, lakini wanaume hutarajiwa kudhibiti hisia na mihemko yao .

Tofauti katika lugha ya matendo baina ya watu wa jinsia mbili hutokana na maumbile ya kujenetiki pamoja na utamaduni wa jamii husika. Yote yakizingatiwa, matakwa ya mwanamke ndiyo hupewa kipaumbele zaidi. Kwa ufupi, matendo ya kutongoza ya mwanamke huwa wazi zaidi, lakini mwanamume hulazimika kuficha hisia na mihemko yake.

IFAHAMU SAYANSI HII
Wajibu wa kufikisha ujumbe kwa mtu wa jinsia tofauti ni wa kila mmoja – mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, wanaume ndio wenye jukumu kubwa zaidi la kuanzisha, kwa kuzingatia utamaduni wa jamii nyingi. Unaweza ukaona ugumu, lakini ipo sayansi itakayokusaidia. Kama una wasiwasi na uwezo wako, ni vizuri kuyazingatia yote yaliyobainishwa hapa.

Monday, 26 January 2015

SIRI MUHIMU UNAZOTAKIWA KUZIJUA KUHUSU WANAWAKE.

UKWELI ambao haukwepeki kuhusu uhusiano na mapenzi ni uwepo wa furaha, amani na maelewano. Hivi ni vitu muhimu sana. Msingi wa yote ni pendo la dhati. Ikiwa wapendanao wana upendo wa kweli toka mioyoni mwao ni rahisi kutunza vitu hivyo.
Hakuna asiyependa kuwa na uhusiano wenye furaha na amani. Uhusiano wenye masikilizano huzaa matunda mema – kama ni marafiki tu, basi ujue ndoa inanukia lakini kama tayari ni wanandoa, maana yake mafanikio ndani ya nyumba yatakuwa rahisi kupatikana. katika yote hayo, inategemewa zaidi na namna wahusika wanavyoendesha uhusiano wao; kwa maana kwamba, yote yanahitaji ushirikiano wa wote. Hapo ndipo mwanzo wa matatizo. Wenzi wawili huwa na tofauti za hulka.

Kwa wanawake, wengi hupenda sana kufuatilia na kuhakikisha uhusiano unakuwa imara. Likitokea tatizo, mwanamke huwa mstari wa mbele kulishughulikia ili mambo yaishe. Wanawake wengi hawapendi kuwa wamewaudhi wenzi wao.
Ikitokea wakiona kuna tofauti ya kimawasiliano, mara moja husaka mbinu za kutatua na kubakisha uhusiano ukiwa kwenye hali nzuri. Hiyo ni tofauti na wanaume ambao mara nyingi wao ni watu wa harakaharaka.

Ni wepesi wa kusahau mambo au kuyachukulia kwa wepesi. Mfano, mwanamke wake akikasirishwa na jambo fulani, ni rahisi tu kuishia kusema: samahani. Wakati mwingine anaweza asiseme kabisa, akijua mambo yameshaisha. Wanawake ni tofauti. Wanafanya mambo yao kwa taratibu sana. Hasira zao zinachelewa kuisha, lakini ni rahisi zaidi kuzimaliza kwa kumwambia tu: nakupenda mpenzi, najua nimekosea, samahani mama.

Ni sentesi fupi sana lakini kwao ina maana na thamani kubwa sana. Mapenzi ni sawa na bustani, wakati mwingine inahitaji kumwagiliwa na kuwekewa mbolea. Kama ni kweli unampenda, tuliza akili na muda wako kuhakikisha furaha yake inaendelea kuwepo.

Inamaanisha kuwa, upendo wake kwako ukitamalaki muda wote – mafanikio ya kazi ya mikono yako yapo jirani tu. Mfanye mwanamke wako atabasamu. Pamoja na ubize wako, tenga nafasi kidogo kwa ajili yake.

MSAMAHA SI KUJISHUSHA!

Wanaume wengi wanaamini kumwambia mwanamke samahani ni kujishusha na kuwa chini yake, si hisia sahihi. Msamaha ni uungwana. Kama kweli unampenda kwa dhati, una shaka gani kumwambia akusamehe ili uhusiano uendelee kuwa wenye nguvu?

Hutapungua mahali popote kukubali kosa, ikiwa umekosea au kumrekebisha mwenzako badala ya kubaki bubu huku ukiwa umenuna na kusitisha baadhi ya huduma. Kama ilivyo kwako, tambua kuwa mwanamke naye ni binadamu, anaweza kufanya makosa lakini asijue!

Kumwambia kwa upole ni jambo zuri. Atakusikiliza, atakuelewa na atajirekebisha alipokosea. Kukaa nalo moyoni hakuna maana.

PUNGUZA UBABE.

Wapo baadhi ya marafiki wanaamini kuwa ubabe ni sehemu ya ukamilifu wa uanaume. Siyo kweli. Huna sababu ya kuwa mkali sana au mwenye amri muda wote. Mwanamke anahitaji kubembelezwa, upendo na kuonyeshwa namna anavyothaminiwa.

Wengine wana tabia ya kuwapiga wenzi wao, kitu kidogo tu, tayari kipigo. Vipi akikutana na mkarimu, asiyepiga na anayebembeleza? Akiachana na wewe utamlaumu nani? Ni kweli kuna wakati mwanamke anahitajika kukaripiwa akikosea, lakini si sawa kuwa mkali kupitiliza wakati wote.


Sunday, 25 January 2015

ETI UKIMPA MPENZI WAKO KINYUME NA MAUMBILE NDIO ATAKUPENDA DAIMA?

Kuna siri moja ambayo nahisi ipo kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa na hata wale walio kwenye uhusiano wa kawaida kwamba, wanafikia hatua ya kutoa aina hiyo ya penzi eti ili wapenzi wao wasiwasaliti. Jamani hii inaingia akilini kweli?

Unafikia hatua ya kuhatarisha maisha yako kisa unataka kukamilisha ile sentesi ya kwamba unampa mumeo kila anachokitaka? Huo ni ulimbukeni na kama wapo wanaoendelea kufanya hivyo, wanajitafutia matatizo yatakayowafanya waje kujuta baadaye.

Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampatiliza katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?
Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?

Ni kamchezo ka’ nyumba ndogo

Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaoongoza kwa mchezo huo mchafu ni wale wezi wa mapenzi ambao hufahamika kwa jina la nyumba ndogo.
Hawa eti wanatumia mbinu hiyo kuwashika waume za watu. Kimsingi hii ni aibu na wanaokubali kufanyiwa hivyo wanajidhalilisha na hawawezi kudumu na wanaume wao.

Usithubutu kabisa

Mapenzi kinyume na maumbile licha ya kwamba yamekatazwa hata na vitabu vitakatifu, madhara yake kiafya pia ni makubwa. Wapo wengi ambao sasa wanajuta kwa kufanya mchezo huo kutokana na kupata matatizo wakati wa kujifungua lakini pia wengi wao imekuwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa ukiwemo Ukimwi.

Ni laana

Wanaofanya hivyo wamelaaniwa na wanaweza kushangaa uhusiano wao unakumbwa na matatizo kisha kusambaratika kwani Mungu hawezi kuubariki ule unaokwenda kinyume na maagizo yake.
Ni suala tu la kukaa na kujiuliza, wewe mwanamke unapata raha gani kufanya mapenzi kwa njia ambayo haijaruhusiwa? Wakati mwingine nashindwa hata kuwaelewa hawa wanaofikia hatua ya kujisifia kuwa eti wanawaachia waume zao ‘wajisevie’ wanachotaka kwa kuwa wanawapenda.
Hivi watakuwa na akili timamu? Kumpenda mtu ndiyo uwe tayari kuhatarisha maisha yako kiasi hicho? Tena kwa taarifa yako wale wanaowakubalia wapenzi wao mapenzi kunyume na maumbile wanaonekana wajinga na wanadharaulika. Hakuna mwanaume anayeweza kumheshimu mwanamke anayeweza kuuweka rehani mwili wake kwa njia hiyo.
Nimalizie makala haya kwa kusema kuwa, kanuni ya kwamba unatakiwa kuhakikisha unampatia mpenzi wako kile anachokipenda inabaki palepale lakini umkubalie katika yake yasiyo na madhara kwako. Yale ambayo unaona yatakuletea matatizo, mkatalie kwa kumpa sababu za msingi. Kama ni muelewa atakuelewa, asipokuelewa kuwa tayari akuache lakini usihatarishe maisha yako.