Saturday, 11 June 2016

ANA MTAZAMO GANI KUHUSU PESA?


Watu tunatofautiana katika mitazamo kuhusu fedha, baadhi huiangalia fedha kwa jicho la kutoa (giving) na wengine kwa jicho la kuitunza (saving) na wengine kutumia (spending)

Kama wewe ni kijana wa kiume au kike ambaye upo katika harakati za kusaka mwenzi wa maisha basi ni muhimu sana kuwa na makubaliano au kufahamu mtazamo wa huyo mtarajiwa kuhusu fedha.


Judy ni mwanamke ambaye mume wake Jeffy akipata mshahara huamuriwa akabidhiwe na anachofanya ni kugawa zile pesa na kuziweka kwenye bahasha tofauti tofauti, bahasha moja kwa ajili ya kununua chakula, bahasha nyingine usafiri, nyingine pango la nyumba, nyingine kununua nguo na nyingine sadaka kanisani na nyingine kwa ajili ya dharura.


Mume akitumia pesa kutoka moja ya bahasha lazima aeleze ni bahasha ipi alichukua pesa, na amefanyia kitu gani, na risiti ziko wapi na change zipo wapi na duka gani alienda kununua na alikuwa na nani na ametumia usafiri gani na amelipa kiasi gani.

Jeffy hujikuta oppressed, frustrated na hawezi kuvumilia tena!


Je, unadhani hiyo ndoa itadumu kwa muda gani?


Kumbuka wengine hutumia pesa kama emotional agenda, kama kwenye huo mfano bahasha za Judy si bahasha tu bali ni mfuko anaotumia ku-mcontrol Jeffy.

Kuna watu walitembelea ndoa moja na ilikuwa ni summer time na joto lilikuwa limepanda nyuzi 40 centigrade.

Ikafika mahali watu wakawa wana sweat utadhani wapo ndani ya sauna wakati huohuo nyumba ilikuwa na viyoyozi vya uhakika ila vimezimwa kwa utaratibu kwamba hadi ifike tarehe iliyowekwa ndipo huwashwa.

Wanandoa walipoulizwa kwa nini kuzima wakati joto linatuua, wakawajibu tarehe tuliyoweka kuwasha viyoyozi haijafika bado na kuwasha sasa ni matumizi mabaya ya pesa.

Hawa wanandoa wanafurahia ndoa yao kwa kuwa wanamtazamo sawa kuhusu fedha na hakuna kulemba!

Kuna wanawake ambao kwao fedha za mume ni za familia, na pesa zake ni zake.

Hii ilitokea kwa Suzy na Simon wakati fulani ambapo Suzy alikuwa anafanya kazi na Simon naye alikuwa anafanya kazi.

Simon akipata mshahara, Suzy humkomalia na kupanga bajeti namna ya kutumia hizo fedha kwani anachojua ni kwamba mshahara wa mume ni wa familia na mshahara wake ni kwa ajili yake tu.

Hata Simon alipotaka kununua kitu kutokana na ule mshahara basi Suzy huja juu kwa kuanza kutoa lecture kwa Simon namna watoto wanavyohitaji nguo na vifaa vingine wakati huohuo yeye Suzy pesa anayopata kazini kwake anaila kisirisiri.

Mitazamo kama hii huweza kuharibu ndoa kwa kasi ya ajabu kama dhoruba.

Angalia kwa makini yule unategemea kuwa mke au mume anazielewaje fedha kama unaona mtazamo wake ni wa ajabu ajabu ushauri wangu ni kwamba fikiria kwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwa naye.

No comments:

Post a Comment