Saturday, 11 June 2016

TOFAUTI YA MAWASILIANO KTK NDOA.


Mtazamo wa mwanaume na mwanamke kuhusiana na suala la mawasiliano ni vitu viwili tofauti kabisa.

Wanaume huwa na ulimwengu wao sawa na wanawake ambao nao huwa na ulimwengu wao linapokuja suala la kuwasiliana au maongezi kati ya mke na mume.


Wanaume huwa na ulimwengu wa ngazi (hierarchical social order) kwa kujiweka nafasi ya kutawala, kuwa na amri au kuonesha mafanikio au uhuru na mamlaka aliyonayo kwa wengine. Hii ina maana kwake kuongea ni pamoja na kuhakikisha hayo yametajwa ni jambo la msingi.


Lengo kubwa la mawasiliano au kuongea katika ulimwengu wa wanaume ni kutunza uhuru wao na kuimarisha nafasi yao katika ngazi ya kijamii.


Wanawake kwa upande wao, linapokuja suala la mawasiliano au kuongea ni yeye mwanamke binafsi kujihusanisha au kujijumuisha katika ulimwengu wa wengine (networking).

Kwa mwanamke kuongea ni kuimarisha ukaribu (intimacy) kwa maana kwamba kwa mwanamke kuongea ni suala la feelings.

Mawasiliano au kuongea ni gundi ambayo huwaunganisha wanawake pamoja wao wenyewe au mwanaume na kuongea humfanya kujisikia karibu na yule anaongea naye na wakati mwingine huondoa upweke.


Tangu wanawake wakiwa na umri mdogo, akitokea binti mwingine akawa haongei basi wenzake kumlaumu kwa tabia yake ya kuwa antisocial.


Kwa kuwa wanaume huongea ili kuimarisha status zao ndiyo maana utakuta wanaume wengi huongea kwenye public.

Wanapenda kutoa reports kwenye mikutano, hutoba katika makundi ya watu na kubadilishana habari kazini na wafanyakazi wengine na huko wanang’aa lakini wakifika nyumbani wanakuwa kimya kwani wanajua nyumbani ndipo kwenye uhuru wao wa kuwa silent.


Kwa wanawake nyumbani ni mahali pa kuongea kwa uhuru na ukaribu (intimately), nyumbani ni mahali mwanamke anasubiri kwa hamu kuongea na mume wake anayempenda.


Data nyingi zinaonesha wanaume wengi huongea kwenye public kuliko wanawake na wanawake wengi huchonga sana majumbani.


“Kumsikiliza mwanamke maana yake umesema unampenda”


Kwa mwanaume kuongea ni kuwasilisha habari, kuimarisha status au njia ya kutatua tatizo, kwa mwanamke kuongea ni kuhusisha ukaribu wa ndani (sharing) na mwingine.


Wanawake huwa wanawashangaa sana wanaume kuhusiana na suala la mawasiliano.

Mwanaume A na mwanaume B wanaweza kuangalia TV bila kuongea na kesho wakasema ni marafiki, kitu ambacho kwa wanawake ni vigumu kwani urafiki kwa mwanamke ni pamoja na kuongea.

Wanaume hutumia mfumo wa kuwasiliana kwa kutumia kitu cha tatu (triangulation)

Hii ina maana mwanaume A na mwanaume B ni marafiki kwa kuwa wametumia kitu cha tatu TV kuwapa attention na kujikuta wameunganishwa.


Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba kama mwanamke ana mume ambaye anachonga sana kwenye public na akifika nyumbani anakuwa bubu ili huyu mwanaume aongee inabidi mke atafute kitu cha tatu inaweza kuwa kufanya kazi yoyote kitu ambacho wote pamoja watakuwa wanafanya na katika kufanya mwanaume utajikuta anaongea.

No comments:

Post a Comment